Uzi wa kupeana machimbo mbalimbali ya vifaa vya ujenzi na bei zake

Shakir

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
1,602
1,819
Kwema Wakuu,

Ujenzi umekua gharama sana sababu ya kuongezeka kwa bei za bidhaa kunakoendana na ongezeko la bidhaa zingine zisizo za ujenzi pia.

Kwa aliejenga miaka 10 nyuma gharama hizo hizo akitaka kujenga sasa kwa nyumba ya aina ile ile anaweza asifike hata 60% ya nyumba aliojenga mwanzo kutokana na kupanda huko kwa gharama za Ujenzi.

Lakini sio kupanda kwa bei tu ambako ni "involuntary" kunakochangia kuongezeka kwa gharama za Ujenzi, bali pia uwepo wa wafanyabiashara na madalali wenye tamaa ni changamoto ingine.

Hivyo basi kupitia uzi huu tusaidiane kujulishana gharama mbalimbali za bidhaa mbalimbali za ujenzi kuanzia ufundi mpaka materials ambapo unadhani vilikua nafuu. Viwe ni vifaa halali tu ili tusileteane matatizo baadae.

Najua kuna kitu kinaitwa soko huria ambapo muuzaji akitoa bei na mnunuzi akaridhika nayo inakua halali yao wote wawili. Na pengine labda kuna wanunuzi wenze wako na wauzaji wao maalumu lakini kupitia uzi huu basi mnunuaji anaweza kufaidika kwa kujua bei ya kitu ili akienda kwa muuzaji wake ajue ana bargain vipi.

NB;
Lengo kuu la uzi huu sio kumtangazia mtu biashara ili afaidike yeye mfanyabiashara au mtoa huduma, bali kumsaidia consumer.

Karibuni.
 
Naanza na Mimi.

Nilipata mbao kutoka kwa Ustaadhi mmoja hivi pale Buguruni. Fundi wangu aliniambia nimtume yeye akachukue yeye kwa TZS 450/futi 2x2 na TZS 900/ft Kwa 4x2. Alisema nikienda mimi nitapewa mbao mbichi, zisizo na dawa au zenye vidonda.

Nilivyoenda mwenyewe nilipata kwa TZS 350 mbao za 2x2 na TZS 700 mbao za 4x2. Yawezekana najiona cheaper kumbe nami nimepigwa bado ila ni angalau kuliko hardware za hapo napojenga.

Bati geji 30 nilipata kwa TZS 11,500/mita kiwandani Dragon.
 
Cement ya 42 ile kali inauzwa mtaani 17,500 na kuniletea mpaka home niongeze buku. Kuna jamaa nlimuona Facebook anajiita Michael Ngus aliniletea mpaka saiti Kwa 15,500 sharti tu uchukue kuanzia mifuko 100
Ahsante sana aisee,
Hata huku mtaani bei ya cement ni kubwa.
 
Naanza na Mimi
Nilipata mbao kutoka kwa Ustaadhi mmoja hivi pale Buguruni. Fundi wangu aliniambia nimtume yeye akachukue yeye kwa TZS 450/futi 2x2 na TZS 900/ft Kwa 4x2. Alisema nikienda mimi nitapewa mbao mbichi, zisizo na dawa au zenye vidonda.

Nilivyoenda mwenyewe nilipata kwa TZS 350 mbao za 2x2 na TZS 700 mbao za 4x2. Yawezekana najiona cheaper kumbe nami nimepigwa bado ila ni angalau kuliko hardware za hapo napojenga.

Bati geji 30 nilipata kwa TZS 11,500/mita kiwandani Dragon.

Ukiona unauziwa mbao kwa futi ujue umepigwa. Mbao za kuezekea nunua 4 x2 za futi 12 kwisha kazi.
 
Back
Top Bottom