Chronovisor: Kifaa kilichotumika kutazamia matukio halisi ya kale (Sodoma na Gomora na kusulubiwa kwa Bwana Yesu)

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,369
Sabal-kheyr wakuu,

Na DA VINCI XV

59E93549-3654-4517-A575-36455FFFD0FC.jpeg

Siku chache kabla ya Pasaka na Siku ya Pasaka yenyewe nlipata wasaa wa kupitia , makala tofauti tofauti kuihusu.

Huku wengi wakiadhimisha siku hiyo na wengine wakiandika kuonyesha udhaifu na mapungufu ya siku ya hiyo na Utaratibu wake.

Wengine wakatoa na shahidi tofauti tofauti za maandiko kuonyesha kinachoadhimishwa katika siku hiyo ni tofauti na kilichosemwa na Mungu katika vitabu kiadhimishwe.

Nikapata pia wasaa wa kupitia makala inayoelezea Vatcan namna walivyopika hii sherehe isherekewe kwa namna ipi na kwa kufuata tukio Lipi tofauti na maandiko yalivyotaka? Na mwandishi wa makala hiyo alitoa Vifungu vyake.

Ilipotajwa Vatcan nikakumbuka mengi nikakumbuka Story nyingi zinazoawaandama, nikakumbuka Holy Grail, Nikakumbuka DNA iliyohifadhiwa ya Bwana Yesu isitambulike, nikakumbuka habari ya Sanduku la Agano na Silver Hammer inayotambua Mortality ya Watu hasaa maPope.

Vyote hivyo vinashutumiwa dhidi yao Vatcan kwamba vimehifadhiwa Sehemu maalum visitambulike na Ulimwengu kama bado vipo.

(Hata sisi hatujui lolote kama ni Shutuma tu au ni habari ya Kweli)

Baada ya hapo nami nikaona nikumegee kidogo habari ya Kifaa hiki ambacho inadaiwa nacho kimehifadhiwa ndani ya kuta za Vatcan kwa ajili ya Manufaa mengine.

23A81705-75E6-483F-8E50-16BA9B140EC0.jpeg

Ningeweza kupata wasaa wa kusafiri au kushuhudia matukio na mambo ya miaka ya kale basi ningetamani kwenda kutazama Kipindi cha Adam na Hawa pale Eden, ningetamani kusikia Mama yetu Hawa alipata kuongea mambo gani mengine na Nyoka ukiachana na Masawala ya Tunda la Uzima.

Halafu ningetamani kwenda kumshuhudia, Musa na Sakata la Miujiza yake ya Nyoka pale kwenye Ardhi ya Firauni, na kule jangwani baada ya wana wa Israel kumnenea Uongo Mussa na Mungu wake.

Halafu ningetamani kwenda kushuhudia ya Bwana Yesu na miujiza yake ya kufufua wafu, hapa ningetamani kumuuliza vingi lakini sidhani kama wakati huo ningeupata.

Pia ningetamani sana kumshuhudia ,Mtume Muhammad na Harakati zake kusambaza dini ya Uislam halafu na miujiza yake na ningetamani kuona pia jinsi alivyoutawanya mwezi vipande Viwili magharibi na Mashariki,

Ningetamani kuona vingi sana hata kumsuhudia Chief Mangungo wa Msovero na jinsi alivyosainishwa Bogus Treaty ,ningemuuliza ilikuwaje tena nae mzee wetu dhoruba hii ikamkuta?

Unadhani hilo lingetosha ningetamani hata kuwaona hao dinosour kama walikuwepo kweli, Ningetamani kumshuhudia tajiri Mansa Musa, ningetamani kuona hizo jamii za kiafrika zilizoendelea kama Misri ya Kale, Ethiopia hata huko Mali, kifupi yapo mengi sana ambayo ningetamani kuyashuhudia.

THE CHRONOVISOR

CE817AB6-6BCD-41B1-B2E4-9CCAF1FAC918.jpeg
Mwamba mmoja kutoka huko Italiano mtaalam, Na mwanafizikia mtu wa kanisa Father Pellegrino Erneti , ukitaja jina hilo basi moja kwa moja Kifaa hicho kilichohusika na kutazma matukio ya zamani alihusika nacho kama mtengenezaji na mvumbuzi wa kifaa hicho kiitwacho Chronovisor.

74D48EBD-B5D8-4D9A-AD40-7B1CB7DD5021.jpeg


FATHER ERNETI
Habari hizi zilianza kusambaa miaka ya 1972 baada ya Gazeti la habari la Italia liitwalo La domenica del Corriere. Kuchapisha habari za bwana Erneti na Madai yake ya kifaa hicho.

Father François Brune katika kitabu chake cha mwaka 2002 alichokipa jina la “Le Nouveau Mystere du Vatican,” akadokeza kuhusu uwepo wa kifaa ambacho kimesahaulika ambacho ni Time travelling device iliyotumika kuangalia na kutazamia matukio ya zamani na yajayo.

ED3867C0-4862-455E-BB2F-48B2351EA4B8.jpeg

Father Bruno anapata kusema alijifunza habari za Chronovisor miaka ya 1960s , alipobahatika kuketi na Mwanafizikia na Mvumbuzi wa kifaa hicho ambaye ni Father Erneti mwenyewe.

Father Bruno anaeleza kwamba alikutana na Father Erneti kujadilialiana na kufafanua habari za Biblia kwa Ujumla, hivyo akapata na wasaa wa kufunzwa na Bwana Erneti kuhusu kifaa hicho namna kinafanya kazi, na alikiri sio tu kuona matukio hayo yaliyopita bali pia kilimwezesha mtazamaji wake kuskia kila kilichozungumzwa katika aliyoyatazama.

Hivyo kuwezesha kutambua kitu halisi namna kilikuwa tofauti na kupokea masimulizi au maandishi.

B9CFD79B-2B67-45E7-9343-B16C27D28CD9.jpeg
Kama ilivyo vifaa vingine vya Thamani wengine hudai kama ilivyofichwa na kuhifadhiwa Holy grail, Sanduku la Agano na vinginevyo basi kifaa hiki pia kimehifadhiwa na Vatcan na ni moja ya nyenzo yao ya Siri sana.

Kifaa hiki kimeundwa na Metalic za thamani tofauti tofauti ambazo husaidia kupokea Sauti na lightwave na pia kimeundwa na Madini yenye thamani sana, Pia kuna Cathode (a negatively charge Electrode) na Vitu vingine vingine ambavyo kwa Pamoja humwezesha mtazamaji kushuhudia kama anavyotazama Televisheni matukio yaliyopita na yajayo kwa Ujumla, na hiki Erneti mwenyewe alisema ni Moja ya Uthibitisho wa kuwepo Bwana Yesu, Tofauti na Masimulizi ya Maandiko matakatifu.

Kifaa hiki kilitengenezwa na Jopo la wanasayansi kadhaa kwa Siri ambao wengine majina yao yamefichwa kutoka Italia, waliojulikana ni Father Ernerti mwenyewe (Mfumbuzi) Pamoja na Mwanafizikia Enrico Fermi huyu, uwezo wake hauna wasiwasi kabisa alishashinda tuzo ya Nobel kwenye maswala ya Fizikia 1938 ("for his demonstrations of the existence of new radioactive elements produced by neutron irradiation and for his related discovery of nuclear reactions brought about by slow neutrons.”)

D8A1F185-32A8-43A5-8910-DEDAB2E5CA7B.jpeg
ENRICO FERMI
Hivyo ni miongoni mwa wanafizikia wakubwa sana ambao wakosoaji wa kifaa hiko walipata kidogo kigugumizi kusikia nguli huyu wa Fizikia ni miongoni mwa wanajopo hilo.

Kuhusu Erneti wengi walijawa na Imani nae kwakuwa alikuwa mwanakanisa pia hapo Italia.

Kuhusu Mwanafizikia Fermi kidogo watu walihoji kwanini hakuwai kuongelea chochote, kuhusu kifaa hicho hata hivyo jina lake lilihusishwa na Jopo hili baada ya kifo chake hivyo baadhi ya Wakosoaji kupata la kusema.

61285EB0-E5E8-4DF0-A440-A34C2C1AB64D.jpeg


VON BRAUN
Mwamba mwingine ambaye fununu zilimtaja kwamba alishirikiana na Vatcan katika kutengeneza hicho kifaa ni Wernher Von Braun, ambaye alikuwa miongoni mwa wanasayansi wa NAZI na alitumika pia na NASA, alihusika katika kuunda Saturn V ambayo ilitumika katika Mission za NASA kama Apollo mission na pia alihusika katika uundaji wa Chombo kinachodaiwa kilitumika kutengeneza Silaha za Hatari za NAZI na Adolph hitler alikitumia kufanyia Time Travelin kinachoitwa Die Glockie.

Nilizugumzia hii issue katika nyuzi ya Die Glockie hivyo likapelekea jambo hili kutiliwa mkazo hasa kutokana na uwepo wa watu hapo wazito

CCF5DD18-22B4-45EE-8B07-F8D695C937F3.jpeg

Kuhusu Die glockie soma: https://www.jamiiforums.com/threads...a-za-ajabu-na-kufanya-time-traveling.1968457/

USHAHIDI NA MATUKIO YALIYOONESHWA NA CHRONOVISOR

F42A84C1-D266-4EA6-8738-1102D061E81C.jpeg

Naam, Hili ndilo haswa lililenga, akili za watu hakuna asiyetamani kuona Bwana Yesu alifanania vipi?

Lakini kama iwapo Father Erneti hatupigi tukio (kutudanganya) basi huenda (hii) hizi zikawa taswira za kweli za Matukio aliyodai kwa mtazamo wake yakuwa yalitokea dhahiri na katika uhalisia wake. Who knows?

Ushahidi pekee ambao utathibitisha kwamba kifaa hiki kilikuepo au kipo ni uwepo wa Taswira na Picha hizo ambazo zimetumika kutazama kupitia kifaa hicho.

ED7BA55D-96AD-47BB-87D9-A20A61BD0A6F.jpeg

Hiki ni kitu cha kwanza ambacho Father Erneti alidai kufanikisha kukitazama kupitia chronovisor, humo alipata kuona Yesu akiwa msalabani akisulubiwa japo, jopo kubwa la wanasayansi waliibuka na kupinga vikali kwamba picha hizo zina utata wa hali ya juu (Dubious Photographs)

Si hilo tu bali alisikia pia hata kilichokuwa kikizungumzwa hapo wakati wakimsulubu Bwana , na matukio baadhi baadhi ambayo yalifanywa na Bwana Yesu.

Tukio lingine ambalo Father Erneti alipata kusema aliweza kushuhudia Mlo wa mwisho wa bwana Yesu na wanafunzi wake (The Last Supper).

Pia alipata kuona Hotuba na Mikutano mbalimbali ya Viongozi wa miaka hiyo wa Roman Empire na akaongeza zilikuwa ni miongoni mwa Jamii zenye nguvu sana wakati huo kama namna alivyoshuhudia mienendo yao.

F65D3F45-C2E4-4152-84E3-A18B98602C82.jpeg

Pia alidai kushuhudia namna Miji ya Sodoma na Gomora ilivyoangamizwa na Mungu baada ya Miji hiyo kukithirisha tabia za Ushoga na Liwati miongoni mwa wanaume wakati huo.

Pia Father Erneti alidai kumwona Mshairi wa Zamani wa Kirumi aitwaye Quintus Ennius na kuelezea baadhi ya kazi zake ambapo pia alileta na vifungu kadhaa vya kazi za Ennius ambazo sasa hivi zimepotea lakini alipata ukinzani baada ya watafiti kubaini kuwa Maneno ya kilatin aliyotumia Erneti yalianza kutumika miaka 200 baada ya Ennius.

Hivyo ni dhahiri kwamba maneno hayo hayakuepo katika kazi za Ennius. Sambamba na hayo yote wakosoaji waliibuka na kupinga na kukosoa kisomi kila walipoona kuna udhaifu kwa namna moja ama nyingine.

