Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Jan 25, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  1. Waislamu wameahidiwa Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC.
  2. Hii imewafanya waweke matumaini makubwa kwa Serikali ya Awamu ya Nne na kwa rais Jakaya Kikwete kuwa amesikia kilio chao cha muda mrefu.
  3. Je, haya matumaini ndiyo yanayofanya baadhi ya masheikh waanze kuwapinga maaskofu pale wanapotoa kauli dhidi ya serikali ili ionekane wanaiunga mkono serikali? I.e. Wanaogopa serikali isije ikabadili msimamo wake kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC?
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Serikali yoyote ile itakayokuwa madaraka madai hayo hayatafutika..wala hayatabadilika milele..no time limit it is ongoing project ok by any means necessary

  Maaskofu wamepotoka kutoa matamko ya kibaguzi ndio masheikh wanawapa tahadhari, kwa faida ya jamii nzima
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  kwani serikali ndio itakayojiunga au dini??sipati picha sheria za al-shabib zikija bongo
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wewe kwani zitakuhusu ni sharia laws zitawahusu wale wanaozifuata na kuzikubali wewe hazitakugusa pilipili ya shamba wewe yakuwashia nini?????
   
 5. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Tumia akili za kawaida Dr ( award) Jk tangu mwaka 2005 alikuwa akubaliki kwa Waislam waliowengi,hivo akatafuta cheap popularity ya kwa kuwadanganya.Jk hana udini hata siku moja ila amekuwa akitafuta jinsi ya kuwaridhisha wanaojiita the infiriority(tunaonewa,tunafelishwa,hatuajiriwi,hatukubaliki,tuko chini n.k) ndo maana teuzi zake nyingi zimekuwa zikizingatia dini wala si uwezo.Kikwete anasomesha watoto wake shule za Katoliki(Tanga) wala sio Ubungo au kirinjiku Islamic schools, kinywaji anakamata kama kawa.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  basi mi nkajua watu wote itawakamata
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hapana Mkuu sidhani, itawakamata waislamu tu na sio kila sharia bali nadhani baadhi tu. Maana sharia zengine na sie wengine tunakunywa kidogo si tutakatwa shingo wajameni!!!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  lakini mkuu si unaipigia debe? au unaangalia upande mmoja tu wa shilingi....nimeona kule somali al shabib wamempika bakora bibi wa miaka zaidi ya 60 kwa kutovaa vazi walilolibuni wao
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,122
  Trophy Points: 280
  Wishful thinking.
   
 10. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu ndio naipigia debe kwani naona baadhi ya mali za waislamu zinavyoliwa na wajanja mjini? Wewe hujiulizi viwanja vya Chukua Chako Mapema wanavipata wapi? Watoto yatima kibao wanatangatanga. Ni hali ya kusikitisha mkuu hata wewe ungeliona ungeliipigia debe, ila ikae huko katika mirathi ikigusa huko kwengine itakuwa shughuli nzito itabidi tutafute kazi Rwanda!!!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  haha wakikushtukia watakufuata huko huko basi kama inawagusa nyinyi tu basi bana peweni hata mkitaka kuwaleta al-shabib wazisimamie mi ntakuwa sina shda na mtu
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe linapokuja suala la dini akili huwa unaiacha nyumbani!!! Ubaguzi wa kidini uliofanywa na maaskofu ni upi?? Yaani maaskofu wasikemee uovu wa serikali kisa eti wanaofanyiwa uovu ni wakristo kwa hiyo waache kukemea ili wasionekane wabaguzi. Acha upuuzi huo. Mtaendelea kulalamikia masuala yasiyo na mantiki mpaka lini? Tatizo ninaloliona ni kwamba wengi wenu ninyi mmeishia elimu ya madrasa tu na ndiyo maana arguments zenu pamoja na 'mashekhe njaa' wenu hazina mashiko. Watanzania wengi tunamwamini Shekhe Mkuu na Bakwata ambao siku zote wanapotoa maoni yoyote utaona akili, hekima na busara zimetumika. Siyo ninyi akina yakhe wazee wa ubwabwa mnaouza juice za miwa mitaani. Kazi kulalamika lalamika tu. Mnatumiwa na mafisadi kuvuruga nchi kwa kudanganywa kwa SAHANI MOJA PILAU au UBWABWA. Huo ndiyo ukweli na nitaendelea kusema siku zote. Kadri wasomi wanavyoongezeka, ndivyo mtakavyoendelea kubaini kuwa mnayolalamikia kumbe ni upuuzi tu.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hahaha wakinifuata Rwanda nawatimua na Ak-47 si unajua kuna Interahamwe kule hawataki mchezo.
   
