Vanessa Mdee aachia nyimbo mpya - Cash Madame

Mmmmh ngoma nzuri ila umbele mbele mwingi!
Ningekuwa najua kuimba ningehakikisha nateka kwanza soko la ndani baaada ya hapo naelekea nje kama alivyofanya plutnumz!!

Kinyumbani nyumbani sidhani kama itateka nyoyo za watu labda huko ughaibuni
 
Iko poa,seems like anafocus soko la mbele zaidi.
Ila too much auto tune,angeacha sauti yake halisi ingekua poa zaidi.
Mbele wapoi, maana hata Nigeria nyimbo hizo haziuzi.Nyimbo zinazouza Naija ni original kama John ya YEMI ALADE, Bobo ya OLAMIDE,SKELEWU.Huo umarekani ni ulimbukeni tu.
 
Naona wana wake mnazidi kubanwa tu..baada ya MWANA fa kuwaponda msitegemee mwanaume mtafute za kwenu na Vanessa nae ka komaa na cash madame yani Mwanamke ajiweze na atafute mwenyewe sio kutegemea mizinga........saaafi wadada pigeni Kazi
 
Nimegundua vitu viwili kwa hii video... Bila shaka vimemuingizia pesa pia.

Brands ya bidhaa mbili.. Siamini kama zimetokea kwa Bahati mbaya..

1. Dabaga

2. Mkito.com
 
Vanessa my love,tunajua nyimbo zako hazitulengi sisi wa nyumbani kwako,lakini basi jiweke kimuonekano wa tofauti na wakina Beyonce kwenye hizo video zako,japo waone kuwa una kitu tofauti na wao.
 
Vanessa my love,tunajua nyimbo zako hazitulengi sisi wa nyumbani kwako,lakini basi jiweke kimuonekano wa tofauti na wakina Beyonce kwenye hizo video zako,japo waone kuwa una kitu tofauti na wao.
Ahsante kwa kuliona hili.
 
Huyu bibie level zake sio za bongo ndio maana wabongo hawamuelewi...

Labda angefanya muziki kama Snura au Shishi baby
 
Vanessa mdee a.k.a vee money kama anajiita ameachia nyimbo mpya ya kufungia mwaka.
Nyimbo inaitwa cash madame
Nyimbo hii inahamasisha wadada kujitafitia mkwanjwa wao wenyewe sio kutegemea ma suger daddy au sponser

USAHIHI
1.Wimbo mpya....
2.Wimbo unaitwa....
3.Wimbo huu unahamasisha....
 
Vanessa my love,tunajua nyimbo zako hazitulengi sisi wa nyumbani kwako,lakini basi jiweke kimuonekano wa tofauti na wakina Beyonce kwenye hizo video zako,japo waone kuwa una kitu tofauti na wao.
Vipi msanii wabongo anayejiweka kwa muonekano wa Chris Brown tena unakuta kavaa meno kama Birdman?
 
Vanessa mdee a.k.a vee money kama anajiita ameachia nyimbo mpya ya kufungia mwaka.
Nyimbo inaitwa cash madame
Nyimbo hii inahamasisha wadada kujitafitia mkwanjwa wao wenyewe sio kutegemea ma suger daddy au sponser

ngoma nzuri imekaa kimbele mbele sana sio kibongo bongo wakina mwajuma ndala ndefu hawatoielewa,apunguze ubeyonce kidogo,hizi za vannesa sio level za kina shishi trump wala jay dee wala snura teh teh teh komaa mdada ila verse ya kwanza ina sound km ngoma ya AY zigo....

hongera sana mama jux.
 
Vanessa mdee a.k.a vee money kama anajiita ameachia nyimbo mpya ya kufungia mwaka.
Nyimbo inaitwa cash madame
Nyimbo hii inahamasisha wadada kujitafitia mkwanjwa wao wenyewe sio kutegemea ma suger daddy au sponser

Nyimbo ni wingi wa wimbo. Sema hivi "aachia wimbo mpya" ndio kiswahili sahihi
 
Yani tangu amepiga hizi nyimbo sijaona Kali zaidi ya hizi.

1. Hawajui
2. Siri ft barnaba
Ajipange tena zaidi. Hii cash Madame hakuna wa kusikiliza (sisi wa uswahilini)
 
Hii video nimejikuta ghafla nimekumbuka set it off kwa soko la nje lipo vizuri kuhusu nyumbani tusikosoe sana labda anajipanga kwa soko la ndani wapewe support na ushauri pia tusiishie kuponda tu.
 
kwanini beat nyingi za bongofleva zinakuwa kama wanapiga ngoma iliyolowa? ngoja nikasikilize zangu sumu ya panya ya Dogo Nigga.
 
Back
Top Bottom