UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,075
114,596
Vijana wa CCM Zanzibar wametoa kauli ya pamoja kwamba Rais mstaafu Aman Karume afukuzwe CCM kwa kuwa anaungana na upinzani kukizamisha chama.

Vijana hao wanaoonekana kutumwa wamesema asipofukuzwa watatumia njia mbadala.

===================

UVCCM yataka Rais mstaafu afukuzwe CCM

UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umekitaka chama hicho kumvua uanachama Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume.

Kauli hiyo imetolewa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis wakati wa kilele cha matembezi ya vijana wa umoja huo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi.

Alimshushia tuhuma nzito mstaafu huyo kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu chama hicho kikongwe nchini, na kwamba asipofukuzwa umoja umoja huo utatumia njia zingine ambazo hakuziweka wazi.

Sadifa alionya kwamba Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar si mali wala miliki ya mtu kwani Wazanzibar wote wana haki ya kushiriki kuyaenzi kwa vitendo kutokana na historia yake.
 
Last edited by a moderator:
Vijana wa CCM Zanzibar wametoa kauli ya pamoja kwamba rais mstaafu Aman Karume afukuzwe CCM kwa kuwa anaungana na upinzani kukizamisha chama.Vijana hao wanaoonekana kutumwa wamesema asipofukuzwa watatumia njia mbadala.
weka chanzo kiongozi
 
QUOTE="Simiyu Yetu, post: 15074615, member: 150527"]Karume yupo cuf siku nyingi wala siyo leo maana hata yule mtoto wake ameolewa na kiongozi mmoja wa cuf hata mambo yake mengi hufanya kwaajili ya cuf.[/QUOTE]
Nafuu awakomboe wa Znz kutoka kwa mkoloni mweusi wa kupangwa TANGANYIKA
 
Shein amekata mirija ya maslahi ya Amani Karume, ndio maana muda mwingi Amani Karume anatumia kumuhujumu Shein. Kutokana na utawala na kashkash kipindi cha chaguzi za mwaka 2000 na 2005, hivi Amani Karume anapata wapi ujasiri wa kumkosoa Shein?
Na ashukuru sana kwakuwa Shein ni mpole, angekuwa Salmin ni Rais, Amani Karume angekuwa ananyea debe.
Amani Karume anampinga Shein kwakuwa maslahi yake binafsi yamezuiwa, na sio kwamba ana mapenzi mema na Zanzibar au wazanzibar.
 
Maslahi Yapi binafsi?Wapi amempinga Shein?Labda ungeyataja unless Kama hauyajui ni story za mtaani
 
Vijana wa CCM Zanzibar wametoa kauli ya pamoja kwamba Rais mstaafu Aman Karume afukuzwe CCM kwa kuwa anaungana na upinzani kukizamisha chama.

Vijana hao wanaoonekana kutumwa wamesema asipofukuzwa watatumia njia mbadala.
Jina la aliyewatuma tafadhari.
 
Shein amekata mirija ya maslahi ya Amani Karume, ndio maana muda mwingi Amani Karume anatumia kumuhujumu Shein. Kutokana na utawala na kashkash kipindi cha chaguzi za mwaka 2000 na 2005, hivi Amani Karume anapata wapi ujasiri wa kumkosoa Shein?
Na ashukuru sana kwakuwa Shein ni mpole, angekuwa Salmin ni Rais, Amani Karume angekuwa ananyea debe.
Amani Karume anampinga Shein kwakuwa maslahi yake binafsi yamezuiwa, na sio kwamba ana mapenzi mema na Zanzibar au wazanzibar.
Kwani Shein ni Mungu mpaka asikosolewe?
Usiwe muoga kama konokono aliyejificha kwenye gamba lake.
 
Back
Top Bottom