Kila mwanaume ndoto yake kubwa katika mapenzi ni kuoa au kumiliki mpenzi ambaye ni mzuri wa sura na mrembo. Japo wahenga walisema mwanamke Tabia usemi huu umetupiliwa mbali na vijana wa leo wanaoamini kuwa Tabia inafundishika.
Sasa kwa maisha ya sasa na jinsi minavyowaona wadada wa kileo kama ukimiliki msichana mrembo wa kuvutia na hauna hela ujue kuna mambo mawili, kwanza yawezekana una zali la mentali, ambalo kwa miaka hii ya karibuni limepotea, pili unasaidiwa pia kula chakula cha ndoa na mtu mwingine mwenye pesa.
Ili kuondokana na kero hii njia kuu ni moja kupigana kiume, usiku na mchana kuzisaka pesa, ukizipata utapata mrembo wa aina ile unayemtaka vinginevyo kumiliki binti mrembo na mzuri wa sura ni ndoto za alinacha.
Kama wanaume tukiwa wavivu kujituma tutegemee mambo mawili kwanza kukumbatia ule useme wa mwanamke tabia na kutumia usemi huu kama kimbilio letu la kujitenga na mabinti warembo au tusubiri zali la mentali.