Waliovamia uwanja wa ndege Moshi wapewa siku saba kuondoka

Jun 20, 2023
54
51
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameagiza kuondolewa mara moja kwa wananchi waliovamia na kujenga nyumba za kuishi ndani ya eneo la la uwanja mdogo wa Ndege uliopo Soweto Manispaa ya Moshi.

Agizo alilitoa Jana mjini Moshi baada ya kukagua upanuzi wa uwanja huo unaotarajiwa kigharimu zaidi ya Bilioni 12.

Alisema uvamizi huo unaweza ukakwamisha juhudi za serikali za kuupanua uwanja huo uliojengwa mwaka 1956.

"Nakuagiza meneja,wape notice wote ambao hawana hati na nalala umpelekee mkuu wa mkoa,wabomoe wenyewe nyumba zao, hatuwezi kwenda kwa staili hii ya kuogopana", alionya.

Alisema kupanuliwa kwa uwanja huo kutawezesha Ndege kubwa ATR zenye uwezo wa kibeba abiria 42 kutua kwenye uwanja huo ambao kwa sasa unapokea Ndege ndogo.

Waziri Mbarawa alisema kwa sasa Tanzania inapiga hatua kubwa kwenye usafiri wa Anga na kwamba kuna viwanja zaidi ya vinane vinavyojengwa na vingine vinafanyiwa ukarabati.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi.Kisare Makore alisema wananchi 21 wa kata hiyo ya Soweto wamefanya maendelezo ndani ya hifadhi ya uwanja huo wa Ndege.

Alisema kati ya hao watatu hawana hati na tayari Manispaa ya Moshi imeshawapatia notice ya siku saba ya kubomoa nyumba zao.

Notice hiyo iliyolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Novemba 6 mwaka huu kwa barua yenye kumbu namba MMC/R.40/19/66-87.

Ukarabati huo mkubwa ambao kwa sasa upo kwa aslimia 50 na unatekelezwa na Kampuni ya ujenzi ya Rocktronic ya mjini Moshi.
 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi.Kisare Makore alisema wananchi 21 wa kata hiyo ya Soweto wamefanya maendelezo ndani ya hifadhi ya uwanja huo wa Ndege.

Alisema kati ya hao watatu hawana hati na tayari Manispaa ya Moshi imeshawapatia notice ya siku saba ya kubomoa nyumba zao.


Kwenye hifadhi ya uwanja,weninge walipataje hizo hati? Kama hati walikuwa nazo,serikali ilitengaje hifadhi ya uwanja kwenye makazi ya watu!?
 
Back
Top Bottom