Mapenzi na pesa ni vitu viwili tofauti sana, na matumizi yake yako tofauti sana
Pesa hufanya kukidhi mahitaji yenu tu ambayo siyo lazima yatimizwe na upande mmoja wa wapenzi, haya mambo ya kuwa lazima ahudumiwe mwanamke pekee ni desturi na mila tu ambazo kulingana na uhitaji wa haki sawa kwa jinsia zote ktk nyakati hizi inaondoa kabisa dhana ya mwanamke kuwa tegemezi wa huduma
Huduma huendana na uwezo wenu wahusika, na hili ndio hufanya mapenzi mengi kujifia kifo cha kawaida sababu ya kushindwa kupima kipato na matumizi ya mwenzi wake, hivyo mwanaume kujikuta anabeba mzigo mzito sana moyoni mwake kiasi ambacho inafika mahali anashindwa kuhimili
Mapenzi na pesa ukiyafanya yaendane bila kuyatenganisha basi hapo hakuna upendo ndani yake ila kuna kutumika tu, na siku huna uwezo wa kuhudumia utakimbiwa na kwenda huko ziliko
Mwanamke kama una kipato kikubwa kuliko Mme/mchumba/bwana n.k yanini kuforce lazima huduma zako upate toka kwa huyo mwandani wako! Maisha ya leo ni kutegemeana
Umuhimu wa pesa uko kila nyanja hauiishi kwenye mapenzi pekee yake