Naona type za kina makonda nazo zinajitokeza zanzibar.Vijana wadogo hata huenda mapinduzi hawayajui wanataka raisi mstaafu afukuzwe uanachama tena mtoto wa mwanamapinduzi halisi.Huu ugonjwa unaoitwa makonda umewaingia vijana wengi mno.Kama tiba haitapatikana iko siku hawa vijana watasema raisi alieko madarakani afukuzwe uanachama.Ndio maana awali wenzao wa bara walijifungia kwenye kihoteli kimoja huko pwani wakaja na tamko la raisi ajaye hatatoka kaskazini na kweli hakutoka wakaona ushindi, wakaja na suala la katiba mpya nayo wakaona wameshinda pamoja na kupiga wazee na kuwadhalilisha, sasa wamekuja na ajenda ya raisi mstaafu mwenye heshima ukiacha ustafu wake katika ngazi ya urais ni mtoto wa muasisi wa mapinduzi afukuzwe uanachama na hili likifanikiwa siku wakitofautiana na raisi aliyeko madarakani watakuja na kauli ya afukuzwe uanachama na hapo ndio viongozi wetu watajua kuwa walikuwa wanapalilia upuuzi.Haya matamko viongozi wanayafurahia kwa sababu yanawahusu wapinzani wao ila mtu akishazoea kula nyama ya mtu haachi so wasubiri muda na wao watajikuta wanapitia maswahiba haya haya.Yaani vijana wahuni tu waliokusanywa kusanywa kama magunia ya mahindi wanatoa tamko raisi mstaafu afukuzwe uanachama halafu viongozi wa juu wanakaa kimya?Ama kweli ccm imefika mahali ambapo wapiga debe ndio wanachama na viongozi wenye busara sasa wameisha.