SoC02 Utitiri na uholela wa ufungaji wa ‘cctv’ katika maeneo mbalimbali unavyohatarisha haki ya faragha ya taarifa za watu

Stories of Change - 2022 Competition

madinga

New Member
Aug 30, 2022
1
2
Suala la ulinzi binafsi ni jambo muhimu sana linalopaswa kupewa kipaumbele cha juu kwenye mtiririko wa Mahitaji ya binadamu katika kipindi hiki ili kujilinda na/au kuepukana na vitendo mbalimbali vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika jamii zetu kama vile ujambazi, uvamizi, ukatili na hata vitendo vya ugaidi.

Katika kujihakikishia ulinzi na usalama binafsi, wa familia na mali raia wamekuwa wakitumia njia mbalimbali wakijilinda, njia hizo ni kama vile kuweka walinzi, kumiliki silaha kama bastola, kufuga mbwa, kujenga uzio wa umeme nk.

Kutokana na kukua kwa Sayansi na teknolojia, kwasasa kumekuwepo kwa njia maarufu sana ya kufuatilia matukio mbalimbali yanayotokea katika eneo husika kwa kufunga mfumo wa kamera za ulinzi ujulikanao kama ‘CCTV Surveillance system’, Mfumo huu unajumuisha kamera ambazo zinafuatilia matukio yote kulingana na sehemu ilipoelekezwa na kifaa maalum kinachorekodi matukio hayo (NVR/DVR).

Utaratibu huu wa kutumia ‘CCTV’ umekuwa ukirahisisha kazi ya ulinzi na ufuatiliaji wa matukio katika maeneo, mlinzi mmoja anapokaa kwenye ‘screen’ anaona pande zote zilizofungwa kamera na kama kuna hali yoyote hatarishi anaweza akaiwahi na kuidhibiti. Kwakua Mfumo huu pia unarekodi matukio yote, umekuwa ukisaidia sana kupatikana kwa ushahidi wa matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea katika maeneo yaliyofungwa kamera na kuwafahamu wahusika.

Mfumo wa ‘CCTV’ kwasasa umekuwa ukitumika maeneo mengi sana kama vile ofisi mbalimbali za serikali na binafsi, shule na vyuo, maduka mbalimabli, ‘Shopping Malls’ na ‘supermarket’.

Aidha, kwasasa kumekuwepo kwa ongezeko kubwa sana la matumizi ya ‘CCTV’ katika maeneo mbalimbali ya starehe na migahawa kama vile ‘Night Clubs’, ‘Bars’ ambapo kamera zinafungwa katika kila kona.

Ni ukweli usiopingika kuwa Mfumo wa ‘CCTV’ unaimarisha sana ulinzi wa eneo husika hivyo kufanya mali na watu waliopo katika eneo lenye mfumo wa ‘CCTV’ kuwa salama zaidi kuliko walioko sehemu ambayo hakuna, hali hii inatokana na hofu wanayokuwa nayo wahalifu kufanya matukio katika maeneo wanayoona kamera au kuhisi uwepo wa kamera.

Kutokana na urahisi wa upatikanaji wa Vifaa na uwepo wa ujuzi wa namana ya kufunga, CCTV zimekuwa zikifungwa holela kiasi cha kuingilia uhuru wa faragha wa watu wengine lakini kibaya zaidi ni wamiliki wengi kutokuwa na Sera ya faragha ya CCTV inayolinda matumizi matumizi mahususi ya video zinazorekodiwa, kwa lugha nyepesi wamiliki wengi ambao wamefunga CCTV katika maeneo yao hawana nyaraka yoyote inayoeleza video wanazo rekodi zinatumika katika mazingara gani, zinakaa kwa muda gani kabla ya kufutwa lakini pia haki za

Kamera hizi hazichagui nini cha kuchukua nini cha kuacha, hivyo wamiliki hawa wamekuwa ‘matajiri’ wa taarifa nyingi muhimu za watu kuliko hata suala la ulinzi walilolenga, Mfano taarifa ya Mtu A kuonekana na Mtu/Watu B katika eneo C zimekuwa zikivuja sana lakini source kubwa ikiwa ni uwepo wa CCTV na wahusika kutokuwekewa misingi ya udhibiti wa taarifa wanazozikusanya.

Kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo kwa video nyingi halisi zinazodhalilisha utu wa mtu katika mitandao ya kijamii, mfano wa video hizo ni zile zinazoonesha watu kulewa sana kupita kiasi na kuanza kutapika hovyo, watu kujisaidia katika maeneo ambayo sio sahihi ambapo kamera inafika na kuwarekodi hadi, watu kulewa na kujichafua, Vitendo mbalimbali vinavyofanywa na watu wanaokaa kwenye maeneo mbalimbali na matukio mengine mengi ya video za kufedhehesha kama kushindwa kupanda lifti za majengo, kujigonga kwenye vioo vinavyoangaza nk.

Wamiliki wengi mbali na kutokuwa na Sera na utaratibu unaolinda haki za faragha za watu wanaofika katika maeneo yao lakini wamekuwa wakiweka hadi kamera mficho ‘hidden camera’ ambazo zinahifadhiwa kwenye saa au taa na wamekuwa hawaweki matangazo yoyote kueleza watu wao kuwa maeneo hayo yamefungwa kamera na kila tukio linarekodiwa na kueleza bayana matumizi mahususi ya video hizo.

Mbali na kuvunja na kuhatarisha haki ya faragha za watu lakini pia kwa kusosa udhibiti wa matumizi ya taarifa zinazokusanywa, ufungaji huu horera usio namiongozo wa CCTV umehatarisha hata maisha ya watu wanaoshindwa kuvumilia baada ya video zinazotovuja bila ridhaa yao kuvuja lakini pia uhorera huu wa ufungaji wa CCTV umepelekea kuingia kwa aina mpya ya wizi au utapeli, kwani wamiliki wamekuwa wakichukua hizo video ambazo sio nzuri na kuwatumia wahusika wakitaka pesa ili wasivujishe lakini zile ambazo zinahusiana na mahusiano kama Mume au mke wa mtu kuingia ‘Guest/Hotel’ na ‘mchepuko wake’ wamiliki wamekuwa wakichukua video hizo na kuwatumia wenza wa wale wateja ili kujitafutia kipato suala ambalo wakati mwingine imepelekea chuki kubwa na visasi visivyoelezeka miongoni wa wenza.

Nini kifanyike ili kuhakikisha Ufungaji wa ‘CCTV’ unabaki katika lengo moja tu la kujilinda na sio vinginevyo:
  • Nashauri Mamlaka husika kuwekwe utaratibu mahusus wa kutambua ni maeneo gani yanapaswa kuwa na CCTV sio kama ilivyosasa.
  • Wahusika wote wanaofunga CCTV wawe na sera za faragha za kulinda taarifa wanazokusanya (privacy policy)
  • Kuwekwe ulazima wa kila eneo lenye kamera kutambulisha uwepo wa kamera hizo.
  • Adhabu kali kutolewa kwa wote wanaofujisha ‘footage’ zilizorekodiwa na kamera zao kwa lengo la kudhalilisha utu wa watu wengine, kujipatia umaarufu au kutumia kwa utapeli.

  • HITIMISHO
  • Kamera za ulinzi ni nzuri na ni njia bora nay a kisasa ya kuimarisha ulinzi binafsi lakini lazima kuwe na utaratibu mzuri wa kuzifunga na kudhibiti matumizi ya hovyo ya video zinazorekodiwa.
 
Mkuu wazo lako ni zuri, lakini mimi nengeshauri ufungaji wa CCTV camera uendelee kama kawaida kwa yoyote atakaye hitaji, isipokuwa tu; wamiliki wakuu wa mitandao yote ya kijamii kama vile Twitter, Facebook, Instagram, telegram, Tiktok, LinkedIn, Snapchat, nakadharika ikiwa ni pamoja na YouTube, ni lazima wabuni teknolojia mpya katika sehemu ya machapisho ya video na picha.

Kwamba; hizo sehemu mbili zitekengenezewe teknolojia ambayo ni ya ndani kwa ndani ( yaani software) ambayo itakuwa na uwezo wa kuichuja picha ama video iwapo kama imetoka katika chanzo cha CCTV camera. Kabla mtu haja chapisha video au picha yake, itambidi abonyeze kitufe kinacho ichuja kwanza picha au video kabla haijaenda kwa umma.

Kama picha ama video itakuwa imetokana na CCTV camera, basi mtandao usiruhusu picha au video hiyo kwenda kwa umma.

Na kama picha au video itakuwa imetokana na chanzo kingine kama vile simu au camera halisi, basi mtandao uiruhusu hiyo picha au hiyo video kuchapishwa kwa umma.
 
Back
Top Bottom