VIDEO: Dr. Ulimboka; kwa kinywa chake mwenyewe! | Ambayo hukuyajua...

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Baada ya kusikia maneno toka kwa wadau mbalimbali, toka magazeti mbalimbali na vyombo vingine vya habari juu ya NINI kilimsibu na NANI anahusika; tumeona ni vema kuwashirikisha video hii ili mweze kusikia toka kinywani mwake mwenyewe.

Nikiweka maneno mengi nakuwa nachakachua, ni vema kukupeni alichokiongea kwa kinywa chake.

NB: Video hii ruksa kutumiwa na vyombo vingine vya habari kuwahabarisha wengine wasio na access na JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Namna hii hatuna serikali bali genge la wauaji na wahuni kama kweli kuna mkono wa serikali. Kwanini serikali hata hivyo inakana kwa utetezi mwepesi? Huu ni uhuni piga ua na wahusika watakuja kulipa siku moja watake wasitake.

Kama watanzania wangekuwa watu makini, hili lilitosha kufyatua tufe la hasira zao na kufanya kweli. Ukitaka kujua mtu anajisikiaje anaposoma au kusikia vitu kama hivi, jaribu kupiga picha ingekuwa ni wewe.
 
Thanks invisible. Ni kama mvua za rasha rasha vile maana imekuwa too short. Namuombe apate afya njema Dkt Ulimboka na wagonjwa wengine wengi wanaokosa huduma za afya sababu ya mgogoro huu unaoendelea. I hope we will come our senses and rescue the situation. The earlier the better
 
Tunashukuru kwa hii clip Invisible, ndio nimemuona kwa mara ya kwanza live toka tukio. Hii inasikitisha kwa kweli... In some way hata Ulimboka alikuwa na makosa. Kuonana na mtu ambae hamfahamu vizuri usiku ni hatari saana ukizingatia nafasi, hali, demand na circumstances zake. Maybe ali undermine umuhimu wake, else naamini kabisa alitegeka kirahisi mno.

Pole zake kwa kweli... nasikitika tu kuwa hatuna guts za kufanya lolote, ingekuwa nchi za wenzetu pangekuwa padogo kwa Serkali.
 
Last edited by a moderator:
Namna hii hatuna serikali bali genge la wauaji na wahuni kama kweli kuna mkono wa serikali. Kwanini serikali hata hivyo inakana kwa utetezi mwepesi? Huu ni uhuni piga ua na wahusika watakuja kulipa siku moja watake wasitake.

Kama watanzania wangekuwa watu makini, hili lilitosha kufyatua tufe la hasira zao na kufanya kweli. Ukitaka kujua mtu anajisikiaje anaposoma au kusikia vitu kama hivi, jaribu kupiga picha ingekuwa ni wewe.

JK atakufa vibaya kama ni yeye kawatuma kumfanyia Uli hivi,mungu aliye hai atamuadhibu tu
 
Inasikitisha sana kusema kweli....halafu hii Serikali ya wauaji inajifanya haihusiki katika dhamira ya kutaka kumuua Ulimboka.
 
Hii inasikitisha kwa kweli... In some way hata Ulimboka alikuwa na makosa. Kuonana na mtu ambae hamfahamu vizuri usiku ni hatari saana ukizingatia nafasi, hali, demand na circumstances zake. Maybe ali undermine umuhimu wake, else naamini kabisa alitegeka kirahisi mno.

Pole zake kwa kweli... nasikitika tu kuwa hatuna guts za kufanya lolote, ingekuwa nchi za wenzetu pangekuwa padogo kwa Serkali.

Ndio hivyo tena majuto mjukuu. But he didnt deserve that kind of treatment kwenye nchi yenye sheria na taratibu.
 
Ni hatari sana kwa serikali kutumia njia za namna hii kumaliza matatizo ya wananchi!!
 
Ndio hivyo tena majuto mjukuu. But he didnt deserve that kind of treatment kwenye nchi yenye sheria na taratibu.

Ndahani sema wabongo tumezoea shortcuts na kuchukulia uwepesi wa mambo. Zamani ilikuwa haina shida kukutana na mtu humjui... sasa hivi hali imebadilika sana, na hasa kama wajihusisha/unahusika na mambo amboyo yapo tangled na politics. He surely did not deserve, nobody deserves that, ila tu amini nakuambia he did undermine his position... na ashukuru Mungu yupo hai, ni kumuombea tu kuwa wakute hakuna tatizo lolote kiafya hasa kwenye ubongo.
 
Last edited by a moderator:
Ndio hivyo tena majuto mjukuu. But he didnt deserve that kind of treatment kwenye nchi yenye sheria na taratibu.

Mkuu Ndahani...hakuna sheria na taratibu katika nchi yetu vinginevyo tusingefika hapa tulipo ambapo mambo yanafanyika kienyejienyeji tu watu kulambishwa/kupakaliwa sumu watu kukwapua mali za Watanzania bila woga wala kificho na huku Serikali ikiogopa kuwatia hatiani.
 
safi sana invisible big up sana..japo uwa sometimes nakuchukia kwa BAN ila kiukweli mambo yako murua sana
 
There is light at the end of tunnel...always the fears of coward is to murder! this infedel failed to murder you. poor choice of ideas they choose to throw stones while they living in glass house.
 
Back
Top Bottom