UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

UVCCM Zanzibar: Abeid Karume afukuzwe CCM

Halafu kwa ujasiri wa kinafiki wanataka kwenda kusuluhisha ya jirani huko Bururundi..........unafiki mkubwa sana huu.
 
Niliitazama ile press conference, na iliongelea mambo ya msingi kwa mstakabali wa Zanzibar..kama ilipelekea kuharibika kwa utamu wa sherehe za mapinduzi, either ni coincidence tu, ama ni kwamba utamu wa sherehe hizo ulikuwa wa dhahania tu.
Sio coincidence ni mpango
 
Halafu kwa ujasiri wa kinafiki wanataka kwenda kusuluhisha ya jirani huko Bururundi..........unafiki mkubwa sana huu.
We unakomaa na ishu ya burundi tu umetumwa!? kwani zanzibar na burundi zinatofautiana nn? Mbona hujaandamana kuhusu mpango wa kagame kuendelea milele rwanda?
 
Hivi huo muungano unaolindwa sana una faida gani kwa sisi watu wa Tanzania bara? Kuna nchi ambazo hata hatujaungana lakini zina faida kibiashara kuliko hata hiyo tukiyoungana nayo. Mapato tunayoingiza kupitia nchi ambazo hatujaungana nazo ni makubwa sana kuliko hayo ya Zanzibar. Serikali itaendelea kutumia nguvu hadi lini kule Zanzibar. Suluhisho la mgogoro ni kuwaachia Wazanzibar wenyewe waamue kama walivyoamua kwenye sanduku la kura. Wazanzibar waheshimiwe maamuzi yao kwenye kura kuliko kikundi cha watu wachache kuwaamulia Wazanzibar. La sivyo kila uchaguzi lazima mgogoro uibuke
Kuna suala la udugu, hao wanaoitwa wazanzibari wengi wao babu na bibi zao wana asili ya pwani ya Tanzania, kuanzia Tanga mpaka Mtwara. Mpemba akiyatamka yale maneno yanayoanzia na M ataweka N, mfano Mtoto atasema Ntoto, Mtu atasema Ntu, sawasawa na wenyeji wa mkoa wa Mtwara jinsi wanavyoongea. Kuna wanyamwezi wengi visiwani Zanzibar, kuna wagogo na makabila mengi ya huku Bara. Mwasisi wa Mapinduzi marehemu Karume ni mtu mwenye asili ya huku bara. Damu ni nzito kuliko maji, hizo nchi unazosema tujiunge nazo, hatuna uhusiano nao wa damu, ni rahisi kukorofishana nao na uhusiano ukafa moja kwa moja, kuiliko ambavyo mtu wa bara anavyoweza kugombana na mzanzibari halafu akaja kupata naye kwani damu zao zina uhusiano.
 
Karume yupo cuf siku nyingi wala siyo leo maana hata yule mtoto wake ameolewa na kiongozi mmoja wa cuf hata mambo yake mengi hufanya kwaajili ya cuf.


karume anataka kuwakomboa ndugu zake kutoka kwa mkoloni tanganyika
 
Ya kwetu wapi?
Ya umeya Dar? huyaoni kazi kunyosha kidole tu.
Tafuta kazi za kufanya acha wanyarwanda wajiamurie mambo yao wenyewe, CCM kinalazimisha kutawala hauoni kwa sababu unapewa pesa na ccm. Kibaraka wa ccm hawezi kuwa na mawazo mbadala.
 
Wazoea vya kuiba kura lakini mwishowe upo, watulie dawa ziwaingie
 
ukianza kumbagua jirani mwisho uta mtenga nduguyo. Na mwalimu alitahadharisha hii dhambi ya ubaguzi...wengi hawaku mwelewa mwalimu alidhani anawambia cuf....kumbe alikua akiwambia ccm znz kuwa mkiwabagua cuf kuwa ni wapemba basi hamtatosheka mtasema huyu ni mmakunduchi na huyu ni mtumbatu ccm ni ya wafrika!!!
Leo imedhihiri dhambi ya ubaguzi ccm znz imeenea mwili mzima...mara huyu hizbu mara huyu chotara....
Ccm kinakufa znz ...kinamegeka kitaisha kwa sumu ya ubaguzi.....
Watanganyika wana kazi kweli ya kuwalinda wabaguzi wa ccm znz....sijui mtatoa ulinzi huo mpaka lini maana makaburu mnao walinda wanazidi kukimbiwa.....
 
Shein amekata mirija ya maslahi ya Amani Karume, ndio maana muda mwingi Amani Karume anatumia kumuhujumu Shein. Kutokana na utawala na kashkash kipindi cha chaguzi za mwaka 2000 na 2005, hivi Amani Karume anapata wapi ujasiri wa kumkosoa Shein?
Na ashukuru sana kwakuwa Shein ni mpole, angekuwa Salmin ni Rais, Amani Karume angekuwa ananyea debe.
Amani Karume anampinga Shein kwakuwa maslahi yake binafsi yamezuiwa, na sio kwamba ana mapenzi mema na Zanzibar au wazanzibar.
Maslahi yapi hayo?
Hebu funguka mkuu...
 
Asiyekosolewa ni mngu pekee, kama anazengua arudishe kadi kwan nn, kahama lowasa itakuwa yee
 
Hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa rais Zbar maana haina maana kama watu wanachagua halafu wanakataa matokeo.
 
Vijana wa CCM Zanzibar wametoa kauli ya pamoja kwamba Rais mstaafu Aman Karume afukuzwe CCM kwa kuwa anaungana na upinzani kukizamisha chama.

Vijana hao wanaoonekana kutumwa wamesema asipofukuzwa watatumia njia mbadala.

===================
Njaa inawasumbua sana hao
 
Back
Top Bottom