Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji.
Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri.
Ili kuonyesha uwezo wao katika utawala huo, ndio raia pekee wanaokubaliwa kubeba bunduki zilizo na risasi karibu na kiongozi wa taifa lao, sana sana huwa bunduki zinazodaiwa kuwa automatic pamoja na silaha nyengine.
Licha ya kubeba silaha, ulinzi mkubwa wanaompatia rais Kim jong un ni ujuzi walio nao katika kuwachunguza watu walio karibu na kiongozi huyo na kukabiliana na tishio lolote kwa kutumia mikono yao na mwili.
Walinzi wa Kim Jong Un ikilinganishwa na wale wa babake ni wachache na hawaonekani mara kwa mara. Walinzi hao huvalia suti za magharibi kama wanavyoonekana nchini Singapore .
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.