UTEUZI: Rais Samia ateua Majaji wa Mahakama Kuu

mbona date ni August 23, 2022? Au mimi ndiye sielewi? Lusungo
Funguwa macho yako vizuri, uteuzi umefanyika tarehe 4 mwezi wa 8, tangazo la uteuzi limetoka leo tarehe 6 mwezi wa 8, hiyo tarehe 23 iliyopo chini inasisitiza kampeni ya sensa inafanyika tarehe 23 mwezi wa 8.

Punguza K- Vant.
 
Mayala vipi, maana naye hujinasibu kama mwanasheria.
Mayala hajawahi kupractice uwakili, hapo wenye sifa ni kariba ya Kibatala na awe amefanya kazi yake ya uwakili kwa miaka 15 ndio anakuwa kwenye sifa yakuteuliwa kuwa Jaji na bado kuna mambo mengi yanazingatiwa pia.
 
Wana tuchosha tu hawa watu, angalia huu mfano, yule sheikh anayeswalisha au kuita adhana kwa mtu asiyefahamu anaweza dhani huwa halali, kisa muda mwingi anashinda msikitini, NO!.

Anapata muda mwingi na mzuri wa kulala (kupumzika) hata kufanya kazi, sema anapanga ratiba yake kwa uzuri, ndivyo hawa wanasiasa wanatuchezea hapa.

Anafanya mambo yake mchana then anampa mtoa habari karatasi anaambiwa itoe usiku wakiwa wamelala ionekane tupo busy masaa yote.

✍🏾 Naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
Mbona uteuzi umefanyika tarehe 4? au hamsomi documents?
 
Mkuu Lusungo , kwanza asante sana kwa taarifa hii, ila kwa vile mimi ni mtu wa media, natatizwa sana na hii mikeka inayotoka time hizi!. Hawa watu wanalala saa ngapi?.
Hizi time za hii mikeka kutoka!. Hawa watu wanalala saa ngapi?!. NB, kwa nile kuna mtu aliishawahi kutanka kuwa yeye na mtu fulani wanafana kwa uchapakazi, na kuna mchapakazi alikuwa anachapa kazi round the clock na kupelekea kuingia na mafaili hadi room!, tusiruhusu uchapakazi wa hivi kwa mtu wetu!, tutamchosha!. Kazi yes tuchape kazi, ila muda wa mambo mengine, ikiwemo muda wa kupumzika, lazima apumzike!, hata ikitokea mtu wetu hana usingizi, then aangalie hata katuni, lakini sio kwa uchapakazi huu!.

Hongera zao kwa wateuliwa, ila hongera sana kwa mteuzi, kumbe uswa wa kinsia unawezekana kabisa!, katika teuzi hizi mpya za majaji wapya 22, majiji 11 wana majina ya kiashiria cha Kike!,!
P
Mkuu Pasco,tafadhali jiangalie katika kipindi hiki,vinginevyo lile jambo letu litayeyuka punde.
 
..Nimeona kuna Mzanzibari ameteuliwa.

..Hii ni mahakama kuu ya Tanganyika, ndugu zetu wa Zanzibar wanayo.mahakama kuu yao.

..Mzanzibari anaweza kuteuliwa ktk mahakama ya Rufaa kwani hiyo ni ya muungano.
 
Mkuu Pasco,tafadhali jiangalie katika kipindi hiki,vinginevyo lile jambo letu litayeyuka punde.
Kiukweli nimekuwa natatizwa na kuwa mkweli daima. Kwenye lile jambo letu, nimeliomba kwasababu najijua nina uwezo wa kusaidia kitu, kama nitakatwa kwasababu ni mkweli too much, then be it!.
P
 
..Nimeona kuna Mzanzibari ameteuliwa.

..Hii ni mahakama kuu ya Tanganyika, ndugu zetu wa Zanzibar wanayo.mahakama kuu yao.

..Mzanzibari anaweza kuteuliwa ktk mahakama ya Rufaa kwani hiyo ni ya muungano.
Elimu ya uraia inahitajika sana hata kwa GT wetu humu. Mzanzibari kwanza ni Mtanzania ana haki zote za Mtanzania kama Mtanzania mwingine yoyote ikiwemo haki ya ajira ndani ya serikali ya JMT.

Uzanzibari wake ni an added advantage kwa Zanzibar ambayo Watanzania Bara don't enjoy!.
P
 
Hao wasajili na Naibu wasajili wa mahakama wengi kama sio wote hutokea kwenye uhakimu.

Sheria haimlazimishi rais kuteua mahakimu tuu mradi aliyeteuliwa kuwa jaji anapaswa kuwa na sifa ya uwakili kwa zaidi ya miaka 15 mfululizo.

Pili ujaji ni kazi nzito na ngumu sio kitu cha kufurahia kupata ulaji.

Kila la heri kwao.
Nani kakudanganya bongo watu wanazingatia weledi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom