Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,039
- 3,486
Kwa hiyo hapo umehitimisha ya kwamba endapo watumishi wa kabila fulani wakionekana wamepangwa kufanya kazi eneo fulani ina maana kinachoangaliwa ni utendaji bora kwa manufaa ya wananchi wengi sio undugu, kabila, kanda, rangi au itikadi kama mleta mada alivyodai?JWTZ Jeshi la Wakurya Tangu Zamani.
Kipindi jeshi linaongozwa na jenerali kutoka Mara mwenye elimu ya darasa la nne hakuna hata mmoja alithubutu kuinua domo lake kuhoji leo hii watu fulani kama Wahaya, Wanyakyusa, Wasukuma, Wamwera, Wamasai au Wadigo kuaminiwa katika nafasi kadhaa na ufanisi ukaridhisha imekuwa nongwa?
Mbona hamjawahi kulalamika enzi za Basil Mramba enzi hizo alijaza Wachagga watupu katika idara nyeti hasa fedha, uhandisi, biashara na viwanda?
Huyo mtoto wa Magufuli aliyepewa ubunge ni nani mbona hatujawahi kumsikia hata siku moja?
Watu waliokuwa maadui wakubwa na walimchukia sana John Pombe Joseph Magufuli kwa asilimia kubwa ni wanaCCM wenyewe wa ndani sio kutoka vyama vya upinzani ambao kimsingi walikuwa wakitumia haki yao ya kikatiba na kisheria kumpa changamoto za kiutendaji ili kuboresha kwa manufaa ya watanzania bila kujali itikadi za kisiasa au kidini.