Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utajiri mkubwa wa Madini Ya Shaba

Mapera yana madini ya shaba ( Trace element copper ) ambayo ni mazuri sana katika ku- maintain ufanyaji kazi wa tezi ziitwazo thyroid.Tezi za thyroid zisipo fanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya kwa mwanadamu.
 
Utajiri wa Madini Ya Manganese

Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya manganese ambayo yanausaidia mwili katika kunyonya ama kupata virutubisho muhimu kutoka kwenye vyakula tunavyo kula.Chakula tunacho tumia kikitumika vizuri mwilini, tunapata virutubisho vyote muhimu kama vile biotini, vitamin nakadhalika..
 
Kuusadia mwili na akili katika ku-relax

Mapeara yana utajiri mkubwa wa madini ya magnesium ambayo hufanya kazi ya kuvifanya akili na mwili wa mwanadamu viweze ku relax. Unashauriwa kutumia mapera baada ya kazi nzito. Hii itasaidia katika kuufanya mwili na akili yako kupumzika
 
Kama hiyo haitoshi, kokwa la mpera huwa linatumika katika kutengeneza vipodozi na losheni kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu.Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi nzuri ya fiber na 'lycophene' vyote hivi ni muhimu kwa afya.
 
Back
Top Bottom