Uchaguzi 2020 Vicent Mashinji achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,476
215,317
Aliyekuwa Katibu mkuu wa CHADEMA kabla ya kuhamia CCM, Vincent Mashinji amechukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Jimbo hilo la Kawe lilikuwa chini ya Mbunge aliyemaliza muda wake, Halima Mdee kutoka chama cha CHADEMA.

Aidha, katika jimbo hilo pia Askofu Gwajima amechukua fomu ya kuwania Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi


MASHINJI ATAKA KUJIPIMA UBAVU NA MDEE JIMBO LA KAWE  - Uchaguzi2020_Aliyewahi kuw ( 592 X 640 ).jpg

Huyu ni miongoni mwa wahamiaji lukuki kwenye chama hicho ambao wamejitokeza kuomba ubunge

WASIFU WAKE KWA UFUPI.

JINA:
Dr.Vincent Mashingi

UMRI: Miaka 43

TAALUMA: Daktari bingwa wa binadamu (MMED) na Daktari wa Falsafa (PhD).

ELIMU:
1981 - 1987 Elimu ya Msingi (Shule ya msingi Iligamba)

1988 - 1992 Elimu ya Sekondari (St.Pius seminary)

1992 - 1994 A-Level PCB (Mzumbe High School).

1995 - 2001 Chuo Kikuu cha Makerere (Degree ya Udaktari MD)

2003 - 2005 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Shahada ya pili - udaktari bingwa (MMED Anaesthesiology).

2004 - 2004 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Astashahada ya Utafiti)

2008 - 2010 Evin School of Management (Shahada ya Uzamili (Masters) ya Public Relations (CSR)

2007 - 2010 Blekinge Institute of Technology (Shahada ya pili (Masters) ya Usimamizi wa biashara, MBA)

2010-2010
University of Carlifonia - Anderson School (Stashahada ya Management Development)

2008 - 2008 University of Maryland School of Medicine (Astashahada Human Virology)

2010 - 2016 Chuo Kikuu Huria Tanzania (Shahada ya uzamivu (PHD) ya Uongozi.

UZOEFU WA KITAALUMA
2001 2002, Daktari wa mazoezi - Intern doctor (Hospitali ya taifa Muhimbili).

2002 - 2003, Mtafiti wa kujitegemea (Freelance Researcher).

2003 - 2005, Daktari (Hospitali ya Taifa Muhimbili)

2005 - 2006, Daktari bingwa (Hospitali ya Regency).

2006 - 2008, Msimamizi wa mradi (Shirika la kimataifa la afya IMA World Health)

2008 - 2016, Mshauri wa tiba (TB and HIV), Shirika la afya la Kimataifa la IMA WorldHealth.

Pia soma:
= > Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM
 
Kila La Heri!!!
Haya Sasa Nimuone Mtu Anampiga Aliyevaa Kijani Ataona Cha Mtema Kuni.
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom