The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 804
- 1,646
Niseme nini hasa? Tundu Lissu ni miongoni mwa wanaharakati, wanasheria na wanasiasa brilliant wanaojua kuelezea jambo kwa lugha rahisi, iliyonyooka na kueleweka na yeyote...
Ni wazi kuwa huyu jamaa kasoma kweli na ameelimika pia na anajua mambo mengi sana...
Hapa anaeleza maoni na mtazamo wake akirejea uchaguzi mkuu wa Kenya juzi kati na namna ulivyofanyika akilinganisha na mfumo wa uchaguzi wa Tanzania...
Fuatiilia kwa kumsikiliza mwenyewe. Utampenda.....
======================
===Point highlights ya alichosema===
MABAYA AMBAYO HAKUYAONA KTK UCHAGUZI MKUU WA KENYA:
1. Mgombea/wagombea wa vyama na binafsi wa nafasi mbalimbali za ubunge & Urais kuenguliwa au kuzuiliwa na hivyo kuwa disqualified kwa sababu yoyote ile..
2. Mgombea akiingiliwa katika misafara au ktk kampeni zake na vyombo vya dola i.e KenPolice, JWK au usalama wa taifa...
3. Hakuona wala kusikia mawakala wa wagombea wa vyama vyote kutoapishwa, kunyimwa IDs, kuzuiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura, kufukuzwa kwenye vituo vya kupigia kura na kunyimwa matokeo ya vituo...
4. Vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa completely neutral. Havikuingilia mwenendo wa process yoyote ya uchaguzi...
5. Hakuna election observers wa ndani ama wa nje, NGOs za ndani ama nje walionyimwa vibali (accreditation)...
6. Hakuona incumbent president Uhuru Kenyatta japo alikuwa na mgombea aliyemtaka ashinde, lakini hakutokea hata mara akipanda jukwaani kumfanyia kampeni....
Wala hakupata nafasi kabisa kutumia mamlaka yake kuamuru vyombo vya ulinzi vifanye fujo ili mradi mtu wake ashinde...
MAZURI ALIYOYAONA;
1. Kulikuwa na complete transparency ktk hatua zote za uchaguzi wa Kenya kuanzia uteuzi wa wagombea, kampeni, usimamizi, upigaji kura na utoaji matokeo hatua kwa hatua kuanzia vituoni hadi kwenye kutangaza rasmi...
2. Matokeo yalikuwa wazi mno kwa kila mtu kuona kila kitu mwanzo hadi mwisho. Ndiyo maana mpaka sasa kuna utulivu mkuu nchi ni Kenya kulinganisha na chaguzi zilizopita zilikuwa zikiishia kwa kunyukana kwa sbb ya kutokuwepo na uwazi ktk mchakato mzima...
3. Tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya haina impunity kama ikifanya uharamia wowote na ndiyo maana matokeo ya ushindi wa William Rutto yanapinga mahakamani...