Vichwa Hivi vya Azania Viliishia Wapi?

Kuna maticha hawa:
Matley-Hesabu
FUVU-Hesabu
Matawa-Kiswahili & Geograph
Mgude-Chemistry
Mkongo-Physics
Hivi Tokyo(jina alilipata kwa ajili ya kuvaa suruali za Tokyo) hivi anaitwa nani jina lake halisi na alikua anafundisha somo gani?
Huyu kobe nlikuwa simmaind kabisa na mwandiko wake wa kike, alikuwa anajifanya yuko dk moja mbele kumbe f.ala tu..sku moja masela walimtaitisha K/Koo wakalamba saa yao..safi sana.
 
Mmh... tupo na watoto humu...

Sana... Wanaongelea kumaliza shule 2007.... Nilikuwa najaribu kusikilizia stories niunganishe na mimi lakini sijaokota hata moja.. Hapa nimempata Mama Shija tuu ambaye alikuwa mtaalamu wa Chemistry alitokea Tambaza kwenda Azania...
 
Mimi sitasahau wanafunzi waliomaliza o-level mwaka 1997, waliweka rekodi ya division one 124, rekodi hii haijavunjwa mpaka leo hapo Azania. Tena wawili kati yao walipata one points 7, mmoja kati yao ya waliopata one ya 7 ni member wa Jamíi forum.

hiyo pwaint 7 kama si yako basi yangu..
 
Mi Najikumbuka mwenyewe kwa Namba miaka ya 1996,
Ticha mnoko Tokyo, Mchwampaka,
Headboy Mwita Mwikwabe wa CDM,
Juisi kwa Mkemia pale nje ya fensi, mabarafu sijui alikua anayatoa wapi yule jamaa,
Kituo Faya kila full kujimiks na watoto wa Jangwani mixer Zanaki,
Bila kusahau bifu na watoto wa Jiteute baada ya Tambaza kuondolewa A-Lavel,

Mabishoo nao

kumbe wewe wa kale shekhe..
Samahani siku ile nilikukosea heshima ndugu..tafwazari sana..
 
Mimi nakufahamu wewe ulipata division three ya points 24. Ila comb ya HKL ilibalance na ukafaulu na A-level ulipelekwa Tambaza. Member wa Jamii Forums aliepata one ya points 7 o-level hapo Azania anaitwa KONGOSHO. Huyu jamaa kichwa sana tumpigie saluti.

Kongosho alipata pwenti saba mwaka gani? Advance alimaliza wapi na alipata ngapi? Chuo alipata GPA ngapi na sasa anafanya kazi wapi?
 
Mchwampaka alikuwa anamuita kwayu kaka!!!! mnoko balaaa!!! kuna jamaa alikuwa anacheza karate mchwa alikuwa anaamuogopa!!, wakina mcheni f 2 akakimbilia south!!, mashanga kiongozi wa migomo ya walimu alikuwa anatafutwa kama al shaababy alikuwa na ofisi Azaboy!!, kuna jamaa alikuwa anajiita BATMAN ukimwita popo ugomvi!!!
 
Kongosho alipata pwenti saba mwaka gani? Advance alimaliza wapi na alipata ngapi? Chuo alipata GPA ngapi na sasa anafanya kazi wapi?

Kongosho alimaliza o-level Azania mwaka 1997 na akapata one ya points 7. Ni mmojawapo ya wanafunzi 10 waliokula chakuka cha mchana na waziri mkuu Fredrick Sumaye kipindi hicho. A-level alipelekwa Ilboru na alichukua mchepuo wa PCM, huko akafumua one ya points 3. Akaingia chuo kikuu mwaka 2000 na facult aliyosoma ni Telecom. Akagraduate na kupata first class, akachaguliwa awe lecture hapo chuoni lakini akakataa kwani alipata schoraship ya kusome Masters ya Telecom nchini India. Baada ya kumaliza kuchukua Masters akachukuliwa na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kwa sasa ndie fundi mkuu pale Vodacom. Je unahitaji kumfahamu Kongosho zaidi? NIULIZE. Nina full data za huyu jamaa.
 
Huyu kobe nlikuwa simmaind kabisa na mwandiko wake wa kike, alikuwa anajifanya yuko dk moja mbele kumbe f.ala tu..sku moja masela walimtaitisha K/Koo wakalamba saa yao..safi sana.

Tokyo jina lake Yengela..alipata jina kutokana na kuvaa sana suruali enzi zile ziliingia ready made ina lebo imeandikwa TOKYO ikawa kauka nikuvae!
 
Je mnamkumbuka Humpherey Polepole yule mtaalam wa kingereza Azania yote. Alituwakilisha kwenye midahalo mingi ya kitaifa na ya kimataifa. Nasikia siku hizi ni Mwanaharakati. Halafu kuna kiongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA tumesoma nae hapo Azaboys. Mnamkumbuka yule headboy ambae alikuwa hajui kiswahili hata kidogo. Alikuwa anapata shida siku ya School baraza. Niliumia sana baada ya serikali kuifanya Azania kuwa shule ya mchanganyiko upande wa A-level. Wangebakisha Boys only.

wameshafuta mchanganyiko.sasa full uboizini
 
1. Wale maticha waliokuwa wanauza past papers - Mosha na mwenzake wako wapi?

2. Mwalimu Hatibu aliyekuwa anajulikana kama 'Ibara' kutoka na kunukuu 'Katiba' naye kaishia wapi?

3. Kulikuwa na ticha kichwa wa kemia alikuja miaka ya 90, anaitwa nani?

4. Ticha wa PE aliyetupigisha mazoezi ya mpira naye anaitwa nani?
 
alikua anajiita Dr weins...baada ya kumwagwa mzizima alikua anafundisha tuition zake magomeni naskia alikuja kufanya pepa ya f6 kama PC...azaboy alikua mbele yangu kwa vidato viwili

nahs kaka utakuwa wa mwaka 2002 unawakumbuka kina onesphory paul,octa javet,leodgad,? Aisee nimekumbuka meng sana
 
Nakumbuka kwenye school baraza mwanafunzi mmoja alisema shule yetu ni kama mwanamke changudoa. Anajiremba nje ili avutie lakini sifa yake ni mbaya.Akatafsiri mfano wake kwa kusema shule ya Azania ina sifa kubwa na inaheshimika sana. Lakini kuna vitu vya kushangaza sana. Laboratory ya Chemistry bunsen burner jiko la mchina, walimu haiwingii madarasani. mazingira ya shule mabovu. Mkuu wa shule alikasirika sana na akamtaka afuate kauli yake ya kuifananisha shule na changudoa lakini yule mwanafunzi alijibu kuwa ameongea kisiasa zaidi.
 
Huyo anaitwa Wenzi aka WENZI MAN, nilishawahi kumkuta Shule ya sekondari George Washngton anafundisha, tukiwa tunaongea akasema anataka kujiunga na UDSM mwaka huo (kumbukumbu zinaonyesha ilikuwa 2008). Wakati rika lake walikuwa tayari kwenye ajira

kabla ya hapo niliwahi kukutana naye pale shule ya msingi Turiani-magomeni akifundisha tuishen za sh. mia mia.
 
Kongosho alimaliza o-level Azania mwaka 1997 na akapata one ya points 7. Ni mmojawapo ya wanafunzi 10 waliokula chakuka cha mchana na waziri mkuu Fredrick Sumaye kipindi hicho. A-level alipelekwa Ilboru na alichukua mchepuo wa PCM, huko akafumua one ya points 3. Akaingia chuo kikuu mwaka 2000 na facult aliyosoma ni Telecom. Akagraduate na kupata first class, akachaguliwa awe lecture hapo chuoni lakini akakataa kwani alipata schoraship ya kusome Masters ya Telecom nchini India. Baada ya kumaliza kuchukua Masters akachukuliwa na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Kwa sasa ndie fundi mkuu pale Vodacom. Je unahitaji kumfahamu Kongosho zaidi? NIULIZE. Nina full data za huyu jamaa.

Mafundi wa voda na maktek wote nawajua sasa kongosho ndio nani kwa jina? Anaonekana ana kipaji sasa mbona mada zake kama jike dume wakt yeye ni dume au gasho?
 
Mafundi wa voda na maktek wote nawajua sasa kongosho ndio nani kwa jina? Anaonekana ana kipaji sasa mbona mada zake kama jike dume wakt yeye ni dume au gasho?

Ningekutajia jina lake lakini sheria za Jamii Forum haziruhusu member yeyote kutaja jina halisi la member mwenzake. Na ukitaja jina halisi la member mwenzako adhabu yake unapigwa BAN. Ukitaka kumfahamu wewe nenda Vodacom halafu uliza mtu mwenye cheo cha Supervisor Engineer na utampata. Kuhusu uchangiaji wake wa mada za humu JF ambazo hufanya asifahamike jinsia yake, hapo lengo lake ni kuchangamsha Jamii Forum. Na hii anafanya sana kwenye jukwaa la CHIT CHAT.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom