Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,779
- 218,404
Tunaendelea na nyuzi zetu za mwezi wa 3, ambao ni mwezi wa Mungu.
Ni wazi kila mwananchi anafahamu kuhusu kampeni za wazi kabisa za kutaka Rais wa awamu ya 5 Dkt John Magufuli aongezewe muda wa utawala wake kinyume kabisa cha Katiba ya Tanzania, yaani baada ya kumaliza utawala wake wa miaka 10, bado aongezewe miaka mingine isiyo na idadi.
Kampeni hii kabambe iliongozwa na kundi lisilo rasmi lililopachichwa jina la "Sukuma gang" na baadaye kuanza kuungwa Mkono hadharani na baadhi ya watu , na hatimaye likatua bungeni likiletwa na mbunge wa ccm Jimbo la Nkasi (zipo taarifa kwamba nyuma yake kulikuwa na kundi kubwa), Huku hoja yake ikiungwa mkono na Spika wa Bunge hilo Job Ndugai , na kwamba inasubiriwa muda ufike lipelekwe bungeni ili lijadiliwe na Katiba ya Nchi ibadilishwe.
Hata baada ya Jambo hilo kupoa kidogo likaibuliwa tena na Mbunge wa Bahi Juma Nkamia , akisisitiza umuhimu wa kumuongezea John Magufuli muda wa uongozi , huku akisisitiza kwamba muhula wa Urais uwe miaka 7 badala ya mitano iliyowekwa kwenye Katiba ya Nchi .
Wale wote waliopinga jambo hili walionekana Wasaliti na walishughulikiwa chini kwa chini na Wateule wa Rais kuanzia kwenye chama hadi serikalini , huku Wateuliwa wengi wakichekelea na kuvimba kwa kiburi wakijua watakuwa wateule milele (Hapa ndipo ilipoanzia sumu aliyolishwa Mangula)
Ushahidi wa wapinga milele kushughulikiwa ulikuja kuthibitishwa na Juma Nkamia mwenyewe , alipokiri hadharani kwamba Alilazimika kutamka kwamba Magufuli aongezewe muda ili kunusuru uanachama wake ndani ya ccm , kwamba kulikuwa na mpango wa kumvua uanachama , na kwa vile mkubwa alifurahishwa na kauli ya Nkamia ya kumuongezea muda , Nkamia hakutimuliwa tena .
Wakati haya yakiendelea , Viongozi karibu wote wastaafu walikuwepo huku wakinyamaza kimya as if hakuna uchafu unaopangwa , Wakuu wa vyombo vya dola wakiwa kimya ikiwa ni ishara ya kuunga mkono uharamia huo .
Sasa Swali letu ni hili , Waliokuwa wanafanya Kampeni hiyo haramu walichagizwa na nini hasa , Je ni Utendaji bora wa Magufuli na kwamba hakuna Mwanaccm mwingine angeweza kutenda kama Yeye , ama walichagizwa na Uroho wa madaraka ili waendelee kula miaka yote baada ya Rafiki yao kuwa madarakani milele ?
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO