Naibu Waziri Kihenzile aagiza kujengwa Cold Room Airport ya Songwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ameuagiza Uongozi wa uwanja wa ndege Songwe kujenga chumba maalum (Cold room) kwa ajili ya kuhifadhia mazao na vitu vingine vinavyoharibika katika uwanja huo ili wanufaisha wasafirishaji bidhaa mbalimbali hususani mazao kwenda mikoa na nchi mbalimbali.

"Mfano Maparachichi yakitoka shambani kule Njombe au Tukuyu yaje yafike hapa ni siku ngapi kwamba yakafike yanakoenda si yatakuwa yameharibika! Coldroom iko wapi meneja!", Amehoji Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile na kuagiza kuanza kwa mchakato kujenga chumba hicho.

Meneja wa uwanja wa Ndege Songwe Pascal Kalumbete, amesema uwanja huo umekuwa ukifanikiwa kupata ongezeko la abiria mwaka hadi mwaka na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya uwanja huo ikiwemo kujenga taa za kuingia uwanjani na taa za kuongozea ndege nyakati za usiku ambapo sasa ndege yoyote inawezakutua wakati wowote usiku na mchana.

Kuhusu jengo jipya la abiria amesema baada ya ujenzi huo kutokamilika mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali sasa wamepanga ujenzi huo kukamilika kufikia Desemba 31, 2023 ikiwa sasa umefikia asilimia 98.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Benno Malisa, amesema kukamilika kwa jengo jipya la abiria kutasaidia kuboresha huduma kwa abiria wanaotoka na kwenda katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Malisa amesema pia ujenzi/upanuzi wa Barabara ya njia kutoka Mlimanyoka Uyole hadi uwanjani hapo kutasaidia kuboresha huduma za usafiri na uaafirishaji katika uwanja wa Ndege Songwe.

F9lMBcvWMAAzGVt.jpg
F9lMClmXUAA_3RF.jpg
F9lMBctWUAA55B_.jpg
F9lMBc6XUAAwOFf.jpg
 
Mbeya yenyewe ni Cold room.
Nilikuwa nikipika nyama, naiacha kwenye sufuria siku tatu, haichachi.
 
Wanunue Refrigerator Containers mbili au tatu pale MAERSK hazizidi milioni 50, lakini watajenga kachumba kadogo halafu watasema gharama zake ni Bilioni 20.

Lengo lao ni upigaji kwanza halafu huduma baadae🤮😤
 
Back
Top Bottom