HesabuKali
JF-Expert Member
- Jan 4, 2016
- 2,880
- 5,879
Inafahamika wazi kabisa watu wengi hawaitaki hata kuisikia Serikali iliyopatikana baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 na kumsimika Rais Samia hali iliyopelekea maandamano yaliyosababisha maumivu makubwa.
Kama Rais Samia anataka utulivu hata wa asilimia 10 tu basi wafuatao asijaribu hata kwa bahati mbaya kuwafanya Mawaziri katika nchi hii.
1. Mwigulu
2. Bashe
3. Makonda
4. Kitila
5. Jenister
6. Ridhiwani
7. Ulega.
8. Mchengerwa
9. Lukuvi
10. Kabudi.
11. Makame
Kwenye uteuzi wako wa Mwanasheria karata imeharibika, ikikupendeza tuondolee huyu raia.
Kwenye RC, tuondolee huyu Monitor wa Dar, huyu ni zaidi ya mpuuzi na amekufanya hivyo unavyoonekana kwa kiasi kikubwa, Makala ondoa Arusha, wengine tutakukumbusha baadae.
Hawa na wengine watampunguzia hasara, wameomba kuwa wabunge basi wabaki hivyo mpaka 2030, na kama Rais unasikia basi hawa ndio chanzo cha machafuko nchini na sio Chadema.
Halafu huyu Abdullah Mwinyi umemteua mbunge ili akusaidie kitu gani ambacho katika wabunge wote wa chama chako hawana? Na huyu Bonah Kamoli mmempa viti maalumu kwa umaalumu gani alionao baada ya kushindwa kwenye kura?
Kama uteuzi wako umezingatia maslahi mapana ya nchi na sio yako binafsi, Ummy Mwalimu alikukosea nini utuambie, Kwamba Bulaya na wahuni wengine waliotoka Chadema walikuwa na maana sana hata baada ya kushindwa vibaya kwenye kura za maoni za chama chako ukaona wanafaa ila Ummy aliyeshinda hafai?
Nafikiri itaeleweka kila kiongozi utakayeteua sio mali yako, anaenda kuwatumikia Watanzania ambao ndio wamiliki wa nchi yao, hao hapo juu na wengine ukiona wanakupendeza wape kazi binafsi za nyumbani kwako.