VETA na double standard salary

kibunjuka

New Member
May 4, 2020
4
5
Pole na kazi Mkuu!

Ni imani yangu u mzima wa afya na unaendelea vyema na kuchapa kazi ya kujenga nchi yetu na ni imani yangu pia ujumbe huu utaupata na kuufanyia kazi.

Kwa ufahamu wangu mdogo nimeona hii ni platfom nzuri kwangu kuweza kukufikishia malalamiko yangu kama siyo yetu sababu sina uwezo wa kukutana na wewe ana kwa ana.

Wakati flani kwenye utendaji wa kazi tunaweza kutupa lawama kwa watendaji wakuu lakini kumbe matatizo yapo kwenye ngazi ya chini kabisa.

Mwaka jana 2019 June tulisomewa waraka ambao ulitutaka wafanyakazi wote wa VETA kuingia kwenye mfumo wa serikali wa malipo ya mishahara

(Lawson),tukatakiwa kukabidhi nyaraka zetu kupitia kwa mameneja rasirimali wetu kwenye vituo vyetu husika(vyuo).Tukafanya hivyo na baadhi ya watu wakaanza kuingia kwenye mfumo mwezi septemba 2019.

Ni miezi 8 sasa baadhi ya watu wameingia kwenye mfumo wengine hawajaingia hadi leo,tumejaribu kufatilia kwenye ngazi ya mamlaka yetu hakuna majibu ya uhakika tunayopata zaidi ya kuambiwa hayo mambo yapo nje ya uwezo wao na hakuna wanachokijua kwahiyo tuvumilie tu.

Hili suala limetukatisha tamaa sana na hivi sasa wale walioingia kwenye mfumo wamepewa barua za kuwatambua pamoja na fomu za madai ya areas zao tunasikia zimefika wanatakiwa kujaza ili wa claim malipo yao kwa ile miezi ambayo hawakulipwa mshahara wa lawson.

Hii imekua na impact kubwa sana kwetu kwenye utendaji maana tunakosa haki zetu za msingi mfano

1. Ukienda bank huwez pata mkopo unambiwa mpaka uwe na chek namba of which sisi ambao hatupo lawson hatuna hizo check namba,

2. Kuna kazi zinatagazwa na taasisi zingine tunashindwa kuomba sababu hatuna hizo cheki namba
Tunaomba tusaidiwe kwenye hili maana sasa kwenye taasisi kuna wanafanyakazi wa mamlaka na wafanyakazi wa Serikali.

Tumesoma kwa shida sana na tunakatwa na bodi ya mikopo maisha yamekua magumu sana,kama kuna tatizo kwenye documents zetu tuambiwe turekebishe lakini kutukalia kimya ni kutuonea na kutuumiza pia.

Wakati mwingine tunaanza kuhisi kama kuna upendeleo flani maana kwenye vituo unakuta management wote wameingia kwenye mfumo sisi watu wa chini ndiyo tuna hangaika na hakuna wakutufatilia.

Tunaomba msaada kwenye hili,natanguliza shukrani zangu za dhati na pole kwa majukumu.
Wako mhanga wa lawson
 
Back
Top Bottom