Vicent Nyerere amuumbua Rais Kikwete..

Nov 30, 2012
67
0
MBUNGE wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), ameanza ziara ya kuimarisha chama chake mkoani Geita, huku akimpiga kijembe Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwa anawachosha bure mawaziri kwa kuwalazimisha kufanya ziara mikoani kuzungumza na wananchi.

Nyerere ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema kuwa mkakati huo hauwezi kuinusuru CCM kwani mawaziri na sekretariati nzima ya CCM hawana majibu ya maswali ya kero za wananchi.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara jana mjini Kasamwa, Nyerere alitamba kuwa kichwa chake kimoja ni sawa na sekretarieti nzima ya CCM na mawaziri waliopita katika baadhi ya mikoa kusafisha hali ya hewa ili chama chao kisife.

Nyerere alifafanua kuwa, mkakati huo wa CCM ni sawa na kulamba matapishi yao, kwani mawaziri hao hao ndio wameshindwa kutekeleza vema shughuli za maendeleo kwa Watanzania, badala yake wamegeuka kunyonya rasilimali za taifa.

"Wanapobandua CCM na mawaziri wao, mimi nabandika hapo, watu hawahitaji ziara za akina Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye na mawaziri, wao wanataka majibu kwa serikali kwamba kwanini baada ya kuwaondoa mawaziri wabovu madarakani wameshindwa kuwashtaki.

"Hawa walioenguliwa ndio walizembea wakati twiga wetu wanasafirishwa nje ya nchi, kashfa ya rada imetokea kwao na madudu mengine mengi, sasa leo wanapokuja kwa wananchi hawana majibu ya hatua gani zilichukuliwa, ziara hizo ni bure tu za kuwachosha," alisema.

Nyerere ambaye alikuwa meneja kampeni wa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) kwenye uchaguzi mdogo na kutoana jasho na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alisema kitendo cha CCM kuwalazimisha mawaziri kutembea nao kwenye mikutano ya hadhara, kamwe hakiwezi kubadili mawazo, mtazamo na mwelekeo wa Watanzania.

Alisema ni lazima wataiweka madarakani CHADEMA ifikapo mwaka 2015, kwani wamechoshwa na ahadi hewa za Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete.

"Kwa CCM hawana jipya tena. Huo mkakati wao wa kutembea na mawaziri majukwaani hauwezi kukinusuru chama hiki tawala kufa. Ni Mtanzania yupi ambaye hadi leo hajui kwamba ugumu wa maisha hivi sasa unatokana na utendaji mbovu wa serikali hiyo wakiwemo mawaziri wake hao?" alihoji.

Alisema wananchi sasa wanataka CCM na Rais Kikwete wawaeleze ni kwanini wameshindwa kuwachukulia hatua za kisheria mawaziri waliozembea na kuisababishia hasara kubwa serikali kwa kununua ndege na rada mbovu, kupeleka wanyama nje na kusaini mikataba mibovu.

Katika ziara hiyo, Nyerere aliyeongozana na viongozi mbalimbali wa CHADEMA, akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilayani Geita, ambaye mwishoni mwa wiki alijiengua huko, Daud Ntinonu, alihoji pia sababu za CCM kupangua makatibu wakuu kila mara.

"Hata wabadili viongozi mara ngapi, kamwe hawawezi tena kuungwa mkono na Watanzania, wananchi wa leo wanahitaji mabadiliko ya kweli ya kimaendeleo, ambayo yatakwenda kutekelezwa na CHADEMA mwaka 2015," alisema.

Katika kile alichodai ni hali ngumu, Nyerere alidai kuwa kama baba mdogo wake hayati Mwalimu Julius Nyerere, angefufuka na kuiona hali hii sasa, asingeweza kukaa hata dakika moja bila kufa tena.

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi, Nyerere aliwahakikishia Watanzania kwamba, baada ya Mwalimu Nyerere kufariki mwaka 1999, CCM imetelekeza rasmi mawazo na sera za kiongozi huyo aliyekuwa adui namba moja wa rushwa na uchu wa madaraka.
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Mkuu hivi Vicent Nyerere naye kweli ana ubavu wa kupambana na Kikwete. Kashindwa Dr Slaa, Mbowe. Ataweza Vicent.
 

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
2,000
Naona daktari wa ziara za nje alikuwa anashambuliwa kama lango la kili stars.Kimsingi raia wanajua anayewasababishia maisha magumu ni ccm wakiongozwa na bingwa wa kusafiri
 

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
0
Slaa na mbowe wameshindwa kivipi kupambana na kikwete?

Hujui wameshindwa vipi? Kweli maumivu ya kushindwa mabaya, yametegua mpaka mlango wako wa Fahamu, Unajua babu hakutegemea kuwa baada ya 2010 angeendelea kubanana na mateja pale manyanya!
 

