Dah Paka Mweusi aka Mtakatifu.
Unachokisema ni sahihi kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!
Ukimjengea mpenzi wako mapenzi katika msingi wa pesa, siku zikiisha imekula kwako.
Unajua ndo naiona hii thread sasa hivi ila nilikuwa naongea na mtu mmoja mawazo kama haya haya.
Kwamba pesa na vitu vingine viwe ni sehemu ya matumizi tu, lakini sio mbolea ya kukuzia Penzi.
Mfahamu mwenzio anapenda nini anachukia nini, mfanyie vile anavyovipenda usimfanyie vile anavyovichukia, hata kama
unaviona ni sahihi kabla hujamuelewesha akakuelewa na kukubaliana na wewe. Sio lazima kila kitu unachokipenda wewe,
ukifanye wakati mwenzio hakipenda. Kwenye mapenzi kuna kujitoa sadaka pia, unaacha kufanya jambo fulani ingawa linakufurahisha,
wewe lakini kwa sababu mwenzio halipendi unaamua tu kuliacha.
Sio lazima mpenzi wako akuombe pesa ndo umpe, wakati mwingine soma tu alama za nyakati,
Na kama nafsi yako inaambatana vizuri na mwezio , unaweza ukasukumwa kumpa pesa pale anapozihitaji kabla hata hajakuambia.
Upendo, heshima na utu katika yenu, pamoja na neema ya Mungu, ndiyo Mbolea ya mapenzi yenu.
Ukiwa na utu wema, utaepuka usaliti kwa mwenzio, utajali pale panapotakiwa kujali.
Na mapenzi yatakuwa yanakua na kukomaa siku kwa siku.
Ndio navyowaza mimi!!!