UTEUZI: Rais Samia ateua Majaji wa Mahakama Kuu

Fine, but aliye mahakamani kwa mtindo huu atakata tamaa maana nafasi za usajiri wa mahakama ni chache. Anyway ni mtindo wa Jiwe, sidhani kama Jaji Mkuu kabadilika..bure kabisa
Msajili wa mahakama yupo mahakamani mkuu. Ni muundo wa utumishi katika mahakama.
 
Ukajua umo, uliipoteza taji yako kizembe sana enzi ya kuhani mkuu KAYAFA, sasa unaishi kama popo usiyejua uwe mnyama au ndege pole sana. Majira hayafwati watu bali watu hufuata majira.

Imagine ungelinda ile taswira yako leo ungekuaje?

Uliitupa taji yako kwenye shingo ya nguruwe pole sana.

Nimekumbuka kitabu cha 'the wreath for father mayor'
Kweli unaamini sasa ni bora zaidi?
 
Tatizo Katiba
Fine, but aliye mahakamani kwa mtindo huu atakata tamaa maana nafasi za usajiri wa mahakama ni chache. Anyway ni mtindo wa Jiwe, sidhani kama Jaji Mkuu kabadilika..bure kabisa
Tatizo Katiba haiendani na taratibu zao za kitaaluma ktk kupata hao wakioteuliwa.
 
Tatizo sisi wananchi hawataki kusikiliza kilio chetu, Bado Mahakama zetu za juu zinaendelea kuandika haki zetu kwa lugha ya kizungu japo sheria ilibadilishwa!!!

Sasa tunaiuliza mahakama, kuendelea kutumia lugha ya kiingereza ni kuwadharau wananchi au ni kulidharau Bunge ambalo lilitunga Sheria baada ya kilio cha wananchi?!!

Mahakama inafanya hivyo kwa masilahi ya nani haswa?!

utafiti unaonyesha hadi sasa bado hukumu za kesi pamoja na mwenendo wa kesi zote zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza ambayo ni changamoto kwa watanzania wanao kwenda kutafuta haki zao mahakamani. kinacho fanyika sasa unapewa nakala ya kizungu na tafasiri fupi sana ya kiswahili!!! wananchi wanataabika kanakwamba hawapo nchini kwao?!!

Je? Mahakama inaendelea kutumia lugha ya kiingereza kwa masilahi ya nani haswa?

Hivi karibuni tumeona maamuzi ya matumizi ya lugha katika taasisi za Kimataifa kama vile; SADC, AU n.k, kwa nini Mahaka za watanzania zinasuasua?!

Kwa nini mahakama hazitaki kutumia lugha ya kiswahili? haswa mahakama za Juuu?!

Tunaiomba wizara ya Katiba na Sheria, Waziri Ndumbaro hakikisha jambo hili linatekelezeka kama lilivyo kusudiwa kwa masilahi ya wananchi na kama sheria ilivyo kusudia, Kiswahili kitumike kikamilifu, hatutaki kutafasariwa kutoka kwenye kizungu kuja kiswahili.....kiandikwe kiswahili maana sisi sote ni waswahili, Majaji ni waswahili na Mahakimu ni waswahili sasa kwa nini hukumu iandikwe kwa kiingereza?!
 
OK, najua but does not practice law ni utawala, I guess, I stand to be corrected
Mkuu wametokea huko kwenye law practice, hata usajili wa mahakama si utawala peke yake na hata huko wanakokwenda ni ku practice law pia.

Ni kama leo useme kwanini mhariri kateuliwa mwandishi kaachwa.
 
Tatizo sisi wananchi hawataki kusikiliza kilio chetu, Bado Mahakama zetu za juu zinaendelea kuandika haki zetu kwa lugha ya kizungu japo sheria ilibadilishwa!!!

Sasa tunaiuliza mahakama, kwa kuanya kuendelea kutumia lugha ya kiingereza ni kuwadharau wananchi au ni kulidharau Bunge ambalo lilitunga Sheria baada ya kilio cha wananchi?

Kwa nini mahakama hazitaki kutumia lugha ya kiswahili? haswa mahakama za Juuu?!
Achana na hekaya na ngano za jiwe mzee. Hiyo kitu ni ngumu tofauti na unavyofikiria.
 
hujajibu hoja, ugumu unaanzia wapi?! mwanzo ilikuwa kikwazo ni sheria, sheria zimebadilishwa, sasa ugumu ninini ? tueleze, kwamba Majaji na Mahakimu wamegoma kutoa haki zetu kwa kutumia lugha ya Kiswahili?! au nini tatizo,
 
hujajibu hoja, ugumu unaanzia wapi?! mwanzo ilikuwa kikwazo ni sheria, sheria zimebadilishwa, sasa ugumu ninini ? tueleze, kwamba Majaji na Mahakimu wamegoma kutoa haki zetu kwa kutumia lugha ya Kiswahili?!
Una terminologies za kutosha?
 
Mkuu wametokea huko kwenye law practice, hata usajili wa mahakama si utawala peke yake na hata huko wanakokwenda ni ku practice law pia.

Ni kama leo useme kwanini mhariri kateuliwa mwandishi kaachwa.
asante sana. Dunia kwenye kiganga cha mkono, knowledge at your finger tips:
 
Practice makes perfect, sasa hawa wengine wana miaka mingi bila ku practise, si wamehasahau some law .............
 
Ili kujua zaidi kajisomee sheria za utumishi wa mahakama zetu na namna hao wasajili wanavyopatikana.
Kwa kukusaidia tu wasajili wengi wa mahakama wametokea kwenye uhakimu kwa kupanda vyeo.
 
Issue ni je these ladies are they capable of handling complex law issues that will come before them? Au ni ,kuwapa kubalance gender without technical know how? Majaji wa UPE!
Huyu mheshimiwa ni kama anataka kuweka watu imradi tu aoneshe amefanya 50/50
 
Sisi kama Taifa tuna cha kujifunza kutoka kwa majirani zetu Kenya namna nzuri ya kupata majaji. Hawa wa kwetu ni majaji wa mwendo kasi! Nao wanafika mahali wanakula rushwa!!
 
Ili kujua zaidi kajisomee sheria za utumishi wa mahakama zetu na namna hao wasajili wanavyopatikana.
Kwa kukusaidia tu wasajili wengi wa mahakama wametokea kwenye uhakimu kwa kupanda vyeo.
Na pia huwa wanafanya kazi za majaji pale mahakama kuu. Nimeshuhudia kesi yangu moja ilisikilizwa na msajili wa mahakama! Ila hawako competent kama majaji!
 
Practice makes perfect, sasa hawa wengine wana miaka mingi bila ku practise, si wamehasahau some law .............
Mkuu, msajili wa mahakama huwa ana majukumu ya kiutawala kuhakikisha shughuli zinaenda vyema mahakamani. Kuhusu kupractice, msajili na manaibu wasajili hawa ndio wanaosikiliza kesi za maombi ya gharama (bill of cost au taxation case), wanasikiliza maombi ya kukaza hukumu (utekelezaji wa hukumu) iliyotolewa na mahakama kupitia Jaji, wanaahirisha kesi pale Jaji asipokuwepo mahakamani nk.

Kesi za maombi ya gharama za kesi na hata za ukazaji wa hukumu ni kesi kama kesi nyingine, msajili husikiliza pande zote mbili, huchambua maelezo yao na uamuzi wake hutoka kwa mtoaji kuweka authorities nk, hivyo ni lazima afanye research.

Ondoa shaka kuhusu weledi wa naibu wasajili, weka shaka kwa Malata kuwa jaji - huyu amepotosha (misled) sana mahakama ili tu ashinde kesi. Mawakili wa serikali wengi wapo kwa ajili ya kushinda kesi na sio kwa ajili ya kuhakikisha haki inapatikana, watafanya chochote kile ili tu wapate ushindi.
 
Na pia huwa wanafanya kazi za majaji pale mahakama kuu. Nimeshuhudia kesi yangu moja ilisikilizwa na msajili wa mahakama! Ila hawako competent kama majaji!
Sio competent sema hawana uwezo kimaamuzi kuliko majaji maana kuna wasajili wana nondo kuliko majaji wa vimemo na michongo.

Wasajili ni mahakimu waliopanda vyeo
 
Mkuu, msajili wa mahakama huwa ana majukumu ya kiutawala kuhakikisha shughuli zinaenda vyema mahakamani. Kuhusu kupractice, msajili na manaibu wasajili hawa ndio wanaosikiliza kesi za maombi ya gharama (bill of cost au taxation case), wanasikiliza maombi ya kukaza hukumu (utekelezaji wa hukumu) iliyotolewa na mahakama kupitia Jaji, wanaahirisha kesi pale Jaji asipokuwepo mahakamani nk.

Kesi za maombi ya gharama za kesi na hata za ukazaji wa hukumu ni kesi kama kesi nyingine, msajili husikiliza pande zote mbili, huchambua maelezo yao na uamuzi wake hutoka kwa mtoaji kuweka authorities nk, hivyo ni lazima afanye research.

Ondoa shaka kuhusu weledi wa naibu wasajili, weka shaka kwa Malata kuwa jaji - huyu amepotosha (misled) sana mahakama ili tu ashinde kesi. Mawakili wa serikali wengi wapo kwa ajili ya kushinda kesi na sio kwa ajili ya kuhakikisha haki inapatikana, watafanya chochote kile ili tu wapate ushindi.
Ungemuongezea kuwa wasajili hutoka kwenye uhakimu pia.
 
Back
Top Bottom