Hospitali ya Taifa Muhimbili yaweka rekodi kuhusu upasuaji wa kifua wakitumia tundu moja

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,142
6,947
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imefanya upasuaji wa kifua ili kuondoa uvimbe kwenye mapafu kwa kutumia tundu dogo, na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kufanya upasuaji wa aina hiyo.

Upasuaji huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza nchini umehusisha jopo la madaktari wa ndani, japo kiongozi wa jopo hili alikuwa ni daktari bingwa wa upasuaji kifua, kutoka Hispania Diego Gonzalez Rivas.

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji (MNH), Dk Rachel Mhaville, amesema, upasuaji huu ni mwendelezo wa azma ya Serikali ya kuhakikisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zinatolewa nchini, zenye kuleta unafuu kwa wananchi.

“Upasuaji huu unaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutumia tundu moja dogo, tena katika hospitali ya umma katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikilinganisha na matundu matatu yaliyozoeleka sehemu nyingine duniani.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa hospitali hiyo tawi la Upanga, Dk Ibrahim Mkoma, amesema mgonjwa akifanyiwa upasuaji huo afya yake inaimarika kwa haraka zaidi tofauti na upasuaji wa kawaida.

“Mgonjwa akifanyiwa upasuaji ambao siyo wa kufungua kifua anaweza asihitaji kukaa ICU kama wagonjwa wengine wa upasuaji wa kawaida na akaruhusiwa siku ya pili au ya tatu yake hivyo kuendelea na shughuli zake mapema zaidi.

Kwa mujibu wa Dk Mkoma wagonjwa wengine wanne wanategemewa kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo na mara baada ya hapo madaktari wazawa wataendelea kutoa huduma hiyo kwa wananchi wenye changamoto mbalimbali.

Mwananchi
 
Hongera sana Daktari wetu Mkuu wa nchi, mama Samia.
 
Back
Top Bottom