King Kong III,
Yule jamaa aliyepiga Div.I point 7 na kuchukuliwa na Mzizima kusoma free Kimtaa alikuwa akiitwa Dk. Wenz, alikuwa maarufu sana pale Magomeni Makuti Mtaa wa Fundikira akiwapigia wadogo tuition pale shule ya msingi Lions Magomeni.
Jamaa alipofukuzwa MZIZIMA kutokana na ulevi, uzinzi na Utoro uliokithiri alikwenda magomeni kuanzisha kituo cha tuition na alikuwa na jina saaaana pale na kutengeneza mkwanja ile mbayaa, but later 2005 alifanya paper-PCM as private Cand.pale Kinondoni Muslims na akapata Div.I.
Baada ya hapo sikupata habari zake kwa muda mrefu hadi mwaka 2010 nilipomuona stand ya dala dala Usalama-Magomeni akionekana kama chizi fresh hivii, ukimuona utamsikitikia na kumuonea huruma, sijui nini kilimsibu yule bwana jamani. Hata Mkuu wake Mzee Kwayu akisikia habari hii kuhusu jamaa atalia sana coz alikuwa akimkubali saana.
Nakumbuka yule mshikaji alitabiri kuwa mwaka wetu lazima Div.I ya 7 itoke (lebo ya Blue) na kweli kupitia jamaa yetu Lordguard utabiri wake ukatimia...kweli msela alikuwa kijukuu cha mtume wazee.
Aza Boys bado tunaiwakilisha huku kitaa na Tanzania kwa ujumla japokuwa matokeo ya mwaka huu yameniudhi saana, yaani Div.Zero 146 jamani??? Shame on these kata students.