Mara nyingi utawasikia
baadhi ya watu wakijirahumu kutokana na kufikiri kuwa sura zao na
maumbo yao kutokuwa na mvuto kwa watu ambao wangependa kuwa nao katika
mahusiano (Mapenzi) lakini kwangu mimi sura yangu na umbo langu sasa
vimenifanya kukosa amani,furaha na uhuru wa kuwa na mahusiano na
nimpendaye na kufikia kusema maneno ya kumkufuru Mungu kwamba labda
alinipendelea alipokuwa ananiumba!!!! kwani nimekuwa nikigombaniwa na
kila msichana na wengine wamekuwa wakinichukia eti kisa sitaki kuwa nao
kimapenzi pia wengine wamekuwa wakinitangaza kuwa mimi ni mchumba wao na
wengine wamekuwa wakiniomba namba za simu na kunipigia wakibembeleza
kuwa na mimi na mbaya zaidi wasichana wengine wamediliki kuanza kutumia
nguvu za giza ili wanipate!! na mambo mengine mengi nimekutanayo mara
baada ya kuingia utu uzima.Jamani nifanye nini ???naomba ushauri
wenu.Naitwa handsome Boy k
ama wao walivyonibatiza!!!!!!!!