Makamura
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 356
- 550
Siku hizi kumekuwa na Kampuni nyingi za Mikopo Online kama PesaX, Twiga Loan, Mloan, Cash X.
Na watu bila kuwa makini mtakuja jikuta mnaingia matatizoni kutoka na taarifa zinazokusanywa na Kampuni hizi.
Nimejaribu kadhaa na hakuna ya afadhali, unakuta inakusanya taarifa hizi:-
Watanzania tuweni makini na maamuzi yetu, hizi ndo huchangia watu kudhalilika mitandaoni, na kutoa siri za watu kama history za bank, miamala, chati za siri na faragha za watu, je unahisi utakuwa salama wewe na uwapendao?.
Mamlaka ishughulikie hawa watu wanapata wapi dhamana ya kukusanya taarifa za watu kama Sensa ya Kidigitali?
Mdau weka screen ya App ya Mikopo tuone taarifa wanazokusanya kwenye Simu yako
Na watu bila kuwa makini mtakuja jikuta mnaingia matatizoni kutoka na taarifa zinazokusanywa na Kampuni hizi.
Nimejaribu kadhaa na hakuna ya afadhali, unakuta inakusanya taarifa hizi:-
- SMS - yan wanaweza kusoma sms zote zilizoingia katika namba yako uliyosajilia, hii ikujumuisha sms za miamala, mapenz, siri za familia na kadharika je unahisi upo salama?
- CONTACTS - wanaweza kuona majina na namba zote ulizosave kwenye simu yako unahisi watu wako watakuwa salama?
- CAMERA - hii wanaweza kurekodi au kupiga picha bila wewe kujua na hapa ndo linapokuja swala zima la connections kuvuja
- STORAGE - wanaweza ku-access picha, video, na files zote zilizoseviwa kwenye simu yako, je unahisi wataacha kushare na wwngine siri zako?
- APPS - wanaweza kuona app zote kwenye simu na kuzifikia, hii ikijumlisha WhatsApp, IG, app za kutunz afaragha zako n.k
- TAARIFA BINAFSI - kama Vyeti, elimu, kazi, mahala pa kuishi, urefu, picha zako, unadhan utakuwa salama mtu kuwa na taarifa zako zote..