Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Uko na mpenzi wako umemuonyesha kila aina ya upendo kwenye matatizo na furaha za familia yake unahudhuria na kuchangia, umemnunulia simu ya bei mbaya sana hadi ukiiona simu ya mzazi wako wa kike unaona aibu unaamua kumpa mama yako simu yako ili uwe umetenda haki maana demu ana simu kali kuliko mama yako mzazi.

Tatizo hujawahi kumpa fedha atumie ila unatatua matatizo madogo madogo yake bila yeye kukuambia unakua umejiongeza MF; (KUNUNUA GESI YA JIKO , kumuongezea vocha).

Siku moja kakutumia msg "Nimevumilia nimeshindwa, matunzo juu yangu zero kama huitaji kunigharamia wewe niambie, hapa sina kazi unashindwa kunihudumia je nikiwa na kazi utaweza kunitunza? Sipo teyari kwa hilo utanisamehe" hebu nipeni jibu zuri la kumjibu huyu mpendwa wangu kaifanya akili yangu igande kwa muda.
 
Mmh leo kumepamba moto humu kila thread ni ya pesa inaletwa tu kidizain
Apo akil kumkichwa kuhudumia ni pesa tu ndugu, pengine ameshindwa sema direct
 
Back
Top Bottom