Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
Nimekuelewa sana mkuu
 
Ninachojua ni kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi Bora zaidi Duniani kwa mafunzo ya ujasusi.
Issue ya Sabaya ni mojawapo ya somo zuri sana kwa majasusi watarajiwa.
 
Sio kila kitu ukiagizwa na Mkuu wako unapaswa kufanya. Ndio maana mtu umepewa akili na utashi WA kung'amua. Sabaya sio roboti, Sabaya sio mtoto, Sabaya halijawahi thibitika kuwa anamapungufu ya akili. Hivyo kivyovyote vile tayari yupo nyavuni.

Na mbaya zaidi kaongea Jambo zito ambalo Kama ni ukweli basi linazidi kumuweka pabaya.

Zingatia;
Hakuna anyemchukia Sabaya, Ila matendo yake ndio yameleta haya yote
Lakini tuvute subira picha lifike mwisho.
 
Nimejiuliza sana. Naona kuna wazito huko CCM/serikalini Sabaya aliwatibua sana enzi za Magufuli.

Hawa watu kwenye kulipa kisasi huwa hawajali aibu. Sasa Ofisi ya Rais (kama taasisi) inachafuka na uharaka wa katiba mpya ndio unazidi kudhihirika ili kuondokana ujinga wa aina hii mapema iwezekanavyo.
Ni noma lakini wametuzoea, tunasahau haraka. Gumzo la tozo liko wapi? Na hili litapita tu
 
... Sabaya kuwemo kwenye Mfumo wa ujasusi wa nchi hii haina mashaka! Toka enzi akiwa mtoto UVCCM aliwahi kukutwa na kitambulisho cha TISS kesi ikafunguliwa. Alivyoachiwa ni mamlaka yake ya uteuzi pekee ndio inajua.

In short, ameandaliwa kwa kazi maalum long time so yanayotokea kwenye sakata hili ni long time plan. Alichokisema mahakamani ni sahihi kabisa.
NI UJINGA KUAMINI HIKI. HII NCHI ITAKUWA YA KIPUUZI KWELI KAMA INAWEKA KATIKA IDARA YA USALAMA WA TAIFA WATU WA AINA YA SABAYA!
 
Angeambiwa akambake mama yake mzazi angeweza?:punguani tu huyo dogo, hata Christopher bagheni alijitetea hivyo hivyo lkn sasa hv anasuburi kitanzi.

Naye asubiri hukumu yake nyani mweusi huyo

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
mama nae inaonkana hakujua misheni kwa ujumla
 
Ukatiri wa Jiwe unaanikwa wazi kwa wale waliokuwa wanamtetea Jiwe kila ukatiri akihusishwa nao sasa hivi wanaumia sana mioyoni mwao baada ya kutambua walikuwa wanamtetea aina furani ya Shwain katiri jiwe
 
Hao ndiyo watu walioingizwa kitengo bila mafunzo wala uzoefu wa kazi.
Mtu anabwabwaja kuwa yeye ana kazi maalum na ana flash kitambulish cha UWT ovyo.
Hao watu wamelalamikiwa sna na wako wengi.
Wanawatia aibu hata Proffessional Intelligence Officers waliofunzwa na kupikika.

\lakini wananchi tunajua kuwa Magufuli is partly to blame kwa kuidhalilisha proffession ya Intelligence, yeye alikichukulia kitengo kuwa idara ya visasi na coercion.
Intelligence ni proffession ambayo si tu infundishwa kwa miaka bali ina practicals ambazo ni za kiuhalisia zinafanyika leaving no trace.

Huyu Sabaya alikuwa kama Boy Scout, sasa anabwabwaja ovyo kuwa alipelekwa kazi hizo na Mgufuli, Mpango na Gavana wa BOT.
What a shame.
Vipi DG Diwani alipata nafasi yoyote ya kutoa ushauri au ndo katika ule mpango kwamba kazi ziendelee?
 
Dah haya ya Sabaya mazito...Mungu asimame haki itendeke...kama alifanya maovu alipie uovu huo na kama hakufanya basi haki yake apatiwe
 
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
Kwa utetezi ule amefeli sana kiuweledi na kimedani. Sasa sijui hili limetokana na maelekezo ya mawakili au ni kwa ubishi wake?
 
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
That's it. Asanteeee
 
Sabaya ndie mwene makosa na ambacho hajui ni kwamba utetezi wa kimahakama unatakiwa uwe umekidhi kisheria, yeye ni dc na sheria ipo inayotambua kazi za dc nje ya hapo no matter what uwezi jitetea kisheria Kama dc...na Kama alitumwa Kama mtu wa usalama kuna misingi ipo kwamba Kama umetumwa kufanya operation ya Siri au ambayo haipo kisheria unatakiwa usiache alama au athari yoyte itakayo kutia hatiani maan ikiwa hivo utakufa mwenyew....sabaya kutaja taasisi ya uraisi and so ever haita mrahisishia njia yake kisheria zaizaid ndani ya mahama zitakuwa ni porojo tu
 
Sabaya anajua anachokifanya. Bila shaka wanasheria wake sio mafala kihivyo na walichekecha pros & cons ya hiyo move na wakajiridhisha kuwa ina faida zaidi kwao kuliko madhara.

Labda Taasisi ya Urais ndio imemwambia aseme hivyo. Tutajuaje? Harafu ni kweli technically bado ni mtumishi wa Serikali ya Samia maana hakufuzwa bali alisimamishwa tu kupisha uchunguzi
Kuwa mwanasheria doesn't mean kila move unayomake inakuwa ni sahihi ndo maan mawakili pia hushindwa kesi...... honestly kusema katumwa na taasisi ya uraisi hakutomtoa hatiani kwene macho ya kisheria....unatumwa kufanya uharifu? Unatumwa kiasi kwamba unasababisha madhara? raisi kukutuma hakuhalalishi uvunjifu wa sheria maana hata raisi yupo chini ya Sheria na taratibu za nchi
 
Anamuonekano na kujiamini kwa Ki TISS, kwenye kesi hii ndio ntajua ya ziada. Namkubali that's me anyway, it doesn't concern any.
Haha Africa bhana jasusi unapotumwa kazi hutakiwi kuacha alama au kusababisha madhara ambayo unaweza tiwa hatiani hata Kama umetumwa.....marekani kuna maafisa wa CIA wengi ambao leo hii wamefungwa na mahakama ya marekani kwa kukutwa na hatia ya ukwikwaji wa sheria wakitekeleza majukumu yao.....
 
Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
Kwahiyo alifanya?
 
Back
Top Bottom