MHESHIMIWA II

Mogambi

JF-Expert Member
May 25, 2012
209
351
Moja

KIJIJI cha Tung’aine kinapatikana mkoani Mara katika wilaya ya Tarime mpakani kabisa na nchi jirani ya Kenya. Huko unapatikana mto mkubwa unaojulikana kama mto mesani. Ni katika bonde kubwa la mto huo kunapopatikana uwanda mkubwa wenye nyasi zilizo wanda mithili ya zulia zuri ndani ya sebule kubwa ya kisasa.
Aghalabu ni uwanda ambao umeipa wilaya ya Tarime umaarufu wa kitalii, ukivutia watalii wengi kila mwaka.
Machera akiwa na Anastazia walikuwa maeneo hayo kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka. Ulikuwa mwaka uliojaa visa na mikasa, waliona ni stahiki yao kupata mapumziko hayo kujisahaulisha matukio ya mwaka huo yaliyosumbua akili zao. Lakini wahenga walisema baada ya kisa mkasa.Ni kama mwaka huu ulitaka kuwavuta wabaki nao. Matukio ya mwaka huo yaliendelea kuwasakama.
Hali wakiendelea kujisahaulisha yaliyopita, simu ya mkononi ya Machera iliita, namba ngeni ikicheza kwenye kioo cha simu hiyo ya kisasa. Aliipokea na kusikia sauti nzito yenye mikwaruzo, haikuwa sauti ngeni, alishawahi kuisikia hapo awali katika moja ya matukio yaliyokuwa yanasisimua ya mwaka huo.
"Bila shaka hujambo bwana Machera, na sauti yangu naamini umeipata vizuri. Nilikueleza huwezi kucheza na mimi, mimi ni bomu la nuclear. Ulikuwa unaniwinda na sasa ni zamu yangu kukuwinda, tofauti ni kwamba mimi nimekupa tahadhari ili ujue unapambana na nani"
Sauti hiyo ilinyamaza ili kutoa nafasi kwa Machera kutoa maoni yake, sauti iliyowahi kumpa mhadhara juu ya kundi kubwa na hatari la siri. Kundi lililodaiwa kusambaza na kuingiza sumu na maadili potofu katika jamii zote za dunia huku wakielekeza siasa, chumi, na mifumo yote ya kijamii kuwa na mwelekeo waliotaka wao kwa kutumia maneno mazuri mazuri kama vile utandawazi, kwenda na wakati, haki za binadamu na Demokrasia. Kwa kutumia siasa na uchumi kwa msaada wa vyombo vya habari walihamasisha mmomonyoko wa maadili kote duniani.
Watu hao walijikita katika nyadhifa muhimu za uongozi na idara muhimu za dunia yakiwamo mashirika makubwa ya umoja wa mataifa. Kwa nje kundi hilo halikufahamika kwani lilikuwa moja ya makundi kadhaa yaliyofanya mambo yao kwa usiri mkubwa wakiwatumia watu maarufu na wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuchumi ili kupitisha ajenda zao. Kwa njia hiyo kundi hilo lilifanya hila na kuhalalisha mambo haramu huku mambo halali yakiharamishwa bila umma wa dunia kutambua kwa haraka, lakini ikawa ni mambo yaliyokuwa yanatendeka kidogokidogo na hatimaye kuanza kuonekana kama ni mambo ya kawaida. Mwisho wa siku ikawa ni mambo yanayodaiwa kwa kigezo cha haki za binadamu, mataifa makubwa yaliyotawala kwa kanuni mahsusi za kundi hilo, yakashadadia na kuyafanya mataifa tegemezi yafanye uhalali wa mambo hayo kwa kigezo cha misaada.
Kwa ubabe huo wa mataifa makubwa dunia ikawa ni ishara kubwa ya utawala wa uovu usiozingatia adili. Kundi hilo likitazama vitu hivyo kama chanzo cha nuru na utajiri wa maarifa batili waliyotengeneza na kuipumbaza dunia kwa hayo. Wakiyaita Uhuru, usawa wa kijinsia na haki za binadamu.
Katika tawala za namna hiyo, mambo yaliyohusika na usafi wa mwili, roho na nafsi yalionekana kupitwa na wakati. Kundi hilo likatumia uwezo wa kifedha, ushawishi wa kisiasa na kupitia sayansi iliyopingana na uwepo wa Mungu, kuhalalisha kila aina ya uchafu katika maisha ya wanadamu, wengi wakikana uwepo wa Mungu kwa kuamini maneno na propaganda za wanasayansi wao waliowatengenezea umaarufu ulimwenguni kote!
Dini za ulimwengu, sasa zilipata wahubiri waliohalalisha maovu na kuyaweka wazi. Wahubiri wengi wakiwa ni wanachama halali wa kundi hilo huku wakikusanya makundi makubwa ya wafuasi. Mafundisho yao yakiwa ni juu ya mafanikio na juu ya kuamini uwezo wao binafsi, kwa sehemu wakiwaaminisha watu kwamba Mungu anajua udhaifu wao na ni juu yao kuamua lipi ni baya na lipi ni jema, na kwamba kama dhamiri na nafsi zao ziliona sawa, basi hakukuwa na ubaya.
Viongozi hao walifanya miujiza mikubwa kwa kutumia nguvu za giza na watu waliwafuata wakiamini ni uweza wa Mungu. Waliamini, kwani tayari kundi hilo lilikwisha waandaa kisaikolojia kuamini katika miiujiza. Wengine wakijitangaza hadharani kuwa wao ni mashoga na kutangazia ulimwengu kwamba huo ni aina mpya ya upendo miongoni mwa wanadamu.
Waliosimama kupinga walibezwa na kuulizwa wao ni nani kuwahukumu wenzao. Dunia sasa ilikuwa inazidi kuchanganyikiwa na wanadamu waliona ni kawaida tu. Uovu huo haukuishia hapo bali zinaa ilionekana ni kitu cha muhimu huku ikihamasishwa kwa kutumia vyombo vya habari vilivyofanya wanadamu waone zinaa ni suala la kawaida na la kifahari.
Sasa haikuwa ajabu tena kusikia kwamba kaka na dada wana mahusiano ya kimapenzi au mzazi na mwanae. Ile enzi ya sodoma ilikuwa imerejea, na wala haikuwa ajabu pale wanadamu waliposema ni haki yao kuishi na wanyama wawapendao kama wanandoa.
Mataifa yaliyopingana na uozo huo yalitengenezewa ajenda na sababu, yakavamiwa na kwa lazima yakaingiliwa kwa kigezo cha Demokrasia.
Sasa Machera aliitambua vema sauti ile, ilikuwa sauti ya The Don, Yule waziri aliyetoroka baada ya kutiwa mbaroni kwa mauaji ya kijana aliyejulikana kwa jina la Elinisa. Akakumbuka maneno aliyatamka baada ya kumtia mbaroni, ‘nina uwezo wa kuishi kokote kule duniani. Kokote kuliko na ushawishi wetu’ na sasa alikuwa amelithibitisha hilo.
The Don Alikuwa anaongea naye kutoka Marekani akimweleza kuchukua tahadhari kwani alikuwa anamwinda.
"Tahadhari? Kama wewe ni mtu makini bila shaka ungekuwa unafahamu kuwa mara zote nakuwa makini na wala siambiwi muda gani nichukue tahadhari. Ninakufahamu vema na watu unaowafanyia kazi, daima nipo tayari kupambana na ninyi hadi kufa". Machera alimjibu Don.
"Ha ha ha, kijana matata sana wewe. Sayansi, siasa, uchumi na hata dini za dunia zipo upande wangu, huwezi kuzima moto huu. Kwa taarifa yako tu hapo ulipo nina watu wangu wanaokutazama, kila unachofanya tunapata taarifa, kwakweli upo ndani ya box kijana. Hebu fikiri, Mimi nipo Marekani, lakini najua kwamba hapo ulipo ni chini ya kivuli kando ya mto na upo na msichana mweupe ambaye amevalia miwani, suruali ya jeans, buti za cowgirl, kofia ya sobrero na fulana ya mikono mirefu, tazama unageuka kumwangalia. Nadhani umethibitisha."
Machera alibaki kimya, kichwani mwake kulikuwa na wasiwasi.
‘Ina maana hawa watu wananitazama hapa nilipo na ninachofanya?' Wakati akitafakari hayo sauti ya The Don Ikasikika tena masikioni mwake.
"Najua unajiuliza vipi nimefahamu hayo, usipate shida, ni teknolojia. Kwa kweli ni teknolojia ambayo sasa imeanza kutumika huku Marekani na tunatarajia kuingiza Afrika hivi karibuni na Tanzania kwa upendeleo itakuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kuipata na kuifanyia majaribio. Inaitwa microchip technology. Kazi yake ni kutuwezesha kumonita akili za walimwengu ili kuondoa dhana za kufikiri kwa ufasaha. Tunajua kwamba tumefanikiwa kwa kiwango kutengeneza akili tegemezi kwa watu wengi na nchi nyingi duniani kupitia mitandao na filamu, lakini hakuna ubishi kwamba hii programu itakuwa thabiti zaidi kwa sababu ina uwezo wa kutawala mfumo wa fikra wa mtu bila yeye mwenyewe kujua, hivyo inakuwa inarahisisha programu hii kuchakachua uwezo wa kufikiri wa mtu na kumpa machaguo ya kutekeleza amri za Komputa zetu.
“Kwa maana nyingine ni kwamba chip hiyo inaruhusu computer zetu kufanya asilimia arobaini na tano ya maamuzi ya huyo mtu kwa kuulazimisha ubongo wake kufanya hivyo. Kama roboti vile. Na nimeona vema nikushirikishe hili kwani naamini vita unayopigana, ni unapigana na wewe mwenyewe. Kwa taarifa tu, kadri unavyoendelea kunisikiliza ndivyo tunavyozidi kuuvamia na kuteketeza baadhi ya mafaili ya ubongo wako."
The Don alimaliza kuongea kwa kicheko cha dhihaka. Machera akajikuta anadondosha simu toka sikioni mwake huku akishindwa kutafakari kwa muda. Mara akaisikia tena sauti ya The Don ikitamka kwa mwangwi kichwani mwake ‘unaona, hata bila simu tayari tunaweza kuwasiliana kwani ubongo wako kwa asilimia kadhaa ni mali yetu. Tutazidi kuwasiliana kijana, jiangalie sana’
Machera alinyanyuka. Kwa muda sasa Anastazia alikuwa akimwangalia kwa wasiwasi. Kadri muda ulivyozidi kusonga mbele Ana aligundua kuwa mpenzi wake huyo hakuwa sawa. Alimjua vema, haikuwahi kutokea Machera apate wasiwasi mkubwa hivyo kwa ajili ya vitisho vya wahalifu, siku zote kuna namna ambayo aliweza kuwashinda. Lakini leo…. Haikuwa kawaida. Kwa vyovyote vile, chochote alichosikia kilikuwa na kishindo kikubwa sana.
Ana alimsogelea na kumkumbatia kama mama anayejaribu kumtoa wasiwasi mwanae kipenzi, halafu kwa sauti tulivu ya kusema usijali mwanangu mama yako niko hapa kukulinda, akatamka;
"Usiumie kichwa mpenzi, chochote ulichosikia ni hila tu, hakuna jipya ni mbinu za kimafia tu ili unyong’onyee upishe wafanye mambo yao. Usiwaruhusu watuharibie muda wetu wa kufurahia penzi letu."
Machera alimtazama binti huyo mrembo kisha akasema
"Ningempata wapi mwanamke anayenifaa zaidi yako mpenzi? Si tu nina bahati, bali nimejaaliwa msaidizi hasa aliyetoka katika mbavu zangu. Naamini ulichosema ni pointi ya msingi kabisa, ya nini watuharibie fursa yetu ya kufurahia maisha, potelea mbali, nitadili nalo baadae" Alimaliza kuongea na kujaribu kumbusu mrembo wake, lakini Anastazia akamzuia kwa kidole chake cha pili baada ya gumba kwa kukiweka mshazari midomoni kwa kijana huyo na kusema;
"Sema tutadili nalo baadaye! au unadhamiria kunificha ulichoambiwa kwenye simu?"
"La hasha kichuna wangu, nisipokueleza wewe nitamweleza nani anayenifahamu vizuri zaidi yako?" Machera alijishaua na hapo akapokea busu mwororo toka kwa mrembo huyo.
Kwa pamoja walinyanyuka huku wameshikana viunoni na kumwelekea mwana punda aliyekuwa anapura majani pembeni yao. Baadae kidogo walionekana wakiwa juu ya mgongo wa mwanapunda Yule wakishuka bondeni kwenye mto mahali penye kina kirefu, mikononi wakiwa na ndoano zao zilizozamishwa kwenye maji tulivu ya mto mesani.
Mara Simu ikaita tena, mapigo ya moyo wake yakadunda kwa kasi mara mbili ya kawaida.
Hofu!
Hofu!
Hofu ya kisichojulikana ikammendea na kuutikisa mfumo wake wa fahamu, kidogo Simu idondoke mikononi mwake kwa kale kajasho ka kihoro kalikototesha viganja vyake. Ikawa hata kuinyanyua Simu yake kuiweka sikioni au basi kuitazama, ni changamoto asiyoelewa nini maana yake. Hapo, Machera akajitia ujasiri, ujasiri wa bandia kwani mapigo ya moyo wake yalieleza kitu tofauti.
Naam, sauti ya Anastazia ikamzindua toka kwenye kimuhemuhe hicho, sauti hiyo ikamkumbusha yeye ni Nani, mpelelezi maarufu nchini, mtu aliyetegemewa na taifa kwenye masuala nyeti yaliyohitaji akili na ujasiri, vitu ambavyo alijaliwa.
"Mpenzi, hiyo Simu vipi? Hujaisikia?"
Sauti laini, nyororo na tamu. Sauti iliyomkumbusha ni mwanaume tegemewa wa mwanamke huyu mrembo.
"Oh, aisee sijui Nilikuwa nawaza nini!" Akazinduka na kuinyanyua Simu yake na kutazama kioo cha Simu hiyo. Kwenye kioo hicho jina la mtu mwenye mamlaka Kubwa zaidi nchini likaoneka. Mheshimiwa Raisi wa serikali ya mpito, mheshimiwa Sebastian Masebo.
Ile kuona jina la mheshimiwa Sebastian Masebo, moyo wake ukashuka, akajipata akivuta mkupuo wenye ujazo wa hewa na kutoa mkupuo mwingine nje ya mapafu yake kwa ujazo ule ule. Aliweza kupumua vema sasa, mapigo ya moyo wake yakirejea kwenye utaratibu wake wa kawaida.
"Naam mheshimiwa raisi, shikamoo Mkuu." Machera akatamka kwa uchangamfu mwingi.
"Marahabaa kijana wangu, habari za likizo bwana?" Mheshimiwa rais akasaili, sauti yake ikionekana tulivu, ikisadifu mamlaka yake.
Mamlaka ambayo kwa kiasi kikubwa aliyapata kupitia ile kamati teule isiyotambulika kisheria, kamati ya fitna wengine huiita hivyo, ikiaminiwa kuwa ni kamati ambayo ikiwa kinyume chako, hata ukafanya nini basi huwezi kuunda serikali, kinyume chake kikiwa kweli. Ukikubalika, basi unaipata nafasi hiyo.
Tetesi nyingi Mtaani zikidai kamati hiyo haikuteuliwa na mtu ila baba wa taifa. Naam, hata ingawa alikuwa ni marehemu, ilisemekana mzimu wake ulihusika kukiunda kikosi hicho cha kamati, ambapo Kila mteule alikula kiapo cha utii kwa ulinzi wa taifa, kiapo cha uzalendo, uadilifu. Ilisemekana kuwa, waliokengeuka anguko lao halikukawia na walianguka anguko la aibu. Hizo zilikuwa ni simulizi mitaani.
Kwa upande wa pili, ni Machera, Mkuu wa majeshi, Mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa na raisi mstaafu walioratibu mkakati uliompatia mheshimiwa Sebastian Masebo cheo chake kipya cha rais wa serikali ya mpito! Kamati teule!
"Sijambo Mkuu, natumaini hali inaendelea vema nchini. Hongera kwa kazi mpya Mkuu " Machera akajibu na kutia udambwi udambwi wa kumkoga mheshimiwa.
"Ah kijana wangu, uko wapi ndugu yangu, una habari huyu nduli analazimisha kutawala nchi hii kwa remote kutokea huko Marekani? Kijana, nchi inakuhitaji haraka iwezekanavyo. Fanya haraka uje tujue tunadili vipi na huyu adui ambaye sasa anaitangaza nchi kifedhuli, na kujaribu kuwachochea wananchi dhidi ya serikali yao. Ni kama amedhamiria sasa nchi iwe anarchy(isitawalike) na nikiwa kiongozi wa taifa hili siko tayari kuona mpuuzi mmoja anaigeuza Tanzania kama Rwanda ya 94" Mheshimiwa raisi akafunguka. Kwa Kila hali, Machera alihitaji kuondoka kurejea jijini kwa ajili ya kuona namna ya kulinasua taifa dhidi ya Mabruki The Don.
"Naam Mkuu, naelewa hali ilivyo, ni kweli tunahitaji kukaa tufanye maamuzi ya kujinasua kwenye makucha yake. Nitajitahidi ndani ya wiki hii niwe nimerejea jijini!" Machera akajieleza.
"Sio wiki kijana wangu, ninakuhitaji kwenye kikao kesho. Tumeshafanya mpango ambapo utasafiri kwa ndege ya kukodi ya shirika la Mogambi Empire hivi navyoongea ndege hiyo ipo njiani kuja huko na tunatarajia kwamba itaondoka huko SAA 11 alfajiri kurejea huku, ili ushiriki kikao kitakachofanyika SAA tatu asubuhi." Mkuu wa nchi alitoa agizo. Naam, pendekezo la mkubwa kawaida ni amri.
Hii ilikuwa taarifa ya ghafula, lakini ilitoka moja kwa moja kwa Mkuu wa nchi, asingeweza kukataa. Nchi ilimhitaji.


Itaendelea
 
II

CHIRUNDUMUSI na genge lake lililomtii mheshimiwa Mabruki The Don, walikuwa mkoani Mara wakimfuatilia Machera. Agizo la The Don, lilikuwa wazi na kamilifu.

"Hatakiwi kutoweka machoni penu, Huyo ndiye tegemeo lao, Bila Huyo hawafanyi chochote."

Ndivyo alivyoagiza. Machera alizungukwa na kundi la adui na hakuwa na habari. Kilichokuwa bayana kwake ni kile kitisho cha Mabruki. Hivyo alijua wazi kuwa Don lazima atakuwa anamuwinda kama alivyomweleza. Alipaswa kuchukua tahadhari Kubwa. Wazo hilo likamfikia kama uvuvio. Naam uvuvio juu ya kuchukua tahadhari.

Waliondoka Mesani ili kurejea nyumbani, alijijengea nyumba ya kisasa kijijini, humo akaweka mitambo ya kisasa ya ulinzi zikiwemo camera ndogo sana za ulinzi, ambazo isingekuwa rahisi mtu asiye jasusi mbobezi kugundua. Pongezi kwa serikali ya jamhuri iliyowezesha kufika kwa umeme vijijini. Mitambo hiyo licha ya kuunganishwa na komputa zilizofichwa kwenye Chumba maalum chini ya jengo lake ambamo pia alitunza silaha nzito na zile za hatari kabisa zikibeba teknolojia za kisasa duniani, picha za video hizo zilirushwa moja kwa moja kwenye simu janja yake.

Ni wakati alipomaliza kuzungumza na raisi, ndipo aliposikia mlio wa Simu aliotega kumpa taarifa pale ambapo jambo lisilo la kawaida lingetokea kwenye nyumba yake.

Alipobonyeza kialama fulani kwenye Simu yake, Machera aliweza kushuhudia bayana kilichokuwa kinaendelea, video iliyokuwa mubashara ikawaonesha vijana wa kazi, vijana wa Don wakiwa kwenye harakati za kufungua mlango waingie ndani. Akajua kazi imeanza, kumekucha. Akatoa tabasamu na kumuonesha Anastazia kile kilichomfurahisha.

"Shit, na hii inakufurahisha kwa lipi? Hivo wewe mwanaume unafurahia hatari?" Anastazia akahoji.

"Ana buana, wewe huoni nachokiona hapa? Hawa mbuzi wameturahisishia kazi. Hapa wakishazama ndani tu, kinachofuata ni usingizi mzito. Nachotakiwa kufanya ni kubonyeza bonyeza namba fulani kwenye Simu yangu hapa. Baada ya Hapo milango ile itajifunga na kuna hewa itaruhusiwa kuenea mle ndani, na kwa jinsi pua zao zilivyo pana, basi wakishaivuta tu, watalala usingizi mzito, na Sisi tutawakuta na kuhakikisha tunadili nao ipasavyo. Imekuwa Heri kwa sababu vinginevyo tusingejua, na huenda wangetufuatilia hata kukwamisha safari ya kesho alfajiri.

"Mh na kweli aisee! Nilihisi tambo za Don ni kwa vile ana watu wake mkiani mwetu. Unaona, huna haja ya kuwa na wasiwasi naye, na hapa umemtia adabu mpenzi. Akijua wambeya wake wamedhibitiwa basi mambo yake yatakuwa yamedoro!" Ana akaeleza, akionekana kusisimka haswa na huo mtego aliouandaa Machera.

Kama walidhani ingekuwa rahisi, basi walipaswa kudhani kwa upya. Wakati vijana wa Don wakizama kwenye jengo la Machera, Chirundumusi yule kibaraka wa Don alikuwa na mpango wa ziada kibindoni. Hakutaka kutia mayai yote kwenye kapu moja! Kwa hiyo aligawa kikosi chake katika makundi mawili. Moja likizama mjengoni na la pili likizunguka nje ya mjengo ule kwa tahadhari. Ikiwa tahadhari Kubwa zaidi kwa kuzingatia mtu waliyekuwa wanamkabili. Walivalia nguo za Jeshi, Jeshi la wananchi. Hicho ndicho kilikuwa kigezo cha wao kuhisi wangekuwa chambo mahsusi ya kumpumbaza Machera. Taarifa za kunaswa kwa mawasiliano kati ya mheshimiwa Rais na Machera ambazo walipewa muda si mrefu ziliwathibitishia kuwa Machera alikuwa amepata kitisho kuwa anafuatiliwa na hivyo huenda angehitaji usaidizi.

Mwendo wa dakika kadhaa baada ya Simu ya raisi, Simu ya Machera iliita. Safari hii hofu alimudu kuizika mbali. Namba ngeni ilicheza kwenye kioo cha Simu yake. Aliipokea na kuiweka kwenye sikio lake la kushoto tayari kupokea Ujumbe.

“Hallow Mkuu, unazungumza na Kamanda Chole wa kikosi kazi Tarime. Tumepokea Ujumbe kutoka ikulu kutuelekeza kufika Mesani kwa ajili ya kuongeza nguvu, Simu hii ni kukujulisha kuwa tayari vijana wetu wapo njiani na wametujulisha kuwa ndani ya robo SAA watakuwa wamewasili huko." Ilikuwa sauti ya kamanda Sosthenes Chole, alimfahamu vema na ingawa sauti yake Leo ilisikika kama yenye mafua yanayoanza hivi, ilikuwa ni sauti yake. Uzuri pia alikuwa na namba yake kwenye shajara yake na ili kujiridhisha, alirejelea alipoaiandika na kuilinganisha na kukiri ni yenyewe.

Dakika kumi mbele tayari Machera na Anastazia walikuwa wanakatiza makutano ya Barabara, moja ikielekea Mesani ilipokuwa nyumba yake na ile iliyonyoosha moja kwa moja kuelekea nchi Jirani ya Kenya.

Alipokuwa anakunja kona kulia kwake ili kuifuata njia yalipo makazi yake, akashituka kumuona mtu mwenye silaha nzito aina ya AK47, alitarajia usaidizi lakini hakudhani ingekuwa mapema kiasi kile, na hata hivyo, askari yule hakufanania kabisa uaskari. Machera alishuhudia tatuu ya nge kwenye shingo yake. Akajipata anapata mashaka, hivyo badala ya kukatiza akanyoosha mbele.

"Vipi, umekusahau nyumbani mpenzi?!" Anastazia akahoji.

"Kumekucha Ana, Don yupo kwenye harakati. Kuna watu zaidi ya wale walioingia ndani, wale walioingia ndani wako na hawa au ni kundi tofauti. Shida ni moja, hawa wa nje wamevaa magwanda ya Jeshi la wananchi. Mmoja kati yao, amenifanya kidogo nishituke, hakuna mwanajeshi anayevaa gwanda anayeruhusiwa kuchora tattoo mwilini na kufuga dreads, niliyemuona anavyo vyote" Machera alieleza huku akiliongoza Gari mbele kabisa.

Alipojihakikishia kuwa walau ni salama, aliipaki Gari yake Toyota Pickup Double Cabin. Alichukua silaha zake muhimu na kuziweka kwenye pensi lake lenye mifuko mingi, halafu akamweleza Anastazia kuwa yeye asubiri wakati alipokuwa anaenda kucheki kama wale walikuwa ni adui au makamanda alioomba waje kijijini kufuatia kile kitisho cha The Don. Haikuwa rahisi kumtuliza Anastazia ndani ya Gari ikiwa yeye pia alitaka kuingia kwenye Uwanja wa vita, lakini kwa kutumia juhudi nyingi alifanikiwa kumtuliza.

Machera kwa tahadhari Kubwa aliondoka kwenye maficho ya Gari lake na kwa mwendo wa kimya, akarejea kulipokuwa nyumba yake akihakikisha haachi dalili yoyote ya kushitukiwa. Aliitazama Saa yake ya mkononi nayo ikamlaki kwa kumtaarifu kuwa ilikuwa yapata SAA moja kasoro dakika kumi na mbili hivi za jioni. Kigiza kilishaanza kuivamia nchi na sasa kulionekana tu wekundu fulani uliochanganyikana kidogo na njano, ukiishilia kwenye vilima vya magharibi kulikojulikana kwa jina la wenyeji 'nguku'.. Kwa mwendo wa haraka usioacha kishindo, Machera alifanikiwa kumfikia mmoja kati ya wale wanajeshi huku kijigiza kile kikimuongezea kujiamini kwani askari wale hawakuweza kumbaini.

Vizia yake ikamwezesha kumtia kabali ya maana askari yule na kumdhibiti vilivyo.

"Ukifanya fujo nakuchinja kama kuku, tulia hivyo hivyo na unipe majibu ya maswali yangu bila ujanja." Aliongea kwa sauti ya chini, sauti iliyosikika barabara kwenye masikio ya mtu yule. Jamaa akawa yupo kimya akisikilizia. Jisu lenye makali pande zote likiwa kwenye mikono thabiti ya Machera likiilamba lamba shingo yake kwa uchu!

"Nyie ni Nani na hapa mnafanya nini?" Jamaa lile lenye misuli ilotuna likajaribu kutoa sauti ikashindikana. Likawa linagugumia kwa mtetemo!

Machera akagundua sauti haikutoka kwa kuwa kabali yake ililibana vilivyo koo yake. Akafanya kuilegeza kiasi ili kumruhusu mtu yule kutoa sauti. Hilo likawa kosa, kwani sauti iliyotolewa ilikuwa ni ile ambayo haikutarajiwa. Sauti iliyolenga kutoa tahadhari kwa wengine. Lilipiga kelele ya kuwajulisha wengine kuhusu kuwepo kwa Machera pale. Liliitoa sauti ile likijua kuwa kwa kufanya hivyo lilikuwa linakata tiketi ya kwenda ahera.

Machera hakukawiza, aliruhusu kisu kile kuzama taratibu kwenye koromeo la adui huku akitumia mwili wa jamaa lile kujikinga risasi zilizomiminwa uelekeo wake, kuonesha kuwa watu wale hawakuwa na cha mswalie mtume wala nini, ilionekana kwamba Kila mwenzao ambaye angeonekana kutumika kama chambo walikuwa na amri ya kumshambulia kwanza, halafu adui akiwa peupe basi alipaswa kufutiliwa mbali.

Machera alilishitukia hilo mapema. Baada ya kukwepa risasi kadhaa, ambazo nyingi ziliishia kuzama kwenye maiti ya yule muuaji wa kutumwa na Don, alimudu kusepa kwenye kijigiza na hapo akachomoa miwani zake maalumu, ambazo hasa ziliundwa kutumika kwenye Giza Nene na hata kutazamia kilichoendelea ndani ya kuta Nene za nyumba. Kilichofanya miwani zile kuwa na ufanisi wa kiwango cha juu sana ni ule uwezekano wake wa kuona mjongeo wowote ule wa kiumbe hai.

Mara baada ya kuivaa miwani ile, Machera aliweza kuwaona adui zake kwa uzuri wakati wakihaha kumsaka,na hiyo ikampa fursa ya kuwatungua mmoja baada ya mwingine. Kitu ambacho hakujua ni kwamba kiongozi wa lile genge Chirundumusi wa Mzindakaya naye alikuwa na miwani ya aina ile, hivyo alichukua tahadhari kwa kujiweka mbali na kutafuta shabaha kwa lengo la kumtumbua kwa kutumia bunduki ya kudungulia aina ya rifle.

Ni katika harakati za kuitafuta shabaha ya kumdungua Machera ndipo Chirundumusi alipobaini kuwa zaidi ya visu alivyokuwa navyo mifukoni, Machera alikuwa ameteketeza karibia askari wake wote na kuishiwa kabisa risasi. Hapo, Chirundumusi akajikuta anapata hamu, hamu ya kutumia ukomandoo wake. Alitaka kumuonesha utabe wake. Chirundumusi akijawa na kiburi cha kuonyesha ubabe akajitokeza hadharani huku akiita jina la Machera kwa kukosea,

"Mashera Mashera ! Nimesikia sifa zako kem kem, Leo nimejionea! Umeteketeza askari wangu wote, lakini Mashera bila silaha za moto huna unachoweza! Nataka nione uwezo wako, kama kweli wewe si ‘mama’ fulani hivi unayemudu mchezo kwa silaha tu, nionyeshe umwamba wako kama waweza kutumia mkono." Chirundumusi alibweka akijitapa kifua mbele. Akapiga hatua kumfuata Machera akizitupia silaha zake mbali.

Muda si muda alimfikia Machera na kumvaa kwa nguvu, lilikuwa kosa Kubwa kwa upande wa Machera, alisikia ubaridi ukipenya kwenye ngozi yake na baadae kushuhudia damu zikiruka kwa fujo na kulowesha fulana yake. Kisu cha Chirundumusi wa Mzindakaya kilipenya kwenye tumbo lake upande wa kuume na kuuchana mithili ya mkasi wa Fundi nguo kwenye kukata kitambaa! Maumivu makali yakapasua kijisehemu fulani hivi kwenye moyo wake kihisia, hii inaitwa coordination kwa wanabayolojia! Mara akasikia mlio wa risasi vuup! Machera akaanguka chini kama mzigo.

Alipozinduka, Machera alikuwa kwenye ndege angani, pembeni yake mwanamke mrembo mithili ya malaika akimtolea tabasamu murua huku sauti ikisikika ikimkaribisha

"Oh, karibu tena duniani, ulikuwa umeishia huko kwa muda sasa!" Ilikuwa sauti ya Anastazia. Sasa aliweza kurejewa na kumbukumbu zake sawia. Alisikia risasi ikiunguruma 'vuup' na kumpeleka chini! Hicho Ndo kitu alichokisikia Mara ya mwisho.

"Niko wapi, hapa ni mbinguni?" Machera akauliza.

"Hapa ni mbinguni kama mawinguni ndio mbinguni. Uko kwenye ndege kuwahi kikao na mheshimiwa rais. Oh mpenzi! Asante sana kwa kurudi, nikajua nimekupoteza." Ana alitamka huku akimbusu shavuni.

"Kulitokea nini mpenzi? Nimeponaje ile risasi iliyovuma sikioni mwangu vuup!?" Wasiwasi ulisomeka dhahiri.

Ikabidi ana kumsimuliamkasa uliotokea Jana ya siku hiyo.


***

Nilibaki kwenye Gari kama ulivyoniagiza. Lakini moyo wangu haukunirihusu kuendelea kuketi, kwa hiyo nililazimika kukaidi agizo lako! Niishuka kwenye Gari na kuanza kunyata kurudi nyumbani. Mdogo mdogo! Wakati napokaribia getini ndio nikamuona yule mjinga akijisogeza huku akitamba kwa mbwembwe, Mara akaanza kutupa silaha. Wakati nasubiri kuona pambano la kufa mtu, si Ndo nikaona damu zikivuja na kulowesha Shati lako. Hapo Hapo nikanusa Mauti na hatari. Nikasema noo! Huku risasi ikikohoa kumwelekea adui kutoka kwenye bastola yangu thabiti. Nikaona mnaanguka wote. Haraka sana nikakuwahi na kuanza kukuongelesha kujua u hali gani, mwanaume hukujibu. Mapigo yakaanza kupwita kwa kasi ya hatari. Nilijua nimekupoteza. Lakini Heri ikawa kwangu, nilipopima mapigo yako ya moyo kwa mgongo wa kiganja changu ndio nikang'amua kuwa u Mzima. Nikakubeba haraka nikupeleke kwenye huduma ya kwanza, hata sasa siamini kama nilimudu kukubeba kwa uzito huo. Kama ulivyosema, nilipofungua mlango tu nikaona watu wenye usingizi mzito wakiwa wamelala kihasarahasara, ndipo nikakumbuka ulichosema. Dawa ile ingeweza kupenya kwenye pua yoyote iliyo wazi. Sikuvunga, haraka sana nikakuburuta huku nikifunika pua zangu kwa kiganja. Hilo lilikuwa kosa, kumbe kuna njemba ilikuwa imeona upenyo na haikutaka kulaza damu, kwa kasi kama kimbunga alinipita, nilijua kapita mtu baada ya kugeuka haraka na kumuona akipotelea getini, ingawa kusema kweli ni kama ulipita mvumo mkali wa upepo!

Nilichomoa kifaa cha oksijeni kwenye backpack yako nikakivaa huku nikikuvalisha chako. Baada ya Hapo ndio nikazama ndani huku ukiwa nusu kaputi mgongoni kwangu. Kitu cha kwanza nilichofanya ilikuwa kuwafunga wale mbuzi kwa kamba za kudu na kuwaongezea dozi ya usingizi. Nikiwa kwenye harakati hizo Simu yako iliita, nilipocheki kwenye kioo chake, ilikuwa ni Simu ya mheshimiwa rais na Bila kusita nikaipokea.

"Kijana wangu nimepata habari si njema sana. Watu wa Don wamemteka kamanda Chole na kutokomea kusikojulikana...."Alizungumza rais na Mimi sikutaka kumwacha aendelee kwa kuhofia kwamba asingejisikia vizuri kufunguka mambo yake kwangu kwa kunidhania ni wewe, badala yake nilijikohoza halafu nikamkatisha kwa kumjulisha kuwa, aliyekuwa anazungumza naye ni Mimi.

"Samahani mheshimiwa, Machera yuko kwenye hali ambayo hawezi kuzungumza kwa sasa na ndio sababu nimepokea Mimi Simu yake." Mheshimiwa kusikia hivyo akahamaki na kutaka kujua kulikoni.

"Kumetokea nini binti, amepatwa na kitu gani?, yuko katika hali gani sasa? Amepata msaada gani kufikia sasa?" Aliyafululiza maswali yake akionekana kuwa na wahka wa hali ya juu. Kusema kweli nilishindwa nijibu Swali gani kwa wakati huo. Akili yangu iliniambia kitu cha kufanya kwa wakati ule ingekuwa kumuondolea wasiwasi wake kwanza.

"Yupo salama Mkuu, anachohitaji ni huduma ya kwanza tu kwani amepoteza damu nyingi sana!" Hiyo ndio kauli niliyoona vema kumweleza. Hapo tena, mheshimiwa alinitaka nimweleze kilichotokea na ndipo nikamsumulia kuanzia kupokea Simu ya kamanda Chole hadi kuwashitukia wale nyang'au na pale nilipokuta ukivuja damu kama bomba la maji na kitendo cha kumuondoa uhai Chirundumusi ambacho nilijikuta nimefanya Bila kuwaza Mara mbili. Mheshimiwa kidogo akaipata amani yake, alipata amani na nilijua kutokana na jinsi nilivyomsikia akipumua kwa nguvu kuonesha alikuwa anatua mzigo wa wasiwasi moyoni Mwake, ni Hapo alipoaniahidi kuwatuma hawa ndugu!

Nilipotua Simu chini niliingia ‘chumba cha upasuaji’ kwa kusudi la kukupatia huduma ya kwanza. Kwa usingizi uliolala sikuhitaji kukuongezea nusu kaputi, nilishona kidonda chako na kukitia dawa, halafu nikajaribu kukurejesha duniani bila mafanikio. Hivi napokuona unamudu kuniuliza maswali, kusema kweli najisikia raha sana. Maana isingefaa uniache hivi hivi hata ukweni hujanitambulisha!! Sasa uone umuhimu wa kunipeleka kwa wazazi.


***

Machera alimtazama mpenziwe akielezea habari za utambulisho akagundua hakukuwepo utani kwenye suala lile. Alilichomekea kiutani lakini akionesha Kila hali iliyomaanisha alihitaji kweli kutambulishwa. Alilizingatia moyoni, ingawa alijua huu usingekuwa muda mwafaka wa kumweleza kusudio lake la kumtambulisha kwa wazazi wake. Alishapanga kulifanya hili na hata wazazi wake tayari alikwishawamegea kiduchu habari yenyewe na walipotaka kujua sana aliwatuliza kama mpira wa kasi unavyotulizwa kifuani kwa mcheza kandanda mashuhuri.

"Umesema kamanda Chole yupo mikononi mwa adui?" Machera alidhamiria kupotezea habari ya utambulisho na hivyo akachomekea Swali hilo.

"Ndio, hata sasa haijulikani alipo."

"Kwa maana nyingine ina maana aliyetujulisha ujio wa makamanda hakuwa yeye?" Alidhamiria kujiuliza lakini tayari wazo lilikwisha kuwa kauli ya ulizo, na masikio sikivu ya Ana yalimsikia Barabara!

"Hilo nadhani atakapopatikana atatueleza bayana" Anastazia alitoa maoni yake.

"Mh Bila shaka".

Hata hivyo hilo halikumzuia kulifikiri tukio lile kwa kina. Isingewezekana kamanda azungumze naye muda aliozungumza na makamanda wale wafike mapema vile!, na kama kauli ya kamanda Chole ilikuwa sahihi ina maana watu wake wangechelewa kuwasili eneo la tukio, Swali likawa je ni kwa nini watu Hao hawakuja baadae?.

Ama kamanda Chole alikuwa upande wa adui au waliomteka walitumia hila kumlazimisha afanye walichotaka wao au sivyo, walitumia program mahsusi iliyoiga sauti ya kamanda Chole, kwa kutumia hiyo, wakafikisha Ujumbe wao. Hapo akakumbuka kuwa, hata alipowasiliana na kamanda kuna kitu fulani kilimjulisha kuwa kamanda alisikika kama mwenye mafua hivi na sauti yake ilionekana kukosa joto la uchangamfu.

'Bila shaka kulikuwa na namna' akazidi kuchanganua.

Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mabruki alikuwa amepoteza kete moja kwenye mchezo Huu.

ITAENDELEA
 
III

Las Vegas, USA

MABRUKI na wenzake wawili, kwenye casino maarufu la ‘Bellagio Hotel and Casino’ kwenye jimbo hilo maarufu kwa starehe Marekani, walikuwa na kikao nyeti. Agenda mezani ilikuwa ni juu ya uchaguzi Mkuu uliokuwa ufanyike Miaka miwili baadae nchini Tanzania. Wote wakiwa ni watu wenye fedha za kutosha na tamaa ya kupata nyingi zaidi, na hasa hiki kilichokuwa kinaendelea kati ya Jasusi la kimarekani Mike MacCulouch, Tajiri Wilbur Smith na The Don Mabruki.

"We would like to be assured of the people you employ in this endeavor Mr. Mabruki, the guys you tailed on that agent were useless, can you explain how one man single handedly terminated a troop of well trained assassins? If we have to sign an agreement to staffing our money into your campaign’s purse we gotta be sure it's worth an investment" (Tungependa kuhakikishiwa kwamba watu unaoajiri ni watu makini, watu gani ulioweka kumfuatilia yule jasusi mbobezi wa Tanzania hata wakateketea mikononi mwake kikosi kizima? Kama kuna ulazima wa kukumwagia mipesa kwa ajili ya kampeni yako, sharti tuwe na hakika kwamba pesa yetu inawekezwa ili baadae ituzalishie faida) alizungumza Wilbur Smith tajiri mkubwa na mwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini na gesi asilia kote duniani.

Huyu alikuwa na dhamira ya kuchota kama ilivyo kawaida ya mabepari kujichotea Mali za Africa, Wilbur Smith alikuwa amejikita zaidi huko Congo na utajiri wake kwa asilia 70 aliupatia huko! Harakati zake za kuuwinda utajiri wa madini uliosheheni Tanzania ulianza kitambo wakati wa utawala wa rais mstaafu lakini rais Huyo mzalendo alimdhibiti vilivyo, kwa sababu hiyo Smith alianza harakati za kumuundia zengwe na ili kukamilisha hilo akamuweka Don kibindoni, akamkaribisha kwenye usharika wao wa siri huku akimwezesha The Don kumiliki migodi kadhaa huko Congo, na hapa nchini Tanzania.

The Don, mwenyeji wa huko Urambo Tabora, aliyetokea kwenye familia duni na kusoma kwa msaada wa chama tawala kufuatia uwezo wake kitaaluma, na ushawishi mkubwa aliouonesha kiuongozi akiwa ni chipukizi aliyefanikiwa kuuza kadi za uanachama kwa vijana enzi za pale Tabora Boys shule ya upili, na hilo likamfurahisha mno Mkuu wa itikadi hata akashawishi chama kumfadhili kijana Huyo kwa elimu ya juu, pale ilipoonekana familia yake inasua sua kwenye ulipaji. Mabruki Ally, akasoma huku akishiriki kikamilifu kwenye siasa mashuleni na vyuoni, hivyo hàikushangaza pale alipojikuta akitwaa ubunge akiwa na miaka thelathini na mbili tu akitokea chuoni.

Mabruki maisha yake yakawa yanaenda kwa kufuata mkondo aliotengenezewa na chama tawala. Kwa tetesi za mitaani wengi waliamini Mabruki alikuwa mtu wa mfumo, miongoni mwa watu wa usalama. Miaka ilivyosonga, Mabruki nae alisonga, akijitengenezea Uwanja mpana wa marafiki ndani na nje ya mipaka. Sio tu marafiki, la hasha, yeyote aliyekuwa na mahusiano na Mabruki, basi alikuwa wa maslahi kwake. Maslahi yake binafsi na ya wale waliotengeneza urafiki naye, ndicho kigezo kikuu alichotumia kuwapata.

Masomo yake ya elimu ya juu aliyopatia Marekani yalimjenga kibepari hasaa! Akili yake iliwaza Mali, vitu, thamani, pesa! Mambo ya ubinafsi tupu!

The Don Hakuwa na utu hata kidogo! Mtu ambaye hakujali wazazi wake baada ya kupata ufadhili wa chama. Mtu ambaye licha ya kuwa na fedha nyingi, ndugu zake wa tumbo moja walikuwa mateja wa kutupa, wakifa kwa uraibu wa madawa ya kulevya, ambayo ilikuwa Biashara iliyomwingizia pato la kutosha The Don. Huyu, alifaa kuitwa dudu mla watu, ambaye alikuwa tayari kuteketeza umma wa Tanzania hata kama angebaki peke yake.

Huyo ndiye Mabruki The Don, tajiri mwenye migodi chungu nzima Congo na hapa nyumbani Tanzania.

"This will not repeat itself, that's why I have brought Agent MacCulough in this meeting, he has a great record with his missions. So I'd like to assure you Mr. Smith, that this man here will carry the assignment perfectly. Agent MacCulough please explain how you're planning to carry out this assignment" (Hili halitajirudia tena Mr Smith na ni kwa sababu hiyo nimekuja na jasusi MacCulough, huyu ana rekodi nzuri sana kwenye uga wa ujasusi. Nataka tu nikuondoe hofu, kwamba jasusi MacCulough hapa ni mtu sahihi kwa kazi iliyo mbele yetu. Tafadhali bwana MacCulough elezea mpango wako ili bwana Smith ajenge imani kwenye uwezo wako)The Don alizungumza huku akimtaka Agent MacCulough kuelezea mkakati wake! na halafu akamalizia,

"...and by the way Mr. Smith, this is the guy who carried the famous assassination of the chairman of the prominent AGC companies!" (....na kwa taarifa tu, Huyu ndo kichwa nyuma ya mauaji ya kitalaamu ya mwenyekiti wa makampuni maarufu huko Asia, AGC) The Don alimalizia.

"You mean to say that guy was assassinated?" (Unamaanisha kuwa yule jamaa aliuwawa?) Smith akaachama mdomo kwa sekunde dalili ya kupatwa na butwaa!

"I thought they said he was ailing from kidney failure?" (Mbona niliambiwa alikuwa anasumbuliwa na figo?) Smith sasa aliuliza akiwa na mashaka.

"Yes, that was the doctors report. The old fellow would not let the heirs know their positions when his retirement was due. So one brilliant son, Yasvaad Veedu had a plan in store for him, he forged the certificates and prepared a brilliant succession plan, making himself the sole heir to the chair and companies. It had to be staged as a normal death for the son to produce the will that his father had to sign on his deathbed." (Ni kweli, hiyo ilikuwa ripoti ya madaktari. Kibabu kile hakikuwa na mpango wowote wa kuachia madaraka wala mkakati wa kuandaa mrithi wa kuchukua uenyekiti wa makampuni, ndiyo maana bwana mdogo Yasvaad Veedu, yule kijana wake mkubwa akaamua kuandaa mpango wa kuichukua kampuni mikononi mwake. Hakukuwa na namna isipokuwa kumtengenezea ugonjwa na kufoji nyaraka za kurithishana mali kwa kutumia saini yake. Kibabu kilikuwa hakitaki kufa wala kilikuwa hakizeeki). MacCulough alichomekea sauti lake zito na kutazama kwake kulionesha ni mtu wa vitendo zaidi tena asiyejali utu isipokuwa pesa. Alizungumza hayo huku akimalizia kwa tabasamu baya kuliko yote dunia nzima. Baada ya Hapo Agent MacCulough akaeleza mpango wake juu ya Machera.

Meza yao ilitabasamu kwa vinywaji vya ghali vilivyowekwa kuwafurahisha matajiri wawili waliojua kutumia utajiri wao, watoto wazuri wenye asili ya kiafrika wakinengua maungo kuyafurahisha macho ya wazito hawa kufuatia muziki uliosikika kwa wastani kwenye maspika yanayochuja muziki ipasavyo. Hawa walijua kufanya Biashara yao, walitumia miili yao kama ma-toy ya kuchezewa na wanaume hawa wenye fedha zao, na wao wakatunukiwa ujira wao!


***

Mary Chalamira, maarufu kama MC 1, mtoto wa kichaga toka Mabogini, kwa muda wa miongo miwili alikuwa akiishi Marekani. Akiwa binti mrembo aliyebahatika kupata ufadhili wa elimu nchini Marekani akiwa na miaka 16 tu baada ya kupata ufadhili wa mzungu Steve Curl, aliyekuja nchini kutalii huko mlima Kilimanjaro. Ufadhili ukizingatia kuwa, alikuwa mtoto pekee aliyebaki hai baada ya wazazi wake na ndugu zake kufa maji kwenye ajali ya kuzama meli maarufu ikijulikana kama MV Bukoba katika ziwa Victoria mwaka 1996. Sasa alijulikana kama Mwajiriwa kwa muda wa ziada kwenye Casino Bellagio, kama mcheza mziki anayesaula nguo kwa kulipwa. Mtoto wa kichaga aliyejaliwa umbo la kiafrika haswaa na sura yenye mvuto wa sumaku. Alipojigeuza na kujipindua kwenye nguzo ya chuma kinachong'aa na kuteleza kwenye jukwaa, basi ilihitaji uzoefu kumtuliza shetani wa mahaba kuamsha jogoo lenye uchu kwa mwanaume rijali. Si ajabu kuwa waliomuona akifanya vituko vyake jukwaani kwa mara ya kwanza waliishia kubadili suruali zao baadae. Maisha yake yalikuwa na sura mbili, sura ya msaulaji maarufu akitembelea makasino mengi yaliyoupa jina Kubwa jiji la Las Vegas, upande wa pili huyu alikuwa jasusi la kujitegemea. Jasusi lililojitengenezea jina Kubwa kote duniani, Queen of the Mountains!

Leo alikuwa Bellagio hotel and Casino kwa kazi maalum, kupata taarifa kuhusu kikao cha The Don na tajiri Wilbur Smith! Kazi ambayo aliianza mapema mara tu baada ya taarifa za kukimbia mkono wa sheria nchini Tanzania kusambaa mitandaoni kote duniani, kwa mwana siasa maarufu, Mabruki. Kwa hiyo ilikuwa kwamba, aliwapa burudani ya kufurahia ubinukaji wa makalio yake, huku akiwa keshatega vinasa sauti vyake na kurekodi mazungumzo yote yaliyofanyika kati ya wale watu watatu.


***


JNIA, Dar es Salaam

Saa 3 asubuhi.


Ndege ya kukodiwa ya shirika la Mogambi empire ilitua uwanja wa ndege wa kimataifa, Julius Nyerere, ikiwa na abiria watano. Daktari, Rubani, Anastazia, Afande Bwire na Machera mwenyewe!

Waliposhuka tu, magari matano yalikuwa kwenye mwendo wa utayari, ulinzi wa kikosi cha PSU ukitamalaki Kila kona. Ving'ora vikitoa sauti ya tahadhari ili kufungua njia. Katika mapokezi haya kulikuwa na Gari la mheshimiwa Mkuu wa mkoa, na maajenti wa PSU. Moja kwa moja msafara ule ukaanza safari ya kuelekea ikulu, Magogoni.

Hadi kuingia jijini Dar, tayari Machera alikuwa na ahueni ya kutosha na alimudu kuketi na kuzungumza vema na wenzake.

"Inavyoonesha The Don hataki kupumzika hadi pale atakapokuwa ameivuruga nchi hii vipande vipande." Daktari Muddy Bonge alizungumza.

"Kabisa, sasa hivi anajaribu kuua ndege wawili kwa jiwe moja, huku kuna vikosi vinawinda maajenti watiifu kwa nchi, kule nje anajionesha kama mtu anayeonewa na nchi yake licha ya kuwa na wafuasi wengi wanaomkubali hapa nchini" Afande Bwire alichangia

"Kinachonishangaza ni namna ambavyo wabongo tunadanyika kwa wepesi, Kila kitu kinaonesha uovu wa Mabruki lakini wanathubutu kukana na hata kuandamana mitaani. Unajua hainiingii akilini, ni kama vile watanzania wote walishalishwa unga wa ndele aisee!" Daktari Muddy Bonge akaendelea kueleza. Kauli yake hiyo ikiibua kicheko kilichomtoa machozi Anastazia. Kila mmoja akalazimika kumtazama mwanamke Huyo kwa alama ya ulizo.

"Vipi bibie, kulikoni kicheko kama chote?" Ilikuwa zamu ya Machera kuongea, na wale wengine wakionesha hamu ya kutaka kujua kile kicheko kiliamshwa na kitu gani.

"Oh jamani, mnavyoniangalia sasa hadi najisikia aibu mjuwe!. Kilichonichekesha ni hili neno alilotumia Daktari Muddy Bonge. Kusema kweli amenikumbusha enzi zile za shule, nakumbuka ni kitabu fulani cha fasihi nilichopata kusoma hayo maneno 'unga wa ndele', sasa hasa kilichonichekesha ni ile kumbukumbu jinsi mwalimu Ndekete alivyokuwa akilitamka kiasi kwamba akawa haitwi tena Ndekete Bali 'wa ndele'." Anastazia alijitetea huku akijifuta tumachozi kwenye pembe za tumacho twake tukubwa mithili ya ka-mwanasesere ka kizungu.

Mazungumzo yao yaliendelea kunoga, tabasamu na vicheko vikipamba sura zao kwa Furaha hadi pale kiliposikika kishindo na kelele za msuguano wa tairi na lami.

Katika makutano ya Barabara ya Nelson Mandela na Julius K Nyerere kulikuwa na kizungumkuti, kilichoonekana kama ajali mbaya kikaibua mazito, moja ya Lorry la kampuni ya tajiri maarufu nchini, Yale yanayosafirisha bidhaa nje ya jiji la Dar Ee salaam, lilikuwa limepiga mzinga na kuziba Barabara yote.

Ajabu ni kwamba msafara ule ambao usalama wake ulizingatia kuwepo kwa maafisa usalama kwenye Barabara iliyotakiwa kupita, hadi unafika eneo hili la ajali kulikuwa hakujatolewa taarifa yoyote iliyohusu kuwepo kwa ajali, ambayo ingewawezesha kutumia Barabara nyingine. Maafisa usalama eneo hilo walikuwa kimya.

Hicho ndicho kilichomsitua Machera, pale Gari lao liliposhika breki za ghafula ambazo hata hivyo hazikusaidia, kwa sababu, Gari la nyuma yao pamoja na dereva kusimamia breki, bado liligonga Gari lao kwa nyuma na kusababisha waondoke barabani na kujigonga kwenye Bikoni za pembezoni mwa Barabara. Hilo likapelekea magari karibia yote kwenye msafara ule kujipata yamegonga au kugongwa na mengine.

Kwa kutumia utaalamu wao wa kiinteligensia Machera pamoja na maafisa wale wa PSU waling'amua Mara moja kuwa ile ilikuwa ni hujuma..

Tahadhari ikachukuliwa Mara moja. Gari la Machera likazingirwa na magari mengine ili kuweka kikwazo kwa silaha ya adui kulifikia Gari hilo. Hilo likawa kosa la kiufundi kwa sababu, kule kulizingira Gari lile kulimpa adui taarifa bayana ya lilipokuwa windo lake. Risasi zikarindima kwenye Gari husika. Ilikuwa bahati kwamba Gari lile lilikuwa na Vioo vya kuzuia kupenya kwa risasi.

Akili ya kuzaliwa ikamtuma Machera kuwashawishi waliokuwemo kwenye Gari, kushuka na kukaa pembeni pale upenyo ulipopatikana wakati maajenti wa PSU wakijibizana kwa risasi na kikosi cha maadui. Ile mtu wa mwisho anamalizia kuruka nje ya Gari, wingu la moshi likatanda angani huku moto mkubwa ukilipuka na kuyameza magari karibia yote eneo lile, ngoma za masikio yao zikipoteza uwezo kwa muda kufuatia sauti ya mlipuko wa kitu ambacho kilidhaniwa kuwa Bomu au kombora. Risasi zikiendelea kurindima na moshi mweusi mithili ya ule unaosimuliwa kwenye miongozo ya kidini kuwa utameza watenda maovu, ukiendelea kutanda juu ya anga la Dar Es salaam.

Ajenti Bwire, daktari na Anastazia walipochomoka kwenye Gari, kama vile timu moja, walimbeba mzobe mzobe mgonjwa wao na kutokomea uswahilini. Ilikuwa wazi lengo la adui lilikuwa kumuangamiza Machera, kwa hiyo wazo la maana kwao ilikuwa kutafuta usalama badala ya kupambana.

Walivuka mtaa wa kwanza, wakawa wameshika wa pili, wakiwa kwenye harakati za kuzama kwenye maficho katika jengo moja kukuu ambalo lilionesha Kila dalili ya kuwa maskani ya wahuni, mara wakakumbana na mitutu ya adui ikiwa tayari kumwaga bongo zao kwenye kona moja kwenye mtaa ule.

"Mikono juu!" Ilitoka sauti mzito Kali ya kiafande.

Hawakuwa na namna, mikono ilinyanyuliwa juu bila ubishi huku silaha zikitupwa mbali.

"Ah kudadeki!" Machera akajikuta ametamka.

Kilikuwa kitendo cha ghafula, mikono iliponyanyuliwa juu tu, wote wanne walijikuta mikononi mwa adui, walifanya kutupiwa kwenye Gari, Van lenye Vioo vya Giza na mapazia yakiongezea Giza mle walikotupiwa. Hadi wanafikishwa walikokusudiwa, walikuwa wamefungwa miguu na mikono, mavitambaa meusi yakiwa yamefunika macho yao.


***

Makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, Dar es salaam. Saa 4 asubuhi.


"Afande, kuna ajali Kubwa sana imetokea hapa kwenye makutano ya barabara ya Nyerere na barabara ya Mandela, Msafara wa Mkuu wa mkoa umevamiwa na watu wasiojulikana, na hivi napozungumza kuna majibizano ya risasi kati ya watu hao na walinzi wa Mkuu wa mkoa. Milipuko ya mabomu inasikika na kuna Kila dalili kuwa adui anashinda. Nashauri tupatiwe msaada wa Jeshi maana watu hawa wanatumia silaha Kubwa za kivita, over." Ilikuwa sauti ya Afande Macha ambaye alikuwa kwenye lindo katika benki ya watu wa Zanzibar iliyo Jirani na eneo yalipotokea mapambano na kufanikiwa kushuhudia kilichokuwa kinaendelea.

"Nimekusikia afande, ngoja nilifikishe kwa wakubwa, over!"

Kwa upande mwingine, kikosi cha PSU kilichokuwa kinaendelea na mapambano, kilikuwa kimepoteza idadi Kubwa ya wenzao hasa mlipuko ule mkubwa ulipotokea. Hapo ndio akili zao zilipobaini kuwa, lile lilikuwa si pambano la majambazi wa kawaida. Kile kilikuwa ni kikosi cha kijeshi. Stallone ambaye alikuwa kiongozi wa kikosi hicho cha PSU kwenye msafara ule, akalazimika kupiga Simu ya moja kwa moja kwa rais.

"Mkuu, hapa tumevamiwa na kinachoonekana kama kundi la wanajeshi kwa maana ya silaha nzito wanazotumia. Tunahitaji usaidizi wa Jeshi la wananchi." Stallone alimjulisha rais.

"Vipi, Machera yuko katika hali gani?" Lilikuwa Swali la ajabu kuulizwa, Stallone akajikuta anapatwa na hasira ghafula. Wako kikundi, wanashambuliwa na wengine wamekufa tayari, wanahitaji usaidizi na Mkuu wa nchi anachowaza ni mtu mmoja tu! Akajizuia kuropoka. Vinginevyo alikuwa amshushie tusi zito la nguoni. Akiwa anajiuliza amjibu vipi rais, Stallone akahisi kitu chenye ubaridi kinapenya kwenye kiwiko cha mkono wake. Simu ikadondoka huku sauti ya kuugulia maumivu ikitoka kinywani mwake.

"Arghh.. Shit," akajitupa chini haraka na kujongea kwenye mvungu wa Gari moja wapo. Stallone akavua shati lake, na singlend, akatazama kulikopenya risasi, jeraha Kubwa likivuja damu, risasi ilipenya na kupitiliza huku ikiacha Bonge la jeraha ilikotokea. Stallone aliitumia singlet yake kwa kutumia mkono wa kulia ambao haukupata madhara na meno yake yakitumika kama sapoti wakati akizungusha Nguo hiyo kuzunguka jeraha kwa lengo la kuzuia damu kuendelea kumwagika. Alipomaliza zoezi hilo, akachomoa tembe mbili za panadol kwenye waleti yake kwa tahadhari sana, asijitoneshe kidonda, akazitupia mdomoni. Kwa Kila hali, timu yake ilikuwa kwenye ukingo wa kushindwa. Aliivuta Simu yake kwa kutumia mguu wake na kuandika namba za Simu halafu akaiweka Simu sikioni akiwa amekaa bwete, miguu kainyoosha na mgongo akiuegemeza kwenye Gari. Alionekana kuchoka kabisa. Simu iliita kwa sekunde kadhaa kabla ya upande wa pili kuipokea.

"Tumepata habari Tuko maeneo ya Jirani." Ilitamka sauti toka upande wa pili wa Simu. Stallone hakuongea kitu, akaikata Simu na kujilaza kifudifudi kwa mbali akisikia maumivu yakipungua, panadol zake zikifanya kazi ziliyokusudiwa.


***

Ikulu ilikuwa haikaliki. Rais Masebo alionekana kutembea huku na huku akili yake ikiwa kwenye Simu, alikuwa anazunguka huku akitegea sikio lake kwa umakini mkubwa kama angeweza kusikia mlio wa Simu yake, apate taarifa nini kilikuwa kinaendelea. Hofu ya kupinduliwa ikiwa bayana. Alijikuta anapoteza imani na watu wake wa karibu, akakumbuka kikichotokea kwa mtangulizi wake, mawaziri aliowaamini walivyomgeuka kirahisi na kukaa upande wa adui, je hawa mawaziri alioteua na wengine kuwarithi walikuwa na utii wa kutosha kwake? Hilo Jeshi lililopambana na walinzi wake walikuwa wameasi au lilikuwa genge tu la Mabruki lililopewa silaha za kivita? Kijana pekee aliyemwamini kwenye harakati za kiinteligensia Machera alikuwa wapi na akifanya nini?

Maswali yakawa yanakuja tu bila majibu kupatikana. Ni Hapo ndipo alipotambua kuwa, muda wote huo alikuwa anasubiri Simu ya Machera! Naam, alisubiri Simu ya Machera impe walau imani kiasi cha mbegu ya haradali ya kwamba mipango ilikuwa inafanywa ili kudhibiti hali. Washauri wake wa mambo ya kiinteligensia walikuwa wanampa wakati mgumu na nadharia zao ambazo hata hivyo, hakuzielewa.

Mara Simu ikaita, Mzee wa watu kidogo aanguke baada ya kujikuta mguu wa kulia unalazimisha kuutangulia wa kushoto ambao nao haukutaka hilo litokee. Mhamaniko wa hisia na hofu kwa wakati mmoja. Alipoifikia Simu, tayari alikuwa anahema kama mtu aliokimbizwa na hayawani.

"Ndio!" Rais akatoa sauti ikiwa imejawa wahka wa kutosha.

"Mheshimiwa kuna Simu yako huku ofisini, anayehitaji kuongea na wewe amekataa kujitambulisha lakini Simu yenyewe inapigwa kutokea Marekani." Ilikuwa Simu ya katibu muhtasi wake Manka. Habari hiyo ikazidi kumchanganya Masebo. Loh! Masebo alihaha kweli kweli,

'Nani Huyo asiyetaka kujitambulisha tena? Marekani?? Hataa! Au ni Mabruki?! Maswali yakazidi kumchanganya.

"Mheshimiwa rais..." Sauti ya Manka ikamzindua kutoka kwenye bahari ya mawazo!

"Iunganishe" akakoroma!

"Sawa Mkuu" Manka akajibu na kufanya alichoagizwa!

"Naam" mheshimiwa Masebo akatamka baada ya kupokea Simu ile kutoka Marekani.

"Tafadhali zungumza na mheshimiwa" sauti ya kike nyororo ikatamka kwa lugha ya kimombo.

Mheshimiwa rais akavuta makini. Akisikilizia sauti ambayo ingesikika. Kama vile alitambua hilo, mpigaji Huyo aliyetakiwa kuzungumza akapisha kimya kiasi, akisikilizia kuhema kwa mheshimiwa Masebo kulikomjulisha kuwa mheshimiwa huyo alikuwa na wasiwasi wa haja, Hapo akajiridhisha kuwa kazi yake itakuwa nyepesi. Akajikohosha na kuongea.

"Ah binamu, yaani hata wewe wa kuniwinda Mimi ndugu yako? Kipi hasa nilichokukosea wewe ndugu yangu hata kunitumia watu wanisweke lupango?" Ilikuwa sauti ambayo Masebo aliitambua vema. Sauti ya Mabruki, binamu yake hayawani. Hakutaka kujibu. Alijipatia dakika ya kujituliza moyo. Halafu akarekebisha koo kwa kunywa funda moja la maji kutoka kwenye chupa.

"Mabruki Ally, my cousin. Habari yako ndugu yangu." Rais Masebo akatamka kwa kujiamini. Hili silo alilotarajia Mabruki. Hii salamu yeye aliitafsiri kama kejeli tu hasa pale Masebo alipoongezea;

"Kitambo sana kaka hatujawasiliana, ajabu unapoamua kunipigia unalalamika bila hata salamu, sio Mimi niliyekukimbiza nchini, na hata kama unacholilia ni uwaziri nimeona si busara kukuteua ukiwa ughaibuni ukitumia nguvu nyingi kuichafua serikali yangu. Najua unapenda vyeo, lakini kwa tabia yako mbaya, sikuteui asilani!" Hapo Masebo akakata Simu. Alijua hiyo ni nini anafanya. Alikuwa anampampu ajawe upepo aropoke mipango yake. Naam, kama alivyotarajia ndivyo ilivyokuwa, Simu ilianza kuita upya. Akaiacha iite na kukata. Akaisubiri ipigwe tena. Ikapigwa tena. Akaipokea,

"Naam"

"Hujui kosa unalofanya we mjinga" sauti ya Mabruki ilijawa hasira. Ilikuwa zamu yake kuhema.

"Oh, ndugu yangu Mabruki umerudi tena? Unajua wewe ni ndugu yangu Simu yako ni ya muhimu kwangu, ila ifike sehemu, utambuwe kuwa nikiwa kama rais wa nchi kubwa kama Tanzania ni mtu ambaye niko bize sana, hivyo Simu yako isipopokelewa kwa muda inakufaa kuwa mpole na kuvumilia hadi itakapopokelewa. Ulikuwa wasemaji binamu?" Masebo aliongea kwa sauti tulivu yenye mamlaka. Mabruki akajihisi amekosewa sana.

"Nitakukomesha mjinga wewe, nitakung'oa kwenye hicho kiti kinachokutia kiburi. Utaona"

"Lawama za nini kaka?, una shida gani kwani?, eleza Mimi ni rais wa Jamhuri ninao uwezo wa kukusaidia! Kama ambavyo Nilikuwa nakusaidia enzi zile za Urambo. Juzi hata hivyo, nimetuma belo la mitumba kwa wazazi wako kijijini, maana ishakuwa aibu, utadhani wazee wale hawana kijana buana, ukirudi nchini pita ikulu nikuwezeshe kuwaona wazee wako ukiwa na walau elfu ishirini mkononi. Mikono mitupu hailambwi ati."

Hii ilikuwa kashfa, kashfa Kubwa kabisa. Mabruki tajiri mwenye kumiliki migodi, viwanda na mahoteli ya nyota tano kwenye mataifa kadhaa ulaya, leo hii anaambiwa apitie elfu ishirini ili kuwapelekea wazazi wake? Dharau gani hiyo? Ilikuwa dharau ambayo ilimchoma kweli moyoni. Dharau iliyoibua kitu kipya moyoni mwake. Kitu ambacho Mabruki alikuwa amekizika ndani kabisa ya mtima wake, kitu ambacho hawakukielewa wengine isipokuwa yeye tu na Hao wazazi wake.

Mabruki akajipata anatoa tusi zito la nguoni na kukata Simu.


ITAENDELEA
 
IV


MWANZONI waliishi karibu na reli ya kati pembezoni kidogo mwa mji wa Urambo, yeye na mama yake, baadae lakini, baba yake mwenye asili ya kiarabu aliwatafutia nyumba maeneo ya Airport na kuwapangishia Hapo. Hapo tena wakaishi kwa kubangaiza bangaiza kwani baba yake mzazi hakuonekana baada ya miezi kadhaa! Ilikuja kujulikana kuwa, mwarabu yule wa kutokea Oman alikuwa kaozeshwa mwanamke mwingine huko huko Oman, binti aliyetokea kwenye familia bora na hivyo akalazimika kubaki Oman kuendesha miradi ya mkewe aliyoachiwa urithi na babake. Hakurejea tena Urambo, na suala la mtoto wake Mabruki likiwekwa siri. Mabruki alikuwa na miaka mitano.

Alipofikia umri wa miaka nane, mama yake akaolewa na mwanaume mwingine. Ally Mustafa, mwenyeji wa Pemba kwa kuzaliwa ambaye alijikuta Urambo kwa Biashara ya duka la jumla. Huyu sasa akawa baba yake. Hata wenyeji ambao hawakujua kwamba baba yake si Mpemba, kwa ule mchanganyiko wa damu ya kiarabu ya baba yake na mama yake Husna binti Mabati mwenyeji wa Uyui huko huko Tabora, watu wengi waliamini kuwa mpemba yule, Ally Mustafa ndiye baba yake kwa vile wote walikuwa ni wenye ngozi za mchanganyiko wa kiarabu na kibantu isipokuwa mama yake mwenye ngozi ya maji ya kunde. Haikuwa kweli, lakini hata hivyo ni wao watatu tu waliofahamu ukweli halisi. Licha ya kuufahamu ukweli, bado baba yake Huyo wa kufikia pamoja na mamaye, waliwaaminisha watu kuwa yeye Mabruki alikuwa mtoto wa Ally Mustafa kwa damu.

Mwanzoni maisha yalikuwa sawa hadi pale mama yake aliposafiri kwenda Uyui kuhani msiba wa bibi yake. Hapo ndipo mateso yalipoanza. Ally Mustafa akaanza tabia ya hovyo kabisa ya kumwingilia Mabruki kinyume na maumbile, akiwa ni mtoto mdogo wa miaka kumi. Mateso hayo yakaendelea hata pale mama yake aliporejea, huku akitishiwa kuchinjwa kama kuku endapo angethubutu kusema kile kilichokuwa kinamtokea.

Hofu na mateso vilipozidi, Mabruki akiwa na miaka kumi na mbili baadae, akaamua kutoroka nyumbani.

Siku mbili za kuzurura mitaani Bila msaada, zikamrejesha tena nyumbani. Mama yake Bila hata kujua kilichomsibu mwanae hata kutoroka nyumbani, akamwanzishia kipigo kikubwa kilichomfanya Mabruki akose mtu wa kumkimbilia. Chuki ikajiotea moyoni mwake. Akaishi nao akiwa anawachukia kweli kweli. Hata hivyo Ally Mustafa hakuacha ukatili wake kwake. Ikafikia hatua kwamba hata alipoingia kwenye balehe, matamanio yake hayakuwa kwa wanawake tena. Alikuwa amezoea ile hali ya kuingiliwa na baba yake wa kufikia. Mabruki akawa sasa anawatafuta wavulana wenzake kumuingilia. Mabruki alikuwa si riziki tena!

Ilipotokea bahati ya kulipiwa ada ya masomo ya chuo Hapo baadae na chama tawala, Mabruki aliona ulikuwa wakati mwafaka wa kujitenga na familia yake iliyomharibia urijali wake na kumlazimisha kuwa shoga, ingawa alichukia sana hayo maisha. Maisha ya kutafuta wanaume kama Malaya. Hakupenda, lakini ni kama alitupiwa jini, na lilipomvagaa, Mabruki aligeuka hayawani. Akihangaika huku na kule kama mbwa jike, ni hadi pale alipokutana na mabasha wake ndipo aliporudi kwenye akili ya ubinadamu na kujutia aina ile ya maisha. Hicho ndicho kitu kilichomfanya Mabruki azidi kuwachukia wazazi wake. Akifanya Kila hila ya kuwakomesha kwa kule kumpoka haki zake za kufurahia maisha kama walivyoishi watoto wengine kwenye familia zingine.

Mazungumzo yake na Masebo, yakamrudishia kumbukizi hiyo mbovu aliyozika moyoni mwake, akimdharau kwa vile hakuwasaidia wazee wake. Wazee ambao hawakujali maisha yake na waliofanya maisha yake yawe maisha hovyo kabisa. Yule mpemba aliyeishi naye kwa hofu utotoni mwake, angewezaje kumpa msaada wowote, mpuuzi ambaye pamoja na kumuita baba alithubutu kumgeuza Mke akijua kabisa kuwa aliwaingilia mama na mtoto? Masebo akathubutu kumkebehi kisa watu hao baradhuli wasiofaa kuitwa wazazi. Leo anadhalilika kisa mabazazi wale?.

'Eti maskini, bado, nitawafanyia maisha magumu kuliko hayo unayodhani ni ya kimaskini, washenzi wakubwa wale' akajisemea kimoyomoyo. Hasira zikampanda Mabruki na kumuondolea ubinadamu. Jini lake likaamka. Akawasha Gari kuelekea kwenye club maarufu ya mashoga huko Las Vegas.


***

Johannesburg, South Africa

Malcolm Stounch alikuwa kaketi kwenye kiti chake cha kuzunguka katika ofisi yake iliyo ndani ya makazi yake yanayolindwa masaa yote kwa mitambo na makamanda wenye mafunzo maalum ya ulinzi.

Kwenye skirini Kubwa mbele yake, alionekana mwanamke wa kazi, Queen of the Mountains – Mc One, akimpa mrejesho wa kazi yake.

"Nitakutumia sauti usikilize mwenyewe, lakini huyu mjinga analenga kuitia nchi kwenye vita ya kidini. Ili hatimae ionekane kuwa utawala umeshindwa kazi, yeye Mabruki awe ndiye mtu wa kuirejesha amani. Hivi inawezekana chokochoko zimeshaanza huko. Kuna haja ya kumpiga stop huyu mpuuzi kwani inaonekana hajali kabisa watu kuuana alimradi tu atimize malengo yake ya ubinafsi." MC One alimaarufu 'Malkia wa milimani' akazungumza. Malcolm Stounch aliguna kisha akauliza,

"Amepanga kufanya chokochoko gani?"

"Kwa mujibu wa mazungumzo yake niliyonasa usiku, amepanga kuteketeza kikosi cha PSU kitakachoenda kumpokea Machera, mpelelezi makini wa serikali ikibidi kumteka au kumteketeza. Anaonekana ana hasira, kwa sababu Machera aliteketeza kikosi cha komando wake aliyekuwa anamwamini sana, Chirundumusi wa Mzindakaya, kuna kitu alitamka kwamba, Huyo Machera anayajua mengi ambayo hakupaswa kuyajua na hivyo si wa kumuachia atembee huru mitaani kwa sababu ni kirusi hatari." MC one alizidi kumfafanulia Malcolm Stounch.

"Kama ni hivyo basi, Huyo mtu anafaa kuwa upande wetu. Najua una watu wako bongo, Fanya kitu kimoja, kabla Huyo Machera hajaingia mikononi mwa Mabruki, tuwe naye mikononi mwetu, tunahitaji taarifa za kutosha ili kumdhibiti Mabruki." Malcolm Stounch akatoa maagizo.

“Haina shaka bosi, kuna watu wangu huko hawajafanya aksheni kwa muda mrefu sana. Wana njaa ya kutosha kuhusu misheni za namna hiyo bosi. Kuwa na hakika kwamba kabla Machera hajaangukia mikononi mwa adui tutamdaka vilivyo." Malkia wa milimani' MC one akatoa uhakika.

"Kazi njema MC one, baada ya haya kuisha itabidi tukae meza moja tujipongeze kwa togwa" Stounch akatamka na kumalizia kwa kicheko laini kifupi. MC one yeye akaachia cheko kubwa kabisa. Habari ya togwa alipata kuisikia kitambo sana!


***

Waliingizwa kwenye jumba lililosheni ubora wa kuitwa jumba. Samani za kileo na mapambo ya kihistoria. Jumba hilo lilikuwa na fensi ndefu mithili ya zile za alqaeda na Isis. Bustani Nzuri za Maua na miti inayovutia. Walifunguliwa kamba na kuachiliwa huru kuzurura ndani ya fensi ile. Mara wakaletewa stafutahi ya nguvu, mihogo ya kuchemsha na uji wa nafaka mchanganyiko. Ulezi, mtama, Karanga, na dagaa. Uji wa watoto! Harakati za safari yao zilikwisha watia njaa na hivyo Bila kuvunga, Machera, daktari Muddy Bonge, Afande Bwire na Anastazia wakavishika hima vikombe vyao na kuyatendea haki matumbo yao. Walipokwisha kumaliza kula, mlinzi mmoja kwenye jumba lile akatokeza mbele yao.

"Nani kati yenu ndiye Machera?" Akauliza.

Kimya!

"Nimeuliza Nani kati yenu anaitwa Machera?" Mlinzi akarejelea kuuliza Swali lake Mara ya pili na safari hii akivaa uso wa beberu.

Machera akajitokeza na kumwendea yule mlinzi. Alipomfikia mlinzi, mlinzi yule akawa anajaribu kumshika mwilini, kosa!

Kosa Kubwa.

Mlinzi akajipata chini baada ya kula kichwa cha kondoo kwenye kidevu chake huku damu zikitokeza pembeni mwa midomo yake.

Kosa!

Kosa Kubwa!

Walinzi walitokeza kusikoeleweka, na kumdhibiti vilivyo Machera.

"We mjinga kukupatia Uhuru tumekosea siyo?" Aliuliza mwanamke pekee kwenye lile kundi la walinzi.

Machera akamtazama tu Bila kutia neno wala kuonesha kusikitika.

"Mpelekeni theater" (chumba cha upasuaji) ilikuwa sauti ya yule mwanamke ikitoa agizo, kitu kilichomtambulisha kama kiongozi wa genge hilo!

Machera alibebwa mzobe mzobe bila kutia purukushani za kujinasua.

Ile kuvuka mlango kuingia kwenye Chumba maalum mlango ukatoa mlio wa tahadhari. Ndani ya Chumba mle mlikuwa na mtu mnene kama nguruwe wa kitoweo, tumacho tudogo tukiwa tumefichwa na miwani mikubwa bila shaka ya kusomea, akiwa kaketi kiutulivu kwenye kiti cha chuma, huenda alishavunja viti kadhaa vya mbao na plastic ndio maana wakamchongea cha chuma. Mtu yule,mbele yake kulikuwa na kioo cha komputa kikubwa. Iliposikika alarm ile, yule mtu akashituka na kutoa sauti yenye wasiwasi;

"Ana chip Huyo, ana chip iliyopandikizwa kwenye jeraha lake la risasi pembeni mwa tumbo."

"Oh, shit! Hebu mlaze Hapo na ucheki namna ya kuiondoa, ingawa sasa tunajua daktari wake ndiye mwanasesere wao hapa. Kamleteni. Mbwa koko mkubwa!" Mwanamke yule akakasirika haswaa.

"Wale wajinga watafika hapa muda si mrefu. Fanya haraka tumuondoe hapa, apelekwe Mabwepande haraka asijekutuharibia!"

Mage Rubanguka ndio jina lake alilopewa na wazazi, lakini yeye alijiita Malikia wa Kiha.

Yule mtu mnene ambaye jina lake lilikuwa Mwananzila, alijinyanyua kizembe kiti kiking'ang'ania makalioni kutokana minyama uzembe mwingi iliyojiachia hovyo hovyo. Akamwendea Machera aliyekuwa amelazwa mithili ya kuwambwa kwani miguu na mikono ilifungwa kwa minyororo kwenye pembe za kitanda kile cha chuma. Machera Hakuwa na ujanja. Alitulia kimya. Sindano ya dawa ya ganzi ikachomwa kwenye eneo la kuzunguka jeraha lake. Baada ya hatua hiyo, mtu mnene, Mwananzila akaanza kazi ya kutafuta microchip iliyohifadhiwa mwilini mwa Machera, akafanikiwa kuichomoa ikiwa bado inafanya kazi, alipomaliza tu kuitoa walinzi walikuwa wamesharudi na daktari Muddy Bonge.

Walimlaza kwenye kitanda Jirani na Machera. Akapigwa minyororo na zoezi la kuipandikiza ile microchip kwenye mwili wake likaanza. Mwananzila akaichomeka chip ile kwenye eneo sawa na ilikotolewa kwenye mwili wa Machera huku Muddy Bonge akipiga kelele za maumivu makali hatari, kwa sababu Mwananzila hakumchoma sindano ya ganzi kuzuia maumivu kusambaa mwilini

ITAENDELEA
 
V


KIKOSI cha Jeshi la wananchi, kikiongozwa na Kamanda Malala Junior, kiliwasili eneo kulikokuwa kunaendelea majibizano ya risasi, kati ya genge la Mabruki na walinzi wa rais PSU. Kama ilivyo kawaida yake, Kamanda Malala, mwenye cheo cha Brigedia Jenerali alikuwa ni mtata linapokuja suala la mapambano ya uwanjani. Alikuwa na tuzo nyingi alizojizolea pale aliposhiriki katika operesheni mbalimbali alizofanya katika kikosi cha kutunza amani cha umoja wa mataifa ambapo ilipobidi walilazimika kuingia kwenye uwanja wa vita. Hapo Ndo palikuwa nyumbani kwake, kwenye Uwanja wa mapambano. Alipotia timu eneo la tukio, Malala Jr alijua kazi imeisha, dakika mbili za kuangalia tu, zilimpa uhakika kuwa atashinda mchezo bila kupoteza mtu wake. Lakini hata hivyo alijikadiria kuwa kama kungetokea uzembe au makosa ya kibinadamu basi si zaidi ya watano.

Aliweka mikakati yake mezani, akawatia moyo vijana wake na Viongozi wa kombania akawapa mikakati mahsusi. Baada ya hapo wanaume na wanawake wale jasiri wakakumbushana kiapo chao cha utii, wakaingia kazini.

Walioshuhudia operesheni ile, walisimula kuwa ni ndani ya nusu SAA tu, Jeshi tukufu la wananchi wa Tanzania lilimudu kuteketeza genge la Don lililokuwa na zaidi ya watu hamsini wenye silaha za kivita na kuwateka baadhi ya Viongozi wa genge lile, wachache sana wakitokomea uswahilini.

"Mkuu tumemaliza genge lote na kuwatia nguvuni baadhi. Wawili wameingia mitaani lakini sina shaka na Jeshi la polisi kwamba watawatia mbaroni. Ndugu zetu watano wa PSU wamelamba ardhi kishujaa, wakipigania Uhuru wa taifa letu" Brigedia Jenerali Malala Junior alitoa ripoti kwa rais, mheshimiwa Masebo.

"Hongera sana Brigedia kwa utumishi uliotukuka, nimeambiwa operesheni imekamilika ndani ya nusu SAA tu, Pongezi nyingi sana nifikishie kwa makamanda wako Brigedia Jenerali. Baada ya hili nadhani tunahitaji kufanya kitu kwa ajili yenu. In fact, nataka nikutane na Hao makamanda niwape mkono wa pongezi. Utanijulisha lini na wapi? Wanastahili pongezi."

"Asante sana mheshimiwa rais, tunashukuru Mkuu, nitakujulisha kitakachojiri."

Rais Masebo tabasamu likachanua usoni kwake. Akatamani angempigia The Don na kumjulisha juu ya kile kilichoendelea. Sasa alimudu kutembea kwa kujiamini kwingi. Alitembea akijua bado anao udhibiti wa Jeshi lake. Kitu kimoja kikatia dosari furaha yake! Hakujua alipo Machera.


***

Ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa chochote kitu cha kujulisha adui maficho yao, malkia wa kiha akaamuru mateka waliosalia kupita kwenye mtambo ule unaogundua hila za teknolojia za kiinteligensia. Alianza Afande Bwire na akamalizia Anastazia. Hao walikuwa safi. Kazi iliyosalia ilikuwa ni kumtoa msaliti wa kundi lake na kumpeleka kwenye jengo la mjerumani lilioishi kwa miaka mamia na sasa lilitekezwa Bila uhifadhi wowote. Ilikuwa ni kama kilometa tatu hivi kutoka kwenye jengo lile la awali. Huko walimfunga thabiti na kumuacha Muddy Bonge akitafunwa na panya waliomuona kitoweo. Bila kelele akagugumia maumivu ya kushambuliwa na mipanya iliyojaa kwenye jengo lile ikiwa na njaa si haba.

Ambacho hakujua, ni kwamba kwa Jirani na jengo lile kulikuwa na mtu wa kuchunguza kile ambacho kilitarajiwa. Naam, malkia wa kiha alikadiria vema kuwa waliomtuma Muddy Bonge kuchomeka chip kwenye mwili wa Machera basi wangekuwa kwenye harakati za kuitafuta na pale ambapo wangefanya hivyo, basi wangeipata kwenye mwili wa daktari Muddy Bonge.

Masaa kadhaa baadae, mwili wa Muddy Bonge ukiwa na majeraha ulichukuliwa na watu wa Don, akiwa kwenye hali mbaya kufuatia kugeuzwa kitoweo na wale panya wenye njaa kali. Hata hivyo, huduma bora za hospitali zilimsaidia.


***

Malkia wa kiha alikuwa kakaa nyuma ya skirini kubwa ya komputa. Kwenye kioo cha skirini ile kulikuwa na mtu akiongea naye. Waliongea ana kwa ana kwa kutumia teknolojia hiyo ya kisasa. Moja kati ya mazungumzo yao likiwa kupongezana kwa kile kilichofanyika na pili ikiwa ni kukubaliana juu ya kazi mpya iliyokuwa mezani.

Alipomaliza mazungumzo yake, malkia wa kiha akaagiza Machera kupelekwa kwake Mara moja. Hilo likafanyika Bila ubishi. Machera akasimama mbele ya mwanamke yule mwenye kuvaa miwani, mwenye sauti ya kusitasita, na urembo asilia, mwanamama wa kiafrika haswaa!

Mwanamke yule alimwangalia kama hakumuona huku akiendelea na shughuli zake kama vile hakutambua uwepo wa mtu pale ndani. Alipomaliza kuchapa kile alichokusudia kwenye komputa yake na kukihifadhi vema, mwanamke yule aliunyanyua uso wake mpana, akashusha miwani chini usawa wa pua, ikawa kama anamchungulia juu ya miwani ile.

Aliketi kwenye kiti kwa kujibweteka kulikoonesha kuridhika na mipango yake. Malkia wa kiha akamtazama Machera kwa jicho la usanifu. Halafu akatoa tabasamu lililoruhusu mwanya wake mpana na meno yaliyopangika vema kwenye safu zake kuonekana. Hakika huyu alikuwa malkia wa kibongo,

‘Mashallaa mtoto kaumbika na anajitambua kaumbika' Machera akakiri mawazoni mwake.

"Nimesikia sifa zako maradufu, 'mpelelezi wa kutumainiwa amekwamisha mpango wa mafisadi, mafisadi walikusudia kuchota mabilioni ya fedha za watanzania kuyakimbizia ughaibuni,ni yule mpelelezi thabiti Machera', Mara,' asingekuwa Machera janga Kubwa lingelikumba taifa, kwa Mara nyingine ameonesha uzalendo wa kiwango cha juu, Bila shaka alikuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa'. Sifa nyingi kem kem! Hebu keti mwanaume. Keti tuzungumze"malkia wa kiha aliongea hatimae.

"Mhh..." Machera akaguna, 'anajua kutumia ulaghai wa ulimi vizuri.' Akajiwazia.

Malkia wa kiha akasimama na kumfuata Machera, akampatia mkono wake na kwa heshima akampigia magoti ishara ya heshima. Loh! Machera akabaki hoi bin hoi. Si kwa heshima hii aliyokuwa anapewa hapa. Hata mtu wake, mpenziwe Anastazia hakuwahi kuonesha heshima ya kiwango hicho. Moyo wake ukadunda kwa kulipuka ufahari. Huyu alikuwa zaidi ya mwanamke. Huyu alikuwa malkia!

"Nimefurahi sana kukutana na wewe kihalisia. Wewe ni mwanaume ambaye nimekuwa natamani kumuona. Kukuona kwangu Leo, ni kutimia kwa ndoto zangu za siku nyingi. Najisikia fahari kwamba umepata kujihifadhi kwangu." Malkia wa kiha akazidi kumchanganya Machera kwa misifa kibao. Hilo la kujihifadhi likampa alarm kichwani mwake. Amemteka, na sasa anamsifu kwa kujihifadhi kwake.

"Wewe ni Nani na unataka nini hasa kutoka kwangu." Sura yake haikuonesha urafiki wowote. Ilikuwa sura iliyochoshwa na dhihaka. Naam. Machera alihisi huyu mwanamke anamchora na kujaribu kumpumbaza.

Hakuwa mjinga kiasi cha kushindwa kung'amua ulaghai na ukweli. Hata hivyo alikuwa mjinga kiasi cha kushindwa kuelewa kama huyu alifeki alichoonesha au la!. Kiujumla, ile kengele iliyomwambia asijileweshe sifa zile ilikuwa inakinzana na matakwa ya moyo wake uliokuwa tayari kupumbazika walau kidogo na Maelezo ya mwanamke yule mrembo.

"Asante kwa kuonesha unajali kiasi cha kuhitaji kunifahamu zaidi. Naitwa Margret Rubanguka, ila kusema kweli napendelea zaidi kuitwa Malkia wa Kiha. Natambua unao wasiwasi, lakini kwa mtu makini kama wewe ningeshangazwa kama usingeonesha wasiwasi." Malkia wa kiha akatamka kisha akaruhusu sekunde kadhaa zipite, halafu akaendelea kueleza.

"Hapa upo kwenye mikono salama, yule Daktari wako Muddy Bonge alikuwa pandikizi tu. Yule alikuwa amepandikiza microchip kwenye mwili wako kiasi kwamba ilikuwa rahisi kwa adui kujua ulipo, na inaonekana alitumia udhaifu wako kwa vile ulizima na kuishonelea mwilini mwako wakati anakutibu. Hivyo hata hapa mahali salama pangeweza kugeuka hatari kwako. Hata hivyo tumemtoa hapa wakamkute mabwana zake huko tulikomtupia.

"Mimi na wenzangu ni majasusi wa kujitegemea na kwa muda sasa tumekuwa tukimpeleleza Mabruki kwa sababu ya mauaji ya kijana aliyeitwa Elinisa ambaye Bila shaka unamfahamu. Sisi tunafanya upelelezi wetu kwa niaba ya familia yake, ili Huyo Mabruki awajibikie madhambi yake. Hivyo, nikuondoe wasiwasi bwana Machera kuwa Sisi si watu wa The Don kama ambavyo bila shaka unatudhania. Tumekuteka? Ndiyo, kwa nini? Ilikuwa ndiyo njia pekee kwa wakati ule. Hivyo basi, tuama moyo na ikiwezekana tushirikiane, kwani adui yako ni adui yetu pia." Malkia wa kiha akaweka kituo kufikia Hapo. Kufikia hapo, tabasamu likaenea usoni mwa Machera. Alijikuta akimwamini mwanamke huyu bila chembe ya wasi wasi.

"Asante sana malkia wa kiha, nimefarijika kwa huduma yako. Nikiri tu kwamba wallah hilo jina linakufaa sana na kwa hakika unalitendea haki. Adui yenu adui yangu, nipo tayari tushirikiane kumuangamiza. Sasa basi, Bila kuchelewa sana malkia, niombe kufanya mawasiliano na ikulu kwa sababu kama unavyofahamu huko ndio Nilikuwa naenda yalipotokea Yale yaliyotokea."

"Bila shaka Machera, ni dhahiri kuna jambo zito lililokuwa lijadiliwe ambalo Don Hakuwa radhi kuruhusu."

"Ni kweli, ni jambo ambalo lisipodhibitiwa litaingiza taifa kwenye machafuko makubwa."

"Haya baba, nalokuomba Ee baba, ni kutuweka nuruni ili tuunganishe nguvu dhidi ya Huyo baradhuli wa kujiita the Don" malkia wa kiha akaweka bayana hoja yake. Wakacheka, halafu Machera akatamka;

"Usiwe na shaka ewe malkia wa kiha, askari wako Tuko kifua mbele kulinda himaya yako." Wakacheka zaidi.


***

Magogoni, Dar Ee salaam. Ikulu.


Simu iliita, haikuwa na namba. Haikuwa na jina, ilikuwa ni logo. Logo ya ikulu, maarufu kama nembo ya taifa. Watalaam wa mawasiliano ikulu wakahaha kutaka kujua kulikoni. Wakaseti mitambo ili kutanabahi ni wapi ilitokea. Walipomaliza hilo zoezi wakamruhusu katibu muhtasi wa rais aipokee.

"Haloo" Manka akaipokea Simu.

"Tunahitaji kuongea na rais." Sauti ya malkia wa kiha ikaweka wazi kusudio lake halafu akaikata Simu.

"Vipi mmefanikiwa kubaini chanzo cha mawasiliano kipo wapi?" Ilikuwa sauti ya rais Masebo akionekana mwingi wa wasi wasi.

"Hapana mheshimiwa, inahitaji dakika mbili kuweza kutambua." Mtalaam wa mawasiliano ikulu akajibu.

Dakika mbili baadae Simu ikaita tena, kama awali, ilionekana nembo tu kwenye kioo.

Mheshimiwa rais akaipokea kwa wahka kutaka kukitegua kitendawili.

"Haloo!" Rais akakoroma

"Mkuu shikamoo! Ni Machera mheshimiwa! "Machera akajitambulisha huko upande wa pili kimya kikakatiza wakati mheshimiwa rais alipokuwa anashusha pumzi za kutua zigo la wasiwasi kutoka moyoni.

"Loh kijana wangu umepitia mengi mno, pole sana. U hali gani Machera?." Mheshimiwa Masebo akatamka na kuonesha Furaha yake dhahiri!

"Mkuu, Niko salama. Katika kujiokoa niliangukia kwenye mikono salama. Pole kwa usumbufu mheshimiwa! "

"Asante, imekuwa Heri, wale wajinga wote tumewadhibiti. Hata hivyo, tunalo jambo la kufanya. Kikao chetu kilivurugwa lakini sasa naona tutafanikisha. Naamini utahitaji usaidizi kutoka huko ulikojificha." Mkuu wa nchi akaeleza.

"Hapana Mkuu, Heri nije mwenyewe. Nimebaini kuna mamluki wengine wapo huko ikulu, unaweza kuamini kuwa daktari uliyenitumia ndiye alishirikiana na adui kusababisha Yale yaliyotokea? Hivyo ndivyo ilivyokuwa Mkuu." Machera akatamka, kauli yake ikiwa kisu kikali kilichofanya kuyakata maini ya Mheshimiwa kikatili. Ikulu ilikuwa na mamluki? angewezaje kuwatambua?

"Mheshimiwa! "Machera akaita.

"Taarifa hiyo imenishitua kijana wangu!" Masebo akakiri huku akizinduka kutoka kwenye mawazo ya ghafula.

"Oh pole Mkuu. Ila ni muhimu kwamba umelitambua hilo ili kuwa na tahadhari. Nipo njiani nakuja!" Machera akamalizia.


ITAENDELEA..
 
VI


Machera alikuwa anaingia katika viwanja vya ikulu. Tayari wahusika wengine wa kikao walikwishaingia mapema na ni ujio wake uliokuwa unasubiriwa ili kikao kianze.

Alipoingia kwenye Chumba cha mkutano Machera alikuta wahusika wakiwa wanazungumza hili na lile kwenye vikundi Bila mwongozo. Nyuso zao zilipomuona zikajawa na bashasha Kila mmoja akinyanyuka apate kumshika mkono. Kuna waliompa pole, waliomtolea tabasamu tu na waliopongeza kurejea kwake ikiwa kama ishara ya kuponyoka mikono hodari ya adui.

Wakiwa kwenye mchakato huo akaingia mheshimiwa rais kwenye Chumba cha mkutano. Mara wote wakasimama na kimya kikatawala.

"Habarini za jioni ndugu zangu." Mheshimiwa rais alisalimia. Akaachia nafasi, wajumbe wakaitikia, halafu akaendelea.

"Naona tumepata neema ya kuwepo ndugu yetu Machera, tunakukaribisha sana kijana wetu, na hii bila shaka ni dalili njema." Machera akainuka na kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote Tanzania kwa saluti.

"Niwaombe tuketi Tafadhali. Ah! nianze kwa kuwapongezeni nyinyi nyote kila mmoja kwa eneo analofanyia kazi. Kwa kweli Nina imani Kubwa na utendaji wenu wa kazi kwani matokeo yake yapo wazi. Yule muasi mmoja kwa kulewa madaraka na pesa haramu, alidhani anaweza kuiweka nchi mifukoni mwake. Lakini kwa uzalendo wenu na wale waliopo chini yenu tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti hila zake.

"Nimeonelea vema tukutane ili tupeane yaliyojiri katika kazi tulizopeana mapema mwezi Huu kama mikakati ya kuhakikisha amani yetu inaendelea kuwepo na tunakuwa hatua zaidi mbele ya adui wa nchi yetu kwa kuwa na taarifa zao na mipango yao mapema iwezekanavyo ili kuzuia baya lolote wanalopanga adui zetu.

"Niseme tu, hii nchi itazidi kuwa imara na hiki ndicho kipindi cha kuonesha uimara huo hasa kwa vile ndicho kipindi ambacho nchi yetu inapitia majaribu makubwa kiusalama na kwenye upande wa mshikamano wetu kama watanzania.

"Karibu katibu Mkuu kwa ajili ya ajenda." Rais Masebo alimalizia maneno yake ya ufunguzi. Makofi ya pongezi yakasikika kufurahia maneno yake yaliyosheheni busara na kutambuliwa kwa mchango wa wana kikao.

"Asante sana mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu rais Sebastian Masebo. Nikushukuru kipekee kabisa kwa hutuba fupi Nzuri yenye kuonesha uongozi uliotukuka. Mheshimiwa raisi nikuhakikishie kuwa Sisi watumishi wa umma tunakupa full sapoti na kwamba Tuko nyuma yako daima.

"Ndugu wajumbe, niombe kutambua kuwepo kwenu na itifaki imezingatiwa. Karibuni sana kwenye kikao hichi ambacho pamoja na mengineyo kitaangazia mustakabali wa usalama wetu kama nchi. Ni wazi kwamba adui anajaribu kutumia Kila njia kutugawa ili iwe rahisi kututawala. Ndugu zangu Huu ndio muda wa kumuonesha kuwa tunao mshikamano thabiti na kwamba misingi ya amani yetu haitatingishika kamwe. Ni muda wa kuwezesha hili kutambulika na Kila raia wa nchi hii......" Maelezo yalikuwa mengi lakini kikao hatimae kikaanza rasmi.

"Kule mkoani Arusha mheshimiwa rais tumefanikiwa kuwakamata raia wawili wa kigeni ambao baada ya kukaguliwa,watu hao walikutwa na bidhaa ya unga iliyokuwa imepakiwa vema kwenye vifuko vidogo vidogo. Vifuko hivyo vilitumwa sampuli kwa mkemia Mkuu wa serikali, na baada ya kufanyiwa uchunguzi ikabainika raia wale wa kigeni ima walikuwa wanakusudia kuua watu mahsusi au kutengeneza uwezekano wa nchi kuyumba. Vifuko hivyo vilikutwa na vimelea vya ugonjwa wa kimeta (anthrax). Upelelezi wetu umebaini kuwa vimelea hivyo vya kimeta vilikusudiwa kuachiliwa Arusha kuibua mlipuko wa ugonjwa huo ambao unaenea kwa kasi kwa kuwa ni ugonjwa ambao ni rahisi kuenea kwa kula nyama ambayo imeathiriwa na ugonjwa na lengo lao ilikuwa ni kuusambaza kupitia wanyama. Mtakuwa mnafahamu kuwa jamii nyingi huko kaskazini ni watu wenye kujihusisha na ufugaji, na kimeta ni rahisi kuenezwa kupitia wanyama hasa kuliko binadamu. Kwa hiyo mnaweza kuona ni kitu gani walikusudia. Walikusudia kuua mifugo na wafugaji, kilio kienee serikali ikiwa mtu wa kutupiwa lawama."

“Je mmejiridhisha kuwa hakuna wengine waliokuwa wamefanikiwa kuingia kabla ya Hao?" Rais akahoji akionekana kusitushwa na hiyo taarifa.

“Kwa tahadhari tu tumekwisha wasiliana na wizara ya afya kwa ajili ya kuweka kambi ya kudhibiti ugonjwa huo ingawa tunaamini wale watu Ndo walikuwa wanaingia. Pendekezo langu ni kuimarisha ulinzi kwenye viwanja vyetu vya ndege na mipakani mwetu." Kamanda wa mkoa wa Arusha alipendekeza.

Kufuatia taarifa hiyo mheshimiwa Rais akatoa agizo la kuwekwa tayari chanjo na tiba dhidi ya kimeta endapo kingeibuka. Mikakati mingi ikaongelewa na taarifa kutolewa. Taarifa nyingine iliyowasitua watu kwenye kikao hiki ikawa ni ile iliyotolewa na Machera. Taarifa iliyoeleza kwa kina kusudio la Mabruki kuigawa nchi kwa kutumia Viongozi wa dini kuu mbili za kiislam na kikristo.

Akawathibitishia wanakikao kuwa Viongozi walikuwa watumike ni wale ambao wapo kwenye dini kama kivuli huku dini yao halisi ikiwa ni maslahi binafsi. Hao walipanga kuingiza ajenda za kugawa wananchi kwa itikadi za kidini ili kuchochea vita vya kidini wao wakikaa meza moja kwenye mahekalu yao ya kishetani na kupongezana kwa uhalifu huo. Majina ya taasisi hizo za kidini yakiwekwa mezani kwa nia ya kufanyiwa uchunguzi na kuyaweka hadharani maovu yao kabla ya kutekelezwa kwa ajenda zao. Hili lilikuwa zito kwani mambo ya dini daima yamekuwa yakiambatanishwa na hisia nzito na hata utayari wa kuhiyari Mauti miongoni mwa waumini katika kutetea imani zao.

“Kwa hiyo mheshimiwa rais tunao wajibu wa kuhakikisha ulinzi wa raia wetu katika madhehebu hayo yenye kujaa waumini wengi, kwani inavyoonekana mkakati uliopo kwenye kundi la Don ni kutumia kundi maarufu la Ali haki fighters kujitoa mhanga na kulipua sinagogi la Nabii Oyono Goodness ili kuchagiza hisia za vita. Nabii Oyono Goodness analifahamu suala hili na ndiyo maana kwa muda amekuwa akihamasisha mahudhurio ya watu kwa ajili ya kitabu chake chenye miujiza. Hofu yangu ni kuwa matangazo na hamasa zinazoendelea kutolewa ni hamasa ya kuteketeza maelfu ya raia wengi siku husika. Kwenye usharika wao wa kishetani wana utaratibu wa kutoa sadaka na kafara za wanadamu, hasa Kila baada ya miaka kadhaa na kunayo Kila dalili kwamba Huu ni Mwaka wa kafara zao." Machera alitoa Maelezo, Maelezo ambayo aliyapata kupitia The Don mwenyewe kwenye ule mkasa wa kukamatwa kwa Mabruki, pale alipojikuta akimwaga hadharani siri zote za kundi lao ambapo bastola ilimtia kiburi Mabruki hata kuiweka mipango yao bayana kwa Machera akiamini ni dhihaka, kabla ya kumlaza kwenye altare ya Mauti kwenye moja ya madhabahu zao chini ya ardhi ya kasri la Don, kutanabahi kibao kikamgeukia.

Ni taarifa hizo zilizopelekea Mabruki kumuwinda Machera na kufanya Kila hila kumtia mikononi mwake kabla Machera hajafikisha taarifa hizo kwenye kikao cha rais. Alijua wazi kama taarifa hizi zingefika ngazi hiyo ingekuwa kazi ngumu kwao kutekeleza mipango yake kuielekea ikulu ya Tanzania, na huenda ingemweka kwenye wakati mgumu kwa wafadhili wake aliowaahidi kuwamegea Tanzania kwa kadri ambavyo wangetaka.

Taarifa hii ikawatetemesha wajumbe wa kikao. Suala hili lilikuwa zito, kiyoyozi cha ikulu kikishindwa kufanya kazi kwa wazalendo hawa wa nchi. Hasa rais mwenyewe ambaye alionekana kumwagika jasho kabisa!


***

Las Vegas. USA.

Don aliingia kwenye club ya mashoga kwenye chemba maalum za watu maarufu ambao kutokana nafasi zao kwenye jamii, hawakuwa tayari kujitangaza kuwa kwenye mahusiano ya aina hiyo ambayo kusema kweli, yalikuwa machukizo makubwa kwa waumini wa dini za kikristo na kiislam. Ni kweli kwamba wapo hata Viongozi wa dini hizo ambao kwa unafiki waliyakemea mahusiano ya aina hiyo huku wakiyashiriki kwa siri. Hilo halikuondoa ukweli kwamba licha ya dini, hata sayansi haikuwahi kuthibitisha uhalali wake zaidi ya kuonesha ni vitendo ambavyo kwa sehemu Kubwa vilikuwa na madhara zaidi kisaikolojia na hata kitabibu.

Magonjwa kama UKIMWI yakihusishwa kuua idadi Kubwa ya mashoga kutokana na njia hiyo ya kujamiiana kueneza kwa urahisi zaidi gonjwa hilo hatari. Ni dhahiri, ni mtu aliye kinyume na ubinadamu halisi tu ambaye ama kwa akili zake za chuki dhidi ya binadamu au kwa kufurahia madhila yawapatayo wanadamu, angefurahia na kuhamasisha maisha ya aina hiyo. Kisaikolojia idadi Kubwa ya watu walioshiriki kwenye aina hiyo ya maisha waliishia kujiua, kwa sababu haikuwa akili ya kibinadamu.

Mabruki alipoingia tu mle ndani aliketi kwenye kiti, akili yake ikiwa imevurugika hasa kutokana na mazungumzo yale waliyofanya yeye na Rais Masebo. Wakati akili yake ikifuka moshi wa hasira, akasikia mlango wa Chumba hiko ukigongwa. Sauti aliyoifahamu vema ikabisha hodi. Sauti hiyo ikamtoa kwenye hasira yake, kwa dakika moja tu, akawa amesahau kabisa habari ile iliyokuwa inakichemsha kichwa chake. Mabruki akanyanyuka hima na kufungua mlango. Alikuwa Didier Masele, mwanamuziki wa Congo aliyefanyia kazi zake huko Las Vegas na kundi lao la Kinshasa Music Troupe. Kwa muda sasa kijana Huyo wa kikongo alikuwa kwenye mahusiano na Don hata ikafikia sehemu, Don aliwaza kufunga ndoa ya Siri na kijana Huyo.

Mabruki akampokea kwa mabusu motomoto bila kuruhusu hata salamu kupita katikati yao. Pepo lake lilikuwa limeamshwa na mpunga pepo ndio alikuwa kaingia kulishughulikia. Watu Hao wakafanya yaliyowakutanisha. Mabruki akili ikatulia, akayaweka mawazo na mipango yake bayana kwa mwenzi wake Huyo. Ambacho hakujua ni kuwa mchumba wake alikuwa na mchumba, mchumba ambaye alimpenda hasa na si hili zee lenye kitambi, chafu la tabia. Mabruki hakujua kuwa Masele alifanya kile alichofanya kwa sababu ya shida za kiuchumi tu na midola ya kimarekani aliyolipwa kwa kuliingilia zee hilo ndiyo kilikuwa kifungo chake, akilazimika kufanya kitu ambacho alikidharau na kilimchukiza kupita maelezo. Mabruki Akiamini kijana Huyo alikuwa basha asiyetamani wanawake!

Masele alikuwa na majonzi moyoni, mchumba wake Grace, alikuwa mikononi mwa watu hatari, usalama wake ukimtegemea yeye kukusanya taarifa za mipango ya Mabruki dhidi ya Tanzania. Akilazimika kupeleleza kishabiki kwa kumsifia na hata kumpa baradhuli yule mawazo yake namna ya kudili na taifa lake. Kwake haingekuwa na madhara, lakini Grace kuwa mikononi mwa maadui wa Mabruki ilimfanya Didier Masele kujenga chuki Kali dhidi ya Mabruki.

Walikuwa wanapiga soga zao, Simu ya MacCulough ilipoita. Bila ya wasiwasi wowote, Mabruki akaipokea.

"Ndiyo Bwana MacCulough, nipe habari.!" Mabruki akakoroma kwenye Simu akiona ufahari kuitwa boss.

"We have the package in our custody boss, we only require to establish the communication and the rest will go as planned" (Tayari tumepata kifurushi bosi, kilichobaki ni kufanya mawasiliano na mengine yatafanyika kama tulivyopanga, mambo yatajipa tu!) MacCulough akaongea.

"Well done Mac, this is going to blow their minds away, I know they're currently celebrating their cheap winning over the failing abduction of that idiot and the failing Anthrax program, but this Mac, this is a our win. Keep that bitch well hidden, and as you said, the rest will go as planned" (Safi sana Mac, umefanya kazi Nzuri sana. Hii Itakuwa baab Kubwa, najua watakuwa wanajisifu kwa ushindi wao mwembamba wa jaribio la kumteka yule mjinga mmoja na kuwatia mbaroni wataalamu wa kimeta, lakini kwa hii, wataisoma namba Barabara. Hakikisha Huyo Malaya anabaki mafichoni) Mabruki aliunguruma kwenye Simu mashavu yake yakitetemeka kama sharubu za paka.


ITAENDELEA...
 
VII


Magogoni, Ikulu. Dar es salaam.

USIKU SAA tano. Mheshimiwa Masebo alikuwa ikulu akitazama taarifa za habari kupitia kituo kimoja maarufu cha kimataifa cha huko mashariki ya kati, kwenye kioo kulionekana taarifa ilioonesha maandamano makubwa kuliko Yale yaliyomuondoa mtangulizi wake nchini. Ilikuwa ni huko Algeria, wananchi wakigomea uamuzi wa rais wa taifa lao kugombea tena kwa kile kilichosemekana kutumia muda mwingi nje ya nchi kwa matibabu akiwa pia amedumu madarakani kwa miongo kadhaa! Habari hiyo ikamsononesha! Hila za Mabruki zinaweza kuleteleza hayo. Akabadili kituo. Haikusaidia. Huko alikutana na habari za Venezuela, ikisemekana kuna marais wawili, nchi ikigawanyika kwa sababu ya chokochoko za serikali za kibepari ambazo wala hazikuangalia maslahi ya nchi husika!

"Ubazazi Huu" Masebo akaghafilika na kutamka kwa sauti. Simu yake ya mkononi ikapata ugeni, akanyanyuka kivivu na kuifuata, namba ngeni ikicheza kwenye kioo chake. Akaiinua, akaipachika sikioni, akatamka 'Halo' yenye uvivu wa kutosha, sauti iliyojibu Hapo ikamtoa uvivu wote huku akiitupia simu kwenye sofa. Wahaka ukamjaa ghafula!

Hofu.

Akairukia Simu yake huku akituliza mapigo ya moyo.

"Binamu, huko kwenu SAA ngapi? Huku ni usiku wa SAA tano, watu wameshalala!" Masebo akajibaraguza huku moyoni akiilazimisha furaha, mikono yake ikitota kwa jasho.

"Taarifa nayotaka kukupatia, hutatamani kitanda binamu, najua unahisi umeweza sana. Ndo kwanza tunauanza mchezo wenyewe. Zingatia hili rais uliyehongwa cheo, Ujumbe unatumwa kwenye Simu yako muda si mrefu, ukishaupata usome peke yako, ukisharidhika na utakachokiona, ufute! Kesho nitakutafuta tena na kukupatia maelekezo. Usijiroge kumshirikisha mtu suala hilo. Utakuwa umejiharibia mwenyewe! Usithubutu kunilaumu, ukishindwa maelekezo haya imekula kwako. Haya, hima kalale zako, Mheshimiwa rais." Mabruki akaeleza kwa dhihaka na kukata Simu.

Kiti kikawa hakikaliki, kitanda hakilaliki,sebule haikanyagiki.

Wasiwasi, hofu!

Awajulishe wanausalama wake? Hapana. Amweleze Machera? Labda! No, hataa! Haitakuwa sawa! Akajitupia kwenye sofa Simu yake ikiwa mikononi, dakika mbili zikionekana kama masaa mawili.

Kizungumkuti.

Mara paap! Ujumbe ukaingia kwenye simu!

Kimuhemuhe!

'Open your WhatsApp account. Look for new number ending with triple zeroes!. Don nation!' ( Fungua account ya WhatsApp, angalia namba ngeni inayomalizia na masifuri matatu. Taifa la Don) ujumbe ukaishia hapo. Hata alipomaliza kuusoma, mheshimiwa Rais alikuwa anatetemeka mikono akihangaika kuitafuta smartphone yake iliyokuwa ikali mikononi mwake wala asiione. Kale kajasho ka uoga sasa kaliuloweka mwili wake tepetepe.

Akasimama huku miguu yake ikikaidi kuendana na kasi ya ubongo wake, ambao hata wenyewe ulifanya kuwayawaya, Mara uwaze hili huku ukitenda lile, kama ungelimuona wala usingemdhania ni yule mwana siasa mkakamavu mwenye haiba ya ujasiri hata kufikia kubandikwa jina la utani Simba wa nyika. Mwili wake wa mazoezi sasa ulitepeta kimdebwedo, miguu ikashindwa kuuhimili uzito wake, akamwagika na kujibwaga chini kama zigo.

Mkuu wa nchi akawa hajui nini cha kufanya, hofu iliyomvagaa sasa ilimdhoofisha bila sababu. Hisia yake ikatokea kuwa kweli. Ama kwa hakika aliwazalo mtu hilo humtokea. Alipomaizi Simu imkononi mwake, Mheshimiwa Masebo akaingia kwenye akaunti yake ya WhatsApp. Kama alivyoelekezwa, akatafuta number yenye kuishia na masifuri matatu! Akaona video yenye kivuli vuli, akabonyeza ka-alama ka-kuishushia, kidole chake kikawa kama hakifanikishi zoezi, Mara ya kwanza, ya pili hola, Mara ya tatu wapi, akajihimu na kubonyeza kwa nguvu zote alizomudu kunuia.

Buff..!

Kioo kikaonesha UFA. Kioo kimepasuka, hata hivyo lengo lake lilifanikiwa aliona kamshale kakizunguka nusu mduara huku asilimia zikiendelea kuongezeka kuonesha zoezi la kuishusha video ile lilikuwa linaendelea vema. Kimbembe kikawa video yenyewe ilipoanza kucheza, mheshimiwa nguvu zikamuishia.

Akadondoka chini toka kwenye sofa puu! Kishindo kikamshitua mkewe aliyekuwa kazama kwenye tamthiliya pendwa iliyokuwa inaendelea kwenye runinga, asijue kilichokuwa kikimsumbua mwenzie. Mama Huyo akanyanyuka na kumfuata mumewe! Kilio kikali cha mshituko kikimkumba ghafula.

Kutanabahi mama yule akakiona alichokiona mumewe, huyu hakustahimili, akashika moyo wake kwa bidii, macho yakamtoka, chini akadondoka puu!!.

Akazimia.

Hilo likamzindua mheshimiwa, hakujua kazitolea wapi nguvu, akamnyanyua mkewe huku akiita wasaidizi. Mama akalazwa hoi kitandani hajitambui. Daktari wa ikulu akihangaika kumrejesha mama yule, first lady!


****

Usiku haukulalika, ikulu walikesha! Asubuhi ikisubiriwa kwa hamu kuliko chochote kitu. Rais akanyong’onyea kuliko kawaida. Simu ile ikiwa safi kama vile haikupokea salaam kutoka kwa Don, salaam ambazo madhara yake yalikuwa dhahiri. First lady akiwa kitandani hajitambui, Mheshimiwa akiwa na dalili zote za sonona. Hata hivyo akatumia Kila hila kuilandisha huzuni yake na tukio la mkewe kulazwa, huku ukweli kwamba ni Ujumbe wa Don ndio sababu, ukifichika mtimani mwake.

Masebo akawa muda wote ameikumbatia Simu yake ya mkononi akiichungulia Kila baada ya muda akiwa hajui muda gani adui yake Mabruki angemtumia Ujumbe mwingine. Na huo ungekuwa wa aina gani.

Mlio wa kupokea Ujumbe ukaingia kwenye Simu yake, Simu ikadondoka mikononi mwake, msaidizi akajaribu aiwahi, akaambulia kula kikumbo cha haja huku Mheshimiwa akiitia tena mkononi mwake simu yake na baadae kutoa pole kwa msaidizi wake!

'Pole kwa hilo la mkeo, uliambiwa uusome Ujumbe mwenyewe lakini ukakaidi na hayo ndiyo matokeo ya ukaidi. Kama ulivyoona, hitaji langu ni jepesi tu, kwanza ni kuondolewa kwa mashtaka yaliyopelekwa mahakamani, kufutiliwa mbali kwa ushahidi wowote uliopo dhidi yangu na muhimu zaidi, huyu kijana wako Machera namtaka mikononi mwangu akiwa hai au mfu. Sijui utafanyaje, lakini Jana ulinambia wewe ndio rais wa jamhuri ya Tanzania. Don nation' Ujumbe ukaishia!

Mheshimiwa Masebo akaharakisha kuingia chumbani kwake. Akajitupa kitandani. Alikuwa na mtihani mgumu, mgumu hatari!


***

Kutokana na Yale yaliyokuwa yakiendelea kufuatia harakati za Don, Machera na Malkia wa kiha walilazimika kuunda kikosi kazi kwa lengo la kufuatilia mikakati mbali mbali ya utekelezwaji Wa mipango ya Don. Kikosi kazi ambacho kilijigawa Mara mbili kuwafuatilia vinara wa mpango mkakati wa kutumia dini kama hatua ya kufanikisha lengo la Mabruki kuingia madarakani.

Kikosi cha kwanza kikawa ni Machera na Anastazia wakiwa uwanjani na Malkia wa kiha akibaki mitamboni. Kwa upande wa pili Ken, Martha wakiwa uwanjani na Mwananzila akiwa mitamboni. Vijana kadhaa wa malkia wa kiha wao walipewa jukumu la kuwa vivuli vya wale waliokuwa uwanjani na wa mitamboni. Hawa kazi yao Kubwa ikiwa kuzuga na kukusanya taarifa muhimu za kusaidia watu wao. Hilo lilikusudiwa kung'amua kama kungekuwa na wapelelezi kutoka upande wa adui juu ya wenzao.


ITAENDELEA...
 
VIII


Jijini Dar

Harakati za kuzuia harakati.

MKAKATI uliokubalika wa kuzuia harakati za Don kuiingiza nchi kwenye dimbwi la vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu za Kidini, haukupaswa kucheleweshwa muda mrefu, kulikuwa na kila sababu ya kuharakisha zoezi hilo. Machera na Anastazia waliamua hawakuwa na muda wa kupoteza. Don alikuwa amewaachia dondoo muhimu za kufanyia kazi. Kulikuwa na haja kutumia muda vema Bila kulaza damu. Vijana wakaanza kazi.

Safari hii kulikuwa na mengi ya kufanyia kazi. Mbali na kazi ya kitaifa waliamua kuchimba kwa undani watu hao waliomtumikisha The Don, wakimtumia The Don kama kipaza sauti. Kwa sehemu, The Don alikuwa ameonyesha kile ambacho watu hao walikuwa na uwezo wa kukifanya. Sasa iliwabidi kutafuta yaliyosalia. Na hapo wakawa wanaingia kwenye utafiti ambao ungewashangaza.

Kama walikuwa hawaamini kuwa sita na tisa ni sawa, kwa kuamua kufuatilia watu hao wangeamini. Wangeamini kwani ulikuwa mchezo rahisi kwa kundi hilo kuaminisha watu kuwa sita na tisa ni sawa ila inategemea macho ya mtazamaji na upande aliokaa mtazamaji.

Jumapili hii Machera na mwenzie Anastazia waliamua wahudhurie ibada katika sinagogi la nabii na mtume Oyono Goodness.

Oyono Goodness alikuwa mhubiri maarufu sana jijini Dar es salaam. Mahubiri yake yalisikika katika vituo vya redio karibu vyote vya kikristo na kutazamwa kwenye runinga kote jijini. Kanisa lake lilikuwa zaidi ya kanisa, likiwa na ukubwa wa eneo mkubwa ukipungua kiasi kuufikia uwanja wa taifa. Kwa kawaida likiwa linajaza maelfu ya watu kila kukicha.

Ilisemekana kuwa mtume na nabii Oyono alikuwa na uwezo wa kufanya miujiza mikubwa zaidi ya Yesu. Ilidaiwa kuwa aliweza kufufua wafu na hata kuamuru maisha ya mtu kubadilika kabisa. Uwezo huo ulisemekana kuvutia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi. Ilikuwa si ajabu kwamba magari ya kifahari zaidi ya 200 yalipaki nje ya kanisa hilo kubwa kila siku iliyopita. Yeye mwenyewe, Oyono alidai Yesu alitabiri ujio wake aliposema kuna watu watafanya mambo makubwa kuliko aliyofanya yeye. Alidai, kupitia mafunuo, Yesu alimweleza kuwa yeye ana uwezo wa zaidi ya watu million. Pia alikaririwa akisema neno la bwana limo ndani yake na hakuhitaji kusoma biblia, kwa sababu, kila siku bwana alitoa unabii juu ya watu wake kupitia yeye nabii wake baada ya Kristo.

Alidai alipewa unabii na mafunuo na bwana na kuagizwa aandae kitabu ambacho kinabadilisha maisha ya wanadamu alichokiita ‘kitabu cha unabii na mafunuo’. Kitabu hicho, alidai Oyono, Ni chanzo cha maarifa, mafanikio, uponyaji, utajiri na heshima.

‘Unataka kuwa na mafanikio kwenye masomo yako? Kazini kwako? Una afya mgogoro? Umaskini unakutafuna? Jibu lako lipo kwenye kitabu cha unabii na mafunuo. Kitakufungua minyororo iliyofunga maisha yako. Hujazaa na unatamani kupakata mtoto wako mwenyewe? U mrembo lakini huolewi? Kutana na majawabu ya yote hayo kupitia kitabu cha unabii na mafunuo. Mtume na nabii Oyono Goodness ameletwa na bwana kwa ajili yako. Njoo ukutane na muujiza wako’

Hilo lilikuwa moja ya matangazo yaliyosikika kila siku kupitia vyombo mbalimbali vya habari jijini.


‘Ndani ya kitabu hiki kuna mambo unayopaswa kuyafanya ambayo ni mafunuo kutoka kwa bwana. Yafanye mambo hayo kwa kufuata maelekezo yaliyomo ndani ya kitabu na baada ya siku kumi na moja baada ya kusoma kurasa zote 111 utaona muujiza wa kile unataka maishani mwako. Haijalishi dhehebu lako wala dini yako, imani yako na umakini wako katika kufuata maelekezo yaliyomo humu, itakukomboa, jihimu nunua kitabu cha unabii na mafunuo uone maisha yako yakibadilika’

Alisikika mtume na nabii katika moja ya kituo cha redio jijini. Redio ufunuo.

Kuhudhuria kwa Ana na Machera kanisani kwa mtume na nabii Oyono Goodness, yeye mwenyewe aliliita sinagogi au hekalu, kulitokana na fununu kuwa mtume huyo alikuwa miongoni mwa wale ambao The Don alidai walikuwa upande wake. Lakini pia walitaka kujionea kitabu cha unabii kilichokuwa gumzo jijini, baada ya kusikia matangazo redioni kuwa siku hiyo ungefanyika mnada wa nakala elfu moja za kitabu cha unabii na mafunuo.

Kama kawaida ya sinagogi la mtume na nabii, nje yalipaki magari utitiri ya waumini wa mtume na nabii Oyono Goodness. Ndani ya sinagogi zilisikika sauti za maelfu na maelfu ya watu wakimtukuza Mungu kwa nyimbo. Nyimbo zenye ujumbe mzuri ambao waumini hawakupata kuutafakari kama walivyoweza kutafakari maneno matamu ya matumaini ya mtume na nabii Oyono.

Waliingia ndani ya sinagogi wakitembea juu ya sakafu ya marumaru na kujichagulia sehemu ya kuketi katika kona ya kushoto ya sinagogi. Mbele yao kulikuwa na skrini kubwa iliyoonesha madhabahu safi iliyopambwa kwa vito vya thamani. Skrini ile ilitumika kuonyesha taswira ya mtume na nabii kwa wale waliokaa mbali na madhabahu.

Mapambio, nyimbo na kwaya mbalimbali vilitumbuiza kabla ya mtume kusimama. Aliposimama mtume na nabii alishangiliwa na maelfu ya waumini waliosimama kuonyesha heshima kubwa waliokuwa nayo kwa mtume wao. Katika hoi hoi na nderemo vikiwamo na vigelegele na vifijo zilisikika sauti tamu za kundi Fulani la waimbaji likiimba

"Mkombozi, mtume wa bwana, haleluya kwa mtume mkuu wa bwana" ilikuwa pambio.

Mtume hali amesimama madhabahuni, mbele ya kadamnasi, alitoa tabasamu mwanana halafu akabusu Pete kubwa aliovaa katika kidole cha mwisho cha mkono wake wa kulia na kunyoosha mkono wake wa kulia kuwaelekea waumini wake huku akigeuka pande zote kama baba anaewajali wanae wote asionyeshe upendeleo. Hapo zikasikika tena zile sauti za furaha zikimshangilia mtume na nabii Oyono.

Machera alikuwa anamwangalia kwa udadisi mtume, alishapitia kidogo historia ya kundi la wakina The Don, alikuja kugundua kwamba kundi hilo lilikuwa na ishara maalum zilizotumika kutambuana, ishara za kuona ufahari kuwa mwanachama.

Aliponyanyua mkono wake kusalimia waumini, mtume alionyesha ishara ambayo alijifunza kuwa ilimaanisha kujitambulisha kama mwanakundi. Kwa vile alifanya ishara ile kwa mara ya kwanza, Machera alidharau, hakuipa uzito. Huenda alifanya vile bila kujua maana. Hata hivyo mkononi alikuwa na kalamu, na yawezekana hiyo ndo ilifanya ishara ile kuonekana.

"Haleluyaaa!!Oh haleluyaaaaa!!!" Sauti ya mtume iliunguruma. Sauti nzito yenye mamlaka na ushawishi. Aliyatamka maneno hayo kwa mfululizo na kila alipoyatamka aliinyoosha mkono wake wenye pete kubwa na kwa makusudi akionyesha ile ishara kwa namna ambayo si kila mtu aliyegundua, huenda ni Machera na Ana tu waliogundua na huenda waligundua kwa sababu walienda kuchunguza.

"Haleluyaaaa!!!! Haleluyaaa"

Mtume alitamka tena, mara hii sauti ya waumini ikiitikia kwa sauti ya juu

"Ameeeen" na kumalizia kwa shangwe.

Alipomaliza kutamka maneno yale alimalizia kwa lugha ngeni. Hakuna mtu aliyeijua hiyo lugha. Wao walisema wananena kwa lugha. Si mtume pekee aliyeweza kunena kwa lugha, waumini wake pia walinena lugha kama ile lakini kila mtu akitumia lafudhi na hata maneno tofauti. Ilijulikana kwamba ni lugha muhimu kwa waumini Hao.

Alipoanza kunena kwa lugha ni kama mtume aliambukiza na waumini wanene pia. Sinagogi zima likawa linarindima kwa mchanganyiko wa lugha mbalimbali. Hapo wakina Machera walishuhudia watu wakijigaragaza sakafuni na wengine hali wakirusharusha miguu huku na huko walitoa kelele za ajabu na za maumivu. Hao ilisemekana walikuwa na mapepo. Walichukuliwa na kupelekwa ndani ya vyumba mle sinagogini kwa ajili ya maombezi zaidi.

Zoezi hilo liliendelea kwa muda wa robo saa hivi. Kwa muda wote huo Machera alikuwa macho akichunguza matendo ya mtume. Mara ikasikika sauti ya mtume kwenye maspika makubwa yaliyofanya kazi yake vema.

"Bwana amenipa taarifa, humu ndani wapo watu wawili, mwanamke na mwanamme. Watu hao wapo si kwa ajili ya ibada bali wana mambo yao mengine. Wamekuja kuchunguza nguvu ya bwana itendayo miiujiza. Kwa mamlaka niliyonayo, nawaamuru watu hao wapite mbele haraka sana kabla moto wa bwana kuwatafuna hapo walipo. Kwa usalama wenu, piteni mbele"

Machera alibaki mdomo wazi. Alijikuta anarejea mazungumzo aliofanya siku chache zilizopita na The Don. Alitambua alikuwa anadili na watu hatari sana. Akakumbuka kisa alichowahi kusikia hapo zamani kwamba kulikuwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao walitumia nguvu za giza ambao ulipoingia dukani mwao wao walikuona ukiwa mtupu, na kwamba kama isingekuwa hivyo wangekutimua kwa maana kwamba wewe ungelikuwa tishio kwa biashara zao. Sasa alijiuliza. Yawezekana sisi tunaonekana watupu mbele za mtume na nabii? Bila shaka mtume aliwazungumzia wao.

Kwamba wapite mbele? Wasingethubutu!

'Hizo ni janja janja tu!'Machera aliwaza.

Anastazia alikuwa kimya tu akimtazama Machera, alikuwa mbali kimawazo. Alimgusa begani, Machera akajikohosha uongo na kumtolea Ana tabasamu.

"Umemsikia mtume na nabii, ni kama anatuzungumzia sisi, so inakuwaje? "Ana alinong’ona.

"Achana nae huyo, anacheza na saikolojia za watu tu" Machera alitamka lakini hakuwa anaamini alichokisema. Akilini mwake maneno ya The Don yalikuwa yanajirudiarudia. Maneno aliyomweleza kwenye simu kuhusu microbiochip technology, Kwamba tayari wamevamia ubongo wake? Yawezekana kwamba hata hili ni matokeo ya kuvamiwa kwa ubongo wake? Alihisi kengele ya hatari. Asipokuwa makini atajikuta anachanganyikiwa. Moyoni mwake akajiambia

"Hebu tulia, tulizana, hakuna kitu hapo, huu ni ukanjanja tu"

Wakati akitafakari hayo minong’ono ya watu ilisikika, alipotazama skrini iliyokuwa mbele yake, aliona watu wawili. Mwanamke na mwanamme. Hao, walikuwa wanatetemeka na kulia. Wakionekana watu wasio na ujanja walisikika wakiomba msamaha huku wakigalagala sakafuni chini ya miguu ya mtume na nabii.

"Nilishasema usicheze na mimi, mnajua hawa wametoka wapi?" Mtume aliuliza umati wa watu.

"Kuzimu" zilisikika baadhi ya sauti.

"Watuelezeee" wengine walitamka.

"Hebu tuelezeni, mmefuata nini hapa?" Mtume aliunguruma. Bila shaka wakati wa kujipatia jina ulikuwa umejitokeza. Sauti yake ilijaa mamlaka. Mwanaume alikuwa mzee wa makamo hivi, lakini aliyejaa misuli vema. Kwa mbali mvi zilianza kutokeza kichwani mwake. Mashavu yake yaliyonona enzi za ujana sasa yalionekana kunyauka. Huku akitetemeka alianza kuongea.

"Tuhurumie bwana, turuhusu twende, tumekoma, hatutarudi tena, tunaunguaaa" sauti iliyolandana na pepo waliotimuliwa na Yesu kwa mujibu wa biblia na wakawaingia nguruwe ndiyo ilisikika kwa Mzee yule.

Mwanamke kwa upande wake alionekana akijongea sakafuni mithili ya nyoka huku akijikuna hapa na pale na kutokwa na povu mdomoni. Miaka 40 Hadi 45 Hivi. Ingawa Hakuwa na afya njema sana, lakini mavazi na haiba yake vilionesha alikuwa si mtu shida shida upande wa fedha.

Waumini walibaki wanastaajabia yaliyokuwa yanatendeka pale altareni. Kila mtu alionekana kuelekeza mawazo yake penye tukio.

"Mmetoka wapi" mtume aliendelea kuhoji.

"Shimoni, tumetoka shimoni, tumetumwa kuiba siri za kitabu cha unabii na mafunuo. Tumetumwa tuziibe na kuziharibu kabisa" Mwanaume alitamka kwa sauti ya kukatika-katika mithili ya mtu aliyetiwa kitanzi shingoni.

"Ha ha ha a" mtume aliangua kicheko kwa sauti kubwa.

"Eti kuiba siri za kitabu cha unabii na mafunuo. Ha ha ha" Ilikuwa sauti ya kicheko iliyoashiria kusema kama kuna mwingine huko, hii ni onyo. Cheko la dhihaka!

"Hawa ni sawa na bahasha, ndani ya bahasha mnawekwa barua ambayo inakuwa inatumwa kwa aliyekusudiwa. Hivyo sina shida na hizi bahasha, shida yangu ni barua ambayo ina ujumbe kutoka kwa nani? Adui. Kwa hiyo ninatumia mamlaka niliyopewa kuamuru ujumbe uliomo ndani yao utoke na wabaki huru, haleluyaa"

"Ameen" waumini waliitikia

"Kaeni tayari kushuhudia muujiza. Muujiza wa ajabu." Alitamka mtume na halafu akaendelea

"Wajumbe wa uharibifu wa mipango ya bwana wajumbe mlio ndani ya watu hawa, kwa ishara ya ushindi ya bwana, naawaamuru, toka ndani yao." Alipotamka maneno ‘ishara ya ushindi wa bwana’ mtume aliitazama sanamu ya nyoka msalabani iliyokuwamo mle madhabahuni. Kidogo hilo likamtatiza Machera. Sanamu ya nyoka msalabani? Ndani ya hekalu? Tangu akiwa mtoto aliaminishwa kuwa nyoka ni ishara ya shetani, sasa inakuwaje leo iwe ni alama ya ibada? Na vipi kuhusu wale ambao walionyesha mfano wa Yesu msalabani? Nini hasa ilikuwa alama sahihi ya ibada? Hilo lilihitaji kufanyiwa utafiti. Aliamua kuliweka pembeni kwanza.

Wale watu waliokuwa "mabahasha" wakigaagaa miguni pa mtume ghafula walianza kutapika. Kilichoshangaza wengi ni kilichotapikwa. Tu-nyoka. Nyoka wadogo wadogo mithili ya minyoo aina ya ascariasis wakiwa hai wakitoka vinywani mwa binadamu hai. Huu ulikuwa ni muujiza wa aina yake. Kila mtu alishikwa na butwaa. Minong’ono ikisikika hapa na pale

" Sasa huyu ndio mtume wa kweli. Tazama, si nyoka kabisa wale!."Kijana mmoja alihoji. Bila shaka alikuwa mgeni.

"Sasa wewe unashangaa hiyo! Juzi tu alifikishwa mgonjwa mahututi hapa, kakonda utadhani hajala miaka kadhaa, mahospitalini walidai walishashindwa kumtibu. Ugonjwa pekee waliouona ni kukonda. Unajua kulitokea nini? Vyura! Vyura wadogo wadogo wakiruka ruka madhabahuni, tena wakitoa ile misauti yao inayokera kama nini!! Sasa, unaona lile beseni limenunuliwa juzi juzi tu kwa ajili ya watu kutapikia, na pembeni pale kuna pipa la kuwateketeza hao mapepo." Alinong’ona kijana wa pili, huyu alikuwa mwenyeji wa sinagogi hili.

Ana aliwasikiliza vema wale vijana na kujikuta anauliza swali

"Eti wakishatolewa mapepo, hao watu wanakwenda wapi?" lilikuwa swali la kipuuzi lakini likitafuta maana.

"Wanakwenda wapi? Wataenda wapi wakati sinagogi hili linakuwa limewaweka huru. Wote wanabaki humu. Mtume huwa anasema hakuna watu wanaonea njaa na kiu kitabu cha unabii na mafunuo kama hao watu" alijibu kijana wa pili.

"Oh, unajua mimi ni mgeni kabisa humu, hivi nilisikia habari za hicho kitabu nikasema hebu na mimi nifike huko. Sasa unaweza kuniazima hicho kitabu ndugu yangu niione hata yaliyomo tu?" Ana alihoji.

"Hapana, kwanza kabisa hairuhusiwi kuazima, kwa kufanya hivyo kitabu hakitakusaidia. Mtume anapenda ugharimie kwa sababu hata dhambi zetu ziligharimiwa kwa damu. Ni muhimu kununua. Kwa sasa mimi sina ila nafanya bidii nipate nakala yangu hivi karibuni. Ukishanunua utahitaji kuhudhuria semina ya jinsi ya kutumia nabii na mafunuo yaliyomo ndani ya kitabu hicho." Ana alijibiwa na hata kujikuta anapata na maelezo ya zaidi.

Binadamu kweli tunatofautiana, swali moja linaweza kuwa na majibu sahihi tofauti, wengine wamejaliwa kuongea.

"Kinauzwa bei gani….?’ Ana aliuliza na hata kabla ya kumalizia sentensi majibu yalianza kutiririka kutoka kwa kijana Yule aliyekuwa amevaa jeans mpauko na tshirt fulani hivi za zamani zenye manamba makubwa kifuani na mgongoni, zikiwa na mwonekano wa wavu. Kwa muda sasa t-shirt hizo zilikuwa zimepotea sokoni, ni mara chache ungemkuta kijana anaedai anaenda na wakati akiwa amezivaa. Huenda Huyu alikuwa anatokea kwenye koo za wahenga.

"Inatofautiana, waumini wa sinagogi ni shilingi laki moja tu na unakuwa na uhakika wa kuirejesha fedha hiyo baada ya mwezi mmoja, kwa watu wengine wanaotafuta kufanikiwa ni laki moja na ishirini tu. Wote hao hulazimika kulipia semina ya matumizi ya kitabu shilingi elfu ishirini tu."

"Ni ghali lakini!?"

"Hapana, ukilinganisha na matokeo! Wala si ghali" Hapo tena ilifuatia simulizi. Kijana Huyu alistahili malipo kwa jinsi alivyojua kumpamba mtume na nabii Oyono Goodness.

"Ndugu mmoja aliingia hapa sinagogini miaka miwili iliyopita akiwa amevaa ndala miguuni. Huwezi amini alipokuwa anatoa ushuhuda alieleza alichofanya na akawa ametubariki kweli.

Hapo sasa ikawa ni mwanzo wa simulizi, Yule kijana akisimulia kama vile alitarajia mshahara baada ya maelezo yake. Alikuwa msimulizi hasa wa habari! Mtume alikuwa amejipanga, kwa hadithi hizi na zinginezo nani angekataa kutoa moyo wake na waleti yake kupokea muujiza na Baraka zilizopatikana hekaluni kwake?

Simulizi iliendelea;


ITAENDELEA....
 
IX


ALIPOANZA kuhubiri, mtume alitoa kichwa cha somo. Machera kama walivyofanya waumini wengine alichukua kalamu yake na notebook na kuandika

‘MUNGU WA WOTE’


Katika mahubiri yote aliyowahi kusikia, Machera alikubali kwamba mtume na nabii Oyono alijaliwa ‘lugha tamu sana’. Bila shaka alikuwa mtu anayejua alichotaka na jinsi ya kukipata. Alijua nini waumini wake walitaka na aliwapatia hicho. Ikawa ni nipe nikupe. Maridadi kabisa.

Si ajabu kwamba mtume alitumia usafiri wa ghali sana akiendesha gari aina ya Hammer na kuzingirwa na magari kadhaa na walinzi binafsi almaarufu 'bodyguards'. Msafara wake ukikaribia ule wa mkuu wa nchi.

Oyono alikuwa bepari hasa! Kwa utafiti wa haraka tu, Machera alibaini kuwa Oyono alimiliki ranches kubwa katika mikoa ya Arusha, Singida, Mara na Dodoma. Mtume alimiliki mapande makubwa ya ardhi karibu kila mkoa huku akisimamisha mahoteli ya kitalii kama uyoga. Tetesi mitaani zikaenea, mtume alimiliki vitalu vya thamani kwenye migodi ya madini huko Mererani, Geita na North Mara.

Oyono Goodness. Huyu alikuwa mtu mwenye mipango yake. Hata lugha yake ilipangiliwa kurejesha gharama ya kila neno alilotamka. Waumini waliokuwa na kiu ya mafanikio walikuwa mtaji tosha. Hao walichanga vijisenti vyao na kuvipeleka kwa mtume, aliyevipokea kwa shukrani na kuwamwagia mibaraka tele. Wenye imani wakavuna mafanikio. Wenye imani haba wakazidi kulowea kwenye umaskini wa kutisha. Na kwa nini wasipeleke kwa mtume ilhali umaskini wao uliwaelemea na yeye alikuwa ni mkombozi wao akiwapa habari njema. Habari za mafanikio. Habari za matumaini ya mafanikio, waliolala wakayaota na walipoamka wakayatafakari! Habari za unabii na mafunuo!

Kwa sehemu kubwa jina la Oyono lilikuwa ni mada katika mitaa ya jiji la Dar es salaam. Wanasiasa, wasomi, walalahoi na wachambuzi wa mambo, wote walijadili kwa namna moja au nyingine habari za mtume huyo.


***

Oyono Goodness, raia kwa kuzaliwa wa Nigeria ambaye aliutupilia mbali uraia huo baada ya kugundua nchi yake ilijaa wajanja wengi na labda kama wasemavyo ‘nabii hakubaliki kwao’, Sasa alikuwa ni raia halali wa Tanzania akiwa na haki zote za raia wa Tanzania. Alifanyika Baraka kwa watanzania wazawa, ambao kwa hiari na labda kwa ujinga wao walishindwa kutumia raslimali zao wakiwaachia wageni kutoka ulaya na Marekani. Akiwa mtu mwenye kuona mbali na kutamani mazuri, Oyono aliona fursa ya mafanikio Tanzania. Elimu yake na uwezo wa kifedha aliokuwa nao ulikuwa mdogo mno kumwezesha kuwekeza nchini. Lakini kitu kimoja alijua. Hakukuwa na mafanikio nje ya watu. Watu walikuwa mtaji. Alisoma biashara zilizohusisha watu. Hakuna biashara ambayo angeiweza zaidi ya kutumia maneno.

Utafiti wake ukamuonesha kwamba, kadri maisha yalivyozidi kuwasonga watu, ndivyo walivyozidi kuwa na sonona. Wengine hata kufikia hatua ya kujinyonga na kujiua. Hilo halikumpendeza. Kwa nini watu wafe kwa sababu tu ya kukosa tumaini. Hapo aligundua kitu. Watu walihitaji neno la tumaini. Hii ilikuwa nafasi pekee ambayo angeweza kufanikiwa kwayo. Saidia watu wakusaidie. Hiyo ikawa falsafa yake. Bila hiyana, akaanzisha kituo cha kutoa ushauri na msaada kwa watu waliosumbuliwa na matatizo mbalimbali ya msongo wa mawazo na sonona. Kwa muda wa mwaka mmoja akagundua kulikuwa na kitu cha zaidi kilichofanya maisha ya watu yawe sawa.

Mungu.

Ushauri ukaongezewa kionjo kipya. Habari za matumaini kutoka kwa Mungu, ushauri ukaanza, maombezi yakamalizia. Hilo likawa ni chanzo cha kumiminika kwa watu kituoni kwake. Pesa zikaongezeka. Akaamua apate ukumbi kuwahudumia wateja wengi kwa wakati mmoja. Kutahamaki, akaja kugundua ana kipaji cha kuongea kwa ushawishi na kwa busara. Akajenga ujasiri, taratibu kituo kikawa ni ukumbi akiwa na wateja zaidi ya mia kwa siku. Wengine wakihudhuria kila siku kupata mawaidha yake yalioonekana kuwasaidia. Mwisho wa siku, Oyono si mshauri tena! Kituo si kituo. Ikajulikana ni kituo cha kiroho na maombezi. Akazichanga na kupata uwanja, huko akajenga kanisa akaliita Sinagogi.

Kanisa lake likapata jina jijini. Watu wakamiminika kila siku kwa ajili ya kufanyiwa maombezi. Watu wa kada mbalimbali wakadai kupokea miujiza kwa mtume. Wanasiasa kwa wananchi wa kawaida, wasomi kwa mambumbumbu, wamama kwa wababa, vijana na watoto. Wengi wakamiliki ‘ishara ya ushindi wa bwana’ na wakashuhudia kufanikiwa kwa kufanya maombi kupitia hiyo. Wakadai ishara hiyo iliondoa kabisa mikosi na balaa majumbani mwao. Wakasema nuksi na vikwazo makazini mwao sasa vilikuwa ni historia.


***


Machera akiwa anatafakari yote hayo simu yake ya mkononi ilianza kutetemeka, akashituka, taratibu akaichomoa mfukoni mwake. Namba ngeni ilikuwa inacheza kwenye skrini. Ghafula akakumbuka maneno ya The Don, ‘kadri unavyoendelea kunisikiliza ndo tunavyozidi kushambulia uwezo wako wa kufikiri'.Kidogo akahisi woga, kukubali kutishiwa ingekuwa kujitia kitanzi shingoni. Lakini kama The Don alikuwa anasema ukweli? Hakuwa tayari kupoteza uwezo wake hata kwa nukta moja. Hali hii ilimpa wasiwasi mkubwa. Kama adui zake wataamua kutumia njia hii ya mawasiliano itakuwaje? Tayari alikuwa keshakosana na boss wake mmoja baada ya kuipuuza simu yake kwa kuhisi ni janja ya The Don. Kama hali itaendelea hivi itakuwaje? Kama atapuuza onyo la The Don matokeo yanaweza kuwa mabaya zaidi. Lakini kama atalizingatia, tayari alishaanza kuona matokeo yake.

Aliitazama simu yake kwa wasiwasi mkubwa. Walitakiwa kufanya kitu. Ikiwezekana kubadili hata namba. Alitafakari na kuona bado haingesaidia kitu. Kwani namba yake hii waliipata vipi? Hakujua. Inawezekana wana watu wao miongoni mwa maboss wake.

Muda ulisonga mbele, simu ilikuwa imeita na kukatika mara tatu sasa na bado ilikuwa inatetema kwa mara ya nne.

Alimshika Ana mkono na kumuashiria watoke nje ya sinagogi.

"Lakini mnada wa kitabu cha unabii na mafunuo utafanyika baadae, tukiondoka unadhani itakuwaje?"Ana alinong’ona. Machera alimtazama kama kwa kumshangaa.

"Utumie laki moja na arobaini kwa ajili ya kitabu chenye kurasa mia moja na moja cha unabii na mafunuo?" Machera alinong’ona kwa mshangao zaidi.

"Tumefuata nini hapa machera?" Ana alimtupia swali na wakati huo akamshuhudia Machera akinyanyuka.

"Bado hujapata ulichofuata? Nitakueleza njiani, Kwa sasa kuna simu ya muhimu hapa" alimwonyesha simu iliyokuwa bado inatetema.

Walitoka nje ya sinagogi. Baada ya kuingia kwenye gari lao Machera alimpa Anastazia simu. Anastazia aliipokea simu na kusikiliza. Machera akimwangalia kwa shauku ya kutaka kujua kulikuwa na habari gani. Kadri alivyozidi kumtazama ndivyo alivyojua kulikuwa na habari mbaya.

"Ni nini?" Machera aliuliza kwa shauku iliyochanganyika na wasiwasi.

"Kuna mauaji yametokea" Ana alitamka huku akionyesha huzuni kubwa.

"Nani?"

"Mkurugenzi wa HRO"

"What? Umesikiliza vizuri? Machera aliuliza, safari hii alishindwa kuficha hisia zake na hata ule wasiwasi wake sasa ulisomeka vizuri kabisa kwenye sura yake. Kajasho kalianza kuonekana kwenye ngozi yake angavu, yenye weusi wa kibantu halisi.

"Maisha?" halikuwa swali, ilikuwa ombolezo. Ombolezo kutoka moyoni, hii ilikuwa ngumu kuliko kawaida.

"Ameuwawa kwa kuchinjwa shingo" Ana aliongea kwa upole.

Machera alihisi tumbo likikata na kuishiwa nguvu kabisa. Maisha alikuwa zaidi ya rafiki, alikuwa kama ndugu, mshirika wa kweli. Sasa alianza kuona ni vita gani alikuwa anakabili. The Don alimwambia ni vita aliyokuwa anapigana na nafsi yake, yeye mwenyewe.

Maisha alikuwa kapitia misukosuko mingi sana hasa baada ya kuweka bayana nia yake ya kupambana na mafisadi na wahujumu nchi. Wakina The Don. Mara ya mwisho aliokolewa na Machera wakati ambapo alikuwa anahesabu dakika tu kabla ya kuchinjwa kama sadaka na The Don.

Kama mkurugenzi wa HRO, Maisha alikuwa kikwazo dhidi ya mipango ya kundi la wakina The Don, kundi ambalo kwa sehemu kubwa lilishika usukani wa shirika hilo kubwa la haki za binadamu duniani.

Mara kadhaa alipinga mapendekezo ya watu hao waliotaka kuingiza haki za kimagharibi hapa Tanzania, haki ambazo alizikataa kwa sababu hazikukubalika na tamaduni za watanzania wote. Haki za kutetea mtu mmoja mmoja kwa sababu tu anataka kufanya mambo ambayo yalikuwa kinyume na tamaduni na ustaarabu wa mwafrika.

Kwa muda sasa akawa ni kikwazo kiasi cha kujijengea maadui wakubwa kwa wadogo ndani na nje ya taasisi hiyo maarufu duniani iliyokuwa imepelekea mataifa mengi duniani kuruhusu ndoa za jinsia moja ikiwamo Afrika kusini kwa upande wa Afrika huku kukiwa na vuguvugu la kuelekea huko nchini Malawi.

Taarifa za kuuwawa kwa maisha kwa kuchinjwa kwanza zilikuwa tisho kwa Machera. Ilikuwa ni kama kusema ‘umeona? Mwenzio akinyolewa wewe tia maji’. Pili, ilikuwa habari ya majonzi kumpoteza mtu wa karibu katika maisha na katika vita.

Bila shaka vita yenyewe aliyozungumzia The Don ndio kwanza ilikuwa inaanza. The Don alikuwa ameanza kuwashambulia watu wa karibu wa Machera. Swali sasa likabaki, ni nani atafuata?

Walitia gari moto kuelekea eneo la tukio. Kwa taarifa walizopewa, tukio lilitokea maeneo ya mbande katika shamba la marehemu.

Walipofika mbagala rangi tatu, gari lao lilizingirwa na pikipiki za maafisa wa usalama barabarani. Afande mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ndimbo aliwaamuru kupaki gari pembeni. Kwa haraka waliokuwa nayo isingekuwa rahisi.

"Afande tupo kazini hapa kuna tukio tunawahi Mbande" Machera alimweleza afande Ndimbo huku akimuonyesha kitambulisho chake. Ndimbo alitoa saluti na kupisha gari lao lililoondoka kwa kasi.

Eneo la tukio, tayari kulikuwa na askari waliokuwa wamefika kufanya tathmini na uchunguzi wa tukio hilo baya. Kwa taarifa walizopewa, ni kwamba vijana wa kundi lilojulikana kama Al-haki fighters ndo walikuwa wametekeleza tukio hilo la kinyama.

Akilini mwake Machera alijaribu kutafakari hali ya kutenganishwa kichwa na kiwiliwili kwa mwili wa mpambanaji mwenzake Maisha. Machozi yalimtoka Machera alipoushuhudia uliokuwa mwili wa Maisha, ukiwa umetenganishwa kichwa na kiwili wili mithili ya kuku wa kitoweo, taswira iliyotokeza akilini mwake. Jambo hili lisingepita hivihivi, Machera aliapa moyoni mwake.

Tukio la kuuwawa kwa Maisha kwa sababu eti alisimama kupinga harakati za kundi la Al-haki fighters pale alipolaani kitendo cha kupigwa mawe mwanamke Amina aliyetuhumiwa kwa uzinzi huko Zanzibar halikumwingia akilini.

Uchunguzi wa awali wa kifo cha Maisha ulionesha kuwa tukio la kuuwawa kwa Maisha halikuwa la kidini tu bali pia la kisiasa ambapo Maisha alionekana kuingilia maslahi ya chama cha A.S.R.P kwa kukituhumu kuchochea ghasia visiwani Zanzibar na kupelekea kuwepo hisia za udini miongoni mwa raia. Ilidaiwa kuwa kitendo hicho kilisababisha wafadhili wa chama hicho kujiuliza kwanza juu ya kuendelea kukipatia ufadhili au la, hasa wafadhili wa chama hicho kutoka ulaya, walioamini wanasaidia kuinua demokrasia nchini Tanzania.

Hata hivyo, chanzo cha kifo cha Maisha kilikuwa bayana kwenye fikra za Machera, alijua ilikuwa ni kazi ya Don. Ilikuwa kazi ya Don na tayari Maisha alikuwa kwenye orodha ya wabaya wa Don waliopaswa kushugulikiwa kwa kifo. Kifo cha kuchinjwa ilikuwa ni ibada ya Don, Maisha alikuwa ametolewa kafara.


Vuguvugu la Don ambalo walikuwa kwenye harakati ya kulizuia, kuhusisha dini na siasa, moshi ulianza kufuka. Don alikuwa hatua moja mbele.

ITAENDELEA.....
 
X



AFANDE Ndimbo alichepuka na kuingia mitaa kadhaa kutoka pale barabarani walikokuwa wanaendelea na kazi yao ya kuhakikisha usalama barabarani. Alichomoa Simu yake ya tochi, aina ya tekno, zile ndogo ambazo sio janja. Akabonyeza tarakimu kadhaa halafu akaipachika sikioni. Simu ikawa inaita kwa muda kabla ya kupokelewa

"Naam Ndimbo, nipe habari!" Ilisikika sauti toka kwenye spika za Simu ile.

"Wamepita sasa hivi Mkuu. Wanaelekea Mbande. Gari ni Lexus RX nyeusi T123 DNS. Ina abiria wawili, wa kiume na kike. Sura ni zile ulizonionyesha. Kazi kwako boss!" Ndimbo alijibu na kukata Simu.

Alirejea tena barabarani na kuaga wenzake kuwa amepata Ujumbe wa kurejea kituoni. Akatembea mwendo wa haraka haraka kulielekea Gari lake lililopakiwa umbali wa mitaa kadhaa toka walipokuwa wamesimama. Akazama ndani, akaitenya starter, injini ikakohoa akaingiza Gia na kuliondoa Gari hilo Toyota spacio kwa mwendo wa Usain Bolt.


***

Walikuwa wanaiacha Chamazi wakiitazamia Mbande, ghafula akajitokeza mtoto mdogo umri wa kukadiria miaka 8 hadi 10 hivi akiingia barabarani Bila tahadhari. Dereva akapambana na breki ili kuokoa maisha ya mtoto yule. Tairi zikanyanyasika na kutia maombolezo yaliyoushitua umma uliokuwa maeneo Jirani. Watu wakimiminika kushuhudia kelele zile za tairi zilimaanisha nini. Mtoto alikuwa kaguswa kidogo na ubavu wa Gari lile na labda kwa mshituko alionekana kama amezima. Machera akateremka kwenye Gari na kumuwahi mvulana yule. Anastazia naye hakubaki nyuma. Aliteremka huku kashika kichwa kwa masikitiko, mdomo ukitengeneza ‘O’ ya bumbuwazi. Kadamnasi ile sasa ilikuwa imezingira eneo lile kukionekana Kila dalili ya kuanzishwa vurumai.

Wananchi wenye hasira Kali. Miongoni mwao alikuwemo kijana mmoja. Alivalia hood la kijivu lililofunika kichwa. Huyu alikuwepo hapa kwa jukumu maalum. Wakati wananchi wengine wakiwa kwenye harakati za kujua hali ya mvulana yule aliyegongwa, Huyu alionekana akizunguka nyuma ya Gari la Machera na wenzake. Kosa walilofanya ni kuacha mlango wa Gari lile wazi. Jamaa yule alitazama huku na huku, alipojihakikishia kuwa yuko huru kufanya alichokusudia Bila mtu kumtilia shaka, alifungua mlango wa Gari uliokuwa umerudishiwa tu na kuzama ndani, kwa wepesi ulioonesha si mtu hivi hivi, alihifadhi kifuko cha kaki eneo nyeti kwenye Gari na kama vile hakuwepo akapotea eneo la tukio.

Machera alimbeba yule mtoto na kumpima mapigo ya moyo, akayasikia kwa mbali, akamfanyia CPR, kumpulizia pumzi mdomoni ili kurejesha uhai. Mtoto akatoa chafya. Akazinduka na kupata uhai akiwa na mawenge hasa kutokana na umati ule uliokuwa umemzingira. Kelele za wananchi wenye hasira zikipungua kuona mtoto yu Hai bado.

Machera akambeba mtoto mikononi mwake. Akawa anawaza kumuwahisha kituo cha afya Mbande. Lakini akiwa bado anatafakari hayo akasikia sauti ya kike aliyoifahamu vema ikihoji kadamnasi ile;

"Kuna ndugu yeyote wa mtoto huyu hapa? Kama yupo ajitokeze ili tumpeleke kituo cha afya kwa huduma zaidi."

Aliponyamaza kuongea tu alijitokeza mama wa mtoto, mwanamke wa miaka thelathin hivi na kidogo.

Ilikuwa waingie kwenye Gari waendelee na safari alipojitokeza mwanaume mwenye miraba minne, Huyu alionekana kujawa Shari tupu.

"Mnadhani mnaenda wapi nyie wauaji, mnaendesha magari kwa mwendokasi kwenye makazi ya watu, mnadhani wanaishi wanyama huku sivyo?" Jamaa alikohoa maneno, akibenua midomo yake kwa hasira huku kidole chake kikimsonta Machera kifuani kiasi cha kusababisha maumivu.

Hasira ikamwingia Machera akajaribu kuukamata mkono wa mwanaume yule mwenye kujaa Shari! Hilo lilikuwa kosa, mwanaume yule akatafsiri hasira na kitendo cha kukamatwa mkono kama tangazo la vita. Akaikusanya ngumi yake na kuijaza ujazo wa kilo kadhaa na kumshushia Machera usoni, pua ya Machera ikavunjika huku damu zikivuja kwa fujo. Mwanaume yule aliyekuwa anashangiliwa sasa na kadamnasi kwa kitendo cha kumwadhibu, alikuwa sasa anajitapa kwa kujigonga gonga na ngumi yake kifuani kwake.

Alikuwa ashushe ngumi ya pili yenye ujazo wa kilo kadhaa kwenye paji la Machera kilipotokea kisichotarajiwa. Mwanaume yule alidondoka hatua kadhaa kwenye mtaro akianguka na watu kadhaa kwa pigo ambalo Machera alilitoa kwa kukita goti lake panapo kidevu cha Mangulu, yule mwanaume jeuri.

Jamaa akazima.

Huku akijifuta damu puani kwa kitambaa alichopewa na Anastazia, Machera alimnyanyua mtoto na kulielekea Gari. Hapo ndipo kilipotokea kitu kingine tena kisichotarajiwa. Mlipuko mkubwa ukasikika huku Machera na watu wengine kadhaa wakirushwa mbali na Gari, moshi mzito mweusi ukitanda eneo lote la tukio. Ilikuwa mlipuko wa Bomu. Bomu likaimeza Gari ile na kuifutilia mbali. Ni kama hakukuwa na Gari mahali pale.

Hata hivyo, Machera na mwenzake Anastazia walinisurika wakiwa na majeraha ya michubuko midogo midogo kwenye miili yao kutokana na kuruka kule walikorushwa na mlipuko. Baada ya muda, Gari la traffic likawasili mahali pale kuangalia matokeo ya ajali.

Walikufa raia wasio na hatia watatu akiwemo na yule mtoto! Majeruhi wakiwa wengi kufikia thelethini na ushei hivi!


***

Joze Kijo, Ndo jina lake. Mara baada ya kukamilisha kazi yake ya kutega Bomu na kuondoka eneo la tukio. Alibonyeza namba kadhaa kwenye Simu yake, tekno sawa na ile ya Afande Ndimbo. Namba alizobonyeza ndio zile zile alizobonyeza Afande Ndimbo. Simu iliita kwa muda halafu ikapokelewa.

"Joze Kijo, nipe habari!" Ilisikika sauti kwenye spika za tekno ya tochi kama zilivyofahamika uswahilini Simu hizo.

"Kazi imefanyika kama ilivyokusudiwa. Naamini watakuwa wamepotea. Hapa mambo ni moto faya, kazi kazi bosi." Joze Kijo aliongea akionesha kufurahishwa na kazi yake aliyofanya kwa ufanisi mkubwa.

"Vema." Sauti ile ikajibu na kukata Simu.


***

Gari za wagonjwa(Ambulance) kadhaa zilifika eneo la tukio na kuwawahisha hospitalini baadhi ya majeruhi waliokuwa eneo la tukio.

Wakijua hatari iliyokuwa inawakabili, Machera na Anastazia walikodi bajaj na kurejea mjini. Walibaini kwenda Mbande kusingewaepusha na hasira za Don. Ilikuwa wazi sasa!

Kifo cha Maisha ulikuwa mkono wa Don, ajali ile pia ilikuwa kazi ya Don, na hata mlipuko ule ulikuwa ni kazi ya Don. Walipaswa kuchikichia mitini. Kwa ajali ile, kulikuwa na sababu za wategaji Bomu kuamini wametekeleza kazi yao kama ilivyokusudiwa. Ni kwa wazo hilo, ndio waliamua kubadili utaratibu, kuondoka haraka eneo lile ili wabaya wao watakaporejea wawe na fikra kwamba wamekufa. Bajaj ile ikitokea Mbande sasa ilikolea spidi kurudi Chamazi. Ambacho hawakujua ni kwamba wakati wanaingia kwenye bajaj, kulikuwa na jicho la pekee eneo lile likiwatazama wanapoondoka, jicho la kibaraka wa Don, Afande Ndimbo!


***

Ikulu, Dar

Masebo, rais wa jamhuri alikuwa kwenye hali iliyofanania maombolezo. Kwa siku mbili hizo alikuwa haoneshi tabasamu hata kidogo. Don alimshika pabaya. Pabaya hasa! Kiasi cha kumfanya akose raha kabisa.

Leo hakuingia ofisini, alishinda hospitalini akimuuguza mkewe ambaye mshituko aliopata usiku ule wa kimuhemuhe, ulitishia kumsababishia kiharusi. Madaktari bingwa wakijaribu kuirejesha afya yake kwenye mstari. Lakini zaidi, alikuwa hapa kukwepa kile ambacho kingeweza kutokea kama angeamka na kusema yale ambayo yalipaswa kuwa siri yake yeye pekee. Siri ambayo kuvuja kwake kulipelekea Mke wake kulala hapo akiwa hajitambui kwa zaidi ya masaa 30 na ushei sasa.

Mipango iliendelea kuratibiwa kumhamishia India kwa matibabu ya kina. Akiwa hapo, akiwaza hili na lile, Simu yake ikaita, akaishika na kuitazama akiwa na hasira wazi wazi.

"Unafurahia sana kunifanyia huu ukatili sio, sikiliza wewe mpuuzi.." Hakumalizia kwani aliisikia sauti ya Machera.

"Mheshimiwa, sielewi...."

"Oh, Machera kijana wangu, Dah hii ofisi itaniwehusha sasa. Vipi kijana, salama?" Masebo akaongea akijaribu kuficha mshituko wake.

“Mkuu, naona hatari zinazidi kuniandama, hivi nimeponea chupu chupu kupotezwa na watu wa Don. Huyu mtu hana simile hata kidogo. Nadhani Nahitaji kuingia mafichoni kwa muda ili wajue nimekufa napojipanga upya." Machera akatoa mapendekezo yake.

"Sawa sawa kijana wangu, kuna mtu mwingine anayejua taarifa hii?" Masebo akauliza.

"Hapana Mkuu ila..." Kabla hajamaliza Masebo akadakia.

"Vema ibaki hivyo, kwa sasa ni hatari kushirikisha watu wengine. Endelea kubaki mafichoni na ukiona lolote lisiloeleweka nijulishe. Ni vema pia uwe na namba wasiyojua watu ili iwe kwa mawasiliano kati yangu na wewe. Mie pia nna hofu kunaweza kuwa na mamluki ofisini kwangu na kwa wasaidizi wangu. Hivyo ni vema uendelee kutumia hii namba yangu ambayo ni kwa matumizi binafsi haihitaji kuhakikiwa na mtu." Mheshimiwa Masebo akapendekeza. Wakazungumza mengi na kuweka mikakati kadhaa dhidi ya adui.


***

Nusu SAA baada ya mazungumzo na Machera, mheshimiwa Masebo akapokea Simu, namba ya Don, aliihifadhi baada ya kuzungumza na Machera na kubaini kosa alilofanya awali alipombwatukia kijana Huyo kwa kumdhania ni Mabruki.

"Nakusikiliza" alijibu Masebo akionesha namna gani alivyochoshwa na upuuzi wa Don.

"Na unisikilize vema!" Akaunguruma Mabruki.

"Sikujua kama ungeweza kujishusha chini kwa kiwango hicho Mabruki, umethubutu kumfanyia mtoto wa binamu yako ukatili huo ...." Masebo hakumaliza sentensi yake. Mabruki akamkatisha kwa karipio Kali.

"Cut the crap, you should know I can do worse than that. (Hebu niondolee upuuzi hapa, naweza kufanya ubaya kuliko hilo) Unajua wewe nimekulealea sana na ukasahau kuwa undugu hauegemei upande mmoja. Ulitaka kunipoteza mazima, kuniaibisha kwenye umati, na hukuwaza kuwa mie ndugu yako. Leo ndio unakumbuka? Swine (nguruwe) wewe. Let me remind you that you're in no position to claim anything right now, all you have to do is listen to me, and perhaps I might spare your bloody ass like I have done for quite long. You surely don't know where to poke your nose, do you? (na labda nikukumbushe tu kuwa hauko kwenye nafasi ya kudai chochote, unachopaswa kufanya ni kunisikiliza Mimi, huenda nikakuonea huruma kama ambavyo nimefanya siku zote hizi. Inaonekana hujui kwa kunusisha hizo pua zako, sivyo?" Alimpa nafasi Masebo kusema kitu.

Kimya.

Alipotaka kusema kitu, akasikia sauti ya Masebo ikitamka kwa kiwango cha juu sana cha chuki.

"I'm going to kill you bastard, I'm going to kill you!” (Naapa nitakuua wewe, nitakuua mwanaharamu wewe) Kilio. Kilio kikasikika.

"Not before I'm done with you cousin, no! No! No! you wanted this on yourself bro (si kabla ya kukushughulikia kwanza, hapana, kamwe, hili ulilitaka wewe mwenyewe), hivyo nyamaza kimya na unisikilize Mimi." Mabruki alikuwa na ujasiri wote wa kusema na hata kufanya lolote. Ndiyo! Lolote alilotaka, Masebo Hakuwa na namna. Mke wake kipenzi alikuwa kitandani sababu ya Mabruki, mwanae, binti yake wa pekee Hellena, alikuwa mikononi mwa Don na genge lake wakitishia kumuua kama asipotekeleza matakwa yake.

Mamlaka yake kama Mkuu wa nchi yalikuwa wapi kumsaidia?. Alikuwa hana msaada wowote licha ya kuwa na majeshi yote chini yake. Licha ya kuwa mtu mwenye mamlaka na nguvu kuliko yeyote yule nchini. Machozi yakamtoka! Mwanaume akalia.

"Yule mbwa wako mtiifu amekwepa mishale yangu mingi sana. Inavyoonekana ameijulia vema akili yangu. Nakiri kumuwinda imekuwa changamoto kwangu. Lakini katika kutafakari kwangu nikajua Mie pia Nina mbwa wengi sana lakini wote wameshindwa kumtia mikononi kwangu. Nataka wewe umlete kwangu. Binamu nakupa siku mbili. Maisha yake kwa maisha ya mwanetu mpenzi Helen. And mind you, she shouldn't have to know I was involved, my plan is to be a hero, I'm going to be the one that rescues her, if you know what I'm saying. (zingatia hili, tukishakumuokoa hapaswi kujua kuhusika kwangu, natarajia kuwa mjomba wake shujaa, kwa sababu ni Mimi nitakayemuokoa mikononi mwa watekaji kama unaelewa nachozungumza) Mabruki hakusubiri kujibiwa. Akaikata Simu!

"Damn you, bastard!" Masebo akabwata lakini ikawa bure. Upande wa pili ulikwishaondoka hewani.


***

Queen of the mountains, Mc one, alikuwa kaketi nyuma ya laptop yake usiku Huu wa SAA NNE usiku. Mwilini kajisitiri na Nguo nzito, sweta la kufunika shingo, juu yake jacket, soksi miguuni na mikononi. Masikioni mwake headphones Kubwa zimetulia. Alikuwa akisikiliza mazungumzo ambayo yalimchanganya zaidi. Mazungumzo ambayo yalimfedhehesha na kumsononesha, mazungumzo ambayo yaliamsha ndani yake kiu ya uzalendo. Uzalendo wa kuilinda nchi ya mama yake dhidi ya haya aliyokuwa anayasikiliza.

Alipenda fedha na alilipwa vema lakini kwa hili hata kama itakuwa bure alikuwa tayari kulitekeleza. Kupigania nchi yake ambayo kama mtoto yatima mikononi mwa mama wa kambo katili, alikuwa matesoni. Mama wa kambo ambaye sasa alikuwa anamlazimisha baba mzazi kushiriki mateso ya mwanae mwenyewe, Kwa kile kilichosemekana ni tishio la kunyimwa chakula, na baba akionekana kuridhia, japo kwa shingo upande.

Alijinyanyua upesi na kuwasha mitambo yake. Skirini kubwa la runinga likaamka. Mbele yake haikutokea chaneli ya kuonesha vipindi, alionekana mtu, mwanamke mwingine mrembo, malkia wa Kiha.

"Mambo Mage?" Mc 1 akasalimia

"Poa bidada, Kwema? Maana si kwa kujisiliba huko mwanamke. Una homa weye?" Malkia akahoji kiumbeya zaidi!

"Mh mwenzangu, baridi la huku utaliweza? Nakuona mwenzangu ulivyojiachia na joto la huko, haya mama, Leo sina habari njema kabisaa. Huzuni imenikaba hadi pomoni. Nikuombe tu, umshitue mtu wako, Namba moja si upande wake tena!" Mc 1 akapasua jipu.

"Wee, namba wani si wake tena?" Malkia wa kiha akawa kama haamini anachoelezwa. Alijua ukaribu uliokuwepo kati ya Machera na Mheshimiwa Masebo, hivyo hii taarifa ilikuwa si sawa au kulikuwa na namba moja mwingine!

"Si mwingine, ni Huyo huyo !" Ni kama Mc one alimsoma wazo lake.

"Mh haya mapya sasa" Malkia wa kiha akaduwazwa.

"Ni mapya hasa. Nakutumia clip usikie mwenyewe."

"Loh! Tunafanyaje sasa?" Malkia wa kiha akahoji.

"Isikilize kwanza" Mc one akamaliza na kuituma clip husika halafu akaunganisha namba ya Malcolm Stounch. Kioo kikapata ugeni, Malcolm akitokezea kwenye skirini.

"Mc one, nambie mama!" Akasabahi

"Salama kiasi, kwa taarifa nayokutumia bosi una wakati mgumu wa kufanya maamuzi. Ila Du! Adui yetu ni adui kweli kweli aisee" Mc one akatoa Maelezo na kumalizia;

"Ukimaliza kuisikiliza nitakuwa bado hewani, utanijulisha maamuzi yako." Mc One akaondoka hewani.

Malcolm Stounch akazuñguka na kiti chake akitafakari nini cha kufanya. Akiwa ndio anajiuliza nini afanye, Ujumbe wa Mcee one ukaingia kwenye Simu janja yake. Ujumbe wa sauti ikiwa ni mazungumzo kati ya Mabruki na rais wa serikali ya mpito wa Jamhuri, Mheshimiwa Masebo.

Aliyasikiliza mazungumzo yote na kubaini ni kweli alikuwa na wakati mgumu wa kutafakari maamuzi ya kuchukua. Kila dalili ilionesha hatari iliyokuwa inalikabili taifa. Huyu mjinga alikuwa anaiendesha nchi kwa kutumia remote control. Ni dhahiri sasa Masebo alikuwa hana namna. Alipokumbuka kuwa ndugu yake, pacha wake, Elinisa Urio aliuwawa na hilo zee ambalo bado liliendeleza mauaji ya watu Bila kujali, taarifa ya karibuni ikiwa ni mauaji ya yule mkurugenzi wa HRO, kifo cha Maisha Nchagwa, mtu ambaye kutekwa kwake ndio kulipelekea kukamatwa kwa zee hilo hapo awali kabla hajafanikiwa kutorokea huko Marekani, kifo kilichofanana kwa Kila kitu na kile cha mdogo wake, tena kikifanyika kwenye shamba lile lile alikokutwa maiti ya mdogo wake, hasira zikampanda. Akafikia maamuzi.

Malcolm akarudi mitamboni na kumtafuta Queen of the mountains.

ITAENDELEA.....
 
XI



ALIKUWA kajipumzisha kwenye bembea katika ufukwe wa hotel ya Sea Cliff. Hakuwa kwenye likizo wala mapumziko, hapa alikuwa kazini. Akifuatilia taarifa nyeti iliyohusisha mpango wa Don kutumia chokochoko za dini ikiwa ni mpango ambao ungemwezesha Don kurejea nchini kwa kishindo na kuchukua madaraka.

Kwenye moja ya kumbi muhimu za hoteli hii, kulikuwa kufanyike kikao maalum cha kuratibu mpango huo. Hivyo, Martha, yule binti wa waziri Mkuu, mpenziwe Kened, alikuwa hapa kuhakikisha yanayojiri kwenye kikao hiki yanakuwa sio siri tena. Walihitaji kufahamu ABC hadi Z za kikao hicho ili wawe hatua kadhaa mbele ya Don.

Tangu Jana ya Leo, Martha kwa kushirikiana na Atupele, mhudumu katika hoteli hii ambaye alikuwa sehemu ya mtandao maarufu uliojulikana kama 'ulipo Tupo', walimudu kutega vinasa sauti vya kisasa kabisa ambavyo vilipokea mazungumzo kwa kiwango cha juu na kuzihamishia kwenye mitambo yao kule kwa Mwananzila katika mjengo wa Malkia wa kiha. Yeye mwenyewe, Martha, pia akiyasikiliza kwa kadri yalivyozungumzwa kupitia headphones zake alizokuwa kazitia masikioni mwake.

Ungemuona ungejua ni hawa mabinti wa siku hizi wanaoshinda wakiposti mapicha yao wakiwa nusu uchi kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Alikuwa na rununu janja mkononi, na mwilini akiwa yu uchi isipokuwa maeneo ya nyonga aliyofunika kwa mtandio mwepesi uliyoruhusu kuona bikini yake yenye Rangi ya pinki na huku kifuani sidiria za kamba zikifunika chuchu zake zilizosimama wima kiuchokozi. Mtoto Martha mwenye umbo la kimisi ambalo lilipendelewa wowowo Kubwa kiasi miguu laini yenye ujazo toshelevu, tumbo la kutitia na kifua kilichobeba maziwa madogo kiasi, sura ya kitoto yenye kuita. Si ajabu kuwa mara nyingi wanaume walijikuta wakiitika walipotazamana na Martha hata bila kuitwa. Hicho ndicho kilichofanyika kwa kijana Joze Kijo alipomuona binti huyu.

Joze Kijo, yule kijana aliyetekeleza jaribio la kumuua Machera na Anastazia na baadae ikathibitika hawakufa. Taarifa ambayo ilitumwa kwa Mkuu wao na yule Afande mpuuzi Ndimbo, ambaye hata Joze Kijo hakumfahamu.

Ndio, kwa kazi yao, wao walimjua kiongozi wao, mtu aliyetoa maagizo, lakini wenyewe kwa wenyewe hawakujuana. Misheni zao nyingi, zilikuwa za mtu mmoja mmoja. Hapa, Joze Kijo alikuwepo kwa kazi maalum ya kuhakikisha kikao kilichokuwa kinaendelea ndani kinafanyika Bila shida. Kinafanyika kwa usalama stahili. Yeye alipewa kusimamia upande Huu wa ufukweni.

Ni Hapo alipomuona mtoto mzuri akiwa kajiachia Bila wasiwasi. Kwa jinsi alivyomuona, Joze Kijo akabaini ni wale warembo wa Instagram, wale ambao huishi maisha fulani hivi ya maigizo, ambao ukiwa Kubwa jinga unaweza kuhonga Gari, nyumba na 'tembo card' yako. Joze Kijo Hakuwa mgeni wa hawa mabinti, aliwajua vema, na Mara kadhaa aliwagonga na kuachana nao Bila kutoa shilingi zaidi ya kinywaji tu walichokunywa pamoja. Alijua kuwachezea hata wakawa wanamtafuta wenyewe, na yeye Bila hiyana alikuwa anawatumia tu na kuachana nao. Alijisifu kwa ujanja huo. Akajiona mjanja, akajipachika jina, sukari ya warembo.

Alipomuona Martha, alijua ndio wale wale, ila huyu alionekana kuwa matawi ya juu kweli. Ni kweli kuwa, wale watu wake wa Instagram, wengi waliigiza maisha, na alikuja kubaini wengi walikuwa choka mbaya, Malaya tu waliojiuza ili kumudu vipodozi na bando za kupostia picha na video zao mitandaoni, lakini huyu, hakuelekea kuwa choka mbaya. Huyu, urembo wake ulikuwa halisi, sio wale ambao huko Instagram walionekana malaika na alipokutana nao ana kwa ana akabaini ni wa kawaida tu. Huyu alikuwa anga zingine kabisa. Alionesha alikuwa na pesa za kutosha, alikuwa na maisha.

Hisia za hofu zikamwingia, ule ujasiri wake wa kawaida kwa viumbe hawa Ni kama ulimponyoka. Kijo akabaki anaduwaa, anamtazama mtoto wa kike kwa huba. Kijo alikuwa anaangukia pua hapa. Alichohisi hapa si tamaa. Alichohisi hapa ni mapenzi. Swaga zote ziliyeyuka. Kijo Hakuwa na ujanja. Mara mtoto wa kike akamtazama, tabasamu lake laini likaonekana.

"Naam!" Joze Kijo akaitika Bila kuitwa, huku hatua zake zikimbeba mdogo mdogo kumuelekea binti yule. Akili yake ikigeuka ya zuzu.

Akamfikia Martha, Hapo ndio akagundua kinachoendelea. Yule binti sasa alimtazama kwa mshangao! Loh! Joze Kijo akabaki kakodoa macho, hajui cha kusema. Anamwangalia tu mdada wa watu!

"We kaka vipi?" Martha akatamka, ile sauti yake anayotumiaga kama silaha kwa watoto wa kiume sampuli hii. Wanaume wakware! Joze Kijo akajipata anasalimia;

"Shikamoo Dada"

Martha akaangua kicheko cha haja, kicheko cha kishua. Joze Kijo akabaini kosa lake. Akaachia cheko la nguvu,

"Ha ha ha"

Kicheko kilichokuwa mahali fulani kati ya kulia na kucheka. Ungeona sura yake. Msomaji ungecheka hasa. Sura yake wakati akicheka Joze Kijo, ungedhani yupo kwenye haja Kubwa inayoambatana na maumivu ya gonjwa la bawasiri.

"Kaka vipi wewe, una shida gani jamani, mbona sikuelewi." Martha akazungumza kwa ile sauti, sauti iliyozidi kumwehusha Joze Kijo. Martha alijua nini anachofanya. Alikuwa ananunua muda ili Kened atoke mjengoni Bila kutiliwa shaka na watu wa Don.

"Dada, haki ya Mungu nimekupenda!" Joze Kijo akatamka kwa ubembelezi. Ubembelezi uliosikika kama ombolezo.

"Kha! We kakaa! Hivi tuseme umenionaje hasa hata unanambia hivyo?" Martha akajitia kuhamaki, lakini akiachia nafasi ya kuendeleza mazungumzo. Halafu akaongezea;

"We unanijua Mimi?"

"Kusema kweli sikujui, lakini Dada nipo tayari kukujua sasa. Kila kitu kina mwanzo wake, Huu unaweza kuwa mwanzo wa Mimi na wewe kujuana Dada, Mi anaitwa Joze, Joze Kijo! " wakati Joze akiongea hayo alikuwa kapiga magoti chini na sasa alikuwa anaunyosha mkono wake asalimiane na Martha.

"Nisikilize kaka, Mimi sijui umenichukuliaje lakini nakuomba tu tuheshimiane. Umeniona mlupo kiasi gani sijui, utoke huko ulikotoka na kuja moja kwa moja kwangu eti nimekupendaje Dada? Kha, ama kwa hakika dunia hii watu tunadharauliana sana. Mimi siko hapa kujiuza kaka, Mimi nipo hapa kujipumzisha. Nipo hapa kula upepo mwanana wa bahari. Kama umekosea njia, uliza uelekezwe!" Martha akazungumza. Kwa mbali akamuona Kened akimuonesha ishara kuwa mchezo umekamilika.

"Kwanza umeniboa sana, sioni haja ya kuendelea kukaa hapa. Wacha nijiondokee zangu." Martha akajinyanyua na kuanza kuondoka. Chini akadondosha kijikaratasi kwa makusudi. Joze Kijo akaganda huku akiangalia makusudi aliyofanyiwa na Martha kwa mwendo wa madaha ulioacha wowowo zake zinesenese kiuchokozi.Joze Kijo akalazimika kuketi chini kuficha aibu. Ni Hapo alipoona kile kijikaratasi.

'Nitafute baadae, hapa kuna mtu wangu na ana wivu wa hatari. Asante kwa kunipenda Joze, Joze Kijo. Niite Amina, ukiniita Amy ndio napenda zaidi. 075489.....' Alipomaliza kuusoma Ujumbe huo, Joze Kijo hakujali tena, alisimama na kuinua mikono juu huku akishangilia

"Yyes! Yyes! Mtoto kakubali swaga za mtoto wa town!! Aliruka Bila kujali, alichojali kwa muda huo Ni Ujumbe alioachiwa na Amy. Hakujua kuwa, Kama Ni karata, alikuwa amelamba joker.


***

Wa kwanza kuingia alikuwa Halfani Mjuni, mwanaharakati maarufu wa lile kundi lililojipatia umaarufu nchini siku za karibuni, kundi la lililodai kutetea haki za kiislamu, kundi ambalo hivi majuzi lilitekeleza mauaji yaliyopigiwa kelele na mataifa mbali mbali, na kuiweka jamhuri kwenye Ramani ya kimataifa. Mauaji yaliyohusisha kuuawa kikatili kwa kupigwa kwa mawe, mwanamke aliyeitwa Amina. Sababu iliyojulikana ni kukutwa akifanya mapenzi na baba yake mlezi. Baba ambaye ilisemekana alikuwa anambaka na ikiwa ni kelele zake za kutaka msaada zilizopelekea wao kukutwa kwenye kitendo hicho. Amina alikuwa akihitaji msaada na alichoambulia ni kuvuliwa Nguo hadharani na kupigwa mawe hadi kufa. Lilikuwa tukio ambalo lilivuma mitandaoni na kuibua mashirika ya haki za binadamu, likiwemo lile la HRO chini ya mkurugenzi Maisha Nchagwa, aliyejitokeza na kulikemea vikali. Ikadaiwa kitendo hicho kilimtengenezea maadui ndani ya kundi hilo maarufu kama Alihaki fighters! Sasa lilijulikana ni kundi la kigaidi baada ya kutangaza kumuua mkurugenzi Maisha Nchagwa.

Aliyefuatia alikuwa mtu maarufu sana jijini Dar na nchini kwa ujumla, umaarufu wake ukivuka mipaka hadi nchi Jirani. Alikuwa anajulikana kimataifa sasa. Mtume na nabii Oyono Goodness. Mtunzi wa kitabu maarufu cha unabii na mafunuo, mmiliki wa sinagogi Kubwa na Oyono Ministries International. Huyu alivalia joho lake la kinaijeria na kofia za kibandiko mithili ya zile za wayahudi.

Mtu wa tatu, Martha alimfahamu vema. Ilimshangaza alipomuona akiingia kwenye kikao kile adhimu kwani taarifa walizokuwa nazo ni kwamba mtu yule alikamatwa na taarifa zake kuenea magazetini, mitandaoni, na kwenye vyombo mbali mbali vya kimataifa, Ester/Evans Brown, maarufu kama Estivan Brown, yule mrwanda maarufu kwa mauaji yaliyoacha vi-mikufu vya mafuvu kwenye wahanga wake! Huyu aliwashitua. Haikuyumkinika ni namna gani Estivan alikuwa huru, tena akitamba hapa nchini. Kengele ya hatari iligonga kichwani mwa Martha. Hakutakiwa kuonana naye, hivyo alihakikisha anakuwa mbali na macho yake.

Mtu wa nne ndio aliwashangaza zaidi. Hawakuamini macho yao. Ingawa alikuwa kajaribu kujibadili na kujificha ficha, asingeweza kujificha kwenye macho ya Ken na Martha. Walimfahamu vema. Mara kadhaa walikutana naye kwenye vikao nyeti kabla hajawa kwenye nafasi hii aliyokuwepo sasa. Mheshimiwa Masebo, rais wa Jamhuri. Kidogo walichanganyikiwa na kuanza kuona ugumu wa kazi yao.

Kwa siku kadhaa, mawasiliano na Machera yalikuwa shida. Haikuwa rahisi kuwapata, Yeye na mwenzie Anastazia. Njia pekee ilikuwa kupitia malkia wa Kiha. Martha alichukua Simu yake na kumpandia hewani malkia wa kiha.

"Dada, hapa tuna mtihani mkubwa, namba moja ni mwalikwa kwenye kikao." Martha alitoa taarifa.

"Najua, nimepata taarifa toka Jana na sikuwa na hakika kama zilikuwa kweli, ndio maana nilitaka muwepo Hapo ili tujihakikishie taarifa ile. Loh! Nadhani unaweza kuona namna gani hili suala lina kina." Malkia wa kiha alitamka.

"Kwa hiyo tunafanyaje?" Martha akahoji.

"Hakikisheni tunapata mazungumzo yao Barabara." Malkia akazungumza na Simu ikakatwa.

Malkia ambaye alikuwa ameketi na Machera pembeni yake, akamgeukia na kumtazama kwa mtazamo ulioonesha kusema, 'umeelewa sasa?'. Hakusema kitu. Machera akatikisa kichwa kwa masikitiko.

"Lo! Don ametushika pabaya. Siamini imefikia hatua hii. Mzee yuko tayari kunitoa sadaka ili binti yake awe huru." Machera alikuwa na masikitiko. Jana usiku alipopewa taarifa kuwa mheshimiwa Masebo anaunda njama ya kumtoa kafara kwa niaba ya Mabruki, alikataa katakata! Alikataa kwa sababu ni miongoni mwa Viongozi thabiti aliowafahamu. Ni kiongozi pekee aliyekuwa safi kwa mujibu wa ile kamati teule yenye kuamua mustakabali wa nchi.

Hakuamini kama mheshimiwa Masebo angeweza kugeuka, Kusaliti na hata kuridhia kutoa watu wake kuwa sadaka, hadi pale alipoyasikiliza mazungumzo ya Don na Masebo. Na sasa taarifa hii ya Martha. Alipojumlisha na mazungumzo yake na Rais Hapo awali, jinsi Mheshimiwa Masebo alivyopokea simu kwa jazba na shutuma kabla ya kubaini ni yeye, Machera akahitimisha kuwa ulikuwa ukweli, ukweli mchungu sawa na shubiri!



ITAENDELEA......
 
XIII




SIMU ya Machera iliita. Alipotazama kioo cha Simu hiyo, jina la mheshimiwa Masebo likaonekana likidunda kwenye kioo hicho. Bila shaka muda wa Mabruki ulikuwa wayoyoma. Masebo Hakuwa na namna. Alidhamiria kumtoa yeye Machera kafara ili kutimiza lengo la kumrejesha mwanae mpenzi, Hellen.

"Hujambo kijana wangu? Aisee naona tukutane kwa siri pale mahali petu pa siri. Kuna jambo muhimu nimebaini ambapo laweza kutusaidia kumkabili The Don." Masebo, alimtamkia Machera. Hapo tena Machera akajua kumekucha.

"Sawa Mkuu, muda gani?" Machera akahoji.

"Vema iwe sasa maana baadae nitakuwa na ugeni wa Balozi wa Cuba. Naamini hukumweleza mtu yeyote juu ya wewe kuwa hai, maana mamluki wapo Kila kona. Ni dhahiri Mabruki aliwekeza vilivyo kwenye ndoto ya kuikamata hii nchi kama rais." Masebo aliendeleza ulaghai. Machera naye akajifanya kondoo akienda sambamba na mpango wa Masebo.

“Kwa kweli hakuna anayejua zaidi yako mheshimiwa. Ni wewe pekee nayekuamini kwa sasa, na hii ni kutokana na ukweli kwamba hata kuvamiwa kwangu kulidhihirisha kuwa kwenye timu yangu tayari kuna watu walioko kwenye orodha ya malipo ya Mabruki. Mimi nadhani utanikuta eneo husika maana hivi sihitaji hata kujiandaa na navyoongea niko njiani tayari." Machera naye akazidi kumpanga Mheshimiwa Masebo.

“Safi kijana wangu. Utayari wako ni tunu kwa nchi yako" Masebo akatamka kwa sauti iliyojaa majonzi.

Machera hakutaka kupoteza muda. Haraka sana alijipanga pamoja na kikosi tiifu cha malkia wa Kiha.

Pamoja na ukweli mchungu kwamba Masebo alikuwa tayari kumtoa kafara, Machera alitaka kumtazama usoni kiongozi Huyo wakati akigeuka adui wa watu wake mwenyewe.


***

Takribani SAA 11 jioni. Kwenye nyumba ya mheshimiwa Masebo ambayo allishi kabla ya kuingia ikulu. Machera aliingia getini na kukaribishwa na ulinzi mkali wa PSU. Hakupewa nafasi ya kusikilizwa. Alibebwa juu juu na kuingizwa ndani ya Gari lenye Vioo tinted aina ya Toyota Hiace. Gari hilo likavurumushwa toka ndani ya jumba la mheshimiwa Masebo. Mwendo wa kama nusu kilometa toka yalipo makazi ya Masebo, Gari hilo likakumbana na vizuizi vya kikosi cha Malkia wa Kiha. Silaha Kali zikiwa zimeelekezwa dhidi ya Gari hilo. Sauti ikasikika kutokea kwenye kipaza sauti.

"Tunamhitaji mateka, Kama ilivyo makubaliano yetu." Sauti Kali ya mwanamama Anastazia ikakoroma na kisha ikamalizia kwa neno la utambulisho wa watu wa Don.

"Don nation "

Ni hilo neno lililosubiliwa kwa hamu na kikosi cha PSU. Hiyo ilikuwa password ya kifurushi cha Don, yaani Machera.

"Mbona huku na si eneo la makubaliano?" Kamanda Stallone wa kikosi cha PSU akatupia Swali.

"Change of plan. Tahadhari ni muhimu. What if kulikuwa na informer wa package from either sides?" (ni tahadhari tu, kwa sababu huwezi jua huenda kuna mamluki kwenu au kwetu, hivo ukakuta adui anatungoja huko.)

Kauli hiyo ikamshawishi Stallone. Haraka sana wakakabidhiwa mtu wao, wakidhania kuwa walimkabidhi kwa watu wa Don. Msafara wa malkia wa kiha ukapotea huku ule wa PSU ukirejea kwenye viunga vya ikulu.


***

Mnamo SAA mbili za usiku baada ya Machera na kikosi chao na kile cha malkia wa kiha kujichimbia kwenye machimbo yao, ulikuwa muda wa kumuonesha Mkuu Huyo wa nchi hatari Kubwa aliyekuwa anaikabili baada ya kuamua kuunda njama na adui wa taifa na hata serikali yake.

"Hallow!" Ilikuwa sauti ya Masebo akipokea Simu iliyokuwa imeingia kwenye Simu yake. Simu ngeni.

"Naam mheshimiwa rais. Habari za majukumu Mkuu." Ilikuwa sauti aliyoifahamu vema. Sauti ya Machera. Hakutegemea kusikia sauti yake. Mshituko wa moyo ukamkabili mtukufu rais. Ujasiri wake ukayeyuka. Mikono yake ikashindwa kumudu kuiweka Simu sikioni. Simu ikadondoka chini pamoja na yeye. Hali ile ikawashitua wasaidizi wake. Hamadi!! Wakamfikia ili kujua kulikoni.

Mheshimiwa akajibaraguza na kujiweka sawa wakati wasaidizi wake wakihaha kumsaidia.

"Uko sawa mheshimiwa?" akahoji Manka katibu muhtasi wa mheshimiwa rais.

Mheshimiwa Masebo akajaribu atamke neno. Kinywa kikamgomea. Akali akirudisha akili yake sawa, Simu yake ikaita tena. Mheshimiwa akajikusanyia nguvu kadri alivyomudu, akitaka kuipokea Simu.

Akamudu kuikamata Simu mkononi. Kwenye kioo cha Simu jina 'Bastard' (mwanaharamu) likaonekana bayana. Hilo ndio jina alilohifadhi namba ya Mabruki kwenye Simu yake. Masebo jasho likamtoka huku kiyoyozi cha ikulu kikiwa kimekoleza baridi sawa na la makambako huko Iringa. Kigugumizi cha ghafula kikamvaa Mzee wa watu. Hata alipoifikisha sikioni, mikono na mwili kwa ujumla vilikuwa havifanyi kazi sawa sawa, kilichooneka ni kutetemeka kwa ajabu kabisa. Wasaidizi wake wakabaki wakimshangaa.

Akabonyeza alama ya kupokelea Simu na kuibandika sikioni Simu hiyo akiwa bado kaketi chini.

Akajaribu atamke neno, sauti ikamkwamia kooni. Akaishia kutoa mguno wa;

"Mh!!"

"Isingekuwa kuwa kwamba ni binti yetu Helen, ningekuonesha ukatili ambao maisha yako yote usingesahau. Kwa sababu ya Helen, nakupa benefit of doubt, na kwa vile bado masaa kadhaa kufikia muda kamili wa masaa 48 niliyokupa, basi Nakutahadharisha kwamba baada ya muda huo, tusilaumiane. Kitakachojiri wewe mwenyewe utashuhudia kwa sababu nitakutumia video clip yote ili ushuhudie uzembe na ujinga wako unavyokushughulikia." Mabruki akazungumza kwa karipio lililoonesha ni kwa kiwango gani makubaliano yake na Masebo juu ya kumkabidhi Machera kulikofeli kulivyomuudhi. Akaikata simu bila kumsikiliza mtu wa upande wa pili.

Makubaliano yao awali yalikuwa kukabidhiana kijana Huyo huko Mabwepande, ambako kikosi cha Don chini ya yule mtu katili, raia wa Rwanda Estivan Brown, kilikuwa kimeweka kambi tayari kwa makabidhiano. Matokeo yake hadi kufikia SAA mbili za usiku watu wa Masebo hawakuonekana.


***

Jijini Los Angels, Marekani.

Leo ilikuwa iwe siku ya tukio la Furaha kwa upande wa Don. Ilikuwa siku ya kumtia mikononi mwake yule kijana matata aliyesumbua harakati zake na kuwa kikwazo kikubwa sana kwenye jitihada zake za kuiweka Jamhuri chini ya utawala wa lile kundi Kubwa la Mabruki. Kundi lililokita mizizi yake zaidi huko Marekani na Ulaya. Lakini kilichotokea kilikuwa kinyume kabisa na matarajio yake. Hata hivyo akajifariji kuwa muda wa ukomo wa agizo lake ulikuwa bado na kwa vile binti wa Masebo alikuwa kwenye nyayo zake, alijua bado ana nafasi Kubwa zaidi ya kushinda vita yake. Pili alijua kesho ya Leo ingeleta msisimuko mpya kwa Masebo kutekeleza mpango wake.

Kile kikao cha Estivan, Don na Halfani kilichomshirikisha Masebo kwenye baadhi ya mambo huku akifichwa ajenda ya kesho, kilikuwa kitekeleze mpango kabambe kesho. Karata ya dini, ingechezwa kesho. Hayo yalikuwa mafikra yake ambayo hakusita kumshirikisha basha wake, kijana wa Congo DRC, Didier Masele.

Don alikuwa hana siri ilipokuja habari ya Didier Masele, Furaha zake alimshirikisha, sonona zake pia alizianika Bila kificho kwa Masele. Hata alipojipata njia panda, Mabruki alimweleza Masele. Uhuru aliohisi juu ya kijana huyo, ulimfanya Mabruki kuwa kitabu kilicho wazi mbele ya Masele. Ama kwa hakika, ndege mjanja hunaswa penye tundu bovu. Mabruki aliangua kicheko chote Bila kubakiza alipokuwa na Masele faraghani, na hata alipokuwa na sonona nyingi, alilia kama katoto kadogo kifuani mwa Masele.


***

Las Vegas, Marekani.

Mc One, alilipokea agizo la Malcolm Stounch juu ya kuondoa mzizi wa fitna. Alijua maana yake nini. Hata hivyo, kulikuwa na jambo la msingi la kufanya kabla ya agizo la Malcolm Stounch. Ilikuwa juu ya Helen Masebo yule binti wa rais wa serikali ya mpito nchini Tanzania.

Si kwamba kulikuwa na haja sana ya kufanya jambo zuri kwa ajili ya rais aliyekuwa tayari kuuza nchi yake kwa ajili ya mwanae, Bali binti huyo hakuhusika na haya mambo na kushikiliwa kwake kulikuwa kinyume na utaratibu wowote ule timamu. Hakustahili kuhukumiwa kwa kosa la baba yake. Mc one aliamua kwanza kumtoa binti huyo kwenye makucha ya Don kabla ya kuhitimisha zoezi lenyewe.

Hatua aliyokuwa amefikia hata hivyo, ilikuwa inaleta matumaini ya kukamilisha zoezi kwa wepesi. Taarifa zote juu ya mipango ya Don, licha ya kudukuu mawasiliano ya Don, bado alipata nyeti zote juu ya Mabruki kupitia kwa Didier Masele. Hili alilimudu baada ya kubaini kuwa hila yake ya kutumia mwili wake isingefanikisha kitu kwa sababu, zee lile lilikuwa chafu kupindukia. Lilikuwa halina hisia kabisa juu ya wanawake Bali lilikuwa linapenda tu wanaume wenzake, lenyewe likigeuzwa mwanamke.

Baada ya kubaini suala hilo Mc one akaamua kutumia udhaifu wa Don alipogundua uhusiano wa Don na Masele, Mc one alijua amemaliza kazi. Ikawa kama amepata unafuu kwenye kazi zake. Hakuhitaji tena kujidhalilisha kwa lengo la kujifanya chambo. Chambo kilikuwa Don mwenyewe.

Ilimchukua masaa kadhaa Mc one kubaini upenyo wa kuingilia kwenye moyo wa Don. Pale alipobaini kuwa Didier Masele ana mpenzi, mpenzi mwingine tofauti na Don, mtoto wa kike, mrembo mwenye sifa zake, Mc one akajua kumepambazuka. Akawa amepata wazo. Wazo mujarab, akamtia Grace mikononi mwake. Akawa yupo chini ya uangalizi wa watu wake masaa 24 kwa siku. Didier Masele akaoneshwa picha zilizoonesha jinsi mwanamke wake alivyokuwa anatazamwa muda wote. Hakuishia Hapo, Masele akaoneshwa picha zake akiwa na Don. Picha ambazo kama zingewekwa mitandaoni, angepoteza sifa, angepoteza washabiki, angepoteza heshima, angepoteza mpenzi na huenda angejilipua na kupoteza maisha yake.

Masele hakuwa na namna bali kufanya Kila alichotakiwa kufanya kwa maelekezo ya Mc one. Kwa njia hiyo Mc one akapata taarifa zote alizohitaji kutoka kwa Don Bila kujiweka kwenye hatari yoyote.

Alipohitaji kujua alipowekwa Helen, Mc one alipata taarifa zote kwa usahihi. Jengo, walinzi na vielelezo vyote vya kiusalama. Kazi ikawa rahisi. Akawapanga vijana wake kwa ajili ya operesheni maalum. Operesheni ya kumkomboa Helen Masebo.


***

Khalidi alipotoka nyumbani kwenda kukutana na Halfani Mjuni, alikuwa na amani moyoni. Amani isiyoelezeka. Fukuto la ujasiri likawa linamkereketa moyoni. Ujasiri uliozidi ule wa hayawani. Alitembea kikakamavu akijua anaenda kutimiza wajibu, kulipiza kisasi cha mama yake mpenzi Maimuna binti Hamis Juma. Ilikuwa siku ya kujipatia thawabu. Naam. Halifani alikuwa kamweleza kinagaubaga juu ya suala hili na thawabu nyingi kem kem zilizoambatana nalo. Alikuwa tayari.

Mnamo SAA 12 asubuhi, Khalidi na wenzake wawili, jumla wakiwa watatu. Wote wenye umri ulioshabihiana, wakiwa wenye historia zilizofanana na wote wakitokea kwenye madrasa ambayo ilifadhiliwa na kundi la Alihaki fighters, kundi hilo likiwajenga wanafunzi wao kiitikadi na kivita. Madrasa yao ilikuwa na mtaala wa peke yake tofauti na madrasa zingine zile. Hii ilikuwa kama chuo cha kijeshi. Wanafunzi hapa waliandaliwa kuwa wapambanaji. Wapambanaji dhidi ya dhuluma. Walifundishwa mbinu mbali mbali za mapambano, upiganaji na hata matumizi ya silaha nzito nzito za kisasa. Waliaminishwa na kula yamini kupambana kwa ajili ya dini. Hawakujua kama walikuwa silaha za Don na genge lake. Hawakujua kama lengo la shule yao lilikuwa kutumika kwa maslahi mapana ya Mabruki na genge lake.

Hawakujiuliza kwa sababu, madrasa hii iliwawezesha kuishi, wengi wao hawakuwa na wazazi, wengi wao waliokotwa mitaani na kupewa maisha Hapo, wengi wao hawakuwa na Tumaini na Hapo kituoni kwao walipata Tumaini. Madrasa iliwapa kusudi la kuishia, ikiwatoa kwenye Lindi la umaskini, ikiwachomoa kwenye makucha ya dawa za kulevya. Ikawa kimbilio dhidi ya umauti wenyewe. Hapa walimpata Mungu, na wakaweka Tumaini lao kwake. Maisha yao wakayatoa sadaka. Wakaishi ili kutekeleza matakwa yake. Madrasa yao ilikuwa ndio maisha kwao. Walikuwa tayari kufa kwa kusudi mahsusi, kufa wakiwa na tiketi ya kuona pepo mikononi. Kufa kwa kumpigania Mola na dini yake tukufu. Heri wangeng'amua mapema kwamba hii ilikuwa si vita kwa ajili ya Mola, Bali vita ya kumpa utukufu shetani. Ilikuwa vita ya kumtolea ibilisi sadaka ya binadamu.

Halifani na waalimu wengine walikuwa wamo ndani ya chumba maalum kwenye sinagogi la mtume na nabii Oyono Goodness. Khalid alipoingia aling'amua ni yeye pekee aliyekuwa akisubiriwa. Wengine wote tayari walikwishaingia.

Aliingia na kutoa salamu ya heshima kwa Viongozi wake na wapambanaji wenzake wawili. Walimpokea kwa heshima, huku Viongozi wake wakimkumbatia na kumbusu kama baba afanyavyo kwa mwanae. Wakamtia moyo yeye na wenzake wawili. Wakawasifu kwa kujitoa kwa kusudi Kubwa. Wito wa kinabii na kitume. Wakawahakikishia walikuwa wamekwisha kujihakikishia thawabu na sehemu kwenye makasri ya peponi.

Vijana Hao watatu wakajawa ujasiri, wakiwa tayari kwa kazi iliyokuwa mbele yao.

Baada ya kuwa na hakika na kile kilichokuwa mbele yao na kuridhia kwa dhati ya mioyo yao. Halifani na walimu wenzake wakaanza kazi yao. Kazi ya kuwageuza vijana wale silaha madhubuti ya genge la Mabruki. Mabomu ya kujilipua yakafungwa kwenye matumbo yao tayari kwa milipuko, milipuko ambayo ilitarajiwa kuteketeza maelfu ya waumini kwenye Sinagogi la mtume na nabii Oyono Goodness. Ilikuwa siku maalum ya Oyono kutoa sadaka Kubwa zaidi kwa yule aliyempa uwezo wa kukusanya maelfu haya ya watu. Watu ambao tayari alikwisha watumia na kujikusanyia ukwasi wa kiwango cha juu zaidi. Ilikuwa siku ya usharika wao wa siri ule wa kishetani kutoa sadaka maalum ya kujiimarisha katika kile walichokiamini, na kuhakikisha ikulu ya Jamhuri inakuwa chini ya miguu yao. Chini ya kiongozi wao, Mabruki The Don.


***

Ingawa kwa muda wa wiki nzima kulikuwa na matangazo juu ya kusanyiko kubwa la ibada kwenye sinagogi la mtume na nabii Oyono Goodness, jumapili hii mambo yalikuwa tofauti, kuanzia alfajiri jiji lilirindima kwa matangazo yaliyohamasisha watu kuhudhuria ibada kwenye sinagogi la mtume na nabii Oyono Goodness kwenye vituo karibu vyote vya TV na radio nchini. Waamini wengine wakisafiri kutoka mikoani ili waweze kuhudhuria kwenye ibada hiyo ya kipekee. Ibaada ambayo Oyono na watu wake waliwaaminisha kuwa ingekuwa komesha ya shida na matatizo yao. Mitaani nako mabango yalipamba Barabara za mitaa kuhusu tukio la ibada ya aina yake kwa jumapili hiyo.

Watu walihamasika, wakajitokeza kuhudhuria ibada. Mitaani kukajaa watu, Boda Boda kazi ikapamba moto, Magari ya abiria yakakodiwa kukusanya watu mitaani kwenda kanisani. Mitaa ikawa hai.

Kufikia Saa nne asubuhi, sinagogi la mtume lilikuwa limekwisha jaa watu na watu wengine wakiwa wamejaa nje kwenye viwanja vya sinagogi lile. Kitabu cha mtume na nabii Oyono Goodness, kilikwisha uzika nakala karibia elfu kufikia muda huu. Oyono alikusudia kuzikusanya kwanza fedha walizokuja nazo waumini na waamini wengine, na zoezi la kuwatoa kafara lingetekelezwa baada ya kukusanya matoleo yote ya sadaka. Hawakutakiwa kulipuka na fedha zao mifukoni.

Halfani na wenzake wakiwa wameshaondoka mahali hapo. Khalid na wenzake wawili wakaingia hekaluni wakiwa tayari kwa tukio ambalo lingeacha historia. Tukio ambalo lingewapeleka moja kwa moja kwenye utukufu wa milele. Mabomu yaliyofungwa viunoni mwao wakiyaona kama tiketi ya kuingia peponi.

Mtume na nabii Oyono Goodness, alikuwa bado kuingia sinagogini. Lakini makusanyo yote ya mauzo ya vitabu na sadaka za matoleo, alikuwa keshayakusanya na kuyahifadhi eneo salama. Alikuwa na kikosi maalumu kwa kazi hiyo ambacho kilijua nini kinaendelea.

Alipokuwa anaingia kanisani, Khalid alikuwa na ujasiri mwingi sana. Alikuwa na amani ya kutosha moyoni mwake. Alijua gharama ya kuingia peponi ilihusisha kujitoa maisha yake, kifo cha moto, lakini heri moto wa siku moja kuliko ule wa milele. Alijipa moyo. Hata hivyo, alipokuwa ameingia mlangoni tu, hali ambayo hakuitarajia ikamwijia. Hakuwaza peponi, hakuwaza kuishi. Alimuwaza Maimuna.

Alipiga hatua ya kwanza, ya pili, ya tatu, hatua ya NNE akaushuhudia umati wa wa watu maelfu. Watu waliokusanyika ndani ya mjengo. Walikuwa wanalia. Wanamlilia yeye, huku wengine wakimlaumu kwa kusudio lake la kutaka kuwaua. Wahka ukamshika Khalid, kuangaza huku na huku, Kila anayemuona katika wale maelfu ni sura ya Maimuna binti Hamis Jumaa. Watu wote walikuwa ni mama yake kipenzi. Anaanzaje kumuua mama yake. Akili yake ikacharuka kwa muda, kutahamaki akawa amerukia kipaza sauti.

"Bomu, kuna Bomu jamani. Ondokeni humu." Akapaza sauti. Watu wakabaki wanamshangaa. Kuona haeleweki, Khalid akavua koti lake lililofunika Bomu la kufungiwa. Likawa liko wazi. Kila mmoja akashuhudia kilichokuwa kinaelezwa. Ukumbi ukacharuka kwa vurugu za kutaka kuokoa maisha yao. Hakuna aliyekumbuka kuwa alikuwa kanisani.

Wale wawili wenzake kusikia vile wakaona mpango unatibuka, wakaachia vitufe kwenye mabomu yao, milipuko ikasikika.

Kimya kikatawala kwa muda kufuatia mlipuko ule. Dakika mbili baadae maafa yaliyokuwa yanaendelea yakawa dhahiri. Moto mkubwa ukimeza maisha ya waumini na waamini wa mtume na nabii Oyono kama vile ni kitu kidogo. Maafa makubwa yalilikumba taifa.

Zima moto wakahaha kuzima moto, hata hivyo hali ilikuwa tete. Moto ulikuwa umekula maisha ya watu wengi tayari. Vyombo vya habari vikiwa vimetinga eneo la tukio kurusha taarifa za moja kwa moja. Ilikuwa ni kilio cha taifa.


***

Mnamo SAA mbili za usiku, raia waliogubikwa na majonzi kufuatia Mauti ya ndugu zao wakiwa wameganda kwenye TV zao, kuangalia taarifa za habari, ikajitokeza taarifa ya ya ghafula, habari za punde hiyo, ilikuwa hatari. Ilikuwa ni taarifa ambayo iliachiwa na kundi la Alihaki fighters wakikiri kwa tambo juu ya uhusika wao kwenye tukio hilo lililomeza mamia ya raia wasio na hatia kwa chuki tu ambazo zilihusishwa na dini, Kumbe uongo, Ilikuwa kafara ya Don pamoja nabii wa uongo Oyono Goodness. Kundi hilo, al haki fighters wakitamba kuwa matukio mengine yalikuwa njiani kutekelezwa.

Jamhuri nzima ikatikisika. Kila kona kulikuwa ni hali ya sintofahamu. Taarifa hii ikazunguka dunia nzima. Wananchi wakaingiwa na ganzi la woga, hofu na sintofahamu.

Malcolm Stounch akaipata kupitia vyombo vya habari vya kimataifa. Kulikuwa na haja ya kulisimamisha hili janga mara moja na kulikomesha kabisa. Na njia pekee Bila shaka ikiwa ni kushughulika na kiini cha tatizo. Juu ya kuzuia tukio Hilo, alikuwa amechelewa.


***

Asubuhi SAA mbili siku moja baada ya milipuko iliyoteketeza takribani waumini maelfu moja na mamia mawili, huku shughuli za uopoaji wa miili iliyokwamia ndani ya Sinagogi ikiendelea, taarifa nyingine ikatolewa na msemaji wa sinagogi la Oyono Goodness, ikiwa neno la Faraja kwa wafiwa ambao ndugu zao walipatwa na umauti ndani ya Sinagogi. Baadae ikasemekana mtume na nabii Oyono Goodness naye alirekodiwa Hapo awali alitoa salamu za rambirambi na pole kufuatia tukio lile zito. Kauli yake hata hivyo, ikaenda mbele zaidi kwa kile ambacho wachambuzi wa mambo walidai ni jibu Kali dhidi ya kundi la Alihaki fighters. Mtume na nabii akasema suala hilo lisingepita hivi hivi. Waliohusika watapata kula jeuri yao maadam wameingia madhabahuni na kuinajisi. Tangazo hili, Bila shaka likiwa tangazo la kuhamasisha waumini wake kutoliacha tukio lile lipite hivi hivi.

Waumini wake mamia kwa mamia wakajitokeza mitaani, wakiandamana na kuipatia serikali muda wa Massa 48 kulifuta kundi la Alihaki fighters, la sivyo, wakadai wangeifanya kazi ya serikali kwa njia walizofahamu wenyewe.

Walichokitaka washirika wa Don, kilitimia. Don, Oyono na Halifani walikuwa wamemwaga damu ya kutosha ikiwani sadaka yao ya kipindi maalum. Walitarajia kuona mwitikio ule, watu wakikamatana, kushutumiana na kuuana. Hicho ndio kitu pekee walichotarajia.

Nchi isitawalike, watu wauane, halafu wao wajitokeze kutuliza ghasia hizo halafu wajichukulie sifa na hatimaye waitiishe nchi chini ya utawala wao.


ITAENDELEA......
 
XIV



ALI-IITA Dark Thursday (Alhamis ya Giza). Matukio ya siku hiyo licha ya kutimia kwa baadhi ya mipango yake, mpinzani wake alimudu kumchezesha shere. Don hakuamini kilichotokea. Chambo chake kilichokuwa silaha madhubuti dhidi ya adui yake hakikuwako mikononi mwake tena. Helen hakuwa kwenye himaya yake tena.

Chini ya jengo Kubwa la kanisa la kinabii, Discipleship church of all nations, ndipo alipokuwa amehifadhiwa Helen Masebo, bintiye rais wa serikali ya mpito huko Tanzania. Chumba hicho kilikuwa kama studio ya radio. Chochote kilichofanyika humo kiliishia kumezwa na kuta thabiti za Chumba hicho. Mlikuwa na kitanda, Chumba cha choo na bafu na vitabu mbali mbali kwenye shelves zilizolandishwa kutani. Kilichokosekana tu, ni uwezekano wa kuona nje. Chumba chenyewe kilikuwa na nafasi Kubwa ya kutosha hata kufanya mazoezi ya mwili, na labda kwa kutambua hilo, waliweka vifaa mbali mbali vya mazoezi ikiwamo treadmill.

Huenda waliamini chumba hicho kilikuwa salama sana kiasi cha kuweka ulinzi hafifu eneo hilo. Watu wa Mc one walipofika walimkuta mlinzi wa kanisa ambaye hawakuhitaji kutumia nguvu ili kujua alipo Helen Masebo. Alikuwa ni Mzee wa miaka sitini na ushei.

"Hello sir" (Habari mkuu?) Muywanga, kijana mtata kwenye ujasusi wa kimjini mjini, wenyewe wakijiita 'misheni town', alimaarufu jipu kuu, alimsabahi Mzee yule.

"What's up young man?" (Mambo vipi chalii?) Mzee yule alijibu akitumia lugha ya vijana zaidi kulinganisha na umri wake. Muywanga akajua, safi, kazi imekwisha.

"Cool buddy."(Poa sana mzee baba) Akajibu huku akimwangalia kwa makini usoni Mzee ambaye alijiita black Jesus, jina la utani. Jina halisi likiwa ni Musangu. Mbena kutoka Iringa aliyezamiaga Marekani miaka ya tisini kwa kujificha kwenye maboksi yaliyosafirisha tumbaku za kutoka huko Tabora. Akaingia Marekani kwa usafiri wa meli ya mizigo. Inasemekana Mzee Huyo alipofika Marekani alikuwa kachoka hoi na aliponea mortuary (chumba cha maiti) siku ya tatu. Ilikuwa ni muujiza wa aina yake. Ni Hapo alipojiita black Jesus kutokana na hilo tukio la kukaa mortuary kwa siku tatu akiwa kama mfu na kutoka akiwa Mzima.

"You might have been told about my coming here sir, I'm here for the Package Helen Don-nation!" (Utakuwa ulipata taarifa juu ya ujio wangu. Nipo hapa kwa ajili ya kifurushi, Helen Don-nation) Muywanga akatupia kamba ya kwanza, pap, kamba ikanasa shingo ya black Jesus. Jipu kuu alikuwa tapeli la kiwango cha daktari wa falsafa. Kamba ya kwanza tu ikanasa mtu.

"Oh yeah, been expecting you gentleman, the package is in the basement, you have the code word? Of course you do, you just mentioned it hahaha" (Ahaa! Nilikuwa nakusubiri, kifurushi kipo Chumba cha chini, Bila shaka una namba ya kufungulia Chumba, haha unayo, umeitaja) Musangu akasema kwa sauti lake zito, sauti la zege huku akitoa kicheko cha kindezi. Jipu kuu kusikia vile kichwa kikachemka haraka. Hakutaka kupoteza muda, akaelekea moja kwa moja kwenye Chumba cha chini akishuka ngazi kwa tahadhari. Alipofikia lango la Chumba kile, akasikia sauti kutoka kwenye moja ya spika zilizofichika.

"Please produce the pass code word." (Tafadhali taja neno la siri) Hapo Jipu kuu akajua mlango ule uliendeshwa kwa program mahsusi ya komputa. Muywanga akajikuna kichwa na kutamka kwa sauti ya kujiamini.

"Don-nation!"

Mlango ukachanua kwa uwazi, tapeli akazama ndani. Kulikuwa na uwazi kama vile njia panda. Hapa alipoingia tu mlango ulijifunga na kujipata kwenye kachumba mithili ya lift. Mwanga hafifu ukitawala kachumba hako. Kutani kukiwa na taswira ya vioo.Hapo tena Jipu kuu akajikuta njia panda. Akili ikazunguka, akajikuta anatoa tusi la nguoni. Mara akasikia ile sauti ya komputa.

'Please confirm your pass code word!' (Tafadhali thibitisha neno la siri) Hakujiuliza tena, akatamka

"Don-nation"

Hapo tena ule mwanga uliokuwa unaakisiwa na Vioo ukaleta kitu mfano wa interface (muonekano wa skirini ya monitor Kubwa ya komputa). Neno 'Package:_____________!' Likawa linacheza kwa ule mtindo wa kuonekana na kufifia, kuonekana na kufifia tena. Jipu kuu akajiongeza. Akapeleka kidole pale kwenye deshi. Mara yakatokeza maandishi ya herufi za keyboard


QWERTYUIOP

ASDFGHJKL

ZXCVBNM


Jipu kuu Muywanga likabonyeza herufi zilizoleta neno ‘Helen’. Mara ukajitokeza uwazi mwingine. Chumba kikajitokeza, mbele yake mtoto wa kike, akiwa amemakinika na kitabu mikononi mwake, akionekana kazama kwenye maandishi yaliyosheheni ndani ya kitabu chenye kava lenye picha ya msichana mdogo mwenye huzuni, na mshumaa unaowaka. Maandishi makubwa juu ya kava hilo yakisomeka bayana 'Tineja.' Chini jina la mwandishi wa kitabu hicho David Ngocho Samson likisomeka vema.

Mwanzo Helen Masebo akajua ni mtu wa chakula. Aliponyanyua kichwa akakutana na sura ngeni. 'Leo kaja mtu mwingine' akawaza.

"Mambo Helen, jiandae twenzetu, Hatuna muda mwingi hapa, hawa nyang'au hawana msalie mtume wakinikuta hapa wanakula kichwa!"

Helen akasituka, ina maana huyu ni Nani kama sio wale jamaa watekaji.

"Wewe ni Nani kwani, na alokwambia nataka kutoka hapa Nani? Na umwambie Huyo mjinga mwenzio kama hii ndio adhabu alonikusudia, Mie wala sioni shida, kujichimbia Ndo zangu. Hapa kanileta kwenye liwazo langu hasaa" Helen Masebo akaongea, kwa nyodo. Hakujua kuwepo kwake hapa kulikuwa kunauza nchi. Alijua ni mchezo wa mapenzi akifanyiwa na boyfriend wake wa kimarekani Donald Spence. Hakujua kama Donald Spence mwenyewe alikuwa akihaha kumsaka Kila kona asijue aliko. Hakuwa na wazo kuwa alikuwa kwenye mikono ya adui aliyedhamiria kumtumia kama chambo cha kujimilikisha nchi.

"I didn't think the Helen Masebo, a daughter to a third world country President would be so naïve. You don't understand in what shithole you're in, do you? Get up!" (Sikujua kama Helen Masebo, mtoto wa rais wa nchi moja wapo maskini ni mpuuzi hivi. Huelewi upo kwenye msala gani hapa sivyo? Haya, nyanyuka!)

"Who the hell are you?" (Wewe ni nani?) Helen akabwatuka huku akijifanya kupandwa hasira.

"As naive as you are, you wouldn't understand a thing. Come, let's go! You'll learn on the way!" (Hata nikikueleza hutaelewa. Hujitambui wewe. Hebu twende huko. Utaelewa mbele kwa mbele) Jipu kuu aliongea huku akimshika binti Huyo mkono na kumvuta. Hao, wakatokomea nje.

"Hey man, gotta go now" (Sie tunasepa zetu mzee baba)Muywanga akamuaga Musangu aka Black Jesus.

"So long buddy!" Musangu akajibu huku akitoa Saluti ya kikamanda. Hakujua alikuwa anatoa saluti ya mwisho. Bila shaka Don asingeruhusu mzembe kama Huyo aendelee kudunda huku yeye akizurura Marekani nchi ikiwa mikononi mwa Masebo.


***

Dark Thursday iliyomkumba Don, ilimtia simanzi. Sonona ikamkumba. Akawa analia kama mtoto mdogo asijue nini cha kufanya. Angekuwa na Bomu la nuclear, mwendawazimu huyu angelipua nchi ili wakose wote, na si huku kushindwa alikokuwa amebwagwa vibaya na Masebo. Hofu juu ya usalama wake ikazidi kumtafuna. Angewaeleza nini wale mabwana zake waliomwezesha na mapesa mengi kwa ajili ya harakati zake za kuiweka Jamhuri mikononi mwa mabepari ya kimarekani. Sasa kulimpambazukia jinsi alivyokuwa kwenye shimo refu lenye Kila aina ya hatari. Anatokaje! Ni Swali lililogeuka msumari likimuwamba kwenye msalaba.

Akamwazia tajiri Wilbur Smith na mapesa aliyokuwa kawekeza kwenye harakati za urais, mabilioni ya pesa ambayo yalikwisha tumika kwenye harakati. Akajiuliza kama kafara ya mamia ya watu kwenye sinagogi la Oyono yalikuwa na maana gani kwenye harakati zake kama uwezekano wa kuishika nchi ulikuwa gizani.

Kama ataendelea kuwaza, Mabruki akabaini atachanganyikiwa. Shetani lake likamvagaa. Ashiki zake zikichukua nafasi kubwa kwenye ubongo wake. Akainua Simu yake na kupiga namba ya Didier Masele.

"Didier mpenzi, Fanya uje haraka. La sivyo nakufa mwenzio" Mabruki akatamka kwenye Simu, deko la mtoto wa kike likiipamba sauti yake.

"Nakuja.." Didier Masele akajibu akishindwa kumalizia neno ambalo kawaida alilitumia walipowasiliana na Don. Neno ambalo alilazimika kulisema huku likimchefua roho yake. Neno 'mpenzi'

Kwanza hakutaka kulisema kwa vile siku zote lilimkera kulitamka na kutamkiwa na mwanaume mwenzie. Pili, wito Huu ulikuwa unamweka kwenye ukurasa mpya. Ukurasa wa kutenda jambo ambalo hakuwahi kuwaza angelifanya kisa mapenzi. Agizo la Mc one, lilikuwa litekelezwe Leo.

Nusu SAA baadae Didier Masele alikuwa kawasili kwenye kasri la Don Mabruki Ally. Alizama ndani na kumpata mheshimiwa Masebo akijimiminia vinywaji vikali vikali venye kilevi cha kiwango kikubwa sana.

"Oh dear, you have come" (Oh, umefika mpenzi) sauti la mlevi likamtoka Don.

"Hey, what are you doing? Look at you! You're a mess, sir" (Unafanya nini sasa, umejiona? Unatisha kwa kweli Mzee) Masele akatamka.

"Hey, you don't call me sir, you call me the sweet name, 'darling','dear', 'love,' not sir! You hear me? Huh!" (We, Nani Mzee? Hebu niite 'mpenzi', 'mahabuba', 'barafu wa moyo', unasikia, ha!) Don aliendelea kuongea kwa sauti la kilevi.

"Ok, 'darling'" (sawa basi 'mpenzi') Didier Masele akatamka! Don akafurahi, meno thelathini na mbili yote yakawa nje. Akamvuta kijana huyo na kumbusu midomoni na kumvuta shati lake akimpeleka chumbani.


***

Aliposimuliwa kilichokuwa kinaendelea, Helen Masebo alibaki na bumbuwazi la bayana. Alipopewa habari za mama yake kupooza baada ya kuona ile video iliyorekodiwa wakati akikamatwa na kuvuliwa Nguo mbele ya wanaume waliokuwa majabali wakiwa vifua wazi, Helen nguvu zilimwishia na magoti yake yakashindwa kumbeba akaanguka chini kama zigo. Hiyo haikuwa habari pekee aliyopokea. Habari kuwa sasa baba yake alikuwa tu kibaraka wa Don ilimnyong'onyesha hakika. Akajilaumu kwa kuendekeza upuuzi wakati wazazi wake wakiwa hatarini, akajilaumu kwa kuwaza mapenzi wakati taifa lake likiwa kwenye hatari ya utumwa wa kisasa. Kilio cha kwikwi kikamtoka.

Akapanga safari ya kwenda kumuona mama yake huko hospitali ya Appolo nchini India. Muywanga kusikia hivyo akaangua kicheko cha dhihaka. Helen akakunja sura kwa hasira kufuatia kitendo hicho.

"You're the dumbest woman I have ever met!" (Wewe ni mwanamke mjinga zaidi kuwahi kukutana naye) Muywanga akatamka huku akimalizia kwa kicheko chake kilochomkera zaidi Helen.

"Huwezi kufikiri hata kidogo? You're the only bait Don can use to rule your dad and the country, wake up girl. Use that big head of yours." (Wewe ndiye chambo pekee Don anaweza kutumia kumwendesha baba yako na hata nchi. Amka binti, tumia vema hilo bichwa lako kubwa!) Muywanga akamkejeli tena. Helen akangua kilio. Akahisi amedhalilika sana!

"Haya, unalia? Basi mama nyamaza. Wewe una akili sana!" Muywanga akamsogelea Helen na kumpa kitambaa chake.

Helen akakipokea kitambaa na kufuta tumachozi twake. Alipomaliza akanyanyua kichwa, hamadi, akakutana na uso wa Muywanga, macho kodo yakimwangalia. Akanyanyua mkono wake na kumpiga kibao dhaifu mwanaume Huyo mwenye tambo. Akanyanyua tena amtandike kibao chenye shibe, akakutana na mkono wa Muywanga, mkono wenye shibe kuliko wake. Muywanga akamkamata na kumvutia kwake, mtoto wa kike akaangukia kifuani mwa tapeli. Tapeli Muywanga akaanza kumpeti peti mgongoni huku akimwimbia

“mtoto nyamaza kulia, mtoto nyamaza Tafadhali"

Lo! Mtoto wa kike akanyamaza kimya huku akionekana kuburudika vilivyo na ubembelezi ule.

Baada ya muda kidogo, Muywanga akiwa katopea kwenye wingu la mahaba akapokea kibao kizito mgongoni huku akisukumiwa nyuma.

"A bad boy!" Helen akapaza sauti yake akiwa amemaanisha kijana huyo ana tabia mbaya.

Muywanga tabasamu likamtoka utadhani mchaga kaona hela.

***

Siku ya ijumaa baada ya Dark Thursday, ilimpata Don kwenye ulimwengu wa wafu. Taarifa za kifo chake zikisambaa kwenye vyombo vya habari kote duniani. Taarifa hiyo haikukawia kufika Tanzania.

‘Katika kile kinachoonesha madhara makubwa ya dawa za kulevya, si kwa nguvu kazi ya taifa kwa maana ya vijana tu, Kifo cha mheshimiwa Mabruki, Waziri mstaafu wa Tanzania, ambaye amekumbwa na umauti kutokana na matumizi ya kupitiliza ya dawa za kulevya, kumedhihirisha ni kwa namna gani vita juu ya dawa za kulevya inapaswa kuendelezwa kwa bidii zaidi. Kwa masikitiko makubwa, dawa za kulevya zimetunyang'anya mpiganaji makini wa demokrasia nchini.

‘Mheshimiwa Mabruki atakumbukwa kwa utumishi uliotukuka alipokuwa waziri hapa nchini na kuleta maendeleo makubwa nchini. Wananchi wa Urambo wataendelea kumkumbuka mheshimiwa Mabruki kwa jinsi alivyokuwa mpambanaji ambaye aliwezesha maendeleo makubwa kwa wakina mama, vijana na wazee jimboni. Alikuwa Nguzo Kubwa ya siasa za kidemokrasia nchini. ....”

Liliandika gazeti la mwana-Tanzania


***

Didier Masele aliliweka gazeti la ‘La Vegas Tribune’ chini, akishindwa kuamini nini kilitokea. Kumbukumbu zake zilikuwa sawa kabisa. Ni kweli alikwenda ili kutekeleza agizo la Mc 1, lakini mkongo huyo, roho yake nyepesi, uwezo wa kuondoa uhai wa mtu hakuwa nao. Baada ya kushindwa kabisa kutekeleza mauaji hayo, Didier Masele aliteleza na kumuacha Mabruki, akikusudia kujificha kabisa asipatikane na Mc One. Akili yake ilimshawishi kuamini kuwa hata kama angemuua Mabruki, usalama wake haungekuwa na uhakika. Tayari angekuwa ni mtu wa kuwindwa na labda kwa kile ambacho kingeonekana kuwa yeye ni shahidi, wabaya wa Mabruki wangemteketeza kuufuta ushahidi huo. Hivyo, alikusudia kukimbia. Kama angekimbia, bila shaka Grace asingekuwa na faida kwao na kwa hivyo akajipatia tumaini kuwa angeachiliwa huru.

Taarifa kuwa Mabruki amekufa kwa kuzidisha madawa ya kulevya, ilimwacha mdomo wazi Didier Masele. Ni kweli Mabruki alionekana kuwa na sonona sana, lakini kujiua! Hakupata jibu. Kama ilivyokuwa kwa wengi, Masele akaamua kuridhia kuwa inawezekana kweli, alijizidishia dozi ya dawa za kulevya bila kusudio la kujimaliza.

Akaamua kurejea ghetto kwake, kama Don amekufa, bila shaka hakukuwa na haja ya kukimbia tena, kwa vyovyote vile, Mc One atajua ni kazi ya mikono yake, Masele akajitia ujasiri, akidhamiria lolote liwalo na liwe, alitaka kujua kama Grace sasa atakuwa huru au la, baada ya hapo angeamua ama kujichimbia au kuendeleza maisha yake ya muziki kama kawaida.

Alifika ghetoni kwake saa mbili za usiku, akaingia nyumbani kwake kama mwizi, akitazama huku na kule kujihakikishia kuwa kulikuwa na usalama. Alipoingia tu sebuleni, alikuta mlango wa chumbani kwake ukiwa wazi, mapigo ya moyo yakajipata yanaruka kichura bila ridhaa yake, nguvu zikamwishia, akajua sasa lile alilokuwa anawaza sasa limemfika. Hofu yake sasa ikawa bayana.

Wamekuja kuniua, akawaza

Hata hivyo akaamua kuchungulia kulikoni huko chumbani kwake, akavuta pumzi ndefu na kutuliza moyo, furaha ya kumkuta Grace, akiwa kajipumzisha kitandani kwake ikamuondolea wasiwasi wote aliokuwa nao! Masele akavua viatu na kuingia kwa kunyata, alipomfikia mpenziwe huyu, alimtazama huku akimshukuru Mungu, kwa kufumbata mikono yake kifuani na kisha kuinyanyua juu na kunong’ona

“Asante Mungu”

Akambusu shavuni, Grace akafumbua macho yake na kumpiga kofi la mahaba,

“Ndio nini kuniacha nikusubiri muda wote huu na simu yako hata haipatikani?” Grace akalalama kwa sauti ya kudeka.

“Dah! Kwanza ungeniuliza kulikoni, mwenzio nimetoka kupambana na zimwi mtu, ni maombi yako tu yameniokoa, nakupenda sana mpenzi” Didier Masele akamkumbatia Grace, machozi yakimtiririka, labda aliomboleza kifo cha Mabruki, au hakuamini kuwa sasa alikuwa huru dhidi ya zee lile.


***

Taarifa kutoka kurugenzi ya habari ikulu ilirusha matangazo ya moja kwa moja kutoka ikulu, rais wa serikali ya mpito mheshimiwa Sebastian Masebo akilihutubia taifa kufuatia kifo cha mheshimiwa Mabruki. Rais akimwelezea marehemu kama mpiganaji asiyekata tamaa na kudai alimfahamu hivyo tangu walipokuwa watoto, na kwa Mara ya kwanza Masebo akaujulisha umma juu ya undugu wao.

"Ni kwa masikitiko makubwa sana tumepokea taarifa za kifo cha ndugu yetu Mheshimiwa Mabruki Ally kilichotokea huko Marekani. Mabruki ambaye binafsi yangu nilimfahamu tangu utotoni tukicheza pamoja, alikuwa mtu asiyetaka kushindwa hasa pale alipoamini kwenye hoja yake. Alikuwa mpambanaji asiyekata tamaa. Ni mtu aliyetumia nafasi zake serikalini kwa faida ya wananchi wote. Amekuwa mhimili imara katika maendeleo ya nchi yetu tukufu. Kwa hakika, tutamkumbuka daima.

Tunapoendelea kumkumbuka marehemu Mabruki, tukumbushane pia, kwamba madhara ya dawa za kulevya hayana macho kusema yanatambua huyu ni Mheshimiwa au mtu wa kawaida. Matokeo ya madhara ya dawa za kulevya ni dhahiri. Tunapoteza watu wetu kutokana na dawa za kulevya.

Hayaangalii kuwa huyu ni mtu mwenye wafuasi, au muhimu kwa taifa. Nitoe rai kwetu sote kama watanzania kuungana mikono kwa ajili ya kupambana na Biashara ya dawa za kulevya. Na nikiwa kama rais, kwa mamlaka niliyopewa na katiba yetu, natangaza Kila Ijumaa ya pili ya mwezi wa Sita, Itakuwa siku ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini. Niwapeni pole wote ndugu zangu watanzania kwa msiba Huu wa taifa.

Mungu ibariki Afrika.

Mungu ibariki Jamhuri."


***

Ilikuwa siku ya Furaha. Malcolm Stounch alikuwa kwenye jumba lake huko Johannesburg, muda mfupi uliopita alikuwa kwenye mitambo akiwasiliana na Mc one. Mc one akimthibitishia kuwa Don ni habari ya Jana. Kifo kilichoandaliwa kuonekana kama kifo cha kujitakia. Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya kulikopindukia.

Moyoni, Malcolm Stounch alihisi Faraja kulipa kisasi cha pacha wake Elinisa Urio. Lakini pia akijiona mzalendo kwa kuwezesha kufa kwa mpango dhalili wa Mabruki kuikabidhi nchi kwa mabepari mahasimu wake Wilbur Smith na wenzake. Watu ambao pamoja na utajiri wao walikuwa na ajenda mbaya sana za kishetani za kutaka kuitawala dunia kwa kumong'onyoa maadili safi na kubomoa ubinadamu na kutawaza ushetani.

Safari ya kurejea Tanzania kuzuru kaburi la Elinisa ndicho kitu kilichokuwa kinaendelea akilini mwake.


***

Kilikuwa kikao cha ile kamati teule. Kikao cha dharura! Agenda ilikuwa moja tu. Rais Sebastian Masebo kujiuzuru. Kwenye historia ya nchi angekuwa ni rais aliyehudumu kwenye nafasi hiyo yenye heshima Kubwa kwa muda mfupi zaidi. Kikao hiki kilikusudia hilo. Kifo cha Mabruki hakikumhakikishia uwezekano wa kuendelea kudumu madarakani.

Alipotakiwa kujitetea juu ya hoja ya kamati teule, Masebo Hakuwa na kitu cha kusema zaidi ya kuomba samahani kwa kuliangusha taifa na kukubali kujiuzuru wadhifa wake. Wadhifa ambao kwa muda mfupi alioutumikia, alijikuta anazeeka huku akiishi maisha ya wasiwasi. Ni katika nafasi hiyo ambapo Mke wake mpenzi alikopatia ugonjwa wa kiharusi.

Kesho yake, Mheshimiwa Masebo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza rasmi kujiuzuru wadhifa wake wa urais wa serikali ya mpito.

Wakati hayo yanatokea, Malcolm Stounch alikuwa nchini Tanzania pamoja na familia yake. Binti yake Jackline na mjukuu wake Davidson kwa upande mmoja, na mkewe Asha na mtoto wao mdogo Elinisa Junior kwa upande wa pili! Walionekana wenye Furaha mno. Baadae wangekuwa na tafrija ndogo Malaika Hotel ya kumpongeza Dina kwa uamuzi wake wa kuingia kwenye Kinyang’anyiro cha ubunge baada ya Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ndugu Dule Moringe kutangaza tarehe za uchaguzi Mkuu. Bila shaka angeshinda. Kamati teule iliutambua mchango wa familia yao kwenye ile vita ya Don.


***

Gazeti la ‘Sauti ya mwananchi’ lilitokeza mitaani na habari iliyosisimua. Likipambwa kwa picha na maandishi ya herufi kubwa.

‘VIONGOZI WA DINI WALIOKULA NJAMA NA KUTEKETEZA MAELFU YA WAUMINI WATIWA MBARONI.’

Ni yule mtume na nabii mwenye kitabu cha miujiza pamoja na kiongozi wa kundi la Ali haki fighters.

Lengo lilikuwa ni kutumia uhasama wa kivita ili kutengeneza njia ya kisiasa kwa kundi lao la kishetani, sauti ya mwananchi limetonywa na mtu wa karibu wa viongozi hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Sauti ya mwananchi linao ushahidi wa sauti na video za kikao cha watu hao kabla ya kutekeleza tukio lililoangamiza ndugu zetu, watanzania wenzetu.

Hakika kuna haja ya kufanya kilichofanywa na rais wa Rwanda hapa nchini, kufuatilia kwa undani madhehebu na vikundi vyote vya kidini nchini kabla ya kupitisha usajili wake……….

Maelezo yalikuwa mengi juu ya taarifa hii iliyoandikwa kwa mfumo wa makala.

Mitaani nako, hali ilikuwa tulivu. Raia wema wakiendelea na pilika pilika zao za kulijenga taifa.


Machera alikuwa ukweni, utambulisho rasmi ukifanyika. Tabasamu la kuvunja na shoka likitamalaki, wakati anasalimiana na wakwe zake. Tukio hilo likihudhuriwa na Malkia wa Kiha, Ken na mchumba wake Martha ambaye alikuwa burudani tosha kwa wapendanao hao aliposimulia tukio la Sea Cliff Hotel alipokutana na Joze Kijo.

Tamati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom