SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,923
What, when and how you wear says a lot about you.
Umenikumbusha vituko vya mdogo wangu; yeye tabia yake ni kutoongea kiswahili akienda ofisi za watu anaojua ni wasumbufu. Basi wanababaika kuwa yeye ni foreigner na wanampa huduma faster. Hata kwenye simu nimeshajaribu kutumia kiinglish na sijawahi pata tabu ya kuwa connected na bosi ninaowahitaji. Ongea kiswahili uone. Nadhani wabongo tuna tabia ya kubabaikia foreigners pia. Utanashati peke yake wala haulipi kwani ukawii kuchuniwa na masecretry wa ofisi unayotembelea; wewe piga ngeli tu.
Dada,dada,dada,haya umeanza!!Hivi Eiyer Bro.... ma'swagga ana habari juu ya jicho lako juu ya them lips?? lol
Shosti mzima?
Naomba tupanue wigo kidooogo ili pia watu wengi zaidi wafaidike na mazungumzo haya.
Nitachangia kwenye bold hapo kuhusiana na kupata/kukosa fursa zaidi ya kuhudumiwa.
Nitaanza kwa kusema kuwa uzoefu umenifundisha kusoma mazingira kama unatafuta kazi.Niliwahi kukosa kazi nzuri sana huko nyuma kwa kushindwa kujua nifanye nini ili kuuza zaidi ya CV. Kazi ya mwanzo ilikuwa ya kimataifa lakini zenye kutaka mhusika kutembelea maeneo mbalimbali yakiwemo makambi ya wakimbizi. Nilshangaa nilipokosa kazi ya mwanzo kwa vile nilionekana sitamudu kazi za field na kwamba nina uzoefu zaidi na mambo mengine ya kimataifa ( kisa ni kwa vile CV yangu inaonyesha uzoefu anga hizo na jinsi nilivyovaa au kujiweka!)
Kazi ya pili nilishajifunza. Nilipoitwa kwenye interview nilivaa mavazi ya kiafrica na kupunguza makali ya CV na kusisitiza zaidi uzoefu wa grassroots.Kujibu maswali kwenye medani ya kimataifa haikuwa issue.Ajabu na kweli kazi niliipata na kujulishwa in less than 2 hours baada ya interview. Hivyo basi utanashati unaweza kumpoza mtu vilevile.
Mafundisho ni mengi lakini nitashare huo mfano mmoja tu kwa sasa.
"Annadhafa Minnal Imaan" Unadhifu uko kwenye imani.
Hapa ndio penyewe haswa. Ikiwa yeyote hana imani unadhifu atautoa wapi? Iwe anahudumia au anahudumiwa. Iwe tajiri au maskini. Ni wapi maskini anatakiwa asiwe nadhifu? Hakuna.
Unadhifu wa kwanza ni wa moyo au roho, kama hauna huo, unaweza kuwa nadhifu wa nguo lakini roho yako isiwe nadhifu na hiyo itajionesha na kujitokeza katika uso wako, au mdomo wako, au mwendo wako.
Kwanza tuwe nadhifu kwenye nyoyo na roho zetu na mengine yatafatia.
Kweli, unadhifu ni imani.
..........Hapo kwenye nyekundu kumenikumbusha mbali sana, kazi yangu ya kwanza niliipata baada ya kumaliza form 6...........hata CV nilikuwa sina tena ni kazi ya kimataifa. Basi nikapewa ushauri jinsi ya kuvaa kwenye interview.........nikaambiwa kwa kuwa una umri mdogo hapo nilikuwa na 19 basi natakiwa kuvaa kiafrica zaidi ili nionekane nipo serious.
Sasa basi hata nguo ya kitenge nilikuwa sina..........ikabidi nikaazima nguo ya mama, nikavaa kiafrica na kiremba juu mtoto wa kike. Nilikutana na watu wengi wamevaa suti, u know what?? Kati ya wanawake tuliokuwepo pale mimi nilipata ile kazi japokuwa umri ulikuwa mdogo.
AishaDii
Thank you for this very, very useful thread
Kusema ukweli umegusia jambo zuri sana, hasa ulivyotoa mifano ya hao wabunge wawili. Mh kwa kweli inasikitisha. Nitachangia kidogo tu maana Tanesco wameniazima nusu umeme!! sitaki deni mie!
Uzuri:
- Katika hili kusema ukweli nadhani kuna makosa yanayofanyika kwa kumpatia mtu upendeleo kwa kigezo hikli (Na ni kweli inafanyioka sana tu na mfano mzuri ni hao wabunge). Yaani kwa kuangalia uzuri wa mtu tu basi unambebesha na sifa nyingine asokuwa nazo!! Hii inatucost sana kimaendeleo. Lakini pamoja na hayo labda ningependa kujua definition tuliyoitumia ya Uzuri......kama ni ule wa asili (sijui ndo sawa na urembo?!) ambao mtu hauchakachui, kama ni mzuri, ni mzuri tu.....apale matope au poda ni mzuri. Haijalishi kama kichwani ni safi au la sehemu nyingine za kazi, huduma atapata huduma,kazi kisa ni mzuri (Hii kwangu imekaa kinyanyasaji nyanyasaji vile- mtu anakuthamini wewe kwa uzuri wa sura!!)
- lakini kwa upande mwingine uzuri wako unawezakukunyima wewe kitu, huduma au kazi nzuri! au ikakunyima wewe mzuri kufulfill adhima yako ya maisha!! Mfano ushasema wasichana wazuri wanakuwa wabunge- no one will believe kuwa umeteuliwa kiuwezo (kama ni wa kuteuliwa) au kama ni oficn umepandishwa cheo kiuwezo (unless kuna achievements zinazoonekana kutokana na uwezo wako). wengi watahisi uzuri ndio umekuweka hapo ulipo. Hii mara nyingi unawezajikuta unaghairi (kama nia yako ilikuwa ni kuwa mbunge- kama huwezigombea) basi hata kwenye siasa utaogopa kuingia ili kuepusha ikitokea umeteuliwa watu watasema ni uzuri!!!
Utanashati: Hili sina experience nalo inakuwaje hasa, yaani unapata huduma, kazi, kiupendeleo kwa kuwa u'mtanashati au?'
Sometimes nawaoneaga huruma wadogo zetu/wadada walio wazuri......sometimes wanatafsiriwa vibaya.mf. ukimwona mdada mzuri anaendesha gari zuri barabarani, kitu cha kwanza kuja kichwani ni.....c'mon what do you expect kwa msichana mzuri kama yule' implying that lazima kuna pedejee kajipinda!! Au ule usemi wa kina kak wengi wa mwanamke mzuri si wa kuoa! unajitafutia presha tu.....as if mwanamke mzuri hawezi kuwa mke mwema! Mahusiano!! mwe
Habari zenu JF Ladies and Gentlemen.....
From my perspective and experiences mbali mbali katika maeneo mbali mbali nime observe saana hili suala la Uzuri/Urembo/Utanashati unavyochukua nafasi kubwa saana katika kupata huduma mbali mbali katika jamii – yaani ni kwamba tunapotembelea/tembelewa katika office, organizations, groups, institutions mbali mbali the way wewe personally unaonekana ndio itayo pelekea aina ya huduma na mapokezi utayopata…
Pamoja Saaana…
AshaDii (ADI)
You are quite right AshaDii.
Katika ulimwengu wa impression suala hili haliepukiki.
Lecturer wangu Mjerumani, miaka mingi imepita sasa, aliwahi kusema"The first impression is the deepest".
Ikiwa first impression hailingani na suala unalofukuzia , ni rahisi kutupwa kapuni.
Du wewe Rejao, yaani sisi weusi , tena weusi tii kama mimi-mpaka nakaribia weusi wa deep blue, hatuwezi pata kazi benki?Nimeobserve hili swala kwenye banks nyingi hapa tanzanzania.
Wanaume watanashati, wenye mvuto na tena wakiwa weupe ni an added advantage ya kupata kazi.
Du wewe Rejao, yaani sisi weusi , tena weusi tii kama mimi-mpaka nakaribia weusi wa deep blue, hatuwezi pata kazi benki?
Naweka picha ya GF wangu ambaye vile vile ni blue black-isnt she a beut at first impression?
![]()
Huwa inatokea, na mara nyingi nikiwa blue black imenitokea.Nimependa the quote and it is soo true.... However Lole G, tatizo linakuja pale kua
you have tried your best na unajikuta katika Disadvantage hio... wat do you do??
Huwa inatokea, na mara nyingi nikiwa blue black imenitokea.
Hii inakuwa stereotype kwa mtu wa upande wa pili, na inaweza kumuumiza yeye mwenyewe akija gundua kuwa alikuwa akifanya a grave mistake.
Nitatoa mfano hai, miaka kadhaa nilienda Mwanza kumrelieve a collegue of mine ambaye alikuwa anahamishwa.Mwenzangu ambaye alikuwa na kitambi kikubwa na mwili mrefu ilibidi anitambulishe ofisi fulani ya waAsia ambayo ingewajibika kwangu.
Bahati mbaya sana I did not make a good impression kwenye ofisi ya hawa jamaa kabla ya introduction-kwa hiyo tulipofika ofisini kwao sikuchngamkiwa wala sikukaribishwa kiti.Kwa vile kiti kilikuwa kimoja out of respect mwenzangu wala hakukaa vile vile.
Baada ya introduction ndio viti vikaletwa tena mbio.
I took note.
Probably it was my problem, I did not act bossy enough and I was black to the teeth!!
Kwa wenzetu mnao wafahamu waAsia, alisikitika sana kufanya kosa hilo, and of course it cost him.