Uzi wa kupeana machimbo mbalimbali ya vifaa vya ujenzi na bei zake

Naombeni elimu ya bati.

Naona humu watu wanataja mita mita...kwani bati linaloezekwa kwenye nyumba lile linakuwa ni mita/futi ngapi? Na linauzwaje likiwa lote lote kama linavyobandikwa kwenye nyumba?

Alternativelly,

Bati linaloezekwa kwenye paa ya kawaida(paa za siku hizi zinazotumiwa na wengi) linakuwa na mita/futi ngapi?
 
Kiwanda kinaitwa sunbank Kiko Banda la ngozi
Bati za bundle upana 80 cm urefu 3m
Bei 22,000 (30g) (IT5 & CORROGATED)
Bati za vipimo (IT5 & CORROGATED)
30g upana 90cm 11,000
28g upana 90cm 13,500
Versatile ( muundo WA kigae)
30g upana 90cm 13,500
28g upana 90cm 15,000

Offer
Misumari 20 pc
Free transport
Warranty 10yrs
CONT 0685572320
Naomba unielimishe mkuu, bati linaloezekwa kwenye paa ya kawaida (hizi paa za kisasa) linakuwa na futi/Mita ngapi? Ili kupata bei kamilifu ya angalau bati kamilifu
 
Hakuna bati isiyo pauka ila ni mda Gani bati iyo inapauka
Mfano kama bati za sunbank at least ndani ya miaka kumi Kuna uwezekano ikaaza kupauka that why...inatolewa legally warranty ya 10 yrs
Ukianza kudai warrant yako ..wanakuja kuanza kupima ulipauaje..angle ilikuaje mwisho wa siku watakuambia fundi wako ndo alikosea kuezeka
 
Naombeni elimu ya bati.

Naona humu watu wanataja mita mita...kwani bati linaloezekwa kwenye nyumba lile linakuwa ni mita/futi ngapi? Na linauzwaje likiwa lote lote kama linavyobandikwa kwenye nyumba?

Alternativelly,

Bati linaloezekwa kwenye paa ya kawaida(paa za siku hizi zinazotumiwa na wengi) linakuwa na mita/futi ngapi?
Mabati kivipimo yana şifa kuu tatu;

1. Ujazo (thickness) au gauge (geji kiswahili cha mtaani). Hii ni kipimo cha unene wa bati ambapo bati nyingi ni kati ya gauge 26 na 32. Kadili number inavyokuwa kubwa ndio ujazo unapungua na bei pia huzidi kushuka. Unashauriwa kwa ujenzi wa majengo tumia gauge kati ya 26-30 ambapo 30 ni bei nafuu lakini sio bora japo kigumu unaweza kuitumia.

2. Urefu. Mabati huuzwa kwa urefu wowote utokao japo ya kukata kwa bando mengi huwa mita 3. Lakini kwa Tanzania unaweza kupata bati hadi la mita 12 kiwandani kwa order. So unaposikia watu wanauza kwa mita wana maanisha mita za urefu.

3. Upana. Mabati hutengenezwa kwa upana tofauti tofauti ambapo mengi ni kati ya sentimeta 95 hadi 125. Na zingatia kuwa upana utategemea zaidi aina za mikunjo ya bati. So hapa utakuta kuna mikunjo aina nyingi, kama vile IT4 & 5 mitaani mnaita msauzi, CIS mtaani ndio yale ya kawaida yanayouzwa kwa mabundle etc. Na zingatia unaponunua bati unatakiwa ujue upana unaouziwa ni upi (upana wa bati vs upana wa eneo bati linaloezekwa). Hili ni muhimu kwa sababu kila bati lina upana standard wa kuezeka na nafasi inayobaki ni kwa ajili ya kuvalishia bati jingine (kava).

Kwa hiyo ukienda kiwandani utauziwa mita zozote utakazo ilimradi hazizidi 12. Na upana utachagua kutokana na mikunjo. So kwa Tanzania nyumba haiwezi kuwa na bati moja lakini pia si lazima yawe mengi kama utanunua kwa urefu. Ukinunua ya bundle lazima yawe mengi na yatakusumbua kukata kata.
 
42 na 32 huwa inamaanisha nini kwenye saruji?
Kwa kifupi 32.5 na 42.5 ni viwango vya uimara wa simenti ikikauka. 42.5 ni simenti imara zaidi kulinganisha na 32.5. Kwa kazi kubwa tumia 42.5 na 32.5 kwa ujenzi mwepesi.
 
32.5 na 42.5 ni cement strength after 28days. Maana yake, ni kwamba after 28days Cement ya 42.5 inatakiwa iwe na strength zaidi ya 42.5Mpa. The same applies to 32.5. Strength ya Cement inapimwa kwa siku 1, siku 2, siku 7 na siku 28.
 
kwa lay man haya uliyoandika hawezi kuelewa hasa habari ya vipimo vya Mpa. Na hata upimaji kwa siku itategemea kama simenti husika ni N au R grade. N ndio hufuata zaidi kanuni hiyo ya kupima uimara kwa siku hizo, R hupata uimara mapema zaidi.
 
Mabati kivipimo yana şifa kuu tatu;

1. Ujazo (thickness) au gauge (geji kiswahili cha mtaani). Hii ni kipimo cha unene wa bati ambapo bati nyingi ni kati ya gauge 26 na 32. Kadili number inavyokuwa kubwa ndio ujazo unapungua na bei pia huzidi kushuka. Unashauriwa kwa ujenzi wa majengo tumia gauge kati ya 26-30 ambapo 30 ni bei nafuu lakini sio bora japo kigumu unaweza kuitumia.

2. Urefu. Mabati huuzwa kwa urefu wowote utokao japo ya kukata kwa bando mengi huwa mita 3. Lakini kwa Tanzania unaweza kupata bati hadi la mita 12 kiwandani kwa order. So unaposikia watu wanauza kwa mita wana maanisha mita za urefu.

3. Upana. Mabati hutengenezwa kwa upana tofauti tofauti ambapo mengi ni kati ya sentimeta 95 hadi 125. Na zingatia kuwa upana utategemea zaidi aina za mikunjo ya bati. So hapa utakuta kuna mikunjo aina nyingi, kama vile IT4 & 5 mitaani mnaita msauzi, CIS mtaani ndio yale ya kawaida yanayouzwa kwa mabundle etc. Na zingatia unaponunua bati unatakiwa ujue upana unaouziwa ni upi (upana wa bati vs upana wa eneo bati linaloezekwa). Hili ni muhimu kwa sababu kila bati lina upana standard wa kuezeka na nafasi inayobaki ni kwa ajili ya kuvalishia bati jingine (kava).

Kwa hiyo ukienda kiwandani utauziwa mita zozote utakazo ilimradi hazizidi 12. Na upana utachagua kutokana na mikunjo. So kwa Tanzania nyumba haiwezi kuwa na bati moja lakini pia si lazima yawe mengi kama utanunua kwa urefu. Ukinunua ya bundle lazima yawe mengi na yatakusumbua kukata kata.
Samahani kiongozi!! Hv ukinunua Bati kwa BANDO na ukinunua kwa VIPIMO kwa Galama inapoa? Na je UBORA unakuaje?

Asante
 
Kwa kawaida ni heri ununue bati kwa vipimo. Bati la kipimo linakusaidia kununua exactly vipimo unavyotaka toka Kiwandani na kupunguza waste (vipande ambavyo huitaji). Pili kwa mfano unaezeka sehemu ya urefu wa mita 9 (za bundle itahitaji nne kufidia na overlap) wakati za kupima unaweza kununua mita 9 net (hili halihitaji cover limeungwa) utakuwa umesave gharama ya mita tatu, umepunguza uwezekano wa kuvuja na umeongeza ufanisi wa kufanya kazi.

Kuhusu ubora wa materials husika ni ule ule. Hata bati za bundle zinazouzwa hukatwa kutoka kwenye sheet ndefu zaidi.
 
Asante kiongozi
 
Kwema Wakuu,

Ujenzi umekua gharama sana sababu ya kuongezeka kwa bei za bidhaa kunakoendana na ongezeko la bidhaa zingine zisizo za ujenzi pia.

Kwa aliejenga miaka 10 nyuma gharama hizo hizo akitaka kujenga sasa kwa nyumba ya aina ile ile anaweza asifike hata 60% ya nyumba aliojenga mwanzo kutokana na kupanda huko kwa gharama za Ujenzi.

Lakini sio kupanda kwa bei tu ambako ni "involuntary" kunakochangia kuongezeka kwa gharama za Ujenzi, bali pia uwepo wa wafanyabiashara na madalali wenye tamaa ni changamoto ingine.

Hivyo basi kupitia uzi huu tusaidiane kujulishana gharama mbalimbali za bidhaa mbalimbali za ujenzi kuanzia ufundi mpaka materials ambapo unadhani vilikua nafuu. Viwe ni vifaa halali tu ili tusileteane matatizo baadae.

Najua kuna kitu kinaitwa soko huria ambapo muuzaji akitoa bei na mnunuzi akaridhika nayo inakua halali yao wote wawili. Na pengine labda kuna wanunuzi wenze wako na wauzaji wao maalumu lakini kupitia uzi huu basi mnunuaji anaweza kufaidika kwa kujua bei ya kitu ili akienda kwa muuzaji wake ajue ana bargain vipi.

NB;
Lengo kuu la uzi huu sio kumtangazia mtu biashara ili afaidike yeye mfanyabiashara au mtoa huduma, bali kumsaidia consumer.

Karibuni.
Kwa mitaa ya kigamboni nenda pale karibu na hospitali ya serikali vijibweni, Kuna duka kubwa la vifaa vya ujenzi linauza mazaga ya ujenzi bei poa. sana.
Mfano juzi nimenunu tiles 50*50 @ 31,000/-, 25*40 @ 16,500, 40*40 @25,000
 
Nilishanunua,
40 x 40 nilinunua Kwa 21,500/- Goodwill
 
Kwa mitaa ya kigamboni nenda pale karibu na hospitali ya serikali vijibweni, Kuna duka kubwa la vifaa vya ujenzi linauza mazaga ya ujenzi bei poa. sana.
Mfano juzi nimenunu tiles 50*50 @ 31,000/-, 25*40 @ 16,500, 40*40 @25,000
Tiles za kampuni gani hizi? Goodwill or Twyford?
 
Back
Top Bottom