Halii hii ilizua taharuki wakati huo na kufanya wakosoaji wengi kutafuta kila namna ya kufanya majadiliano dhidi ya Father Erneti, wasomi wengi waliibuka na hoja mbali mbali kibaya zaidi Erneti hakupata kueleza ni namna gani kifaa chake hicho hufanya kazi na kila alipoulizwa uwepo wa kifaa hicho alitoa majibu ya kwamba kimesambaratishwa ili kuepusha kifaa hicho kuangukia mikononi mwa waovu na kutunza kizazi kijacho na kukiweka mbali na Matatizo kwasababu ni kifaa hatari sana.

Kabla ya kifo cha Father Erneti alipata kuandika barua na kuendelea kusimamia msimamo wake kwamba kifaa kile ni kitu cha kweli na halisi , na akasema Papa Pius XII aliwaonya kutotoa taarifa zozote kuhusu kifaa hiko kwasababu kifaa hicho ni miongoni mwa vitu vya hatari sana. Watu wengi baada ya hapo wakahitimisha huenda kifaa hiki kimehifadhiwa hapo Vatcan.

61FDB548-BDB1-4D3D-A3A4-8E739327E334.jpeg
POPE PIUS
UPI MTAZAMO WAKO
  • JE, KIFAA HIKI KILIPATA KUWEPO AU NDIYO DRAMA ZA ULIMWENGU?
  • KAMA KILIKUWEPO JE NI KWELI KILIWEZA KUCHUKUA PICHA NA MATUKIO YA ZAIDI YA MIAKA 2000 HUKO NYUMA?
  • KAMA ILIWEZEKANA, JE, HIZI PICHA AMBAZO ZIMEHIFADHIWA NI ZA WAHUSIKA KWELI NA MATUKIO YA KWELI?

• Kama anavyodai Father Erneti kwanini kifaa hiki kiharibiwe? Ili kuficha nini? Kwanini kisingetukimika kwa mkakati maalumu ili kuthibitisha mambo tofauti tofauti?

•Je, Unadhani Vatcan watakuwa wamehifadhi kama wanavyodaiwa kuficha Vitu vingine vitakatifu?

WHO KNOWS
DaVinci XV
 

Attachments

  • 76F74E73-EA50-4BA4-89A4-21DB67981D52.jpeg
    76F74E73-EA50-4BA4-89A4-21DB67981D52.jpeg
    46.4 KB · Views: 18
Anyways sina la kusema Sana kuhusu hao wataalamu na mambo Yao

Ila

Nina la kusema kuhusiana na ardhi kuweka kumbukumbu ya kila kitu katika Maisha yetu,nasikia sasa hivi kuna kamera ambayo inaweza kukamata kivuli cha kwenye ardhi,Kwa mfano mpo kwenye mkutano watu kadhaa na baada ya kuondoka ukumbini,basi mtu akija kupiga picha pale ataona vivuli vyenu na kutambua mlikuwa wangapi.

Kwa upande wa Imani ya Dini hasa ya kiislamu,kuna ushahidi Kwa mujibu wa mafundisho yetu kwamba ardhi itatoa ushahidi Kwa Yale ambayo tuliyafanya hapa duniani,kama ulienda gesti basi kipande Hicho cha ardhi husika kinahifadhi kumbukumbu zako na kuja kuzileta baadae

Kwahiyo ni kweli ardhi inahifadhi taswira sasa ni Kwa namna gani huyo mwamba alikuwa na mkweli na kifaa chake ndio hatujui.
 
Hao jamaa nao wasiri sana, na ubaya miaka hii ndo hawajibu kitu wanapiga kimya tu.
 
Naweza kuamini kwakua tech haina mwisho,Ila nina weza kuhoji ili kujiridhisha na hio tech, mfano aliwezaje kudili na habari za watu maharufu tu?Mfano dunia ilikua na watu 200000 alitumia code gani kupata story za watu 20 tuu?.Pia hicho kifaa kama kina uwezo huo kwanini hawakuwa na wazo la kumwona mungu mwenyewe ama kuona ulimwengu wakati wa upya wake?.Ni hayo tuu
 
Anyways sina la kusema Sana kuhusu hao wataalamu na mambo Yao

Ila

Nina la kusema kuhusiana na ardhi kuweka kumbukumbu ya kila kitu katika Maisha yetu,nasikia sasa hivi kuna kamera ambayo inaweza kukamata kivuli cha kwenye ardhi,Kwa mfano mpo kwenye mkutano watu kadhaa na baada ya kuondoka ukumbini,basi mtu akija kupiga picha pale ataona vivuli vyenu na kutambua mlikuwa wangapi.

