Inategemea wahusika walikuwa na agenda ipi na ngapi vichwani mwao walipoingia kwenye uhusiano.
1.Kuna watu umri wao si rahisi sana kuonekana na hii inawawezesha kupendwa hata na wale ambao wana umri mdogo.Hawa kwa kweli wanaweza kuendelea tu na mapenzi maana huenda ni penzi la kweli lisilo na agenda mbaya.
2.Kuna wanaoonekana kabisa kuwa umri umeshasogea lakini bado wanajikuta "kupendwa" na wenye umri mdogo. Hawa lazima wajiulize maswali magumu kwanini bado wanang'ang'aniwa?
3.Kwa wenye kujikuta kwenye hali hii kimahusiano, wajaribu kufikiria mbali zaidi ya leo.Wajiulize je, miaka kumi kuanzia leo bado nitajisikia nampenda huyu mtu au interest zitabadilika? Je nitakuwa comfortable naye mbele ya wenzangu? Je interests zitakavyozidi kuachana nitafanya nini? Nitachukulia umri mkubwa ndio sababu ya kumfanyia kinyume na hasa hili hufanywa sana na akina kaka ambao hawaishi kusingizia mara ohh mwanamke hazai, mwanamke alinirubuni nk.
4.Kadhalika akina dada/mama wenye umri mkubwa wajiulize itakapotokea natolewa visababu kama hivi nitafanya nini?Nina kifua cha kuvumilia kejeli na kebehi kama hizi?
5.Mwisho wa siku uamuzi utakuwa wa mhusika.