Pori la Mbweni ndo jehanamu mpya?

Pori la Mbweni ndo jehanamu mpya?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,697
Reaction score
39,154
Pori la Mbweni na Ununio ambayo ni sehemu Moja kijiogrofia au yanapakana yameukuwa tishio Kwa maisha ya watu

Mfano

1. Mzee Ali Kibao alitekwa na baadae mwili wake ukakutwa umetupwa kwenye pori hili

2. Makaburi ya halaiki
CNN ilihabarisha ulimwengu kuwepo Kwa makaburi ya halaiki kutokana na mauaji ya oktoba 29

3 David Jumbe,
Huyu ni mlinzi wa Lissu, Leo amesema alitekwa na wauaji wakawa wanampeleka kumuuwa kwenye pori la Mbweni

4 Roma mkatoliki
2017, Msanii Roma mkatoliki alitekwa na kusema kuwa aliokotwa porini Ununio kwenye hilo pori

5. Humphrey Polepole
Taarifa zilidai kuwa watekaji walimpeleka kwenye hilo pori.
Hadi Leo hajawahi kuonekana.

6. Stephen Ulimboka Dk
Alitupwa Mabepande

Hawa ni baadhi ya watu maarufu, hatujui watu ambao sio maarufu waliopotelea kwenye hilo pori.

Pori la Mbweni na Ununio kama yanatumikanna vyombo vya ulinzi na usalama Kwa ajili ya shughuli zao za kiulinzi basi wahakikishe lisitumiwe na wahalifu hasa watekaji kuuwa Watanganyika

Serikali ya Wilaya Kinondoni na Jiji la Dar es salaam yapo hicho la umakini haya mapori ya Ununio, Mbweni na Mabepande
Au myagawe yawe makazi Kwa raia ili kuondosha uhuni wa utakaji
 
Siyo pori la mbweni, bali ni TISS training centre ndo kubaya
Lile ni pori kweli kweli, yaani ikitokea umefungwa kitambaa, halafu ghafra ukashushiwa pale bila kujua uko wapi unaweza kudhani umetupwa pori la masumbwe.

Halafu nyumba zao zipo ndani kabisa katikati ya pori.

Huko hata wakikubinya, hakuna mtu atajua.

Huko nadhani watu sampali ya Polepole ndio hupelekwa huko.

Kila siku wanampa wali wa nazi, sie huku tunahangaika kumtafuta
 
Kuna huyu jamaa 'Mafwele' amepata headlines sana zaidi ya mwaka ila hadi Leo anadunda.

Haya mambo hayaendi na Imani Wala matamko ya kulaani pekee ila kuchukua hatua.
Training_bijstandseenheid_12_(molotov_zoom).jpg
 
Hiyo namba 6 ungerekebisha kwa ajili ya kumbukumbu ya baadaye. Aliyetupwa kwenye msitu wa Mabwepande enzi za utawala wa JK alikuwa ni Dr. Steven Ulimboka, aliyekuwa kiongozi wa chama cha Madaktari nchini (MAT), aliyeongoza mgomo wa madaktari.

Daudi Mwangosi yeye alikuwa ni mwandishi wa habari aliyeuwawa na polisi mchana kweupe eneo la Nyololo kule Mufindi Iringa, wakati wa ufunguzi wa tawi la wakereketwa wa CHADEMA.
Asante sana kwa masahihisho
 
Lile ni pori kweli kweli, yaani ikitokea umefungwa kitambaa, halafu ghafra ukashushiwa pale bila kujua uko wapi unaweza kudhani umetupwa pori la masumbwe.

Halafu nyumba zao zipo ndani kabisa katikati ya pori.

Huko hata wakikubinya, hakuna mtu atajua.

Huko nadhani watu sampali ya Polepole ndio hupelekwa huko.

Kila siku wanampa wali wa nazi, sie huku tunahangaika kumtafuta
johnthebaptist tangu kutoweka pole pole huyu jamaa sijui kama aliwahi kuingia jukwaani?
 
Back
Top Bottom