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,626
2,000
Mkuu hivi Vicent Nyerere naye kweli ana ubavu wa kupambana na Kikwete. Kashindwa Dr Slaa, Mbowe. Ataweza Vicent.

Ni kweli mkuu vicenti Nyerere hawezi kupambana na JK kwa kuwa yeye ana ndimi tatu na Nyerere ana ndimi moja.

Pia Vicenti Nyerere hawezi kupambana na JK kama ambayo Mr dhaifu asivyoweza kupambana na EL,

Pia Vicenti Nyerere hawezi kupambana na JK kama ambavyo JK mwenyewe asivyoweza kupambana na wauza madawa ya kulevya, wezi wa EPA, wamiliki wa Kagoda na Richmond, Wezi wa madini yetu na twiga kwa sababu yeye naye ni mwizi na anashare kwa wezi woote wa nchi hii, lakini Pia JK kanaumwa ndio maana huanguka majukwaani.


Vicent Nyerere hawezi kupambana na watu wenye ndimi zaidi ya Moja kwa kifupi, kwani hao si watu bali ni Mashetani, maruhani na Majini ya sisiemu, kwani ndiyo yanayomlinda Dhaifu ikulu alipewa na Shekhe yahya na ndio maana anawalipa mshahara kutokana na kodi zetu waganga woote wanaoenda kumpa majini ikulu.

Unalingine?
 

Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,730
0
Duh natamani nimuone huyo vicent nyerere atakua na bichwa kubwa yani kichwa chake ni jumla ya vichwa vyote vya wajumbe wa sekretariat ya ccm! how big the head of vicent nyerere? mwenye picha yake please!
 

massai

JF-Expert Member
May 2, 2011
654
0
Hivi hao mawaziri wana majibu kweli ya maswali kwa wananchi?
Hebu kwa mfano waziri wa maliasili na utalii aulizwe kuhusu hatua alizochukua juu ya faru waliopanda ndege atakua na majibu gani....
Vipi kuhusu hoteli zilizopo kwenye hifadhi kumilikiwa na watu binafsi ilihali ni mali ya serekali.
Hivi haya majibu hata ukimuuliza jahkaya atakua na majibu kweli.
Sasa hapo kiboko nyerere hajachukua point tatu bado?
 

MCHUMIPESA

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
2,088
0
Kamwe huwez funika jua kwa ungo.Vicent n jembe achen propaganda za kizushi.Chadema ndo mpango mzma mazeeiya!
 

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
19,503
2,000


“Kwa CCM hawana jipya tena. Huo mkakati wao wa kutembea na mawaziri majukwaani hauwezi kukinusuru chama hiki tawala kufa. Ni Mtanzania yupi ambaye hadi leo hajui kwamba ugumu wa maisha hivi sasa unatokana na utendaji mbovu wa serikali hiyo wakiwemo mawaziri wake hao?”


......Labda waende serengeti na mikumi lakini na huko kuna Tumewadhibiti!!!!
 

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
4,898
2,000
Mkuu hivi Vicent Nyerere naye kweli ana ubavu wa kupambana na Kikwete. Kashindwa Dr Slaa, Mbowe. Ataweza Vicent.
Kwa kuiba kura amemweza Dr Slaa. Na hata Vicent atashindwa na Kikwete kwa mbio za wizi wa kura kwa kutumia vyombo vya usalama na tume isiyo huru ya uchaguzi!!
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,996
2,000
Mkuu hivi Vicent Nyerere naye kweli ana ubavu wa kupambana na Kikwete. Kashindwa Dr Slaa, Mbowe. Ataweza Vicent.


Ebu muulize Mkapa, atatoa jibu zuri.... mkumbushie Arumeru Mashariki.... kijana alimtoa jasho alienda mbali akasema nitakutoa ktk ukoo wetu kwani uliomba...!!! hahahaaa.... Ben kijashoooo....aliomba msamahaaa haraka...!!!!
 

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Hivi hao mawaziri wana majibu kweli ya maswali kwa wananchi?
Hebu kwa mfano waziri wa maliasili na utalii aulizwe kuhusu hatua alizochukua juu ya faru waliopanda ndege atakua na majibu gani....
Vipi kuhusu hoteli zilizopo kwenye hifadhi kumilikiwa na watu binafsi ilihali ni mali ya serekali.
Hivi haya majibu hata ukimuuliza jahkaya atakua na majibu kweli.
Sasa hapo kiboko nyerere hajachukua point tatu bado?


Tunataka watakapopita Mbinga, Mbozi, Mafinga, Kagera, Rombo, Moshi, Arumeru na maeneo mengine yanayolima kahawa waje na waziri wa kilimo na waziri wa ushirika na masoko watueleze wanao mpango gani kuwasaidia wakulima wa kahawa ambao wanaathiriwa na anguko la bei ya kahawa. Asipokuja na majibu ya kueleweka si kuwa atazomewa kama walivyozomewa na wakulima wa korosho bali watatwangwa mawe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom