T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 13,290
- 44,744
Kwa sababu hata hizo biashara unazosema zinachakaa wakati zinaingiza fedha.Kwa nini hoteli nyingi zinachakaa wakati zinaingiza fedha?
Nikiwa Manispaa fulani jijini Dar alikuja brother kutoka Dodoma akajenga kwenye kiwanja alinunua kwa 46M mwaka 2018. Akajenga rentals 10 units chumba self na jiko uchwara kwa kutumia milioni 80 na chenji. Mwenyewe yuko kwenye mid 40s.
Jumla hapo katumia 126M+.
Hizo nyumba anapangisha 130k kama mbili hivi na 150k nyingine.
130k×2=260,000
150k×8=1,200,000
Total 1,460,000 kwa mwezi.
Nyumba za kupangisha inategemea na quality ila nina family relative namjua tangu nahitimu sekondari nilimkuta amejenga nyumba mpaka naandika hapa hajawahi zirekebisha lolote wala kubadili mifumo ya umeme wala maji, kwanza hayupo hata nchini. Miaka 10+.
Sasa huyo brother 1,460,000 wa kwa mwezi kwa mwaka ni 17.52M. Kwa miaka 10 ni 175.2M. Sasa cha ajabu ni kwamba eneo lilelile aliponunua ardhi, pembeni kiwanja kingine (exactly nusu ya kama alichojenga) kimeuzwa last year July kwa 45M nikiwepo. Maana yake yeye kiwanja pekee chenye units 10 hata ukizibomoa zote kinabaki na thamani ya 70M kwa bei ya July 2025, kimepanda thamani mara mbili ndani ya miaka 7.
Miaka 10 ijayo kiwanja chake kitakuwa na about 150M valuation. Kodi atakayokusanya ndani ya miaka 10 atakuwa na 175.2M. Total 325.2M.
Sasa hapo ukitoa miezi michache bila wapangaji, yuko mjini sehemu hot. Na miezi michache ya kusamehe kodi wapangaji wasumbufu. Bado anabaki na faida.
Alafu sasa anaweza kopea hicho kiwanja mkopo akafanya hizo biashara zako unazosema haziziki hela. Alafu baada ya miaka 10 umkute hajakarabati nyumba useme hela haikurudi ndio maana kaziacha. Kumbe ameishajifia watoto wake ni vilaza wanalewea pombe, sasa assume hao walevi angewaachia duka la vipuri au bar. Mwaka mwingi duka limepukutika.