Valvu ya Moyo yabadilishwa bila kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa mara ya kwanza Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Pichano.6.jpg

Picha no.3.jpg
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India wakifanya upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI) katika kambi maalumu ya siku mbili ya matibabu ya moyo inayofanyika JKCI.

Taarifa ya JKCI imeeleza kuwa Upasuaji huo mdogo wa kubadilisha valvu umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini Tanzania.
 
Kupitia mshipa mkubwa wa damu pajani, wanaingiza cable na kusokomeza taratibu cable hiyo nyembamba yenye valve ya wavu wavu hadi katika moyo na kupachika valve. Wakisha pachika hiyo valve wanavuta hiyo cable huku hicho kifaa cha valve ya moyo kikibaki ndani ya moyo kufanya kazi husika.

Zoezi hilo hufanywa huku ma doctor wakufuatilia kila hatu kupitia vifaa kadhaa kama unavyoona katika picha aliyobandika mleta mada Roving Journalist, vifaa hivyo vikiwemo screen kuona muenendo mzima wa zoezi, kamera ndogo itakayokuwepo katika cable n.k n.k

Video hapa chini inamalizia kuonesha zoezi :


View: https://m.youtube.com/watch?v=q6erYCbZGMQ
 
Hivi huwa wanafanyaje yaani?? Wanaufijiaje moyo au ubongo bila kupasua?
Hayo ni mambo ya kitaalam sana mwanangu, kwanza unapaswa kulala ndani ya chandarua chenye dawa ili kujilinda na malaria.
 
Back
Top Bottom