Uwekezaji wa majengo haulipi

Uwekezaji wa majengo haulipi

Uki elewa mchezo wa majengo na ardhi, utajua wahindi, wachina au makampuni yana toa wapi fedha.

Majengo na ardhi ni good leverage.
Mfano, umepata milioni 500 leo, ukaenda kuwekeza kwenye apartment. Je, itakuchukua miaka mingapi hiyo fedha kuizalisha kwenye hiyo apartment? Ni bora ujenge na kuuza.
 
Uko sahihi, tembelea hapo mjini zile hoteli zote zilizokuwa tishio miaka mitano iliyopita, ukizikagua ndani na nje utagundua uchakavu, kwa sababu fedha za kurudisha upya wa majengo hayo ni kubwa.​
Kama kuna mji umejengwa sub standard basi ni magorofa ya biashara DSM.. Na yote ni kutaka volumes kwenye gharama kiduchu
 
Sasa hakuna uwekezaji hauna presha na hauangushi km wa nyumba na ardhi aisee hata ufanye nn mm siwezi acha najenga kajumba m 45 unauza 70 ama 65 bila presha ni wapi utapata hiyo faida bila kukimbizana na tra
Ukijenga na kuuza sawa, ila ukitaka upangishe ili uweze kujilipa, fedha ulioiwekeza hutoipata.
 
Hizo ni long term investments...Yaani unakuja kubreak even baada ya miaka 10 hadi 15...Biashara hizo hazimfahi mganga njaaa mwenye fedha za kuunga uunga fedha za hapa na pale ,hizo ni biashara za MOGULZ aka MATAIKUNI watu wenye pesa mingi mpaka wanatamani kujiteka ,watu wasio na pesa za MAWAZO.
 
Ulishajiuliza swali kwa nini zile hoteli zilizokuwa tishio miaka ile, ila kwa nyakati hizi zinaonekana zimechoka? Ni bora ujenge na kuuza, kutokufanya hivyo ni sawa na kuongelea dira ya 2056-20100 ambayo huna uhakika kama utakuwepo.​
 
Faida inakuja kwenye kupanda thamani ya nyumba na ardhi, hiyo 200m house in 10 years itakuwa 500m au zaidi
Ardhi inapanda thamani ila nyumba haipandi thamani, ukitaka nyumba ipande thamani tena, itakulazimu uwekeze tena hela za marekebisho mara kwa mara. Kama ilipigwa bati mjengo wa kizamani miaka 15 iliyopita, itakulazimu kutoa hilo paa la kizamani na kuweka la kisasa.
 
Ulishajiuliza swali kwa nini zile hoteli zilizokuwa tishio miaka ile, ila kwa nyakati hizi zinaonekana zimechoka? Ni bora ujenge na kuuza, kutokufanya hivyo ni sawa na kuongelea dira ya 2056-20100 ambayo huna uhakika kama utakuwepo.​

Tatizo management ,nilitembelea The Kilimanjaro Park Hyatt bado ipo vizuri ,Niliona Embassy Hotel imekufa ,Sheraton ,Royal Palm ,Kempinski ,Move N' Pick bado ipo vizuri ,The Pickcock Hotel bado inakimbiza.
 
Kuwekeza kwenye majengo ni sawa na fedha zako kuzifukia sehemu, na kuanza kuila kidogo kidogo mpaka iishe. Na kula huko unakuwa hauli faida zaidi ya kula mtaji (fedha ulioiwekeza). Wengi ukimbilia kujenga nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k huku wakijipa matumaini majengo hayo yatawalipa na kupata faida zaidi na zaidi. kwa ujumla majengo hayo uwapa hasara, vinginevyo mmiliki hatonufaika zaidi ya kizazi chake kijacho ambacho ndio kitakuwa kinakula faida baada ya miaka kadhaa kupita. Ukitaka kuamini hili, tembelea nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k zipe miaka mitano alafu ukazitembelee tena, utazikuta zimechoka na kama hakutokuwa na hela ya ziada ya ukarabati, ndio hivyo biashara inakuwa imekufa.​
Niko na wewe bega kwa bega. Ukweli ni kwamba Dar imebana. maeneo mapya ya pembezoni yanachukua muda mrefu kuwa makazi rasmi. Na huko ndo kwenye viwanja.
 
Tatizo management ,nilitembelea The Kilimanjaro Park Hyatt bado ipo vizuri ,Niliona Embassy Hotel imekufa ,Sheraton ,Royal Palm ,Kempinski ,Move N' Pick bado ipo vizuri ,The Pickcock Hotel bado inakimbiza.
Ukiona hivyo, ujue kuna fedha ya ziada ndio inatumika kwenye ukarabati ili kulinda brand na inawezekana labda kuna watu wenye hisa zao humo wenye malengo ya muda mrefu sana.
 
Kwa Tanzania uwekezaji wa majengo ni ovyo, isipokuwa kwa maeneo fulani tu. Mfano dar, majengo yanalipa kwa maeneo ya kuanzia mikocheni mpaka city centre na huko masaki etc. Kwingine naona ni neema ya Mungu. Unajengaje jengo kwa bei kubwa unapangisha millioni moja ambayo ni dola 390 Kwa mwezi. Wakati huo jengo kama hilo masaki milioni 5 au zaidi kwa mwezi. Sababu ya location. Huo ni upuuzi mkubwa mno.
 
Back
Top Bottom