Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Tanzania Tanzanian Tanzania. Unaelekea wapi jamani. mwalimu Nyerere we miss you. [emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26].poleni family ya huyo mzee [emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
 
Nimesikitika na kuhuzunika sana nilijaribu kuwa ktk viatu vya huyu mkuu wa idara wallah imenisononesha. Inawezekana kuna majibu mazuri angeweza kuwa nayo na pengine ni mtendaji mzuri aliekosa kueleza anayoyataka muheshimiwa. Najua kuna uwezekano mkubwa wa huyu mkuu wa idara kukosea data lkn haikupasa afanyiwe haya. Tunao utaratibu maalum wa kushughulikia mambo kama haya. Hivi tujiulize kama mkuu wa mkoa angewapa nafasi ya kumpa data kamili ingeharibu nini. Kisha nashindwa kuelewa hivi kila lalamiko ni mgogoro? Maana kama nimesikia vizuri mkuu wa idara kaulizwa kuhusu Migogoro na si malalamiko ambayo mkuu wa mkoa anatakwimu zake. All in all RC hakuitendea haki nafasi yake. Hakuthamini thamani ya utu wa mtu kwani hata pale mtu alipoanguka bila kujua amepata athari kwa kiasi gani aliimba nyimbo kuonesha alichokifanya yuko sahihi. Wananchi pia wamenifedhehesha sana wakati mtu ameanguka akipigania uhai wake watu wamekosa ubinaadamu wakaanza kushangilia... Upo wapi upendo wetu....
Kweli binadam wa tz tumekuwa wanafki sana. Mzee baada ya kuanguka kuna wapuuzi wanashangilia. Ila malipo hapahapa
 
Mtu anayejiamini na Fani yake haogopi kitu!..Mtu anayeamini utendaji kazi wake hatishwi na changamoto!.
Kinyume chake ni sahihi
Ulishawai kuhaso kimaisha wakati unajiamini kuwa unaweza na kweli unaweza? Ulishawai kufanya kazi bora na kweli ni bora halafu mtu akakukosoa kinyume na taaluma na kukufukuza? Ulishawai kudhalilishwa na mtu ambaye ana tu mamlaka ila mengine yote, kuanzia umri, elimu nk umemzidi? Hivi unajua mwanafunzi wa udaktari aliyefuzu, asiye na cheti cha udaktari, akiwa anajaribu kuokoa maisha ya mgonjwa kibinadamu, anayehtaji msaada wa chini ya dakika tano, umbali wa dakika 20 kupata huduma, mgonjwa akimfia, sheria inamfunga kwa swali jepesi
tu, je wewe ni daktari? Labda nilikuelewa vibaya...but the world is not fair, let's wisdom leads the best.
 
Ulishawai kuhaso kimaisha wakati unajiamini kuwa unaweza na kweli unaweza?
Punguza kutetemeka sijaelewa unataka nini hapo
Ulishawai kufanya kazi bora na kweli ni bora halafu mtu akakukosoa kinyume na taaluma na kukufukuza?
Heshima ya uoga ikiwazidi ndio maana wahasibu mnatumwa peleka vitu hata nyumbani kwa boss. Kuna haki zinakulinda akimwaga mboga mwaga ugali wake!..
Ulishawai kudhalilishwa na mtu ambaye ana tu mamlaka ila mengine yote, kuanzia umri, elimu nk umemzidi?
sielewi hata unataka nikujibu vipi kwamba mpige!?.. its your decision sue the fucker or swallow the words!.
Hivi unajua mwanafunzi wa udaktari aliyefuzu, asiye na cheti cha udaktari, akiwa anajaribu kuokoa maisha ya mgonjwa kibinadamu, anayehtaji msaada wa chini ya dakika tano, umbali wa dakika 20 kupata huduma, mgonjwa akimfia, sheria inamfunga kwa swali jepesi
tu, je wewe ni daktari?
Kuna kitu kinaitwa first aid kama akiwa aliamua mtibu hapo hapo that is against the law!.Hana kibali yeah atafungwa!.
Labda nilikuelewa vibaya...but the world is not fair, let's wisdom leads the best.
The world has never been fair even the bible know that!
 
Thibitisha ww uwajibikaji wake.
Amezitaja kesi zote ktk ubora wake na hatua zake, labda tukio zima liwe ni la maigizo, lakini kama ni la kweli, wala hazihitajiki akili hata za kuku kujua kwamba, Mzee alikuwa na data kamili na zote amezifanyia kazi. Na kwa umri wake na kwa utawala huu, asingefanya vinginevyo kabisa.
 
hao watumishi ni wazembe sana hawajui wajibu wao hata angekufa hamna shida wananyima sana watanzania haki yao Makonda yuko sahihi 100%
Ulishawai wahi kufiwa wewe? Dunia ilikuwa na rangi gani siku hiyo. Raha ya msiba uwe kwa jirani, hata kiwango cha chumvi utaijua kwenye chakula, say sorry please... ana watoto na wategemezi na pia inawezekana hakuwahi hata fanya lolote baya ulizanialo. Say sorry to his family please, inawezekana ameshakufa au atakufa kesho ama mwakani kwa maradhi yaliyosababishwa leo tu, say sorry. We all know what happen to family and friends when death occur.
 
Nyie ni poyoyo kweli.watu wangapi wamedhurumika viwanja kupitia kwake.nyie chadema ni nyumbu kweli.
Hili jambo halihitaji siasa, naaamini kabisa hata Rais hakupenezwa na hili. Kwanza jamaa ni wa nyakati za Magufuli, pili alikuwa akienda kwa spidi zake, la mwisho isingewezekana awe mzembe kama mtakavyo tuamini. Kizazi kati ya wale wote yeye tu ndiye majibu yake yameonesha ni muwajibikaji. Na kamwe hatofukuzwa, labda ahamishwe tu kituo. Tunawakatisha tamaa watz walio amua kwa dhati kuwatumikia wananchi, Siasa tupa kule, acha Ukweli u prevail.
 
Na ndipo linapokuja swali la msingi la je...nia ni kutatua migogoro kweli? Kwenye semina au vikao vya kiutendaji kuna uwanja mpana wa kujadili ikiwemo kufahamu changamoto, vikwazo katika utekelezaji majukumu; bila kusahau maoni ya watendaji juu ya kuboresha taratibu za utekelezaji majukumu. Hivi mbona ni vitu vya msingi sana jamani watanzania ndiyo mmefika huku!!??
Wewe nimkomavu wa hoja, Nimekuelewa sana. Na niseme tu wazi, watz wengi wanapelekwa na mihemuko tu, wanadhani ma RC wanaotumbua hovyo ndio wachapa kazi, kuna thread eti inadai Makonda ndiye RC bora kupita wote, hapana, kuna akina Antony Mtaka, yuko kwenye mkoa wenye changamoto nyingi lakini anakwenda vyema sana pasi kutaka sifa, binafsi nampenda, anajua alifanyalo, anazijua changamoto za watendaji wake, na anazitatua haswa. Mkoa mpya, ila unasonga.

Maafisa kilimo hata hawakuwa na usafiri, wala mafuta, siku hizi wanapewa, na hakika wanapiga mzigo. Simiyu ktk kilimo (uti wa mgongo) mwaka huu makampuni yatakimbia pamba. Watu wanafundishwa hata kumwagia dawa, kila idara yuko safi, elimu, afya, viwanda, mashule, nknk. Endeleeni na mihemuko na kushangilia wenzenu wakizimia.
 
Kuanzia sasa ninamlaani Daudi Albert Bashite na laana hii itatafuna mpaka wapambe wake.Nataka kila anayekubali aseme AMEN.
 
Punguza kutetemeka sijaelewa unataka nini hapo

Heshima ya uoga ikiwazidi ndio maana wahasibu mnatumwa peleka vitu hata nyumbani kwa boss. Kuna haki zinakulinda akimwaga mboga mwaga ugali wake!..

sielewi hata unataka nikujibu vipi kwamba mpige!?.. its your decision sue the fucker or swallow the words!.

Kuna kitu kinaitwa first aid kama akiwa aliamua mtibu hapo hapo that is against the law!.Hana kibali yeah atafungwa!.

The world has never been fair even the bible know that!
Hongera na Mungu awe nawe ktk kuudumisha huo ulimwengu usio fair, ubarikiwe. Baraka hadi uzeeni.
 
Nimejikuta natetema kwa hasira baada ya kuona mtu kaanguka na kapoteza fahamu huku huyo huyo mtu alisababisha apoteze faham anasema DAR ES SALAAM OOYEEEE! Atupishe siye tunaendele kuchapa kazi.... Daaah watu ni wanyama zaidi ya mnyama[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
.....
.....na viongozi wa dini wanapiga makofi
 
We unajua hao wakuu wa idara kwa kusababisha migogoro mfano ya ardhi, wameua watu wangap!?
Hawawezi kuona....sera ni pinga,pinga,pinga! Kama kusimamishwa kazi watu wanazimia basi kila dakika kuna watu wanazimia. Hawa watumishi hata wakistaafu muda mfupi tu wanaanza kuteseka....kwanini....?
 
Back
Top Bottom