Kwenye Utawala wa awamu ya 5, Viongozi wa Chadema walikamatwa, walitekwa, walifungwa jela, walipotezwa, walijeruhiwa na wengine waliuawa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,247
Tunaendelea na nyuzi zetu za mwezi huu wa 3, ambao ni Mwezi wa Mungu.

Kwenye utawala wa Awamu ya 5, ulioongozwa na Dkt. John Magufuli, Karibu viongozi wote wa Chadema wa ngazi zote walitekwa, walikamatwa, walijeruhiwa, waliuawa na walirundikwa selo ama walifungwa jela, kwa kesi za uongo ili kuwakomoa.

Wanaouliza kwanini tunayaleta haya leo , jibu lake ni hili , ni kwa sababu hatutaki uchafu huu urudiwe tena kwenye Nchi yetu nzuri, Never and Never again.

Alphonce Mawazo alikuwa kiongozi wa mwanzo kabisa kuuliwa baada ya awamu ya 5 kutwaa madaraka, huyu alipigwa mashoka kuliko hata yale wanayopigwa ng'ombe wa nyama machinjioni.

FB_IMG_1542188762028.jpg

Alphonce Mawazo ni miongoni mwa watu walioua CCM Kanda ya Ziwa, hii ndio sababu kubwa ya kuuawa kwake , serikali ya Jiwe ikazuia mazishi yake kwa siku kadhaa , yaani wamemuua lakini hawataki azikwe , Mawazo anaingia kwenye historia ya Taifa kuwa mwanasiasa wa kwanza kuzikwa kwa Hati ya Mahakama .

Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba anayekula nyama ya mtu haachi, hakika ndivyo ilivyokuwa, baada ya Mawazo mambo ya kukamata viongozi wa Chadema yakashika kasi, Godbless Lema akakamatwa na kupewa kesi na kisha kunyimwa dhamana kwa tuhuma za kutoa unabii hadharani , hata hivyo unabii huo ulikuja kutimia bila hata kupunja .

Screenshot_2024-03-16-15-52-05-1.png
Screenshot_2024-03-16-15-43-55-1.png

Kama haitoshi viongozi wa Chadema wakaanza kuwindwa na kukamatwa kama kuku wa Pasaka, Tundu Lissu akapigwa risasi zisizo na idadi kwa lengo la kumuua, ikaelekezwa azikwe haraka na hotuba ya kusomwa kwenye mazishi yake ikaandaliwa.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu akakamatwa na kufungwa jela kwa kesi ya uongo, Hakimu aliyemfunga jela Michael Mteite akapandishwa cheo.

Screenshot_2024-03-16-15-55-27-1.png
Screenshot_2024-03-16-15-58-18-1.png

Viongozi wote wa Chadema Tunduma walikamatwa akiwemo Meya wa Mji huo Ally Mwafongo na kupewa kesi ya uzushi ya mauaji, yaani viongozi 57 wote wanadaiwa kuua mtu mmoja tu wa CCM haya ndio mambo ya awamu ya 5.

Mdude akatekwa na kuteswa nusu ya kufa, Wakili wake aliyepata msaada wa pesa kutoka kwenye kituo cha utetezi wa haki za binadamu na kuingiziwa pesa akaunti yake ikafungwa ili ashindwe kwenda Mbeya kumtetea mteja wake , shukrani ziwaendee Wazungu walioingilia kati hadi akapatikana.

Karibu viongozi wote wa Kamati Kuu ya Chadema akiwemo Freeman Mbowe walikamatwa na kuswekwa gerezani kwa tuhuma za uongo za kusababisha mauaji ya Akwilina, Ambaye alipigwa risasi na Polisi chini ya Lazaro Mambosasa aliyekuwa RPC, viongozi wa Chadema wakahukumiwa kifungo au kulipa faini ya Mamilioni ya hela za kitanzania, unaweza kushangaa walioua ni Polisi, lakini waliohukumiwa ni Chadema!

Hivyo ndivyo Hakimu Thomas Simba alivyoona, Shukrani sana kwa Watanzania walioamua kuchanga fedha zao ili viongozi hao wa Chadema wasiozee jela

Wanachadema waliopotea, kuteswa na kufungwa ni wengi, akiwemo Bernard Saa Nane ambaye hadi leo hajulikani aliko

Nitasema kweli Daima fitina kwangu mwiko
 
Tunaendelea na nyuzi zetu za mwezi huu wa 3 , ambao ni Mwezi wa Mungu .

Kwenye utawala wa Awamu ya 5 , ulioongozwa na Dkt John Magufuli , Karibu viongozi wote wa Chadema wa ngazi zote walitekwa , walikamatwa , walijeruhiwa , waliuawa na walirundikwa selo ama walifungwa jela , kwa kesi za uongo ili kuwakomoa .

Wanaoliza kwanini tunayaleta haya leo , ni kwa sababu hatutaki uchafu huu urudiwe tena kwenye Nchi yetu nzuri , Never and Never again .

Alphonce Mawazo alikuwa kiongozi wa mwanzo kabisa kuuliwa baada ya awamu ya 5 kutwaa madaraka , huyu alipigwa mashoka kuliko hata yale wanayopigwa ng'ombe wa nyama machinjioni ,

View attachment 2936409

Alphonce Mawazo ni miongoni mwa watu walioua ccm Kanda ya Ziwa , hii ndio sababu kubwa ya kuuawa kwake .

Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba anayekula nyama ya mtu haachi , hakika ndivyo ilivyokuwa , baada ya Mawazo mambo ya kukamata viongozi wa Chadema yakashika kasi , Godbless Lema akakamatwa na kupewa kesi na kisha kunyimwa dhamana

View attachment 2936423View attachment 2936426

Kama haitoshi viongozi wa Chadema wakaanza kuwindwa na kukamatwa kama kuku wa Pasaka , Tundu Lissu akapigwa risasi zisizo kwa lengo la kumuua , ikaelekezwa azikwe haraka na hotuba ya kusomwa kwenye mazishi yake ikaandaliwa.

Mbunge wa Mbeya Mjini , Sugu akakamatwa na kufungwa jela kwa kesi ya uongo , Hakimu aliyemfunga jela Michael Mteite akapandishwa cheo

View attachment 2936433View attachment 2936434

Viongozi wote wa Chadema Tunduma walikamatwa akiwemo Meya wa Mji huo Ally Mwafongo na kupewa kesi ya uzushi ya mauaji , yaani viongozi 57 wote wanadaiwa kuua mtu mmoja tu wa ccm , haya ndio mambo ya awamu ya 5 .

Mdude akatekwa na kuteswa nusu ya kufa , shukrani ziwaendee Wazungu walioingilia kati hadi akapatikana .

Karibu viongozi wote wa Kamati Kuu ya Chadema akiwemo Freeman Mbowe walikamatwa na kuswekwa gerezani kwa tuhuma za uongo za kusababisha mauaji ya Akwilina , Ambaye alioigwa risasi na Polisi chinivya Lazaro Mambosasa aliyekuwa RPC , viongozi wa Chadema wakahukumiwa kifungo au kulipa faini ya Mamilioni ya hela za kitanzania , unaweza kushangaa walioua ni Polisi , lakini waliohukumiwa ni Chadema ! Hivyo ndivyo Hakimu Thomas Simba alivyoona , Shukrani sana kwa Watanzania walioamua kuchanga fedha zao ili viongozi hao wa Chadema wasiozee jela

Wanachadema waliopotea , kuteswa na kufungwa ni wengi , akiwemo Bernard Saa Nane ambaye hadi leo hajulikani aliko

Nitasema kweli Daima fitina kwangu mwiko
Subiri misukule yake ije!
 
CHADEMA katika ubora wake.

Msisahau safu nzima ya serikali hii inayoendelea.

Ieleweke hakuna kitu kama Awamu ya Tano kwa sababu hakujakuwa na Uchaguzi Tanzania wa kuweka Awamu mpya

Karibia baraza zima la mawaziri na viongozi wengine ni wale wale, Including the President Samia Suluhu Hassan

Sasa ukizingatia mabaraza ya usalama wa taifa, na vyombo vingine kama hivyo, uratibu, utaratibu, michakato n.k na sheria zake n.k utaona kwamba kama msaidizi mkuu na mshauri mkuu wa Rais hakuna jambo ambalo lingeweza kumpita. Ikiwa ina maana hata huyu Rais aliepo madarakani alihusika.

Hili mkalitazame, na sio kufanya nit picking kwa lengo la kuchafua, kudidimiza au kuchanganya ukweli.

CHADEMA wacheni kumshabulia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumshambulia Hayat Rais ambaye hana uwezo wa Kujitetea.
 
CHADEMA katika ubora wake.

Msisahau safu nzima ya serikali hii inayoendelea.

Ieleweke hakuna kitu kama Awamu ya Tano kwa sababu hakujakuwa na Uchaguzi Tanzania wa kuweka Awamu mpya

Karibia baraza zima la mawaziri na viongozi wengine ni wale wale, Including the President Samia Suluhu Hassan

Sasa ukizingatia mabaraza ya usalama wa taifa, na vyombo vingine kama hivyo, utaona kwamba kama msaidizi mkuu na mshauri mkuu wa Rais hakuna jambo ambalo lingeweza kumpita. Ikiwa ina maana hata huyu Rais aliepo madarakani alihusika.

Hili mkalitazame, na sio kufanya nit picking kwa lengo la kuchafua, kudidimiza au kuchanganya ukweli.
Hilo uliloandika limeongeza wigo halijamtoa jiwe kwenye uhusika
 
Tunaendelea na nyuzi zetu za mwezi huu wa 3, ambao ni Mwezi wa Mungu.

Kwenye utawala wa Awamu ya 5, ulioongozwa na Dkt. John Magufuli, Karibu viongozi wote wa Chadema wa ngazi zote walitekwa, walikamatwa, walijeruhiwa, waliuawa na walirundikwa selo ama walifungwa jela, kwa kesi za uongo ili kuwakomoa.

Wanaouliza kwanini tunayaleta haya leo , jibu lake ni hili , ni kwa sababu hatutaki uchafu huu urudiwe tena kwenye Nchi yetu nzuri, Never and Never again.

Alphonce Mawazo alikuwa kiongozi wa mwanzo kabisa kuuliwa baada ya awamu ya 5 kutwaa madaraka, huyu alipigwa mashoka kuliko hata yale wanayopigwa ng'ombe wa nyama machinjioni.

View attachment 2936409

Alphonce Mawazo ni miongoni mwa watu walioua CCM Kanda ya Ziwa, hii ndio sababu kubwa ya kuuawa kwake , serikali ya Jiwe ikazuia mazishi yake kwa siku kadhaa , yaani wamemuua lakini hawataki azikwe , Mawazo anaingia kwenye historia ya Taifa kuwa mwanasiasa wa kwanza kuzikwa kwa Hati ya Mahakama .

Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba anayekula nyama ya mtu haachi, hakika ndivyo ilivyokuwa, baada ya Mawazo mambo ya kukamata viongozi wa Chadema yakashika kasi, Godbless Lema akakamatwa na kupewa kesi na kisha kunyimwa dhamana.

View attachment 2936423View attachment 2936426

Kama haitoshi viongozi wa Chadema wakaanza kuwindwa na kukamatwa kama kuku wa Pasaka, Tundu Lissu akapigwa risasi zisizo kwa lengo la kumuua, ikaelekezwa azikwe haraka na hotuba ya kusomwa kwenye mazishi yake ikaandaliwa.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu akakamatwa na kufungwa jela kwa kesi ya uongo, Hakimu aliyemfunga jela Michael Mteite akapandishwa cheo.

View attachment 2936433View attachment 2936434

Viongozi wote wa Chadema Tunduma walikamatwa akiwemo Meya wa Mji huo Ally Mwafongo na kupewa kesi ya uzushi ya mauaji, yaani viongozi 57 wote wanadaiwa kuua mtu mmoja tu wa CCM haya ndio mambo ya awamu ya 5.

Mdude akatekwa na kuteswa nusu ya kufa, shukrani ziwaendee Wazungu walioingilia kati hadi akapatikana.

Karibu viongozi wote wa Kamati Kuu ya Chadema akiwemo Freeman Mbowe walikamatwa na kuswekwa gerezani kwa tuhuma za uongo za kusababisha mauaji ya Akwilina, Ambaye alipigwa risasi na Polisi chini ya Lazaro Mambosasa aliyekuwa RPC, viongozi wa Chadema wakahukumiwa kifungo au kulipa faini ya Mamilioni ya hela za kitanzania, unaweza kushangaa walioua ni Polisi, lakini waliohukumiwa ni Chadema!

Hivyo ndivyo Hakimu Thomas Simba alivyoona, Shukrani sana kwa Watanzania walioamua kuchanga fedha zao ili viongozi hao wa Chadema wasiozee jela

Wanachadema waliopotea, kuteswa na kufungwa ni wengi, akiwemo Bernard Saa Nane ambaye hadi leo hajulikani aliko

Nitasema kweli Daima fitina kwangu mwiko
Lakini Bado hamtoi shukrani Kwa Samia kukomesha hayo.
Niliona video Moja Sugu anayembelea Tanganyika jeki nilicheka sana 🤪🤪🤪🤪
 
Back
Top Bottom