UTEUZI: Rais Samia ateua Majaji wa Mahakama Kuu

Tatizo sisi wananchi hawataki kusikiliza kilio chetu, Bado Mahakama zetu za juu zinaendelea kuandika haki zetu kwa lugha ya kizungu japo sheria ilibadilishwa!!!

Sasa tunaiuliza mahakama, kuendelea kutumia lugha ya kiingereza ni kuwadharau wananchi au ni kulidharau Bunge ambalo lilitunga Sheria baada ya kilio cha wananchi?!!

Mahakama inafanya hivyo kwa masilahi ya nani haswa?!

utafiti unaonyesha hadi sasa bado hukumu za kesi pamoja na mwenendo wa kesi zote zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza ambayo ni changamoto kwa watanzania wanao kwenda kutafuta haki zao mahakamani. kinacho fanyika sasa unapewa nakala ya kizungu na tafasiri fupi sana ya kiswahili!!! wananchi wanataabika kanakwamba hawapo nchini kwao?!!

Je? Mahakama inaendelea kutumia lugha ya kiingereza kwa masilahi ya nani haswa?

Hivi karibuni tumeona maamuzi ya matumizi ya lugha katika taasisi za Kimataifa kama vile; SADC, AU n.k, kwa nini Mahaka za watanzania zinasuasua?!

Kwa nini mahakama hazitaki kutumia lugha ya kiswahili? haswa mahakama za Juuu?!

Tunaiomba wizara ya Katiba na Sheria ilisimamie hili jambo kwa masilahi ya wananchi na kama sheria ilivyo kusudia, Kiswahili kitumike kikamilifu, hatutaki kutafasariwa kutoka kwenye kizungu kuja kiswahili.....kiandikwe kiswahili maana sisi sote ni waswahili, Majaji ni waswahili na Mahakimu ni waswahili sasa kwa nini hukumu iandikwe kwa kiingereza?!
Hizi mambo zenu za uswahili achaneni nazo!
 
Mayala hajawahi kupractice uwakili, hapo wenye sifa ni kariba ya Kibatala na awe amefanya kazi yake ya uwakili kwa miaka 15 ndio anakuwa kwenye sifa yakuteuliwa kuwa Jaji na bado kuna mambo mengi yanazingatiwa pia.
Ingawa huko Serikalini kwa Sasa weledi unakuja nyuma
 
Elimu ya uraia inahitajika sana hata kwa GT wetu humu. Mzanzibari kwanza ni Mtanzania ana haki zote za Mtanzania kama Mtanzania mwingine yoyote ikiwemo haki ya ajira ndani ya serikali ya JMT.

Uzanzibari wake ni an added advantage kwa Zanzibar ambayo Watanzania Bara don't enjoy!.
P
Umeshawahi kusikia mBara kateuliwa znz? au ndio Upendo wa Mshumaaa
 
Funguwa macho yako vizuri, uteuzi umefanyika tarehe mwezi wa 8, tangazo la uteuzi limetoka leo tarehe mwezi wa 8, hiyo tarehe 23 iliyopo chini inasisitiza kampeni ya sensa inafanyika tarehe 23 mwezi wa 8.

Punguza K- Vant.
Nakunywa hard drinks, siyo hayo mataputapu ya kitanzania. Rubbish!
 
..Nimeona kuna Mzanzibari ameteuliwa.

..Hii ni mahakama kuu ya Tanganyika, ndugu zetu wa Zanzibar wanayo.mahakama kuu yao.

..Mzanzibari anaweza kuteuliwa ktk mahakama ya Rufaa kwani hiyo ni ya muungano.
Hizi ni nafasi za Watanganyika, mahakama kuu si suala la muungano.

Halafu utawasikia Wazanzibar na hasa VP wao OMO wakilalamika eti mambo ya muungano yameongezwa, lakini hili hutawasikia kwasababu kuna manufaa.

Na wala si hilo tu, bodi nyingi za Taasisi za Tanganyika wamejezwa Wazanzibar hasa kipindi hiki
Mambo yasiyo ya muungano Wazanzibar wakae pemebeni, hawataki yaongezwe na hivyo hawapaswi kuyatumikia.
 
Wadau wajadili kwa kina Kivuli cha rais ktk uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu


Source: Forbs Media



107A. Mamlaka ya Utoaji Haki.

107B. Uhuru wa Mahakama.

SEHEMU YA PILI
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO


108. Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.

109. Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao.

110. Muda wa Majaji wa Mahakama Kuu kushika madaraka.

111. Kiapo cha Majaji
 
bagamoyo

Hoja ya Wakili Tundu Lissu ni kuwa kwa mujibu wa katiba sifa za ujaji hazikuanisha uraia
Hoja ya pili ni kwamba ' mzingo wa kazi' wa Mahakama kuu (scope) hauihusu Zanzibar na kwamba swala la mahakama kuu si la muungano.

Suala hili linatueleza jambo kuhusu muungano, kwamba, Mzanzibar ana Utanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar. kuna tatizo hapa! hakuna Mtanganyika atateuliwa Mahakama kuu Zanzibar au katika SMZ

Ni kwa msingi wa uteuzi wa Jaji huu tunakuwa na mwendelezo wa Wabunge wa Zanzibar kuwa wajumbe wa kamati za Bunge za kushughulikia sekta zisizo za muungano. Mfano, Wizara kama Tamisemi, Ardhi n.k.

Juzi kumeteuliewa kamati ya watu watatu kutazama utoaji wa mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Kamati hiyo ina Mzanzibar. HESLB si suala la muungano , Mzanzibar anaingiaje katika kamati hii?
Zanzibar wana ZHESL ambayo Mtanganyika hahusiki na wala hatapewa fursa.

Wakati Wazanzibar wakiongozwa na OMO kulalamika kuhusu mambo ya muungano kuongezwa, huwezi kuwasikia wakilalamika kuteuliwa katika taasisi zisizo za muungano.

Wakati wa Zanzibar wakilalamika Tanganyika kuvaa koti la muungano, ni hao hao wanafaidika na fursa ndani ya muungano ambazo HAWAPASWI kupewa kwa namna yoyote.

Katiba mpya ni muhimu ! ni muhimu na kama haiwezekani pasua jahazi tugawane mbao, hakuna cha kupoteza
 
Umeshawahi kusikia mBara kateuliwa znz? au ndio Upendo wa Mshumaaa
Kwenye miungano yote, kuna kitu kinaitwa the majority na minority, kwenye muungano wetu, bara ndio the majority Zanzibar ni the minority, tena siku hizi mna bahati, zamani sisi wenzenu kuingia Zanzibar ilikuwa ni unaingia kwa passport!. Mzanzibari ana haki zote za Mtanzania huku bara kama Mtanzania mwingine yeyote, ikiwemo ajira ndani ya serikali ya JMT, na kumiliki ardhi, lakini m-bara hatuna haki ajira SMZ wala kumiliki ardhi Zanzibar!, ingekuwa tuko huru, saa hizi Visiwa vile vingekuwa vimezama!.

P
 
Kwenye miungano yote, kuna kitu kinaitwa the majority na minority, kwenye muungano wetu, bara ndio the majority Zanzibar ni the minority, tena siku hizi mna bahati, zamani sisi wenzenu kuingia Zanzibar ilikuwa ni unaingia kwa passport!. Mzanzibari ana haki zote za Mtanzania huku bara kama Mtanzania mwingine yeyote, ikiwemo ajira ndani ya serikali ya JMT, na kumiliki ardhi, lakini m-bara hatuna haki ajira SMZ wala kumiliki ardhi Zanzibar!, ingekuwa tuko huru, saa hizi Visiwa vile vingekuwa vimezama!.

P
Mkuu

Hoja hapa ni unafiki (hypocrisy) inayochochowe na akina OMO. Ni unafiki kwa sababu hizi

Wanalalamika mambo ya muungano kuongezwa, lakini wanataka 21% ya mambo yasiyo ya muungano
21% ya ajira za muungano ni ajira za Tanganyika nyingi kuliko za SMZ, hawasemi hili , unafiki

Mifano
Wazanzibar wanasema Mahakama kuu si suala la muungano na waliondoa kupitia marekebisho ya katiba 2010
Wazanzibar wakiteuliwa mahakama kuu Tanzania hutawasikia akina OMO wakisema hawataki tena si hivyo bali analalamika kutoteuliwa kwenye mambo wanayosema yameongezwa. Unafiki

HESLB waliondoa na kutengeneza ZHESLB. Jambo la kushangaza HESLB inadhamini Wazanzibar wengi kuliko ZHESL tena hawarudishi mikopo. Huwasikii akina OMO wakiwakataza Wazanazibar wasihcukue HESLB, unafiki

Wameondoa Bandari katika muungano, lakini wanateuliwa na kuajririwa mamlaka ya Bandari. Unafiki

Hawataki mambo yaliyoongezwa katika muungano lakini wanataka ajira 21% kutoka Tamisemi na taasisi zisizo za muungano. Huu kama si unafiki sijui ni kitu gani.

Wakaondoa mafuta na gesi katika mambo ya muungano lakini leo wanapata 4% ya pato la Tanganyika kupitia mafuta, gesi, madini, kilimo, ufugaji na uvuvi. Huwezi kuwasikia wakisema hawapokei! unafiki

Huwezi kulaani mambo kuongezwa halafu unataka unufaike na mambo hayo hayo unayosema ni haramu

''HUWEZI KUSEMA NGURUWE NI HARAMU LAKINI MCHUZI WAKE NI HALALI''
 
kwa nini uteuzi huu wa Majaji 22 umebezwa sana?!
Tatizo ni nini?
hawana sifa? au mamlaka za uteuzi zimekosea kuteua watu wasio faa?!
nini kifanyike? je? kama ikibainika vinginevyo je? kwa wakati huu Rais anaweza kutengua uteuzi wa Majaji hao kama alivyo fanya kwa RC?
naomba ufafanuzi.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa maafisa ishirini na wawili (22) kuwa Majaji wa Mahakama Kuu
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa maafisa ishirini na wawili (22) kuwa Majaji wa Mahakama Kuu

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa maafisa ishirini na wawili (22) kuwa Majaji wa Mahakama Kuu

View attachment 2315715View attachment 2315716View attachment 2315717
Kwa
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa maafisa ishirini na wawili (22) kuwa Majaji wa Mahakama Kuu

View attachment 2315715View attachment 2315716View attachment 2315717
Ukiangalia list ya wateule wote 22 utagundua kwamba zaidi ya asilimia 80 ya wateule wote kwa nafasi za ujaji wametokea mahakama na baadhi kwenye ofisi za wanasheria wa serikali.

Lakini mahakama kuu inasikiliza mashauri yenye wigo mpana zaidi mfano land tribunal, commercial, labour, tax nk.

Ningetarajia ili kukuza specialization uteuzi ungefanyika pia kupitia tribunals ambazo rufaa huenda mahakama kuu mfano CMA for labour cases, land tribunals for land matters FCC for commercial matters, tax nk. Wafanya maamuzi kwenye vyombo hivyo ambao ndio wanaozijua kiueledi sheria husika ndio wangepaswa kuwa promoted kwenye nafasi za ujaji ili kujenga jurisprudence (specialization).

Kutokufanya hivyo ni kuendelea kutengeneza mazingira ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa kutokufanya kazi kiueledi hadi kufikia kutoa maamuzi kinzani (kama ilivyo kwa maamuzi mengi ya kesi za kazi yanavyoamuliwa kinyume na msingi uliowekwa na sheria husika)

Mfano jaji mteule mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi kwenye uanasheria serikalini aende kuamua rufaa za mashauri ya kazi inayotokea CMA ambako ni purely labour laws tena kwa sasa hivi isiyohusisha serikali hawezi kuwa sawa na ambaye angetoka CMA.

Aidha maamuzi hayo yanademoralize utendaji kazi wa hizi tribunals na kuondoa misingi ambayo sheria ilimaanisha na kutengeneza ustawi katika secta husika

Ni rai yangu kwamba kabla ya uteuzi wa majaji, kigezo kinachohusu, specialization, uzoefu kwenye specialization, uweledi kwenye specialization vingezingatiwa ili kupromote high court yenye wabobezi na kuondoa mazoea ya kila jaji anaweza kufanya kesi yoyote.

Pia nashauri hizi tribunals zitazamwe kwa jicho la kipekee, si tu katika uteuzi wa majaji bali pia kwenye mabadiliko na marekebisho ya sheria husika.

Naomba kuwasilisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom