Uchaguzi 2020 Vicent Mashinji achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM

Yanaenda kutokea kama yale ya 2015 kwny kugombea urais ndani ya CCM kila aliyeenda kuomba baraka kwa mwenyekiti JK alikua anamwambia wewe ndio chaguo langu(wagombea wote 40 na ushee waliambiwa hivyo) kilichokuja kutokea mpk Pinda alilia Ukumbini.
 
Wakati huo Mkurugenzi wa Kinondoni ana matokeo tayari anasubiri kuyatangaza tu
Kwa kawe idadi inatisha, yako majina Ni mazito has a, wasiwasi wangu watalogana sana wagombea, mdee atapita kati yao.wagombea 180+ unakosaje mgawanyiko?
 
Safari hii WASUKUMA wote wanataka ubunge
Hii hoja ya wasukuma hili wasukuma lile kusema kweli siipendi kuisikia. Hii inaashiria kuibuka kwa hoja ya ukabila hapa nchini. Nawaomba wahusika wasipuuzie hili.

Nikisema wasipuuzie simaanishi wawasweke watu ndani, hapana bali lifanyiwe uchunguzi wa kina ili kama kuna kamoshi ka ukabila sehemu yoyote basi litumwe gari la fire kuzima moto maramoja.Hatupendi nchi iingie kwenye mvutano wa makabila.
 
Unasoma mavitu mengi yaani vyeti vyako vinajaa kwenye begi kubwa la nguo lakini mwisho wa siku unaishia kuwa zezeta tu. Hizi elimu za kukariri ni upumbavu tu.
 
Kwani wanalala njaa??

Kwani wanaonunua viroba vya mchele ni wanaolala na njaa? Hawezi kuongeza Stock ndani ya kiroba cha mchele cha kilo 50 kuliko kuichoma laki yake? Ndani ana stock ya kula infinity bila kuisha?
 
CV nzuri. Ila sijui kwanini matunda mengine yana maganda yanayovutia lakini ndani unakuta machachu, halafu sio matamu.
 
Back
Top Bottom