 14. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Wameingizwa cha .....kike...maasikofu kimya hawajibu cheap complaints.
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  'GREAT THINKERS' wa JF @work

  Interesting...
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Magobe T,
  1. ni kweli, unapoahidiwa kitu, kipindi chote cha kusubiria, lazima uwe mpole. Kabla ya ahadi hizo, hao ndio waliokuwa mstari wa mbele kuichachafya serikali.
  2. Kilichofanyika katika Ilani ya CCM, kilikuwa danganya toto kwa jina ya 'engenging the Muslim community'. Lakini kwa vile walipewa legitimate expectation, hata kama lengo halikuwa kweli, lakini sasa litabidi liwe kweli vinginevyo hako mbeleni hakutakalika.
  3. Mimi ni Mkatoliki Die Hard, lakini nawaunga mkono ndugu zetu Waislamu kweli hili la Mahakama ya Kadhi hata kwenye la IOC kwa upande wa Zanzibar.
  4. Uganga ni member wa IOC na pia anayo mahakama ya Kadhi.
  5. Kabla ya uhuru mpaka tunapata uhuru, tulikuwa na Mahakama ya Kadhi, haina problem kwa isiyowahusu.
  6. Jamii ya Hindu, wanayozo mahakama zao, Sunni wana mahakama zao, Ismailia wana mahakama zao na Singasinga pia wana mahakama zao. Kamwe huwezi kusikia kesi mahakama za kawaida wahindi wanadaiana, ukuina tuu imetinga mahakamama zetu, ujue one part sio mwenzao.
  7. Nadhani hata sisi tuna mahakama zetu za mambo ya ndoa, ambazo hukutana kila Alhamisi pale St. Joseph, uzuri wetu sisi, ni upatanisho tuu, hatuvunji ndoa kamwe!.
  8. Na kama zikianza, zitawahusu Waislamu tuu ambao wataridhia kutumia sharia law kwa ridhaa zao wenyewe bila kulazimishwa.
  9. Ikitokea ndoa ya Muislamu na asiye Muislamu, sheria za nchi ndizo zitatumika.
  10. Nasisitiza, waacheni wapate wanacholilia as long as serikali haitazigharimia wala kuwaingilia. Sio vizuri kuwadanganya wenzenu kama danganya toto, watafika mahali wakate tamaa na kuamua kufanya lolote, tusije tukajiundia katawi ketu cha Al-Shabab na Al-Qaeda!.
   
 17. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Dont you think kuwa na UN POPULAR OPINION hawa GREAT THINKERS watakuchukia?

  I salute your bravery kwa kuwa muwazi na mawazo yako japo utashambuliwa

  btw KENYA nao waliiincorperate Kadhi courts kwenye katiba yao BILA MATATIZO na watu wako kimyaaa
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  SLIDINGROOF, asante kwa maona yako, kwa kawaida kwenye kila jambo kuna two sides, side moja ni the truth, na side ya pili ni the Perceived perception. Hii Perceived perception ndio public opinion. Mimi siku zote huwa nafuata the truth, sio public opinion.

  Kuna issues nyingi natofautiana na watu humu kwa vile wengi huamini ile Perceived perception ambayo unfortunately sio the truth.

  The Truth ni mahakama ya Kadhi, haina problem kwa isiyowahusu!.

  Ila pia mimi nasimamia kwenye ukweli ninauamini.
  Mfano,
  1. Liumba anaonewa, huwezi kumshitaki kwa full value ya Twin Tower wakati jengo liko na limesimama. Angeshitakiwa kwa ile addition value iliyozidi ndio ingeitwa hasara. Kwa vile BOT, walibudget kiasi fulani kujenga Twin Tower, baada ya kukamilika walitakiwa wafanye kwanza uthamini wa jango kupata full value, wafanya value for money, any amout ambayo ni access ndio wamshitaki Liyumba kusababisha hasara. Japo rufani imekataliwa, Makakimu wetu ndi binadamu tuu kama binadamu wengine hawajamtendea haki. Kwa msimamo huu, nilishambuliwa sana!.
  2. Kesi ya kina Mramba, Yona na Mgonja, nilisema sio kesi, ni danganya toto kwa JK kujisafisha mbele ya wafadhili na wananchi ili aonekane anachukua hatua, it is very weak case na itakuwa thrown out within no time. Pia nilikula mashambulizi.
  3. Kwenye issue ya Kagoda, mimi ni miongoni mwa waliosema kamwe haitafikishwa mahakamani, huku wengi wakimtaja Rostam, mimi nilikataa na bado nakataa, Rostam ni dalali tuu, wenyewe walikuwepo na bado wapo, watajifikishaje mahakamani?.
  4. Na sasa kwenye hii issue ya malipo ya Dowans, mimi ni miongoni mwa wanaosema lazima tulipe kwa sababu hatuna pa kutokea. Wengi wanamtaja taja tena Rostam, mimi nawakatalia tena kuwa Rostam ni dalali tuu wa wenye mali. Nikasisitiza tutalipa sio kwa sababu ni halali, bali kwa sababu watoa uamuzi wa kulipa ndio wenyewe, hivyo wanajilipa wenyewe kwa fedha zetu!.
  Hivyo nimeshajizoelea kusimama kwenye ukweli ninauamini, hata ukishutumiwa miwa, unabaki na amani moyoni mwako na dhamira yako haikusuti.
   
 19. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Lakini kila mgombea ana ilani yake ya uchaguzi. Hiyo mahakama iliahidiwa wakati wa kampeni, na si katika official activity ya serikali. Kwa hiyo kama kuna mgombea aliahidi halafu haitekelezi, inabidi abanwe kivyake! Usije ukalazimisha wagombea wengine nao waiahidi kama alivyofanya JK, si lazima, na ndio maana kwenye ilani ya 2010 hakuiweka kabisa ili waisilamu wasimsumbue!
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  Strange nakubaliana na wewe:

  1. Liumba was a a scapegoat ili mradi the powers that be wapate their pound of flesh

  Nijuavyo major decisions hakuzifanya Liumba, mle BOT kulikuwa na TENDER BOARD, VALUATION TEAM, MANAGEMENT BOARD na wengineo ambao walishiriki kupitisha maamuzi mazito pale lakini hakuna aliyeuliza muda wote huo PPRA walikuwa wapi? CLERKS OF WORKS alikuwa ni nani? Surely its a joke na ita beggers belief kuona the wrong guy is serving time and makes you wonder ingekuwa RWANDA au CHINA hali ingekuwaje?

  2. Sioni kesi mle na naona kuna political scores zinakuwa settled. Huwezi kuwasimamisha Mramba na Yona halafu mtu kama DAVID JAIRO awe free. Not only that, our political elites ambao mpaka leo utashangaa wako kwenye Cabinet. Cha kujiuliza ni kuwa how did so many corrupt, charmless and incompetent people get away with it? jibu ni very simple , the basically suborned, subordinated and supplanted all the institutions (ambazo nadhani unazijua) which might otherwise have resisted them - often with the assistance of willing collaborators within, in the end we are given this tupid charade ya kuwapeleka mahakamani few dudes kama kina Yona & CO.

  3.Rostam ambaye alikuwa na uswahiba na akina Mengi na Mwakyembe na wengine ambao leo wanamwita all sorts of names ili kutupoteza lengo is NOT and SHOULD NOT be the issue. Mustakbali wa nchi unatakiwa kuangalia beyond few personalities na wamesahau kuwa whatever degree he got huko Cambridge certainly helped him. The man is a HUSTLER na kama alivyosema JAY Z, I cant knock the man's hustle. Wote hawa in 2005 walichukua 5 million each kwa ajili ya kampeni majimbini kwao from Rostam na yes the man proved himself walipotaka pesa na kweli aliwapa pesa (allegedly) from the MULLAH's . Sasa these stupid ****** (the so called wapiganaji) walifikiri jamaa angerejesha vipi pesa zake? To be he is our modern day ROTHSCHILD, he is a gambler who is clever and knows his bets. In the end hakuna document hata moja aliyo sign kwenye hizi so called allegations na most annoyingly ni kuwa hajibizani nao kwenye magazeti ambao stupidly wants us to believe kuwa matatizo yetu yoote yanatokana na ROSTAM!

  4.DAWA YA DENI NI KULIPA na cha ajabu unafiki wetu humu na in our stupid media wanataka tuamini kuwa all buck stops with rostam wakati kumbe haya mambo yalijadiliwa na kuwa approved by TENDER BOARDS, EVALUATION TEAMS, LEGAL TEAMS, MINISTERS, PPRA na wengineo ambao huwaoni wakitajwa kwa sababu tuu our media is entrenched with lazy heads

  I agree with you the PROBLEM is not ROSTAM, the problem ni SYSTEM NZIMA iko rotten. We know it lakini hakuna anayetaka kulisema hilo...to befair nakuwa kuwa some kuna WAZALENDO wachache In particular, kwenye civil service ambao kila kukicha wanakuwa humiliated repeatedly - their advice rejected and their normal command structures replaced by political appointees, expensive outside consultants ambao hata haijulikani wanalipwa vipi and (most sinisterly) by the WATCHDOGS which have been captured by the Political Class .

  As I always say, this country has gone to the dogs
   
Loading...