Uwanja wa Ndege Songwe Kujengewa Chumba Maalum cha Baridi (Cold Room) Kuhifadhi Mazao

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Uongozi wa Uwanja wa Ndege Songwe umeagizwa kujenga chumba maalumu cha baridi (cold room) kwa ajili ya kuhifadhia mazao na vitu vingine vinavyoharibika ili kuwanufaisha wasafirishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao kwenda mikoa na nchi mbalimbali.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile alipotembelea katika uwanja huo ambapo alishangazwa na kutokuwepo kwa chumba hicho maalumu.

"Mfano maparachichi yakitoka shambani kule Njombe au Tukuyu yafike hapa ni siku ngapi? Kwamba yakafike yanakoenda si yatakuwa yameharibika, coldroom iko wapi meneja?” alihoji Kihenzile na kuagiza kuanza kwa mchakato kujenga chumba hicho
Meneja wa uwanja huo wa ndege, Pascal Kalumbete amesema wamepata ongezeko la abiria mwaka hadi mwaka na kutokana na kuboreshwa miundombinu ya uwanja huo ikiwemo kujenga taa za kuingia uwanjani na taa za kuongozea ndege nyakati za usiku ambapo sasa ndege yoyote inawezakutua wakati wowote usiku na mchana.

Kalumbete amesema jengo jipya la abiria baada ya ujenzi kutokamilika mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali sasa wamepanga ujenzi huo kukamilika Desemba 31, 2023 ikiwa sasa tayari umefikia asilimia 98.
 
Watu wanawaza artificial intelligence huko sisi bado tunapambana na Kujenga vyumba airport. Sad. Ilikua ziara ya Nani akaamua kusema hayo?
 
kwaiyo designer alikua wap wakat wana design huo uwanja??
Aliyebeba raman kwan alijenga kwa siri??

hii nchi haijajitayarisha kwa lolote kila kitu kinafanyika kama personal business
 
Uongozi wa Uwanja wa Ndege Songwe umeagizwa kujenga chumba maalumu cha baridi (cold room) kwa ajili ya kuhifadhia mazao na vitu vingine vinavyoharibika ili kuwanufaisha wasafirishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao kwenda mikoa na nchi mbalimbali.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile alipotembelea katika uwanja huo ambapo alishangazwa na kutokuwepo kwa chumba hicho maalumu.

"Mfano maparachichi yakitoka shambani kule Njombe au Tukuyu yafike hapa ni siku ngapi? Kwamba yakafike yanakoenda si yatakuwa yameharibika, coldroom iko wapi meneja?” alihoji Kihenzile na kuagiza kuanza kwa mchakato kujenga chumba hicho
Meneja wa uwanja huo wa ndege, Pascal Kalumbete amesema wamepata ongezeko la abiria mwaka hadi mwaka na kutokana na kuboreshwa miundombinu ya uwanja huo ikiwemo kujenga taa za kuingia uwanjani na taa za kuongozea ndege nyakati za usiku ambapo sasa ndege yoyote inawezakutua wakati wowote usiku na mchana.

Kalumbete amesema jengo jipya la abiria baada ya ujenzi kutokamilika mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali sasa wamepanga ujenzi huo kukamilika Desemba 31, 2023 ikiwa sasa tayari umefikia asilimia 98.
Inatakiwa hivi viwanja viwe na maghala wala sio chumba. Chumba kitahifadhi kiasi gani cha mazao lukuki yanayohitaji hifadhi?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Watu wanawaza artificial intelligence huko sisi bado tunapambana na Kujenga vyumba airport. Sad. Ilikua ziara ya Nani akaamua kusema hayo?
Tupe elimu, IA ingetatuaje hili la mazao?
 
Back
Top Bottom