Unanikumbusha mchizi wangu mmoja Bush dokta Biambax kweli Azania kulitoka vichwa vilivyopinda? Ben hupo wapi mtu wangu?
Haaaaaaaaa kweli lyf nomaaaaaa,Je mdudu yupo?
Jamaa alikuwa best yangu sana...😛oa! bila kumsahau Mama Shija
Sana... Wanaongelea kumaliza shule 2007.... Nilikuwa najaribu kusikilizia stories niunganishe na mimi lakini sijaokota hata moja.. Hapa nimempata Mama Shija tuu ambaye alikuwa mtaalamu wa Chemistry alitokea Tambaza kwenda Azania...
kumbe wewe wa kale shekhe..
Samahani siku ile nilikukosea heshima ndugu..tafwazari sana..
Mkuu kumbe ulimaliza mwaka 2007 bila shaka ni GREEN LABEL.....yule mchizi alikuwa na masifa ya ajabu sana.......yeye na jamaa yake wa karibu BNBkuna msela aliitwa dmx tulimaliza nae 2007........sasa hivi ni dereva wa DALADALA MWENGE---TEGETA....
Mwalimu khatibu yupo njombe njia ya kwenda makete ni mkuu wa shule,jina la shule silikumbuki vzr,nilikutana naye nikienda bush1. Wale maticha waliokuwa wanauza past papers - Mosha na mwenzake wako wapi?
2. Mwalimu Hatibu aliyekuwa anajulikana kama 'Ibara' kutoka na kunukuu 'Katiba' naye kaishia wapi?
3. Kulikuwa na ticha kichwa wa kemia alikuja miaka ya 90, anaitwa nani?
4. Ticha wa PE aliyetupigisha mazoezi ya mpira naye anaitwa nani?
Mwalimu mosha wa physics,hafundishi Kazi yake kuuza pepa
Point saba zilikuwa zinatokea mara nyingi tu Azania. Omary Mtiga alipata 7 mpaka alipewa scholarship kwenda kusoma Uingereza. Nilikuwa Azania wakati wa Omary Mtiga,Mathias Michael,Kipimo,Batman,Sebastian Ndege,Jagna 'footballer'.
Wakati huo Salum Salum mwalimu wa michezo,mama Dath Chemistry O level,Mama Shija Chemistry A level,Peter Lebabu Mashanga(Rip) English huku akiwa ni muwakilishi wa British Council pale Azania.
Vichwa hivyo pamoja nami tulimkuta Kisamo kama Head Master na Mzee Meja second Master ingawa baadae alikuja Kwayu.
Wakati huo tulivaa kaptula za kaki na lazima kitambaa chake ukanunue pale Urafiki. Ilikuwa mwiko kuchomekea shati,ukikutwa umechomekea unachapwa bakora za kutosha! Msosi ulikuwa wa bure na wakutosha enzi zile. Uwe boarding uwe day wote mnagonga menu. Niliyapenda maisha yale sana!
Wadau mkichangia msisahau kuweka signature kwamba wewe ni class gani hapo azaboy
*1995-1998*