Kwa upande wa Imani ya Dini hasa ya kiislamu,kuna ushahidi Kwa mujibu wa mafundisho yetu kwamba ardhi itatoa ushahidi Kwa Yale ambayo tuliyafanya hapa duniani,kama ulienda gesti basi kipande Hicho cha ardhi husika kinahifadhi kumbukumbu zako na kuja kuzileta baadae

Kwahiyo ni kweli ardhi inahifadhi taswira sasa ni Kwa namna gani huyo mwamba alikuwa na mkweli na kifaa chake ndio hatujui.
Naam nishapta kupitia maandiko hayo, just imagine hata viungo vya mwili vitatoa ushahidi hiyo siku itakuwa nzito sana.

Ukiachana na hayo yote , kama hili swala liliwezekana basi walifikia kiwango cha hali ya juu sana cha mafanikio.

Shida mambo huyafanya katika siri sana.
 
Naweza kuamini kwakua tech haina mwisho,Ila nina weza kuhoji ili kujiridhisha na hio tech, mfano aliwezaje kudili na habari za watu maharufu tu?Mfano dunia ilikua na watu 200000 alitumia code gani kupata story za watu 20 tuu?.Pia hicho kifaa kama kina uwezo huo kwanini hawakuwa na wazo la kumwona mungu mwenyewe ama kuona ulimwengu wakati wa upya wake?.Ni hayo tuu
Hapo hatuna wa kumuuliza .Kudeal na watu wachache maarufu ni possible maana utajuwa unaachana na habari usizokuwa interested na unahangaikia unaemtaka tu.Mfano unavyochukua picha au video za harusi unakuwa unachukua matukio ya maharusi kiasi kwamba baadhi hata ya wageni wanaweza wasionekane.
 
Anyways sina la kusema Sana kuhusu hao wataalamu na mambo Yao

Ila

Nina la kusema kuhusiana na ardhi kuweka kumbukumbu ya kila kitu katika Maisha yetu,nasikia sasa hivi kuna kamera ambayo inaweza kukamata kivuli cha kwenye ardhi,Kwa mfano mpo kwenye mkutano watu kadhaa na baada ya kuondoka ukumbini,basi mtu akija kupiga picha pale ataona vivuli vyenu na kutambua mlikuwa wangapi.

Kwa upande wa Imani ya Dini hasa ya kiislamu,kuna ushahidi Kwa mujibu wa mafundisho yetu kwamba ardhi itatoa ushahidi Kwa Yale ambayo tuliyafanya hapa duniani,kama ulienda gesti basi kipande Hicho cha ardhi husika kinahifadhi kumbukumbu zako na kuja kuzileta baadae

Kwahiyo ni kweli ardhi inahifadhi taswira sasa ni Kwa namna gani huyo mwamba alikuwa na mkweli na kifaa chake ndio hatujui.
Acha kuwa na fikra za kipumbavu kiasi hiki.
 
Acheni kushikiwa ubongo kiasi hicho hizo ni hadaa tu angalieni maisha ya watu ktk uhalisia wake huo ndio uhalisia!,viu vya bongo zenu zisifanye muwe mazuzu
 
Hata Aliens pia ni uzushi bin habari za kusadikika tu wala hakuna kabisa ushahidi halisi juu ya hivyo viumbe.
Huenda alliens sio viumbe, kama inavyotafsiriwa hivi sasa.

Huenda kwa namna nyingine kabisa...
Nlipata kupitia documentary moja ambayo inaeleza majini hawa hawa ndio huenda wana play role ya Alliens ili kuupumbaza ulimwengu.
Nalo halina ithibati.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom