Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Ni wasioelewa tu wanaoweza mlaumu Sabaya Kwa utetezi wake , na ni ukweli mamlaka zilimtuma , hakufanya uhalifu alitekekeza majukumu aliyoagizwa na ushahidi upo.

Rais kumfukuza kazi Sabaya na kuruhusu kudhalilishwa kwake huku akijua ofisi yake inahusika moja Kwa moja ilikuwa wrong move....Sabaya shikilia hapo hapo.
Ushaur wa kichup huu! Kazia apo apo endelea kumdanganya
 
Haha Africa bhana jasusi unapotumwa kazi hutakiwi kuacha alama au kusababisha madhara ambayo unaweza tiwa hatiani hata Kama umetumwa.....marekani kuna maafisa wa CIA wengi ambao leo hii wamefungwa na mahakama ya marekani kwa kukutwa na hatia ya ukwikwaji wa sheria wakitekeleza majukumu yao.....
Tunafahamu hilo, na bado haitoshi kwa customized situation marekani sio viatu vya kulinganisha na tz . Amiri jeshi ni kitu ingine kbsa, naona ipo nuru juu ya Sabaya, kapatwa na hayo kwa Sababu ya uchanga na utopolo wa kajumulo!!
 
Rais ana kinga akikutuma kuuwa tukakukamata wewe hautakuwa na kinga kwa sababu rais amekutuma utakuwa mtuhumiwa namba moja wa hayo mauwaji

Sabaya kutumwa na rais haimuondolei hatia zaidi ni kwamba amekiri kosa ameirahisishia mahakama kesi

Ndiyo maana spika,jaji na waziri mkuu walijikinga ili watakapotii maagizo ya mkubwa wabaki salama baadae wasingefanya hivyo kama kutumwa na rais kufanya jambo ambalo ni kinyume na sheria

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sasa unakubali kwamba magufuli alikua muuaji na jambazi? Kama sio kwann amtume sabaya kufanya mauaji na ujambazi?
Hata kama kwenye ukoo wako hakuna kiongozi bora hata jitahidi uwe karibu na kiongozi wa juu ili ujue nini maana ya kuongoza linchi lenye watu waelewa na wajinga ujue ugumu wake.

Ilishindikana angalia hata movie zenye chembe chembe ta uongozi utapata hata point moja.

Tatizo la jf unaweza kujibizana na mdogo wako ukaishia kumlaumu bure ndo bado anasoma form 4b. Sorry huu ni mfano sikujui.

Mtu mwenye uelewa na akili anaejua uongozi ni nini huwezi kusimama na kusema magufuli alikuwa ni mbaya.huo ni upuuzi.

Aisee tumepoteza kiongozi makini hatuwezi pata kama jpm
 
Kumjua mtu kwa nje sio kuijua dhamira na yaliyojificha ndani yake, niishie kusema hivyo!
Nani aliijenga Libya? Nani aliuwa watu wengi Libya? Nani aliyeondolewa Libya na baada ya kuondolewa Libya ikoje hadi leo?
Nani wanayemlilia Libya?
 
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert

Robert Heriel
Wee jamaaa una akili Sana, hili sabaya boya kweli, umenipeleka Hadi kwa Askari waliomwua kombe mstaafu mkuu wa usalama, iliyodaiwa bahati mbaya. Askari wale walikauka Hadi wakahukumiwa na serikali ikalipa fidia familia ya kombe. Ila raisi mkapa kabla hajakabidhi ofisi kwa kikwete akawaachia huru. Hili pimbi sabaya linapenda kujidai jasusi kichwani ziro, uji kabisa
 
Sio kila kitu ukiagizwa na Mkuu wako unapaswa kufanya. Ndio maana mtu umepewa akili na utashi WA kung'amua. Sabaya sio roboti, Sabaya sio mtoto, Sabaya halijawahi thibitika kuwa anamapungufu ya akili. Hivyo kivyovyote vile tayari yupo nyavuni.

Na mbaya zaidi kaongea Jambo zito ambalo Kama ni ukweli basi linazidi kumuweka pabaya.

Zingatia;
Hakuna anyemchukia Sabaya, Ila matendo yake ndio yameleta haya yote
Broda.

Unapewa Assignment na unapewa objectives lakini huchaguliwi means.

Unless hiyo means iwe ndio objective yenyewe.
 
dogo kapaniki sana atulie tu , yaani kushikwa tako siku mbili analialia , mbona wenzie aliwaingizia miti matakoni na kuwaharibu sehemu za siri akiwa madarakani hawakuhangaika, pia alikata watu masikio wala hakuona kama ni kitu, abebe msalaba wake mwenyewe mambo ya kina mwendazake hayahusiki hapa
 
Sabaya aliwahi kushitakiwa kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

Na wakati huo alikuwa mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.

Sasa ukiniambia Sabaya ni jasusi, ninapata mashaka kwamba inakuwaje jasusi ashitakiwe kwa kujifanya jasusi?
Ili ujue Kama ni jasusi au si jasusi kesi iliishaje ishaje?
 
Kwa lugha nyingine Sabaya alikuwa anamaanisha taasisi ya Urais huwa inaagiza watu kama yeye wafanye walichoagizwa kufanya na hakuna mahali wanaweza kuwa questioned hata kama walitenda jinai
 
Hii inatufundisha kufanya kazi kwa weledi, baadhi ya watu aliowataja sabaya wapo hai na walimuacha asote rumande huku wakijua mission yao ilikuwa vipi, hii ina maana kuwa sabaya kuna sehemu alikosea hivyo wakuu wake waliamua kumuacha ili kumfundisha adabu
 
hakuna kesi hapo.
kama alikuwa anatekeleza majukumu yake aliyo elekezwa na aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu ktk kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa. sasa huo unawezaje kuuita eti ni unyang'anyi?!!
ukiangalia hii kesi kwa jicho la tatu imejaa kisasi dhidi ya sabaya kutokana na majukumu yake aliyo kuwa akiyatekeleza, kwa vyovyote vile lazima angechukiwa sana na either;
1. wafanyabiashara au wanasiasa au wote kwa pamoja. ndicho kilicho tokea.
Kumbe Rais akikutuma uue mtu na ww ukamuua ukakamatwa ukisema Rais alinituma unaachiwa?? Ina maana Rais ana haki ya kuua?? Kma ni death squads hazipo TISS au JWTZ mpaka atumie mwanasiasa kupiga mtu??

Kumtetea Sabaya kutumia hoja hii ndio kunazidi kuichafua serikali ya JPM..... Kwani polisi hawakuwepo?? Kwanini asiende na TISS/FIU wenzake ila mabaunsa wake??

Ipo hivi..... Ukitumwa kma haipo kisheria mfano walioenda kummaliza Lissu!! Ukikamatwa unakua kivyako vyako sababu ulilofanya pale lipo off record na nje ya sheria za nchi!!

Sasa kma jasusi unatumwa mission mpka ina backfire hivo then inabidi tutafakari tuna TISS wa aina gani? Hivi huyo Sabaya alishindwa kuhakikisha ushahidi unapotea?? Au kupata taarifa kiintelijensia bila kuhitaji kelele nyingi??

Mnazidi kuongeza maswali bora mkae kimya tu
 
Hakutumwa na mtu wala nini.. life style yake ndo imemponza. Mtu anatembea na wapambe 8 na malaya 8 kila siku bar zote. Bill ikija milioni 1.8 unategemea anazilipaje? Hapo ndo bado amekimbia bill sehemu kibao. Mshahara wake wenyewe hauzidi sh milioni 4. Atavuna alichopanda. Nashangaa anamwaga machozi mahakamani kuwa aliponea chupuchupu kuuawa mara 2. Sasaiv hata akishinda hiyo kesi bora ahame huu mkoa kabisa. Maana watu wa huku hawanaga mbili
 
Kumbe Rais akikutuma uue mtu na ww ukamuua ukakamatwa ukisema Rais alinituma unaachiwa?? Ina maana Rais ana haki ya kuua?? Kma ni death squads hazipo TISS au JWTZ mpaka atumie mwanasiasa kupiga mtu??

Kumtetea Sabaya kutumia hoja hii ndio kunazidi kuichafua serikali ya JPM..... Kwani polisi hawakuwepo?? Kwanini asiende na TISS/FIU wenzake ila mabaunsa wake??

Ipo hivi..... Ukitumwa kma haipo kisheria mfano walioenda kummaliza Lissu!! Ukikamatwa unakua kivyako vyako sababu ulilofanya pale lipo off record na nje ya sheria za nchi!!

Sasa kma jasusi unatumwa mission mpka ina backfire hivo then inabidi tutafakari tuna TISS wa aina gani? Hivi huyo Sabaya alishindwa kuhakikisha ushahidi unapotea?? Au kupata taarifa kiintelijensia bila kuhitaji kelele nyingi??

Mnazidi kuongeza maswali bora mkae kimya tu

Mkuu Zitto Kabwe,
Huyo hajui hata anachokieleza, kumsaidia ni kumuacha tuu na mawazo yake ya kijinga.

Yaani mtu anasimama kabisa Mahakamani anasema ati nimefanya hayo niliyoshtakiwa nayo sababu nilitumwa na Rais,
Hafikirii hata anachokisema kuwa ni kuichafua serikali ya awamu ya tano.
Hajui pia kuwa hata Kama alitumwa bado Yuko na hatia.

Alafu kuna watu wanaona huyo Sebaya yuko sahihi.
Ajabu hii
 
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
Its open secret world over that Governments have monopoly of violence.
 
67 Reactions
Reply
Back
Top Bottom