VIDEO: Dr. Ulimboka; kwa kinywa chake mwenyewe! | Ambayo hukuyajua...

I do not support mgomo but I really feel sad for him, as a human being he did not deserve it. No matter who did it, this was typical inhumanity.
 
Serikali Dhaifu, Usalama wa vasco dhaifu na hata walio andaa mashambulizi ni dhaifu na mambo yao wanayapeleka holela holela ndio maana wanaumbuka na mda si mrefu mambo yata bumbuluka :israel:
yabumbuluke mara ngapi?
 
Rais mpya atakaeingia mwaka 2015 ni vema auvunje kabisa huu usalama wa taifa na kuusuka upya. Nchi haina usalama wa taifa bali ina wahuni tu, wachumia tumbo.
 
Kati ya watu waliohusika kwenye utekaji huo inasemekana alionekana ubalozi wa south afrika akifuatilia visa tayari kwa safari ya sa.nukuu kutoka gazeti la mwanahalisi
 
kauli ya PINDA YA "LIWALO NA LIWE" imetimia, jk na pinda mlaniwe. du! inasikitisha sana, pole ulimboka nmeshindwa kujizuia nikamwaga machozi.
" kifo ni kifo, wengine watakufa kwa panga au kwa shoka na wengine watakufa kwa bila staili, any way it doesn't matter
all is natural dead"
 
Hili linanipa connection na matukio mengi sana ambayo serikali haiwezi kujitenga, kwanini tuumize vichwa? kwanini watu tunayumbishwa kuhusu hili? me nadhani watanzania tunapaswa kusimama imara katika mambo haya, vinginevyo hakuna mtanzania yeyote aliye salama hapa. Hawa jamaa(government) wanaudhi sana, KAMA NI KWELI HAWAHUSIKI WANGEUNDA TUME HURU MAPEMA KABLA SIKU YA PILI YA TUKIO HAIJAFIKA. Hawa hawawezi kujitenga na hili tukio, huyo Msangi waliyempa kusimamia tume husika tumeona na kusikia mangapi kuhusu dili zake za kishetani? wamemng'ang'ania Kwanini kama sio kupoteza ukweli? Me naona hukumu ya kosa hili president hawezi kuikwepa, kama ningeweza ningempa hukumu mbaya sana kova na hilo jamaa lake alililazimisha lisimamie hicho kitume chake cha kipuuzi.
 
Natumia nokia 3310 sing'amui kitu bhana,,,,ah jf imetutenga sana wati wa mobile za bei rahis,,,,hivi kwenye banda lenu pale 77 hakuna jfmbolibe phone(invisible)
 
Ukisikiliza mkanda huu, ni dhahiri waliomteka Dr. Uli na mateso waliyomfanyia walitaka atoe habari wanayoitaka na inawezekana hawakuridhika na yale aliyosema au ni katika kumlazimisha akiri makosa ambayo hakuyatenda. Kwa mara nyingine tunashuhudia udhaifu mkubwa wa vyombo vyetu vya usalama hasa polisi, sina hakika iwapo Afande Mwema atasafisha nyumba yake au atajaribu kupaka rangi kuficha aibu hii. Hebu fikiria; umejua ya Dr. Uli kwa umaarufu make, hivi ni raia wangapi wanasota jela kwa makosa ya kubambikiwa?
 
Pinda sijui huwa anajisikiaje anapokuwaga kanisani Parokia ya Kiwanja cha Ndege tena siti za mbele, eti anaomba Mungu huku kichwani akijua maemtendea binadamu mwenzake unyama huu. Kwa huyu 'jamaa' yetu hatuna la kusema maana ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
 
Kuna mtu yoyote amesikia tamko rasmi la Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na unyama uliomkuta Dr Ulimboka? Tamko lolote, liwe la kupongeza, kulaani, kutaka uchunguzi (huru au wa polisi), lolote. Na kama CCM hawatoa tamko kwanini? Siku 10 hawajatoa tamko lolote?

mkuu, matamko ya chama haya hapa
ccm+2.jpg


ccm+3.jpg


ccm+5.jpg
 
Inasikitisha sana.

Nanukuu sentensi chache nilizoona zina ujumbe mzito.

Ulimboka: ''Nia yao ilikuwa destruction, they were soldiers''

Sentensi hii inatoa dokezo la wahusika

Watesaji: ''We umezidi sana usumbufu sasa leo utaenda mahali ambako hii kitu itakuwa off''

Kulingana na mazingira yaliyopo inawezekana kuhisia hapa anayesumbuliwa ni nani.
Sentensi hii inazidi kuongeza nguvu dokezo la kwanza na pia inathibitishwa na maswali aliyojibiwa Ulimboka hapa chini.

Ulimboka: ''Namsumbua nani mimi nilikuwa kwenye dialogue''

Watesaji: ''We unajua unayemsumbua''

Ulimboka: ''Mimi mmenikuta kwenye dialogue''

Watesaji: ''Huwezi kujua''

Hii inathibitisha kuwa tukio liliandaliwa
 
Mkubwa,thnx kwa kuzidi kuongeza hisia za chuki,ila mi nashndwa kuifungua,natumia nokia,nikifungua pale kwenye "You tube video" inadisplay sms tu!!
 
Wakuu,

Baada ya kusikia maneno toka kwa wadau mbalimbali, toka magazeti mbalimbali na vyombo vingine vya habari juu ya NINI kilimsibu na NANI anahusika; tumeona ni vema kuwashirikisha video hii ili mweze kusikia toka kinywani mwake mwenyewe.

Nikiweka maneno mengi nakuwa nachakachua, ni vema kukupeni alichokiongea kwa kinywa chake.



NB: Video hii ruksa kutumiwa na vyombo vingine vya habari kuwahabarisha wengine wasio na access na JamiiForums


tupieni hapa: 4shared.com - free file sharing and storage tuishushe nzimanzima.
 
Last edited by a moderator:
Thanx for this Invisible ,Sidhani kama kuna ubishi tena juu ya nani waliofanya unyama huu kwa Dr.Ulimboka.

1.Mtu ambaye walikutana naye kabla ya kutekwa ni wa Ikulu.

2.Hao watu watano walikuwa na silaha za kipolisi.

3.Maneno waliomwambia wakati wanamtesa mf."Umetuangaisha sana leo mwisho wa jeuri yako" au "Kwanini hutaki kusaini makubaliano"

4.Gari waliyotumia kumchukua leaders haikuwa na namba.Hii haiwezi kufanywa na watu wasiokuwa wa usalama ni lazima watawekewa vikwazo njiani.Hakuna sehemu inayoonyesha kuwa gari ilisimamishwa hata mara moja njiani.

5.Maeneo waliompeleka kumtesa na hizo nyumba nzuri zisizokuwa na watu wakusaidia hata upige kelele vipi.(Yapo yenyewe mahuni ya Taifa)

6.Aina ya mateso waliyompa yanaashiria kuwa ni skilled people

7.Jinsi walivyomfunika na matawi ya miti.Hii ililenga kuficha maiti isionekane very soon

8.Jinsi watekaji walivyoondoka mmojammoja baada ya kumfunika.Hii ni kuhakikisha kuwa amekufa kweli kwani mkiondoka kwa pamoja anaweza aonyeshe dalili za uhai mara baada ya nyinyi kuondoka.Hii ni technique ya kuextend muda wa kuwa na mateka na kuwa kweli amekufa kama itakavyoshuhudiwa na mtu wa mwisho kuondoka.
 
Last edited by a moderator:
Pole Dr Uli,,,,,,sijaiona hiyo video ila hata nilipoiona kwenye vyombo vya habar inatosha
 
Hii serikali ya magamba nuksi sana. Unaweza kumuumiza mwanadamu mwenzako kiasi hiki kisa u dhaifu wa kukaa meza moja na kutoa hoja!
 
Back
Top Bottom