UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

Karume yupo cuf siku nyingi wala siyo leo maana hata yule mtoto wake ameolewa na kiongozi mmoja wa cuf hata mambo yake mengi hufanya kwaajili ya cuf.
Mimi nimemwoa faiza,tuseme na mimi nipo ccm?
 
Jina la aliyewatuma tafadhari.
hahaha... jina la nini tena mkuu? Vijana wa ccm wakati mwingine hujifanya punguani na kuwadhihaki baba zao...ni kawaida yao tu

inawezekana hawajatumwa..hawana hekima kabisa hawa young chichiyemu
 
Mimi nimemwoa faiza,tuseme na mimi nipo ccm?
Huyu jamaa ana chuki mpaka kwenye mambo ya kifamilia...suala la kuoana cuf na ccm, mbona ni jambo la kawaida tu. Na sidhani kama linaweza kusababisha mtu afanye mambo ya CUF akiwa chichiyemu...
 
Eti wanadai alienda kushiriki Maulidi nyumbani kwa Seif Sharif Hamad hivyo ni mshirika wake! Hawa UVCCM ni makenge kwelikweli!
 
Nimesikiliza mada zilizowasilishwa kwa vijana wa elimu ya juu Zanzibar. Kwakweli si zakutia m atumaini kwa wapenda amani. Kwa maoni yangu ni wakati wa kukemea kauli zote zinazilenga kuondoa umoja lkn muhimu wazanzibari wakumbuke maisha ya dunia ni starehe fupi yenye kupumbaza hivyo hatuna sababu ya kubaguana kutothaminiana wala kukejeliana muhimu tuishi kwa misingi ya upendo na furaha. Yupo mtoa mada alilaumu aliyewaingiza CCM ktk serikali ya umoja wa kitaifa sidhani kama ilikuwa sahihi sana
 
Chokochoko zote za karume, nia yake muungano uvunjike, wazanzbar ni wabaguz sana
Acha majungu kwani huo muungano unakusaidia nini hata ukivunjika.Kinachoendelea Zanzibar ni mtu mwenye akili ya nyumbu tu ndio anaweza kukipongeza au kushadadia.
 
Shein amekata mirija ya maslahi ya Amani Karume, ndio maana muda mwingi Amani Karume anatumia kumuhujumu Shein. Kutokana na utawala na kashkash kipindi cha chaguzi za mwaka 2000 na 2005, hivi Amani Karume anapata wapi ujasiri wa kumkosoa Shein?
Na ashukuru sana kwakuwa Shein ni mpole, angekuwa Salmin ni Rais, Amani Karume angekuwa ananyea debe.
Amani Karume anampinga Shein kwakuwa maslahi yake binafsi yamezuiwa, na sio kwamba ana mapenzi mema na Zanzibar au wazanzibar.
Hilo jina la jamaa unalotumia unalidhalilisha.Assange si mjinga kiasi hichi wewe ulifaa utumie jina la kihiyo.
 
Hiki Chama kinacho sema kina wana Chama hai zaidi ya milioni tano lakini kina hitaji watu wote hao wewe na mtazamo uno fanana.ccm ni kaburi la watu wote wenye mitazamo chanya
 
Kama kungekuwa na uwezekano kufuta hiki chama kinaitwa ccm na wezao CUF ingekuwa jambo la maana sana,hawa ndio watengeneza matatizo yote hapo kisiwani,
hawa ccm mtu akisema kweli anakuwa adui yao mkubwa ,mlimfukuza mzee moyo na mansoor mpaka sasa mmepata nini? sidhani kama nchi IBAKI SALAMA IKIWA KARUME atafukuzwa,na ukitazama hawa wapiga kelele ni wale hata ujumbe wa nyumba 10 hawajawahi kuwa ,hakuna cha zaidi zaidi ya nchi
 
Ingekuwa bora endapo hao vijana wa CCM Zanzibar wangeshinikiza Maalim Seif atangazwe ili baada ya hapo waendelee kukijenga chama chao, badala ya kuendelea kushutumu watu kama Karume pamoja na kutembea na mabango yanayowabagua Machotara.
CCM wamerukwa akili wanasahau mwenzao Mahmoud Thabit Kombo naye " .5" .
 
Kuna wakati unafika mpaka unashindwa kabisa kuelewa akili za watu wengine huwa zinawaza nini! Mfano ni hawa UVCCM!

Jana kwenye kikao chao na Ali Mohamed Shein ambaye kwa sasa anaiongoza Zanzibar kiimla walitoa mapendekezo eti rais mstaafu wa nchi hiyo Amani Abeid Karume afukuzwe CCM kwa kuwa alienda nyumbani kwa Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria sherehe za sikukuu ya Maulidi! Pia wanamtuhumu kuwa ndiye aliyechangia kuidhoofisha CCM visiwani humo baada ya kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa.

Ifike mahala watu waukubali ukweli kabla ya hatari kubwa kutokea! Leo Shein anaitawala Zanzibar kwa aibu kubwa huku akiendelea kushupaza shingo! Wananchi hawakutaki wewe na chama chako maana hata Magufuli alipigwa mwereka na Lowassa kwa kura za jumla visiwani humo basi ondoka! Shein usizidi kuchefua watu! Umeshachefua vya kutosha ondoka!! Waachie wanaokubalika watawale!
 
Wazanzibar niwabaguz mno, Tanganyika hakuna ubaguz wakipuuz kias kile, ukiskia wamekupa jina la "jibara" (jitu kutoka bara) yaan hata uwenamsaada kias gan kwao lazma wakubague. Hakuna haja yakuwalazmisha kma hawatak muungano uvunjwe kila mmoja ashike 50 zake
 
CCM Zanzibar ishakufa muda mrefu... kwani hamjui..? Sasa CCM wamezidiwa na CUF huko Zanzibar wanaanza kumnyooshea kidole Karume... sasa hapo ndio patamu FAMILIA YA KARUME IKIONDOKA CCM Zanzibar, CCM inakufa kifo cha kibaka... Unguja 70% itaondoka CCM, na hapo itaenda CUF... sasa Pemba 99% ni CUF... Huyu Sadifa ashakuwa Toilet paper... and in a short time, Karume Family will REACT... in a very SHOCKING WAY... hapo sasa CCM itakufa mkiona... Ni kweli Karume kimoyo na Kiroho yuko CUF... hilo halina ubishi... ila najua alikuwa anasubiria MTU ACHOMOE KIDOMO DOMO, ili atoke mzima mzima... nafahamu Karume family will never keep quite for this... Sadifa hana adabu wala heshima... sasa MZIKI UNANOGA...!! Wamegusa moyo wa CCM Zanzibar
 
Last edited:
Nyie UVCCM Zanzibar kwani CCM baba zenu ndio waliianzisha mpaka mumfukuze Rais mstaafu Aman Karume? Acheni upumbavu wenu kosa lake mini?
Ccm hawapendi ukweli na ni wanafiki hasa uyo adifa sijui kashatoka honeymoon anataka adi familia ya waasisi wa muungano wafukuzwe kama baba Yake ndio aliuleta muungano kama vijana walitakiwa wasimamie ukweli jecha atangaze matokeo
 
Shein amekata mirija ya maslahi ya Amani Karume, ndio maana muda mwingi Amani Karume anatumia kumuhujumu Shein. Kutokana na utawala na kashkash kipindi cha chaguzi za mwaka 2000 na 2005, hivi Amani Karume anapata wapi ujasiri wa kumkosoa Shein?
Na ashukuru sana kwakuwa Shein ni mpole, angekuwa Salmin ni Rais, Amani Karume angekuwa ananyea debe.
Amani Karume anampinga Shein kwakuwa maslahi yake binafsi yamezuiwa, na sio kwamba ana mapenzi mema na Zanzibar au wazanzibar.
Mapenzi mema na Zanzibar ni kuwadhurumu CUF ushindi?
 
Nasikia hata hotuba ya Maalim Sefu jana iliandikwa na wanasiasa wa nchi jirani ili kuharibu utamu wa sherehe za mapinduzi leo na ndio maana hotuba ikasomwa jana live ili kupinga mapinduzi yaliyomuondoa Sultani muarabu aliyeacha mbegu za machotara kibao wanaoyachukia mapinduzi na wengi wao machotara hao wametangaza kutoshiriki kwenye sherehe.
Niliitazama ile press conference, na iliongelea mambo ya msingi kwa mstakabali wa Zanzibar..kama ilipelekea kuharibika kwa utamu wa sherehe za mapinduzi, either ni coincidence tu, ama ni kwamba utamu wa sherehe hizo ulikuwa wa dhahania tu.
 
Back
Top Bottom