JKCI kushiriki Kongamano la 8 la Dunia la wataalam wa magonjwa ya moyo kwa watoto nchini Marekani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,991
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto watano kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kushiriki Kongamano la nane la dunia la watoa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto linalofanyika nchini Marekani.

Kongamano hilo linatarajiwa kuanza tarehe 28 agosti hadi 3 septemba 2023 ambapo jumla ya washiriki zaidi ya 4500 kutoka nchi mbalimbali duniani kushiriki.
DSC_0080.JPG

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Daktari bingwa wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naizhijwa Majani alisema kongamano hilo hufanyika kila baada ya miaka minne ambapo mara ya mwisho lilifanyika mwaka 2017 Barcelona nchini Spain.

“JKCI iliweza kushiriki katika kongamano la saba lililofanyika nchini Spain na kujifunza kuhusu msingi wa data shirikishi wa uboreshaji wa ubora wa huduma kimataifa (International Quality Improvement Collaborative Data Base - IQIC) inayosaidia kuangalia masuala ya ubora kwenye huduma za matibabu ya moyo kwa watoto."

“Baada ya kujifunza tuliweza kuanzisha hapa JKCI data base hiyo na hadi sasa Tanzania ni kati ya nchi tatu za Afrika inayotumia data base hiyo inayosimamiwa na wataalam waliopo Boston”, alisema Dkt. Naizhijwa.

Dkt. Naizhijwa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma JKCI alisema kupitia data base hiyo JKCI inapeleka taarifa zote za upasuaji wa moyo unaofanywa, maendeleo ya wagonjwa, na aina ya upasuaji unaofanywa na kulinganishwa na wenzao wa Afrika na nchi nyingine nje ya Afrika.

Aidha Dkt. Naizhijwa alisema katika kongamano la nane wataalam wa JKCI wameweza kutuma majalada 9 ili yaweze kutumika ambapo majalada 7 yamekubaliwa kwa ajili ya kuwasilishwa katika kongamano hilo.

“Ni nafasi ya kipekee kwetu sisi kwani majalada hadi yaweze kukubalika kuwasilishwa katika kongamano hili la kipekee kwa watoa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto lazima yakidhi viwango vinavyohitajika.

“Kupitia kongamano hili JKCI inapeleka kazi zake ili ziweze kuonekana na kuitangaza Taasisi, kutengeneza uhusiano na wataalam kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na kufungua fursa za masomo, utafiti na kubadilishana uzoefu,” alisema Dkt. Naizhijwa
 
Hatua kubwa sana, ni taarifa kama hizi ndio zinatuonesha kuwa kunahatua nchi imepiga
 
Back
Top Bottom